DOLLAR: ( DAKTARI WA HUBA )
Sehemu ya Kwanza
Mtunzi: Layman Donsue
Kwenye Chuo Kikuu cha Uchokozi na Mizinguo, tulikuwa na wanafunzi wa aina zote wenye akili kama ya Einstein na wengine waliokuja chuoni kwa mikwala ya wazazi, si kwa mapenzi ya elimu. Lakini kati ya hao wote, alikuwepo binti mmoja aliyeweza kuyachanganya maisha ya watu chuoni humo kwa urembo wake, ucheshi wake, na kile alichokiita "daktari wa huba" aliitwa Dollar.
Dollar halikuwa jina lake halisi. Jina lake halisi lilikuwa Scolastica Kalunde, lakini nani angetamka hilo? Alipoingia chuoni mwaka wa kwanza, aliamua kujibatiza jina la “Dollar” kwa sababu aliamini anathamani kuliko pesa zote zilizowahi kuchapishwa na Benki Kuu.
Alipokuwa anapita barabarani kuelekea darasani, wanaume waliteleza na kuanguka kama vifaru vilivyochomekwa kwenye sabuni. Kuna siku mmoja wa wanafunzi alijaribu kumrushia mistari, akasema
"Samahani, dada, wewe ni somo gani? Maana kila nikikuona napata stress za midterm!"
Dollar aligeuka na tabasamu la kidewdew, akamjibu,
"Mimi ni somo la uhusiano wa kitaalamu. Ukinifeli, unaingia kwenye msongo wa mawazo na presha ya mapenzi."
Tangu siku hiyo jina lake likabadilika rasmi kuwa "Daktari wa Huba". Alijitangaza kama daktari wa matatizo yote ya kimapenzi kuachwa, kupendwa sana, kupendwa kimabavu, kutojibiwa meseji, na hata wale wanaoota na wapenzi wa watu.
Kliniki yake? Iko kwenye kivuli cha mti karibu na hostel za wasichana, ambapo kila jioni saa kumi na moja, wanafunzi waliokuwa wamekumbwa na matatizo ya mapenzi walimiminika kama wagonjwa wa minyoo ya tumbo.
Wagonjwa walikaa kwenye benchi huku wakijificha na miwani ya jua wakisingizia macho yao yamevimba kwa mapenzi. Dollar aliwasikiliza mmoja mmoja huku akiwaandikia "resepiti" za ajabu kama vile:
“Lala usingizi kumi bila kuandika jina lake”
“Usijibu meseji ya ‘hey’ baada ya saa nne”
“Piga picha na mtu mwingine uposti na emoji ya moyo mmoja tu”
Mmoja wa wagonjwa wake maarufu alikuwa jamaa aliyeitwa Kichaa jina alilopata baada ya kupigwa kibuti na binti wa mwaka wa kwanza aliyeingia chuoni kwa mpango wa kuchukua mwanaume wa gari. Kichaa alilia wiki mbili mfululizo na kula biskuti za chai bila chai.
Dollar alipomuona alisema,
"Tatizo lako ni rahisi, ni kama kukosa password ya WiFi. Mie nitakupa data mpya ya mapenzi."
Kisha alimpa maelekezo ya kwenda kusmile kwa kila msichana aliyemvutia hadi mmoja amuulize, "Mbona una nguvu ya kutabasamu hata ukiwa umeachwa?"
Jamaa alianza kutabasamu hadi meno ya nyuma yakawa kama stima, yanaangaza tu, duh ila haya maajabu ya daktari wa huba yamenishinda tabia.
Chuoni sasa kila mtu alijua, ukiwa na tatizo la mapenzi usiende kwa counselor, nenda kwa Daktari Dollar.
Lakini ndani ya ucheshi huo wote, Dollar alikuwa na siri yake. Ndio alikuwa anawasaidia wengine, lakini mwenyewe alikuwa hajawahi kupendwa hata siku moja. Aliogopa kujiingiza kwenye mapenzi, akihisi kila mwanaume ni mtego kama ule wa panya unaojificha kwenye slice ya mkate.
Siku moja, akiwa kwenye kliniki yake ya kivuli cha mti, kijana mmoja mpya aliyejiunga na chuo akaja. Hakuwa na tatizo, hakukuwa na stress alikuja tu na swali moja,
“Dokta, hivi wewe mwenyewe unajua kupenda au unajua tu kuponya walioumizwa?”
Dollar alinyamaza kwa sekunde tano. Kwa mara ya kwanza, alitabasamu bila kuonyesha meno, na moyo wake ukafanya tuk tuk tuk kama mtu aliyekunywa maji ya baridi akiwa na mafua.
Kijana huyo hakuondoka, aliketi pale pembeni akingoja jibu. Lakini jibu halikutoka.
Na hapo ndipo matatizo ya Daktari wetu wa Huba yalianza rasmi…
Usikae mbali, gonga like mnishawishi kuweka mwendelezo..
ITAENDELEA...
Nishawishini kwa like nishushe sehemu inayofuata fuata chap chap...
Harafu kingine ni hivi wajanja wapo kwenye page kama huja follow page basi utapitwa maana kwenye page huu mzigo utaenda kasi..
Huko mbele ni drama tupu mapenzi kama yote, sana sana ni inachekesha ile mbayaaaaa..
Sehemu ya pili inakuja.