: WATOTO MAPACHA
Sehemu ya 10
Mama Celena alirudi nyumban kwake na akapokelewa na wafanyakazi na wakampa pole kwa kuumwa , sasa akajipunzisha kwenye sofa hapo sebuleni
akajikuta anawaza tena maisha yake ya nyuma ,
Mr Benson au barozi hakufanikiwa kupata mtoto kwa mkewe anaeitwa Celina ,
Sasa Maria ambae ndio mama Celena wa sasa akapanga amzalie mtoto Mr Benson,
Na mapenzi yao yalikuwa ya Siri sana na Celina hakujua chochote ,
Humo humo ndani Mr Benson alikuwa anatoroka usiku anamuacha Celina kalala anakwenda chumbani kwa Maria na kufanya mapenzi ,
Wahenga wanasema ""penzi kikohozi kulificha huliwezi ,"
Maria akaanza zarau kwa mke wa Mr Benson ,heshima ikapungua,akawa sio msikivu tena,
Analala anapojiskia na kuamka anapojiskia ,
Mke wa Mr Benson akachunguza ili ajue shida nini kwa Maria ,akapata jibu kuwa Maria anatembea na mumewe ,
Siku moja usiku Mr Benson aliamka akanyata na kufungua mlango akatoka na kwenda kwenye chumba cha Maria,kumbe Celina mke wake nae alikuwa hajalala ,akawa anamfuata nyuma nyuma , Mr alipozama chumbani kwa Maria ,Celina akasimama mlangoni na kusikiliza kila kitu walichokuwa wanafanya,
Siku hiyo Celina alilia sana na akarudi chumban bila hata kuwastua ,
Mr Benson alipomaliza kufanya yake kwa Maria ,akarudi kwa kunyata asijue kama mkewe yuko macho ,
"Usihangaike mume wangu mimi najua kila kitu ,,"" Celina alimwambia Mr Benson ,na Mr Benson akastuka ,maana hakujua kama mkewe yuko macho.
" Mume wangu nataka nikwambie kitu ,najua unanipenda na mimi nakupenda sana mume wangu ,
" Hayo mambo unayoyafanya yananiumiza ,""
Celina alikuwa ni mwanamke mwenye hekima sana ,alimwambia mumewe kwa kum bembeleza kuwa aachane na hayo mambo ,na kama swala la mtoto mungu yupo atawajaalia tu ,
Mr Benson alimuelewa mkewe ,na akamuomba msamaha yakaisha wakalala zao,
:
Kesho yake Celina mke wa Mr Benson ,akampa likizo Maria , akamwambia aende kwao akakae wiki mbili baadae watamwita ,
"Dada mbona gafra kwani kuna shida ,,""?
Maria aliuliza ,
"Shida ipo ndio maana unapewa likizo na ukirudi ujirekebishe la sivyo utaacha kazi kabisa ,,""
Celina alimjibu Maria ,
Maria akajiongeza na kujua kimenuka ,
Maria akarudi kijijini ,
Kule kijijini Maria alikuwa na rafiki yake aitwae Fatu,
Maria akamuhadisia Fatu kila kitu ,
"Sasa we umekosea ungemzalia mtoto ndo ungekuwa tajiri nakwambia ,maana angekupenda hatari,,"
Fatu alitoa ushauri ,
"Labda wakiniita tena maana nahisi kama mkewe kajua kuwa natembea na mumewe,,""
"Aa basi tuachane nahayo,shoga nataka nikupeleke kwa babu ndere ,,
""
Fatu alimwambia Maria ,
"Babu ndere ,,""?
Maria aliuliza kwa kustuka,
Ndio we huioni hiyo bahati uliyokuwa nayo ,,""?
Sasa hapo kikwazo si huyo mkewe tunamfutilia mbali ,,we unabaki kuwa mama mwenye mjengo heheheeeeeh,,halooooh,,!!!!
Walicheka na kugongeana mikono,
"Sasa huyo babu ndere kazi anaweza ""??
Maria aliuliza kwa shauku ,
We unasema mwenyewe ,kuwa unataka tumfanyeje ,awe chizi ,au tumpeperushe ,au tumuue kabisa , ? Wewe tu utakavyoamua ,,""
Fatu aliongea kwa kujiamini,
"Mi nataka tumuue kabisa na mimi ndo nikae pale niwe mama mwenye mjengo,,""!
Maria akaongea,
Hiyo kazi rahisi sana heeee,, halooooh,,!!!
Wakacheka tena na kugongesheanamikono,
***
Mamaa,, weee mamaa,
Celena alimtingisha mama yake baada ya kumuona hamuitikii ,
," Eeeeh mwanangu umerudi shule saangapi ,"?
Mama Celena alikurupuka kutoka kwenye yale mawazo na kumshangaa mwanae ,
Celena aliingia kwao nakumkuta mama yake kakaa kwenye sofa alionekana mwenye mawazo sana ,akampita na kuingia ndani ,akabadilisha zile nguo na kuvaa za nyumbani ,
Halafu akarudi sebuleni na kumstua mama yake aliekuwa anawaza mambo yaliyotokea nyuma ,
"Nimerudi nikaingia ndani na kubadirisha nguo we umekaa tu hapa ,"
Aliongea Celena kwa kudeka huku akimlalia mama yake ,
""Mama mi nakwambia kitu cha kweli na toka jana mi sipo humu ndani ,na hata kunitafuta hamjanitafuta ,,""!
Celena bado alizidi kuongea bila kujua anamchanganya mama yake ,
""We mtoto mbona muongo hivyo ,we umetoka nyumbani ukaenda shuleni ,ukawa unalia lia mi nikaitwa shuleni kwenu nikaenda tukakubembeleza ukanyamaza ndo mi nikarudi nyumbani ,""
Mama Celena alimwambia mwanae,
"Sawa lakini mimi sijalala nyumbani ,"
Celena alimjibu mama yake ,
"We mbona unanichanganya ,? Yaan usilale nyumbani na hawa wafanyakazi wapo si wangepiga hata simu utafutwe ,"
Mama Celena bado aliona ni mzaha ,
"Basi ngoja tumuulize ant "
Aliongea Celena huku akimuita yule mfanyakazi wao anaeitwa ant,
" Eti anti mi jana nilikuja ,?
Celena aliuliza huku mama yake akiwa makini kusikiliza jibu ,
" Ndio ulikuja tena ukajifanya mgeni kabisa yaani mpaka chumba chako ulikisahau ,"
Aliongea yule yule mfanyakazi,
" Huyo ni Celina sio mimi ngoja
Itaendelea.