WATOTO MAPACHA
Sehemu ya ,,,,,. 9
"Amepitia huku ,"
Mwalimu mmoja aliwaambia walimu wenzake wakati wanamkimbiza Celena ,
Wanafunzi waliwashangaa walimu wao jinsi wanavyokimbizana nyuma ya shule ,
Celena alizunguuka nyuma ya choo cha wanawake lakini hakumuona huyo Celina akawaza haraka akajua kwa vyovyote Celina atakuwa amekwenda kule shuleni kwao kwa sababu alishaendaga na akafanya mtihani ,haraka akazunguuka nyuma ya shule na akaingia darasani kwao na kuchukua begi lake na kutimua mbio , wanafunzi wenzake walimcheka tu bila kuelewa Celena anajambo lake kichwani , na ukumbuke hapo wapo darasa la Tano ,
Wakati Celena anatokomea zake kuelekea shuleni Celina nae ndo alikuwa anaingia darasani kwa bahati mbaya wale walimu wakamuona na kumsimamisha kabla hata hajaingia darasan ,
" Sasa mwalimu huyu si yule yule "
Aliongea mwalimu mmoja baada ya kumwangalia Celina ,
"Sio yule jamani naombeni mniamini huyu amekuja sasa hivi ,"
Yule mwalimu alijitetea lakini walimu wenzake wakampinga ,
Ikabidi walimu warudi tu ofisin huku wengine wakilaumu kuwa wamepoteza muda kwa vitu vya kijinga ,
Celina nae akaingia darasani huku akiwaza itakuwa Celena amekuja huku shule na akaingia darasani bila watu kujua ,alijiuliza sana kwanini wanapishana na huyo Celena ,
Celena nae alifika mpaka shuleni kwao akizani atamuona Celina maana alijua atakuwa amekimbilia huku , lakini hakumuona ,
'"eti mercy umemuona msichana amefanana na mimi hapa shuleni ,"?
Celena alimuuliza mwanafunzi mmoja wanaokaa dawati moja ,
" Kwahiyo sasa hivi ndo umeamua uongee ,yaani tokea asubuhi umekaa kimya unajifanya uko bize na masomo ,"
Yule mwanafunzi aitwae Mercy alimjibu Celena ,
" Mi asubuhi sikuwepo jamani "
Celena aliongea kwa msisitizo,
"We hebu acha mambo yako ,hukuwepo wakati umenipa pensel na ukanicholea mchoro wa geography , hebu achana na mimi kwanza unanichosha "
Aliongea yule mwanafunz na kuondoka zake,
Celena aliingia darasan nakujiinamia akaanza kulia , maana alikuwa anamtaka huyo mtoto waliefanana ili amuone na kwanini wafanane ,?
Mwalimu aliingia darasani akamuona Celena analia na akamuuliza kwann unalia ,lakin Celena hakujibu aliendelea kulia tu,
"Celena hebu njoo ofisini ,,""
Yule mwalimu alimwita Celena ofisini , Celena akanyanyuka na kwenda ofisin huku akiwa bado analia ,
Celena aliulizwa na walimu wote huku wanam bembeleza aseme kinachomliza lakini Celena hakusema kitu ,ikabidi walimu wampigie Mr Benson barozi ,aje maana ile hali ya Celina kulia wakapata wasi wasi ,
Mr Benson alikuwa kazini ikabidi ampigie mkewe ampe maelezo aende shule kuna shida kwa mtoto wao, japo mama yake Celena alikuwa anaumwa na ni ndio alikuwa anatoka anatoka hospitali lakini alipoambiwa mtoto wao anatatizo aliwasha gari fasta nakwenda shuleni ,
Alipofika aliingia ofisini huku akiwa na wasi wasi na mtoto wake ,
"Mwanangu unanini ,,"?
Mama celena alimuuliza Celena ,
Sasa kipindi mama Celena anamuuliza Celena bila kujua kinachomliza Celena,
,mwalimu mmoja alikuwa anasahihisha madaftari na daftari la Celina lilikuwepo maana kabla hajaondoka kurudi kule kwenye shule yake aliandika na akakusanya daftar ,
Sasa katikati ya daftari akakuta picha ,
Picha hiyo Celina aliiba kule kwa kina Celena ,
"Na hii picha ni yanani,,""
Mwalimu aliuliza huku akiiangalia vzr ,
" Hebu nione ""!
Mama Celena aliongea huku akinyoosha mkono na mwalimu akampa ile picha,
Mama celena kuiona tu ile picha moyo ukafanya PAAAH,,,!
,"" CELINA,," mama Celena alijisemea kimoyomoyo,
" Hii picha mi si nilishazichanaga ,,"
Mama Celena aliwaza huku akiishika vzr ile picha ,
Mama Celina alikumbuka mbali sana ,
Alikumbuka maisha yake ya zamani sana kipindi yupo kijijini alikuja mama mmoja anatafuta mfanyakazi wa ndani ,
Yeye akapata bahati hiyo ,akaja kufanya kazi kwenye bonge la jumba la barozi Mr Benson ,
Kipindi hicho alikuwa bado mshamba mshamba ,
Kipindi hicho anaitwa Maria ,
Maria alikuwa mchapakazi haswa kiasi kwamba mpaka mke wa barozi alimpenda ,Maria aliishi ndani ya jumba hilo sio tu mfanyakazi bali alikuwa kama ndugu ,
Kama unavyojua wanaume huwa dhaifu sana kwa wanawake , Mr Benson au barozi akatamani kutembea na Maria yaani mfanyakazi wake wa ndani ,
Mke wa Mr Benson alikuwa mpole sana na alimfanya Maria kama mdogo wake ,alimpa chochote anachohitaji bila kujua mumewe tayari ameshaanza kumtamani mfanyakazi huyo yaani Maria ,
Mahusiano ya Maria na Mr Benson yalikuwa ya Siri sana na mke wa Mr Benson hakujua chochote ,
Penzi likanoga Maria akaanza dharau kwa mke wa Mr Benson ,
"Mama Celena vipi mbona umeduwaa ,,"??
Mwalimu alimshtua mama Celena kutoka kwenye yale mawazo ,
"" Aah hapana ni mawazo tu unajua bado naumwa , " alizuga mama Celena ,
Nahili daftari mbona Kama sio la Celena, maana limeandikwa Celina Mathias, "
Aliongea mwalimu huku akilikagua vzr lile daftari,
" Hebu nilione "
Aliongea mama yake Celena huku akilikagua , daftari Hilo japo lilikuwa rafu rafu lakin mwandiko wake ulikuwa hauna utofauti na Celena , mama Celena akashangaa ,
" Hebu Celena Lete daftari lako , " alisema mwalimu ,
Celena akatoa , lilikuwa daftari safi lakin mwandiko wake unafanana na daftari lile la mwanzo ,
" Mmh sasa hili daftari la nani ,"?
Mwalimu aliwaza ,
Mama Celena yeye hakuwa na mawazo ya madaftri yeye aliwaza tu Je ile picha ya MKE wa Mr Benson imefikaje pale kwenye daftari,
Picha aliyoishika mama Celena ni picha ya mke wa Mr Benson ,na Celina aliiba kule kwa kina Celena ili apate uhakika Je ile picha ni ya mama yake kweli ,"? Maana yule kwenye ile picha kafanana kabisa na mama yake japo mama yake kwa sasa ni kichaa , na kama ni yeye Je ile picha imefikaje kule kwenye lile jumba la kina Celena , na kama niyeye basi mama yake hakuzaliwa kichaa ukichaa aliupata ukubwani , sasa ilikuwaje akapata ukichaa hapo ndo pagumu ,
Inamaana mke wa kwanza wa Mr Benson ni yule kichaa ,ambae aliemukotayule mtoto Celina ,na ndo anaitwa Celina ,na kutokana na ukichaa wake akawa anamuita mtoto aliemuokota jina lakwake yaani Celina, Kama hujaelewa rudi kasome kipande Cha pili ,
Na Mr Benson alipompata mtoto akamwita Celena,yaani jina linalofanana na la mkewe wa kwanza ,ambae ndo yule mama kichaa, na ukumbuke mama Celena hajui Kama mtoto wake alinunuliwa na mumewe kule hospital, ye anajua huyo Celena ni mwanawe kabisa wa kumzaa , na hajui Kama wapo mapacha,
Sasa imekuwaje mke wa Mr Benson amekuwa kichaa,,?? Hapo ndipo story inapoanza ,
Story hii utaipata yote mwanzo mwisho kwa elf moja tu, 0655772653 njoo whtsap, kumbuka ukinunua story hii unapata na story ya PANYA buree,,,
Itaendelea.