Story :: watoto MAPACHA
Sehemu ya ,,,,,,2
Walioifatilia mpaka mwisho wanajua mziki wa story hii , na utaipata yote kwa elfu moja tu,
Ilikuwa yapata muda wa saa 8 au 9 za usiku kichaa mmoja anaeitwa Celina alikuwa kando ya dampo moja ameuchapa usingizi ,
Gafra akastuka nakuangaza kule na huku na kuwaona watu wawili wanatupa kitu kwenye dampo hilo na kutoweka upes,
Kutokana na njaa yake celina akahisi watu wale wametupa mabaki ya vyakula akakimbilia upes
Lakini alipofika akashangaa kukuta nikatoto kametupwa tena hakana hata nguo ,
Pamoja na uchizi wa celina aliweza kugundua kuwa yule ni mtoto ,akamfunga funga na manguo yake machafu huku akiimba ""celina kapata mtoto ,,""Celina,""!!
Asubuhi na mapema celina aliamka na katoto kake akaanza kuzurula nae huku anaimba imba hovyo ,
Watu walistaajabu sana na wengine walimshangaa kichaa yule kwani ,mtoto alikuwa analia sana nayeye Wala hakujali ndo kwanza alikuwa anaimba ""celina kapata mtoto ,,,""celina""!!
""Jamani mnyang'anyeni yule mtoto apelekwe hospitali ,,""
Mama mmoja alishauli.
Vijana wakaitwa na kwa kutumia nguvu sana huku kale katoto kakilia sana ,wakafanikiwa kumnyang'anya kichaa yule mtoto,
Na wakamuwahisha kale katoto kachanga dispensary iliyokaribu na pale ,
Lakini yule Mama kichaa hakukubali aliwakimbilia huku akilia mpaka nnje ya dispensary ile nakukaa nnje ya mlango kuanzia asubuhi ile mpaka jioni huku analia tu ,
Mtoto alihudumiwa ndani ya siku 3akiwa pale Dispensary ,huku yule kichaa akiwa nnje ya dispensary na bado alikuwa akimlilia mtoto aliemuokota .
""Sasa mpeni huyo mtoto lakin awepo mtu wa kumfuatilia kila aendapo ,,""
Docta alishauli .
Kweli yule kichaa akapewa mtoto ,alifurahi sana
" Celina amekuja ,,"celina huyoo,,""
Aliimba yule kichaa .kumbuka mtoto huyo alikuwa Hana jina ,na jina la Celina ni huyo mama kichaa ameamua kumpa tu kutokana na ukichaa wake ,
Nikama mungu alimuongoza mama yule ,kwani pamoja na ukichaa wake hakuweza kumzuru mtoto yule ,alimlea vizuri kabisa na kila mtoto alipolia hukimbia kwenye kibanda cha mama ntilie na kuomba chakula ili ampe mwanae,
Miaka ikasonga huku bado celina akiishi na yule Mama kichaa ,
Hata celina mwenyewe aliamini yule Mama kichaa ndio mama yake mzazi ,
Celina alimpenda mama yake japo mama huyo ni kichaa ,na japo ni mdogo aliweza kuwaza kuwa akikuwa mkubwa lazima akamtibu mama yake mpaka apone,
Walipitia misuko suko mingi ,kulala majalalani nikitu cha kawaida kwao,
Kuna kipindi celina alichukuliwa na mama mmoja akakae kwake lakini usiku alitoroka na kurudi jalalani kulala na mama yake.
Japo wengi walimuona yule Mama kichaa lakini celina alimuona Mama Bora.
Siku hiyo yule Mama kichaa aliamka anaumwa tena sana ,celina hakuwa na hata shilingi ,alichanganyikiwa ,
Akatoka kwenye jumba bovu hilo walilokuwa wanakaa nakwenda kutafuta makopo ili akauze apate pesa ya dawa ,akiwa hana hili Wala lile anaokota zake makopo akastuka kusikia sauti nyuma yake,
""Wewe ni mimi ,,""
Na alipogeuka akashangaa kujiona ni yeye kweli ,
Yaan mbele yake kasimama mtoto wa makamo yake na wamefanana kila kitu ,
Celina alitetemeka huku bado wakishangaana ,
Walichukua kama dakika tatu wakishangaana tu ,
""Unaitwa nani,,""?
Yule binti alimuuliza celina.
"Naitwa celina ,,""
Celina alijibu na akamuona yule bint amestuka ,
"Celeeeenaaa ,"""!
Ilisikika sauti akiita .
""Mama yangu ni mgonjwa sana mi naondoka ,,""
Celina alimwambia kale kabint ,
""Mama yako ni mgonjwa ,,""???
Yule binti aliuliza lakin kabla hajajibiwa celina alivuka barabara,
Celena mwanangu umepatwa nanini,,""?
Mama celena alifika na kumkumbatia mwanae ,
Celena hakujibu alinyoosha kidole kumuonesha mama yake na mama yake alipoangalia hakuamini,
Alimuona bint mmoja kafanana na mwanae kila kitu mpaka tembea yake ,
Celina alitembea na kwa bahati akaangalia nyuma ,
Mama Celena akamuona vizuri usoni ,
AKATOA MACHO,,,!!
Hii story ipo yote mwanzo mwisho na utaipata kwa elf moja tu mwanzo mpaka mwisho ,njoo whtsap 0655772653.