ONE NIGHT ONE MISTAKE 07****08 Rose alienda kununua vitu vyote akivyoagiziwa na kupeleka ofisini kwa Boss.
"Boss vitu vyako hivi hapa. Alisema Rose huku anamuangalia boss usoni bila kummaliza.
"Vipi mbona unaniangalia sana ? Umeleta viti vyangu si uende unataka kushuhudia nini?
Rose aliondoka lakini alipofika kwa wenzake
akaanza kusimulia alichoagizwa na boss.
"Jamani huko sasa mkae mkao wa kula nahisi boss kashafsnya yake, nianze kuandaa na baby
show nahisi Romex junior anakuja.
"Wewe Rose wewe hebu achaga umbea basi.
Sio umbea jamani ninachokiongea ni ukweli mtupu. Boss katika kujitafutia vitu vya udambu udambu na udongo juu.
Wenzake waliangaliana kwa mshangao.
Kwahiyo huo udambu udambu na udongo anakula nani?
Sijui huenda tabia za mimba na dalili
zimehamia kwa baba kijacho.
"Mmmh haya makubwa sasa.
"Jamani tusitumie kichwa kama hilo kipo basi tutajua tu kinachotakiwa ni subira tu.
Kadiri siku zilivyozudi kwenda habari ziliaanza kusambaa ofisini kwa kasi kuwa boss Romex anafanya mambo ya ajabu.
Wafanyakazi walikuwa wakishangaa tabia yake mpya lakini hakuna alimnyanyua mdomo kuuliza. Walikuwa wanasngaliatu.
Siku ziliendelea kwenda salsa hakuishia vituko na hiyo mimba yake na Romex alijikuta akivutiwa na vitabua vya ajabu ajabu mpaka kuna wakati wa siku za weekend akawa anajikuta anammisi sana Salsa.
Siku moja jioni, Romex alikuwa amekaa peke yake bustani ya nyumbani kwake akiounga upepo huku akipata kinywaji, Ghafla alijikuta akimkumbuka Salsa na vituko vyake, alijikuta anaanza kucheka mwenyewe kwa sauti ya chini. Mlinzi wake, aliyekuwa akimlinda alikuwa amesimama pembeni, akamshangaa. "Vipi boss wangu kwema?
"Kwema
"Mbona unacheka mwenyewe?
Romex alitabasamu, macho yake yakiwa kwenye screen ya simu yake.
"Unajua, mambo ya Salsa yananifurahusha sana. Kuna muda natamani sana kuwa karibu nae na
kuna muda natamani na mimi niwe baba kijacho, alisema, huku akicheka kidogo, lakini macho yake yalikuwa na hisia zilizojaza upendo. * Ukiamua unaweza boss wangu, mbona kila
kitu kipo sawa kwako? * Domi sio kama unavyofikiria kuna jambo moja
linaniumiza sana kichwa changu, niliweza mambo sawa naweza kutafuta mwanamke wa kuanza nae safari ya kuanza familia.
Siku moja jioni Romex alimfuata Salsa kwaajili ya matembezi, walikaa sehemu wakawa wanakula ice cream huku wakiwa wanaongea "Salsa naweza kuuliza jambo?
"Uliza tu. Alijibu Salsa huku akiwa anaendelea kula ice cream.
"Huwezi kuchukia?
"Kwani unania ya kutaka nikasirike? "Natoa tahadhali.
"Ongea tu.
Nilikuwa nataka kujua kuhusu hatma ya ujauzito wake na pia kuhusu muhusika wa hiyo mimba yako.
Salsaaluacha kula ice cream, moyo wake ukawa unadunda kwa kasi. Romex alikuwa akimuangalia usoni huku akimsomba hisia zake. Vipi kama nikisema hii mimba muhusika ni wewe ndio maana inajitoa na kujali sana?
Romex alimuangalia, machoni kisha taratibu na kuachia tabasamu, alijua jibu la Salsa ilikuwa kama utani tu lakini kwa upande wa Salsa alikuwa akimaanisha.
Kwahiyo huyo mtoto wa tumboni kwako ni mtoto wangu?
"Ndio.
Sawa kama umeamua kunipa zawadi nizampikea.
Maongezi yao yaliishia hapo. Baada ya hapo walinyanyuka na kuanza kutembea tembea huku wakinunua vitu vidogo vidogo ambavyo Salsa alikuwa akivuta nani.
Siku zilienda Romex aliendelea kujali zaidi maana hata clinic alimpeleka na kutaka kujua maendeleo ya mtoto, mambo ya Romex taratibu yalianza kumvutia Salsa.
Salsa alianza kujenga upendo kwa Romex, akiona jinsi anavyomjali, jinsi anavyomlinda na kuonyesha huruma. Hii ilimfanya moyo wake kufungua mlango wa hisia zake, akaanza
kuelewa kuwa Romex sio boss lakini ni mwanaume sahihi sana kwake na mtoto wake amepata baba mwenye kila sifa ya kuwa baba.
Chapter 8
Siku zilizidi kusonga mbele na tumbo la Salsa lilianza kuonekana haikuwa siri tena watu walijua Romex ndio anamuhudumia kwa huruma tu na wengine walijua ni mimba yake ndio maana anajitoa kuhudumia. Salsa alianza kuonyesha vituko vya kweli vya mimba kwanza alikuwa na wivu hatari alikuwa hapendi kuona Romex akiwa amesimama na mwanamke kwa muda mrefu, akicheka nae yani alikuwa anamuona haswa
Siku moja Romex alikuwa na mgeni wa kike ofisini kwake walikuwa wakiongea huku wakicheka, wakati huo Salsa alikuwa mlangoni akisikilizia, vicheko vilivyozidi alifungua mlango. na kuwavamia.
*Vipi Salsa? Romex aliuliza
* Nimekuja kuchukua koti lako, ni ulle haraka.
Alijibu salsa akiwa kakasirika tena huku kashika kiuno, yule mwanamke alimuangalia kwa mshangao maana Romex sio mtu wallamrishwa hivyo. Taratibu Romex alivua kiti na kumpatia. Salsa
alichukua koti akawa anaondoka lakini alipofika mbele kidogo wakasimama
*Boss utanipeleka nikale Ice cream?
*Ndio.
Salsa aliondoka lakini bado alikuwa analalamika. Yule mwanamke sijui anafanya nini pale si aondoke
Ndani ya ofisi yule mwanamke alimuangalia Romex na kuuliza. *Romex huyu ni nani?
Mfanyakazi wangu.
Hahahaha Romex umeanza lini kutembea na wafanyakazi wako mpaka kuwatia mimba? Mmmmm Melinda usifanyike gari kwa mbele litakugonga. Huyu binti katoka kuniziea tu na
hiyo mimba yake yani kuna muda huwa ananichukulia kama mimi ni mwanaume niliempa hiyo mimba.
* Mmmmh sijui maana ninavyojua mimi mtu anadhaniwa hivi ni yule mwenye mzigo wake
hebu tufikirie vizuri Rome.
Hakuna kitu kama hicho, haijawahi kutokea, tuendelee na maongezi yetu.
Salsa alikuwa na mambo ya ajabu mpaka Romex akaanza kuchoka, salsa alikuwa akiagiza chakula alichokipenda jana, leo akiletewa anasema kinanuka kama tairi ya baiskeli Illyochomwa.
Siku moja ilikuwa siku ya jumamosi majira ya saa tatu asubuhi alimkuta Salsa akiwa amelala kujifunika blanketi. Alikaa pembeni yake na kuuliza
*Vipi upo sawa?
Kidogo
Kwanini kidogo. Tangia jana usiku kuna kitu nimejikuta
nakitamani ila ndio sikuwa najua hakupata wapi. Mmm sema tu, mimi nipo hapa kwaajili yako mama kijacho.
*Romex leo nataka kula maboga yaliyo
chemshwa na chumvi tu
Romex alimuangalia kwa mshangao, "Sasa hayo maboga mimi nitapata wapi? Sijui ila wewe jitahidi uyapate maana sijui kama naweza kuvumilia bila kuyala. Alijibu salsa huku
akinyanyuka na kupiga miayo.
Romex alichukua simu yake na kupiga sehemu "Make sure tunapata maboga. Sijali utapata wapi, ninachotaka mimi mama kijacho afurahi. Kisha akamtazama Salsa kwa upendo. "Nitafanya kila kitu kwaajili yako na huyo mtoto akiwa tumboni kwako.
Salsa alimwangalia Romex kisha akatabasamu. Hakujua kama anampenda kwa dhati au kwa
sababu ya kutimiza matakwa ya mimba tu
Lakini kwa sasa hakuwa na muda wa kujiuliza
maswali mengi alikuwa anahitaji attention.
*Basi nenda kaoge maboga yako yakiha ule.
Sawa
Salsa alinyanyuka kitandani kwa kujikuta, Romex akaona ampe msaada, alimshika mkono na kunyanyua pale kitandani.
Siku nyingine walikuwa wamekaa salsa akamwambia.
Boss Romex unajua natamani kunywa maji ya
mvua tena yale yaliyowekwa kwenye mtungi.
*Khaaaa wewe hayo maji utapata wapi hapa mjini? Na maswala ya mitungi mimi ndio sijui
kabisa huwa naingia kuangalia kwenye movie za kihindi.
*Basi fanya hivi twende sehemu yenye vumbi alafu tumwambie maji mimi ile harufu yake tu nikaridhika.
Jamani, jamani huu ni mtihani gani? *Kwahiyo imechukua hutaki au? Salsa alisahau kama yupo na boss wake akajikuta anaongea
kwa sauti ya juu. *Wewe hili sio jukumu langu mimi najitolea tu.
*Eti unajitolea, hili unatakiwa ukifanye kwa moyo mmoja sababu linakuhusu yani kama ingekuwa Inawezekana ningekupavhili tumbo isingeweza kukaa nalo hata kwa dakika tano ungenirudishia mwenyewe tumbo langu alafu inajikuta wewe. ndio unapata tabu kuliko mimi.
*Khaaaa.... Romex alishangaa.
*Huyo khaaaa unaisoma au unaiandika? Kwanza hebu nipishe huko nisije nikazaa mtoto mwenye
komwe kama lako. Salsa aliondoka na kumuacha Romex mdomo
wazi.
*Hivi hizi ni akili za mimba au anamaanisha anachokiongea?
Kesho yake walipokutana hasira ziliisha sasa alikuwa kama sio yule alimuongelea Romex kwa ukali lakini Romex bado alikuwa na kitu kichwani kwake.
Siku moja Romex alipigiwa simu na baba yake. *Romex uko wapi muda huu? *Nipo mtaani.
Unaweza kufika nyumbani mara moja. *Bila shaka baba. Basi nina kumsubiri hapa kijana wangu. Sawa.
Baada ya kukata simu Romex alimuangalia
Salsa ambae alikuwa amekaa pembeni ya siri ya dereva
Salsa acha mikuwahushe nyumbani kwako...... Kabla Romex hajamaliza kuongea Salsa alimkatisha.
Nyumbani tena kwahiyo hunipeleki kula ice cream? *Ndio nimeitwa na wazazi nyumbani.
Sawa
Romex alimtisha nyumbani kisha nae akaenda nyumbani kwao.
Alipofika alikuta kuna ugeni, binti mmoja akiwa na wazazi wake. Alisalimia na kwenda kukaa kwenye kochi.
Mr Ferix huyu ndio kijana wangu ninae mtegemea sana anaitwa Romex. *Safi sana na hongera sana mzee mwenzangu.
*Romex
*Naam baba.
*Huyu ni mr Ferix, yule ni mke wake na yule pale ni binti yao Lilian. Nashukuru kuwafahamu, karibuni sana.
"Asante.
Baada ya maongezi kidogo Romex na baba yake walienda kuongea pembeni.
Romex nia ya kumuita hapa ni kutaka kukukutanisha na Lilian, tunataka wewe na Lilian mfungwa ndoa.
Romex alishitika.
Baba unamaana mnanitafutia mtu wa
kumuowa?
Hapana ila tumeona Lilian ni binti mwenye
vigezo, anasifa za kuwa mke, anatoka kwenye familia inayojitambua. Romex alitulia kidogo huku akiwa kajiinamia kisha akasema.
Sawa baba ila nipeni muda wa mimi kuzoeana nae.
Full 1000
Whatsp 0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi



Maoni