WATOTO MAPACHA ,
Sehemu ya ,,,,,. 5
Mama stefano moyo ulilia PAAAH,,,!!
Akajishika kifuani na kujiuliza kwanini hali kama ile inamtokea ,
Kule nnje stefano na Celina wakat wanabishana baba Stefano alikuwa anarud kutoka kazini ,akapaki gari lake dogo Toyota Mack 11
Wakati anashuka macho yote yalikuwa kwa Celina ,
Alijiuliza mbona huyu mtoto kafanana na mke wake ,
""Shikamoo baba ,,""
Stefano alimsalimia baba yake ,
"Malhabaa ,,""
Baba Stefano aliitikia huku bado macho yakiwa kwa Celina ,
"" Shikamoo baba Stefano ""
Celina nae alisalimia ,
"Malhabaa bint hujambo ,,"
"Sijambo ,,""
Celina akajibu,
""Celina ona gari ya baba angu ,aaammmh pipiiii""
Stefano badala ya kumpokea baba yake ye aliingia ndani ya gari na kujifanya anaendesha gari hilo , huku akimlingishia Celina ,
" Stefano toka kwenye gari umpokee baba vitu na uviingize ndani ,,""
Celina alimfokea Stefano mbele ya baba yake ,na Stefano akashuka kwenye gari na kuvibeba vile vitu na kuingia navyo ndan ,
Baba yake Stefano aliona kama miujiza ,akashangaa,
Siku zote Stefano alikuwa mtundu ,mjeuri na ukimwambia kitu hafanyi kifupi alikuwa anadeka sana ,
Kitendo cha Celina kumfokea Stefano ,kilimfurahisha sana baba Stefano ,
"Mwanangu ingia ndani ""
Baba Stefano alimwambia Celina ,
Celina alikataa lakini alibembelezwa sana aingie japo wapate chakula cha pamoja ,
Celina alipoingia ndani ya nyumba ile alijihisi tofauti ,alihisi kama yupo sehemu salama na anaweza kufanya chochote atakacho,
Mama Stefano alimsalimia mumewe ,na mumewe akamuuliza kama anamfaham yule mtoto ,mama Stefano akajibu yeye mwenyewe hamjui na anashangaa kwanini wamefanana nae,
Mama Stefano alitenga chakula lakini kila anapojalibu kumsogelea Celina ,mapigo ya moyo wake yalikuwa yanakwenda mbio ,
" Unaishi wapi mwanangu," ?
Mama Stefano alimuuliza Celina ,kabla Celina hajajibu Stefano akajibu ,
" Mama huyu mama yake ni kichaa "
"Weee nani kakwambia wakati wa kula watu wanaongeaga ? Haya macho kwenye sahani na ukae kimya wakubwa wakiongea ,"
Celina alimwambia Stefano na Stefano akatii ,mama Stefano wakaangaliana na baba Stefano maana walichokiona ni kwamba Stefano akiambiwa chochote na Celina anatii na anamchukulia Celina kama dada ,
"Ni kweli mama yangu ni kichaa ila kuna baba mmoja amenichukua ndo ananisomesha ,"
Aliongea Celina kwa upole ,
"Ooh pole sana mwanangu MUNGU atakusaidia ,"
Aliongea baba Stefano na wakaendelea kula ,
Walikula huku wanapiga story za hapa na pale ,
Walipomaliza kula Stefano ndo alikuwa wakwanza kunawa na kunyanyuka ,huku akiacha vyombo pale mezani ,
" Weeewe Stefano unamwachia nani atoe vyombo ? Haya haraka na upesi toa vyombo futa meza ,"
Celina alimwambia Stefano, Stefano akawa anatoa vyombo huku amekunja sura yaan amechukia , huku mama yake na baba yake wakicheka na kusema " tunaomba uwe unakuja kila siku huyu Stefano atanyooka ,"
Na celina alifanya kila kitu pale nyumbani ,
Aliosha vyombo na alipomaliza alimfulia $tefano nguo zake za shule na kumwambia
""sitaki kesho uje shuleni ukiwa mchafu ""
Mama Stefano alikuwa anamuangalia tu Celina maana hajui hata wazazi wake na ni mtoto mtulivu na mpole , na hakuelewa kwanini anafanya yote hayo bila hata kuambiwa ,
Alipomaliza akaaga na kuondoka zake , ila mama Stefano alimpa elfu mbili Kama zawadi tu ya kununua anachotaka, Celina alishukuru Sana ,na kuondoka ,
hali ilikuwa ngumu kwa Mama stefano ,alijikuta anaenda chumbani na kuanza kulia na alipoulizwa na mumewe hakuwa na majibu sahihi ,ila alijihisi tu uchungu na alitamani yule mtoto awepo pale ,
Celina alienda nyumbani kwa docta Mathias ili akabadili nguo za shule na arudi kwa Mama yake kule jalalani,
Lakini alipoingia tu alipokelewa na bonge lakofi ,
"Wee mjinga ulikuwa wapi ,"?
Unataka vyombo aoshe nani ,,? Na kwataarifa yako hakuna kula mpaka uoshe vyombo ufue zile nguo zangu na udeki nyumba nnzima ,,""!
Mke wa docta Mathias alimfokea mfululizo na kumpiga celina kofi lingine ,
Celina alianguka chini na kuanza kulia , aliponyanyuka alitoka zake nnje na kuondoka zake ,
""Na kama unaondoka usirudi hapa mshenzi weweee,,""
Mke wa docta Mathias alimsindikiza na maneno ya chuki,
""Heli niende kwa Mama yangu hata kama ni kichaa ""
Celina alijisemea kimoyomoyo na kuondoka zake,
Zilipita week kama mbili Celina hajakanyaga kwa docta Mathias ,ikabidi docta Mathias aende shuleni kwao ,
Alipoonana nae akamuuliza kwa upole kwanini haji nyumbani ,Celina nae hakutaka kumficha alimwambia kila kitu mkewe alivyokua anamfanyia ,
Docta alikasirika sana na aliporudi nyumbani alimfokea mkewe na kumwambia amtafute Celina popote alipo na amuombe msamaha na Celina arudi nyumbani ,bila hivyo hapa nyumbani hakutakuwa na amani,
Na kweli nyumbani hapo kulikuwa hakuna amani kabisa docta alimchukia mkewe kwa kitendo alichokifanya ,
Siku tatu baadae mke wa docta Mathias alikuwa super market ,akamuona mtoto kafanana na Celina kila kitu yaani huulizi ,mtoto yule alikuwa na mama yake wananunua vitu mbali mbali ,
Akashangaa ,
""Si niliambiwa mama yake Celina ni kichaa ,?Sasa mbona huyu ni tajiri tena ni mzima wa afya,,""?
Aliwaza mke wa docta Mathias bila majibu ,
Mke wa docta hakuamini akamfuata yule mtoto aliefanana na Celina ,akaanza kumkagua ,
"Dada vip mbona unamkagua mwanangu "?
Aliongea mama Celena ,
" Aah Celina hunikumbuki mimi " ?
Mke wa doctor badala ya kujibu swali ye akamuuliza swali Celena akizan ni Celina,
" Mi mbona SIKUJUI ,"
" Hunijui vip Celina twende nyumbani ,"
Watu wote wakashangaa ,
"Wee dada hebu Kaa mbalia na hii familia ,"
Aliongea bodyguard mmoja na kumtoa pale ,
Mama yake na Celena akawa anashangaa na hata Celena pia alikuwa anamshangaa ,
"Mama mbona yule dada ananiita mimi Celina ,"?
Celena alimuuliza mama yake wakati gari inaondoka maeneo yale ,
"Mwanangu mi hata sijui labda amekufananisha tu ,"
Mama Celena alimjibu mwanae ,
Mke wa doctor ikabidi ampigie mumewe pale pale na kumwambia kuwa amemuona Celina lakini mbona huyu Celina kwao ni matajili tena baba yake anaonekana ni kiongozi mkubwa serikalini ,?
" We hebu nitolee upuuzi wako mama yake Celina ni kichaa tena muokota makopo na uchafu ,"!
Aliongea doctor kwa msisitizo,
"Mume wangu hebu nielewe basi "
Aliongea mke wa doctor kwa msisitizo,
" Nikuelewe nini wewe hebu mtafute Celina na uhakikishe anarudi nyumbani sitaki upuuzi mimi "
Aliongea doctor kwa hasira akakata simu ,
KUMBUKA Kuna CELINA NA CELENA ,
KUMBUKA STORY hii utaipata yote kwa elfu moja tu na ukilipia utapewa na story ya PANYA buree, 0655772653 njoo whtsap,
Itaendelea.