WATOTO MAPACHA
Sehemu ya ,,,,, 8
Sasa humo ndani pakawa mtafutano ,,
Celena akimpiga Stefano, Stefano nae hakubali anamrudishia halafu anakimbia , wakakimbizana mpaka jikoni ,Stefano akapanda juu ya meza ya vyombo kwa bahat mbaya akateleza na vyombo vikaanguka na grass moja ya udongo ikapasuka , Celena akakimbilia kwa mama yake Stefano ,
" Mamaa Stefano kavunja grass ,"
Celena aliongea kwa kudeka , mpaka mama Stefano akawa anamshangaa ,na alikuwa anajiuliza huyu mbona sio Celina ,? Maana kinachowatofautisha Celina na Celena ni tabia , Celina hapendi michezo ye ni mtu wa vitendo ,alimaliza kula atatoa vyombo afagie na akavioshe , sasa Celena hata kutoa vyombo hajatoa tayari wamekimbizana na Stefano, na hata hivyo Celina nguo zake ni chafu chafu , huyu nguo zake ni safi na zinanukia kabisa kama mtoto anaeishi maisha ya kitajiri,
" Mamaa nimeteleza bahati mbayaa ,"
Alijitetea Stefano,
" Mamaa huyu Stefano muongo alipanda juu ya meza , akalipiga teke beseni "
Celena bado alimsemea mwenzako ,
" Basi wanangu tutanunua grass nyingine "
Aliongea mama Stefano ,huku akiwaza kuwa akija mumewe lazima amwambie kioja cha leo ,
Celena aliyafurahia maisha ya kwa kina Stefano kuliko yale yakule kwao ya kitajiri,
Japo ni kwa muda mfupi lakini aliinjoi mpaka akaona ni bora hapo ndo pangekuwa kwao ,
Turudi huku alipoletwa Celina ,ye alikuwa mgeni Sana kwenye jumba hilo , kila akiangalia mazingira alijihisi tofauti sana ,ndani ya jumba hilo kulikuwa na kila kitu Cha kupendeza ,
"Wee Celena mbona unashangaa tu ,,? Kabadilishe hizo nguo nizifue,,""
Mfanyakazi mmoja ambae Celena alizoea kumuita anti alimwambia Celina akijua ni Celena ,
""Chumba cha Celena kiko wapi""?
Celina aliuliza na kumfanya yule mfanyakazi kumcheka ,
"Inamaana leo hii hukijui chumba chako ,,""??
Yule mfanyakazi alimuuliza Celina, ye akijua anaongea na Celena ,
"Sikijui nimekisahau ,,"
""Haya twende chumbani kwako ""
Yule mfanyakazi alimshika mkono Celina akijua anamfanyia utani kumbe nikweli Celina hajui kitu kwenye nyumba ile .
""Haya ingia humu,,""
Celina aliingizwa kwenye chumba cha Celena ,
Chumba cha Celena kilipambwa na picha za ukutani za aina mbali mbali ,midoli ya kuvutia ,hakika hicho chumba kilipendeza ,picha za Celena akiwa na wazazi wake ,picha za Celena akiwa mdogo mpaka amekuwa mkubwa ,zilikuwa zimewekwa ukutani zilipendezesha chumba hicho ,
"We vipi leo ,,""? Mbona unashangaa chumba chako ,,""?
Yule ant alimuuliza Celina ,
Celina akajifanya kuzuga tu ,akabadilisha nguo na kuvaa za Celena ,hapo ndo akaonekana Celena mtupu ,
" Huyo Celena akija sijui itakuwaje ,,""
Aliwaza Celena huku akijiangalia alivyopendeza ,
Aliangalia picha za Celena alishangaa kabisa maana ni yeye mtupu ,
Akaanza kuzurula humo ndani bila mtu yoyote kumstukia , maana mama yake na Celena alikuwa bado kalazwa hospital, kwa hiyo ndani ya jumba hilo walibaki wafanyakazi tu maana hata baba Celena alikuwa kazini ,
Huku kwa kina Stefano ,
Celena kutokana na utoto na kuzidiwa na michezo akajikuta analala kule kwa kina Stefano huku wazazi wa Stefano wakijua mtoto huyo mama yake ni kichaa hivyo hata akilala pale hatatafutwa , baba Stefano alirudi nyumbani ,na mama Stefano akamuhadisia kilichotokea siku hiyo , lakini kwa vile ilikuwa usiku na aliwakuta watoto wameshalala , baba Stefano akamwambia kuwa labda itakuwa Leo alichangamka tu ,maana haiwezekani mtoto kufanana kiasi kile , na hata ingekuwa sio yeye huyu ni lazima angeonesha ugeni ,hivyo akapuuzia na kulala ,
Kule Celina nae alishangaa huyu Celena mbona harudi nyumbani kwao ,maana yeye ndo alikuwa anataka amuone ,akajikuta anakula na kulala sehemu nzuri sana ,asubuhi aliamshwa na akaandaliwa kwa ajili ya kwenda shule , alivalishwa nguo nyingine za shule na akapakiwa kwenye gari akapelekwa shule anayosoma Celena , na akashushwa bila yeyote kugundua kuwa sio Celena ,akaingia darasani kama kawaida huku akijua lazima huyo Celena aje na wataonana tu ,
Kule nyumban kwa kina Stefano Celena nae alijiandaa na nia yake ni kwenda kwenye shule ya kina Stefano akamuone Celina ,wakaongozana na Stefano mpaka shuleni kwao nae akaingia darasani na hakuna mtu aliestuka kuwa yule sio Celina ,hata mwalimu alifundisha na akaambiwa Celena akusanye daftari , na azipeleke ofisin , na kweli Selena alikusanya daftari kwa wanafunzi wenzake na kuzipeleka ofisini ,
Celina alikuwa kule kwenye shule ile ya kina Celena akapata wazo la kutoroka ili aende kule shuleni kwao , na kweli akatoroka ,
Akaja mpaka shuleni kwao ,
kuna mwalimu mmoja wa kiume akaingia ofisini humo , cha ajabu mwalimu huyo akaanza kumshangaa Celena ,
"We umefikaje humu ofisini ," ?
Yule mwalimu alipouliza walimu wakashangaa ,
"Kwan vip " ?
Mwalimu alimuuliza mwalimu mwenzake ,
" Huyu nimemkuta nyuma ya shule na nikamwambia aingie darasani yaani sasa hivi "
Celena aliposikia hivyo akajua alionekana ni Celina inamaana Celina amekuja shuleni hapo akaachia madaftar na kutoka spidi nia ni kumuona huyo aliefanana na yeye , mwalimu nae akatoka sped walimu nao wakapigwa na mshangao nao wakafuata nyuma , nia Celena ni kukutana na Celina maana Kama wamefanana kiasi hicho Cha watu kushindwa kuwatofautisha inamaana basi Kuna undugu uko hapo , Celena akapiga Kona ya kwanza tu na akashangaa ,,,
je wakikutana itakuwaje,,?
KUMBUKA STORY HII UTAIPATA YOTE MWANZO MWISHO KWA ELFU MOJA TU 0655772653 NJOO WHTSAP.