WATOTO MAPACHA
Sehemu ya ,,7
Celena alienda shuleni kwao baada ya mama yake kupata nafuu , alipofika ,akashangaa kuitwa ofisini na kupewa hongera kwa kuwa mshindi kwenye mashindano ya kufanya mtihani, celena akashangaa nakuwaambia walimu kuwa " mbona Mimi sijafanya mtihani ,?
Walimu wakaanza kumcheka na kumwambia kuwa ulifanya mtihani , japo Celena alibisha lakini alipewa mtihani wake na kweli aliangalia akakuta mwandiko umefanana na wake kabisa ,akawaza nakujua kuwa kwa vyovyote atakuwa ni yule mtoto aliefanana nae, kwa akili ya utoto aliyokuwa nayo akawaza namna ya kumtafuta mtoto huyo mpaka ampate ,
Siku zilipita huku Celina akiwahi kutoka shule na kuwahi kule kwa mama yake kichaa maana akimuacha peke yake anakuwa mnyonge ,
Kumbe siku hiyo Stefano aliambiwa na mama yake kuwa aende na Celina maana ni muda hajawatembelea ,
Sasa Celina aliwahi kuondoka , shuleni hapo , wakati anaondoka na Celena nae alitoroka shuleni kwao akaja kumtafuta Celina kule shulen ,ili tu amuone maana aliuliza akaambiwa anasoma shuleni hapo ,
"We stefano si ulikuwa unamtafuta Celina yule kule ,,""
Mwanafunzi mmoja alimwambia stefano ,
"We Celina mbona umependeza hivyo ,halafu begi jipya kabisa , nani kakununulia ,"?
Stefano alimuuliza Celena akijua ni Celina ,
" Kwani Kuna shida Gani mi kupendeza ,"?
Aliuliza Celena maana alikuwa hajui huyu Stefano anamahusiano Gani na huyo Celina aliefanana nae Nia yake ni kujifanya ni Celina ili amuone vzr huyo Celina,
" Tuyaache hayo bana mi nilijua umeshaondoka ,"?
Aliuliza Stefano ,
"Sijaondoka kwani vipi ,,""?
Celena akamuuliza stefano ,
Kumbuka Celena hamjui Stefano, bali Celina ndo anamjua Stefano na anaendaga mpaka kwao na kula chakula ,
"Mama anakuita ,anasema twende wote nyumbani amekumisi ,""
Stefano aliongea tena ,
Celena akawaza na akataka kumuuliza Celina yupo wapi,
Akasita ,akaona atazua mambo mengine .lakini inawezekana akienda kwa kina Stefano ndio atajua ukweli Kama atakutana na Celina ,
""Sawa twende ,,""
Wakaongozana ,
Lakini wakiwa njian wakatokea vijana wawili ,wakamkamata Stefano wakaanza kumpiga huku wakidai darasani aliwachokoza ,
Bila hata yakuuliza Celena akaingilia ugomvi ,Stefano akashangaa alimzoea Selina ugomvi ukitokea anawagombelezea halafu anamfokea Stefano kuwa aache ugomvi,
Lakini leo ameingilia ugomvi na kumkamata kijana mmoja na kumshindilia mangumi ,
Stefano nae akapata nguvu akamshika yule kijana mwingine wakaanza kuzichapa ,
Wale vijana wakashindwa ugomvi wakakimbia ,
Daah ,,leo Celina umepigana ,,""!
Stefano alimshangaa Celena ,huku mawazo yake yakimtuma yuko na Celina ,
"Nilijikuta tu moyo unaumia walivyokuwa wanakupiga na sijui kwanini ,,""?
Celena alijibu huku wakiendelea na safari ,
Wakati Celena anakwenda kwa kina Stefano ,
Huku Celina alikuwa anakwenda zake dampo kule kwa Mama yake kichaa,
Wakati anakwenda kuna gari ilipaki kando yake ,
" We Celena mbona uko hivyo , "?
Aliuliza dereva wa gari hiyo huku akitelemka , ye alijua ni Celena kumbe amekutana na Celina, kabla hata hajajibu yule dereva akamwambia apande kwenye gari ili waondoke waende nyumbani ,Celina akataka kukataa lakini yule dereva akamlazimisha Sana huku akidai atafukuzwa kazi , Celina akaona ngoja aende tu ili akajue ukweli huko huko maana anafananishwa na yule mtoto aliefanana nae na hamjui ,
Huku kwa kina Stefano Celena ndo alikuwa anaingia ,
"Jamani Celina karibu ,,""
Mama Stefano alimkumbatia Celena akijua ni Celina ,
"" Shikamoo mama ,,""
Celena aliamkia ,
"Marhaba mwanangu haya za kutususa ,,""
Celena alikuwa anajibu tu ,maana alikuwa hajui Celina anauhusiano gani na hii familia ,
Mama Stefano akampa zawadi ya gauni moja zuuri ,
Na Celena alipolivaa lilimpendeza sana ,
"Huyu mbona kama sio Celina ,,maana Celina ninavyomjua ni mchangamfu sana ,na mbona huyu anasura kama ya upole upole halafu huyu ananguo za kitajiri cheki hili begi lake ,,""
Mama stefano alianza kumgundua Celena ,akaangalia begi lake na viatu vyake ilikuwa ni tofauti na Celina, lakini mama Stefano akaona labda yule baba anaemsomesha itakuwa kamnunulia akaona haina haja ya kumuuliza ,
"Asante mama ,,gauni ni nzuri nimeipenda "!
"Asante kushukuru mwanangu ,""
Mama Stefano alijibu huku nayeye akifurahia kuitwa mama ,
Sasa kikatengwa chakula ilikuwa ni wali na nyama , walipoanza kula Stefano akachukua nyama ya Celena , Celena hajakubali akampokonya nyama yake , huku wakibishana , mama Stefano akashangaa na kujiuliza " huyu Celina Leo amekuwaje , gafla Stefano akampokonya tena nyama na kukimbia , Celena hajakubali akaanza kumkimbiza , humo ndani kukawa vurugu , Sasa kumbuka tabia ya Stefano ni mchokozi ,
na Celena japo ni mpole na amelelewa kwenye familia ya kitajiri lakini tabia yake inafanana Sana na ya Stefano, yaani Celena ni mtundu Kama Stefano ,
" Hebu nyie acheni kugombana haya njoni mniambie nani anamchokoza mwenzake ,"?
Mama Stefano aliwauliza ,
" Mama ngoja nikwambie Mimi nilikuwa nakula zangu nyama Stefano akanipokonya nyama yangu ,"
Aliongea Celena ,
" Muongo ye ndo alianza uchokozi "
Aliongea Stefano ,
Mama Stefano akawa anashangaa tu na kuwaambia haya ntawaongezea nyama kaeni mle ," mama Stefano aliwaambia na wakakaa wakaendelea kula ,
Walimaliza kula ,sasa kwa kawaida Celina hutoa vyombo na kuviosha ,lakini kwa Celena ni tofauti alikuwa hawezi kuosha vyombo ,na ukumbuke kuwa Celena kwao ni matajiri kwahiyo hata kazi ndogo hawezi kufanya ,
"Mama nikupe story,,??
Stefano alimwambia mama yake walipobaki wawili maana Celena aliingia ndani kubadilisha lile gauni ,
"Haya nipe hiyo story,,""
Mama Stefano alimjibu mwanae,
""Leo wakati natoka shule kuna vijana wawili walikuja kunipiga ,basi nikashangaa Celina akamkamata mmoja nakuanza kumpiga ,,""
"Weee Celina alipigana ,,"?
Mama Stefano alishangaa ,
"Ndio tena alikuwa na hasira akawa anasema kwanini unampiga mdogo wangu ,""
Stefano aliongea huku anaonesha mifano ,
"Huyu sio Celina ,maana huyu ni mpole halafu anatabia zinazoendana na stefano ,,"
""Sasa kama huyu sio Celina ni nani, na mbona ameizoea nyumba kama kwao ,""?mama Stefano aliwaza alipokuwa mwenyewe,
MAMAAAAA Celina mchokozi ii,,,"""!!!
Stefano alimuita mama yake ,huku wanakimbizana humo ndani ,
"Hee Celina tena mchokozi ,""?
Mama stefano alishangaa maana ye kashazoea stefano ndio mtundu na mchokozi na ndio humchokozaga Celina kila akija ,SASA HUYU NINANI ,??
Aliwaza mama stefano bila kujua aliekuja leo sio Celina ni Celena ,
Siku zote wanasemaga doto ndio huwa mchokozi na mtundu siku zote ,sasa Celena hakupata muda wa kucheza maana kwao ni matajili ,akienda shule na gari na pia akirudi na gari ,
Sasa alipokuja kwa kina Stefano ndo akaanza kuonesha utundu wake nampaka ye mwenyewe alijishangaa ,alijihisi furaha ya ajabu kuwa nyumbani hapo ,
Mala Celena akamkimbilia mama yake Stefano na kumkumbatia ,
"Mama Stefano mchokozi ,,""
Celena alimsemea Stefano kwa Mama yake,
"Muongo ye ndo mchokozi ,""!
Stefano alijibu huku akiuficha mto nyuma ya mgongo wake ,na alipoutoa alimpiga nao Celena na kukimbia zake ndani,
""Mama umemuona mwanao kanipiga "subili nimuoneshe"!!
Celena aliongea kwa kudeka kama yupo kwa Mama yake mzazi kabisa ,
Na alipoamka akaanza kumkimbiza Stefano ,
Maskin mama stefano,,alibaki ameduwaa tu asijue afanye nini,
Maana Celena na Stefano wamekutana kila mtu ni mchokozi balaa ,,
Sasa humo ndani kukawa ni mtafutano ,,
Na ukumbuke Celina amepelekwa nyumbani kwa kina Celena Je watamgundua kuwa sio Celena ,?
Na Je hapa kwa kina Stefano itakuwaje ,,?
Story hii utaipata yote mwanzo mwisho kwa elfu Moja tu 0655772653 njooWhatsapp,
Itaendelea.