FROM BANGI TO BABY ππ SEHEMU YA 11
Ikabidi tu nikubali kinyongee ila roho iliniuma sanaaa yaani mpaka chozi lilinitoka aiseee...
Tinner akabaki kunibembeleza na hapo hata sijui atakuja linii mjinga kweli huyu kakaa gari yangu tena aah roho iliniuma nilipo kumbuka gari yangu mana ndo kitu changu cha thamani nacholinga nachoo mweeh ..
Ikabidi nibaki kwa Tinner hapo akanipa nguo zake ambazo mara nyingi huwa hazitumii tumii, Nikaanza kutokea hapo, Kama wiki hivi nikipita pale kijiweni hata simuoni Veda naoma tu wanaume wengine wengine, Nikipita na Boda naangaza macho kila kona simuoni ..
Siku enyewe nimerudi kazini hapo nilikuwa natamani kweli nimwambia Tinner siku hizi Veda haonekani ila utani wake ndo unanifanya napata kigugumizi kuongea, Sa hiyo siku nimerudi akanambia kumbe Shem hayupo ndo mana hata simuoni pale
Mmmh nikasema shem gani tena nawewe??"
"Si Veda Bonge la bwana" nikajikuta nacheeekaaaa yaani nilichekaa hata cha kunichekesha hakipo sijui kwanini Baada tu ya Tinner kutaja hilo jina nikapata amani
"We mwehu shemeji yako kwa nani??"
"Unajitoa ufaham au sio.... We akija mie nafanya mambo muwe pamoja bwana weeh"
"Tinner sitakiiii ... tena sitaki kabisaaaa"
"Ndo utataka " lakini mie hapo moyoni ka roho kwatuuuu
Siku enyewe usiku woteee ndoto ni Veda tuuu Veda tuu yaani mpaka nilichelewa kuamka Tinner ndio akaja kuniamsha nachelewa kazini ohoo nilikurupukaaa mbio mbiooo nikajiandaa kwenda kazini
Sasa tena kazini nakutana na kisanga kingine tena nje tu ya geti jamani kuna watoto wawili wa kike na wa kiume walikuwa wanalia lia hapo hata sikuwaelewa wala sikutaka kuwafatilia mie nikapita mana nilikuwa nimechelewa sanaaa
Nikachukua koti langu haraka nikaenda moja kwa moja wodini maana kuna wagonjwa walio kuwa wanatakiwa kupewa Ruhusa asubuhi hiyo na ndio hivyo nimechelewa kuingia tena
Hivi sikusema kazi yaangu Eeh Ooh Mungu wangu yaani ndo nakumbuka hapaaa akili yote imeishia kwa Veda mjinga kweli huyu kaka hahaha yaani mpaka nachanganyikiwa, Okay mie bwana ni Doctor kabisaaaa nipo kwenye Hospital ya serikali ni mwaka wa tatu huu tangu nimeajiriwa ....
Nikakuta kuna mgonjwa mpya naambiwa ameletwa tangu jana usiku ila hakuwa amepatiwa matibabu yeyotee zaidi ya dawa za maumivu tu na hali yake ilikuwa mbaya sana...
Nikawauliza kwanini sasa hajapatiwa huduma majibu niliyopewa ni kwamba hawajalipia chochote ndugu zake, jamanii yaani mpaka roho iliniuma huyu mama ana hali mbaya sana halafu et mpaka walipie daah
Nikauliza ndugu zake wako wapi nijaribu kuongea nao nikaambiwa wapo nje basi ile natoka nikakutana na vitoto yaani miaka kama 10 au 11 hivi wakike nawakiume ndo naambiwa hao ndio ndugu zake duuh nilichokaa
Ikabidi niwaite ofisini kwanza nikawauliza "Enhee nyie mkubwa wenu yupo wapi??"
"Kaka amesafiri na hapatikani tangu juzi " eeh nikashusha pumzi
"Kwahiyo nyie mnaishi na kaka yenu tu"
"Ndio..."
"Hakua akiba yeyote aliyowaachia??"
"Kaka anatuachia hela nyingi tu lakini mama aliumwa gafla tukampeleka hospital ya karibu na nyumbani hela zote zimeishia hapo jana usiku ndio wakatuambia tumuhamishe dada tusaidir kaka akija tu anakulipa pesa zako zote" hapo watoto wanaongea wanalia hadi mafua tena wote haswa wa kiume ndio alikuwa anaongoza kuombe daah nikashusha pumzi kwanza nikaegamia kiti
"Nyie ni mapacha??" Badala ya kuwajibu msaada wao mie niliamua kujilidhisha kwanza maana nilikuwa naumia kichwa kujiuliza hawa mapacha.? Walikuwa wanamfanano wa kila kitu hadi vimo
"Ndio dadaaa"
"Waooh, Hongereni, Okay ngoja kwanza tuchukue vipimo vya mama msilie sasaa" walinishukuru haoo afu vitoto vinaadabu mpaka rahaa yaani ...
Basi ilibidi nitoe hela yangu nilipie vipimo vya huyo mama ili aanze kupatiwa matibabu, kumpima bwana alikuwa na kisukari mwenyewe majibu hakuyapokea kwa kukubali yaani yalimshtua hadi ikapelekea plesha kupanda sana na hali yake kuzidi kuwa mbayaa, Huyo kaka yao na hao watoto sasa hata hapatikani we mbona nilikoma miee ..
Zilikuwa siku mbili ila za motoo jashoo linavuja hatari maana kula ilikuwa kwangu kila kitu yaani ilibidi tu nibebe jukumu la kila kitu, mpaka akawa sawa
Ile siku ya tatu nakumbuka alikuwa na hali nzuri kidogo analidhisha, Jioni wakati natoka nikaenda kumuaga maana asubuhi anaweza kupewa ruhusa nikawa labda sijafika
Nikamkuta amekaa kitandani na watoto wake pembeni ", vipi hali yako mamaa" nikamsalimia hukuu najichekesha chekesha na yeye akaachia kicheko
"Asante sana mwanangu asante sanaa mie naendelea vizuri"
Nikasema "usijali mama utakuuwa sawa, mie naondoka kama mtaruhusiwa kabla sijafika basi hakikisha unatumia dawa na kufata vizuri maelezo ya Doctor hautapata shida kabisaaa" niliongea huku nainuka wakati nimesimama nikawatizama wale watoto yaani niliwapenda sana ni wadogo lakini wanabusara mnoo
"Hayaa watoto wazurii, Mtunzeni mama eeh" nikapiga hatua kama mbili hivi akaniita
"Dadaa...." aliniita kwa sauti ya chini nikageuka
βMungu akubariki. Sijui ningekuwaje bila wewe.
Nikatabasamu kidogo, nikajaribu kuficha uchovu uliokuwa umejikusanya mwilini mwangu.
βUsijali mama, muhimu umeanza kuimarika. Hilo ndilo la kwanza.β
Akanishika mkono " moyo wa mtu haupimwi kwa hela. Umefanya zaidi ya daktariβ¦ umefanya kama binti.β nikacheka maana maneno ya huyu mama kidogo yalikuwa yahuzuni
"Usijali mama pumzika mama"
"Mwanagu anakuja leo yupo njiani anaweza kufika usiku nilikuwa naomba sana ukutane nae akurejeshee pesa zote mwanangu"
"Aah mamaaa, Mungu wangu hakuna haja ya kurudisha pesa hakuna hajaaa bwana hahah mie nimetoa nimesahau nataka fadhira kwa mungu, kwahiyo hata usijali mama angu"
Itaendelea....
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi


Maoni