SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 37
Na Sam Darfur 0717255498
RECAP: SEHEMU ILIYOPITA
Pata pesa tujue tabia yako. Tabia ya mjomba tuliijua mara baada ya kupata, nyie huu umskini tuliokuwa nao tumshkuru Mungu maana unatufanya tujue kama kuna utu ila kama mtu mwenye tamaa akipata pesa basi hutu ataweka pembeni kama ilivyokuwa kwa mjomba Loy.Mbungi lilianza mwezi wa kwanza tu katika kazi alimuoa mwanamke mmoja hivi mpemba kutoka Zanzibar alikuwa anaitwa Samrathy, mwenyewe alipenda kukatiza jina lake na kumuita Sammy. Huyu Sammy ndio alimwambia Loy atuue ili mali ziwe chini yake na taratibu za kufanya haya yote yalikuwa chini yake…
SEHEMU YA 37
Naimani ushaweka Like kabla ya kuanza kusoma...!? Kama hujafanya hivyo, ebu like apa......Kila kitu mwanzoni kinakuwa na uzuri wake, kinakuwa na radha, kinakuwa kitamu lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo kinazidi kukuchosha. Kama ilivyokuwa furaha kwa mwanamke ambaye amepata mimba akiwa katika ndoa, ndivyo ilivyokuwa kwetu ambapo tulikuwa na furaha mno kwa Mjomba yetu kuoa.
Tuliimani kwamba yalikuwa ni maamuzi mazuri sababu hata akili yake ingetulia, uwezo wake wa kufanya kazi kwa weledi ungeongezeka mara ndufu kumbe hatukujua kama tunakaribisha kidudu mtu.
Siku za mwanzo za ndoa yao tulikuwa tukienda kwao, tunaongea mambo mbalimbali nao wanatusindikiza huku tukupiga stori za hapa na pale kwa kifupi hakuna siku ambayo ilikuwa haina tabasamu katika maisha yetu.
Tulikuwa na maisha ambayo nilitamani alau marehemu Mama aje aone jinsi gani Loy alikuwa akitupenda kupita maelezo. Nilikuwa natamani aone jinsi ambavyo ndugu yake wa kiume alivyokuwa mstarabu kwetu kuliko hata alivyowahi kuwa Baba.
“Naimani kila kitu kitaenda sawa” nilimwambia Brandina huku tukiwa sebureni tunatazama runinga
“Mwenyewe pia nimekuwa sina mashaka kabisa na mjomba maana amekuwa mtu ambaye kila siku anafanya vizuri kazini”
“Yaani kuna raha kuwa na ndugu ambao wanajitambua kwakweli” Brandina naye aliniambia.
Maongezi yetu yalikuwa ya namna hii kwa siku za mwanzoni, yalikuwa ni mazungumzo ambayo hata wewe ungeyasikia basi ungefurahia. Tulikuwa ni watu ambao kama Mungu ametupa baraka mara baada ya madhira yote kupita.
Nakumbuka siku moja nilienda nyumbani kwaMjomba ambapo tulimpangia masaki ili kama mambo yakienda sawa basi tumtafutie nyuma maeneo mengine. Nyumba ambayo alikuwa anakaa ni ile ambayo mwanzo Baba alimpangia Mama Brandina, nasi tuliona hakuna haja ya kutafuta nyumba mpya, ingewezekana kwa mjomba kukaa pale bila hata wasiwasi wowote.
Baada ya kufika kwa bahati mbaya sikumkuta mjomba, nilimkuta Shangazi Sammy, naomba nimuite Sammy maana hata kwenye ushangazi yule mbwa hakufika. Alikuwa sebureni akitazama runinga, alivyoniona aliinuka na kunipisha sehemu ambayo alikuwa amekaa huku akisogea katika sofa lingine lakini nilimwambia asante.
“Mnaendeleaje maana tumewasusa” Sammy alianzisha maongezi
“Hahaha! Hata usijali, tupo ni hivyo tumeanza kujiandaa kwa ajili ya chuo”
“Kwani matokeo yashatoka enh?”
“Ndio, ndio yametoka na tumepata division one kila mmoja hapa tunasubiri muda ili tuanze majukumu yetu” nilimwambia.
Niliona akiweka tabasamu katika uso wake huku akinipongeza kwa kila aina ya makofi, sikujua kwa wakati ule kwamba nilipaswa kuchunguza makofi yale kabla ya kusema asante ila nilijikuta namshukuru kwakuwa hakuwahi kuwa mbaya kwangu.
Kumbe mwenzangu muda wote alikuwa akiomba sisi tusifaulu ili aanze mambo yake ila aliposikia kwamba tumefaulu, moyo wake uliweka kinyongo. Uasili wake ulijitokeza wazi wazi.
“Kwahiyo mnaondoka lini au mnaanza lini?”
“Tupo katika kuomba bado ila muda mwafaka ukifika tutaondoka na tutakaa kama familia tuongea vizuri tu” nilimwambia.
Siku ile tuliongea mambo mengi sana, tulipiga stori za hapa na pale kuhusu maisha, kampuni na hata vitu ambavyo nilikuwa navipenda nilimwambia. Kumwambia kwangu kumbe ilikuwa ni sehemu ya kumrahisishia kile ambacho alikuwa anataka kukifanya.
Baada ya Mimi kuondoka, jioni ilipofika yeye na Loy walipata kuongea mambo mengi huku ajenda kubwa ni kuhakikisha kwamba tunakufa hata kabla ya kwenda chuo. Ilikuwa ni ajenda ambayo ilipaswa kutekelezwa kwa wepesi mno, yaani kama ingewezekana basi ingekuwa ndani ya miezi miwili kila kitu kingeenda sawa.
Kwa upande wetu hakuna ambaye alikuwa akifahamu kitu, tuliendelea kufanya maombi ya chuo huku tukiimani kwamba kwenda kwetu chuo kungetufanya tuwe miongoni mwa wanafunzi bora, na sio bora tu bali tungeweza kusimamia kampuni zetu na kukuza kila kitu katika upande wa biashara.
Wakati tunaendelea na maombi nilianza kuhisi kama kulikuwa na kitu ambacho hakikuwa sawa haswa katika upande wa mawasiliano yangu na mjomba Loy, alikuwa ni mtu ambaye muda mwingi anamuita Brandina kisha anazungumza naye huku akimuambia kwamba hayakuwa mambo ya muhimu sana hivyo hapaswi kunishirikisha.
Laiki Brandina hakuacha kuniunganisha kwa kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea. “Brandina nahisi kama kutakuwa na kitu sio bure” nilimwambia Brandina maana nilishaanza kuwa na wasiwasi hivi
“Hata mimi nimeanza kuhisi hilo, tunapaswa kukaa na Mama kisha Baba nao tuwaambie kile ambacho tunakiona” Brandina alisema.
Niliona ni wazo ambalo linapaswa kufanyiwa kasi haraka iwezekanavyo, basi tuliitisha kikao cha familia ambapo Mimi, Brandina, Mzee Jawan pamoja na Mama tungehusika kujadili. Hatukutaka kuwaweka kina Loy maana wao ndio waliokuwa wanapaswa kujadiliwa.
“Baba na Mama! Tumewaita hapa kwa lengo moja tu” Brandina alianzisha mazungumzo “Lipi hilo?” Mama Brandina aliuliza
“Mwezi wa pili sasa, hakuna ripoti yoyote ya kampuni ambayo tunaipata n ahata tukimpigia mjomba amekuwa ni mtu ambaye anatupeleka kulia na kurudi kushoto. Kibaya zaidi amefukuza wafanyakazi bila hata kutushirikisha” Alisema Brandina huku akinitazama kama sehemu ya kuniachia kijiti cha mazungumzo.
Mie nilipoona nimepewa ile nafasi, sikutaka kupindisha pindisha maneno bali nilisema
“Ni kweli, mwanzo alikuwa ni mtu ambaye kama kulikuwa na vikao katika kampuni basi atatushirikisha na kila mmoja angefahamu nini ambacho kilikuwa kikiendelea lakini kwa hivi sasa amekuwa tofauti kabisa”
“Mh! Kwahiyo tunafanyaje?” aliuliza Jawan
“Kama inawezekana tutafute ufumbuzi wa hili, aitwe mjomba awekwe kikaangoni ili kujadili nini haswa kinaendelea maana hatuelewi” Nilisema
“Si wazo baya” Jawan aliniambia kisha akamtazama Mama Brandina ambaye alisema
“Kama ni hivyo hakuna shida tumuiteni halafu tuzungumze naye”
Makubaliano yalikuwa hayo, tulipanga kumuita Loy ili tupate kuzungumza naye. Kwa bahati nzuri siku ambayo tulimwambia kwamba tunataka kuzungumza naye alikubali na alikuja pale nyumbani akiwa na Sammy.
Mwanzoni nilitaka Sammy aondoke maana niliona kama sio kuhisi kwamba hapaswi kuingilia mambo ya familia lakini baadaye waliniweka sawa. Kitendo kile kilimkera mno Sammy ambaye aliiweka sumu katika moyo wake na alipanga kuniangamiza mimi kwanza
“Kuna vikao vitatu ambavyo vimepita yaani cha mwisho wa mwezi uliopita, katikati ya mwezi ya mwezi huu na mwisho wa mwezi huu pia. Vikao hivi hakuna ambaye ameshirikishwa hata mmoja kati yetu” nilisema kumwambia mjomba
“Inahusiana na nini na maendeleo ya kampuni kwani haifanyi vizuri?” mjomba aliuliza
“Sio tatizo ila tunataka kujua namna gani kampuni imekuwa ikienda. Kumbuka tumekweka pale kama sehemu ya msimamizi wa muda tu hadi tukiweza kujisimamia ndio tufanye mambo sisi wenyewe” alisema Brandina.
Nimuona Sammy akimpiga jicho Brandina hadi nilitaka kuropoka lakini aliniwahi, nahisi kwamba alijua nini nataka kuzungumza
“Kwahiyo mnataka mume wangu afanyaje?”
“Atushirikishe kwa kila kitu” Brandina alijibu
“Kama?”
“Vikao pamoja na kwenye uongozi tuwe tunajua nani ameingia na nani ametoka maana tunasikia tu sijui kuna wafanyakazi wameto…” kabla hata Brandina hajamalizia aliguswa na Sammy katika eneo la shingo yake
“Samahani palikuwa na mdudu” Alisema Sammy.
Nilihisi jambo lakini nilikaa kimya hadi pale ambapo kikao kiliisha lakini nilishangaa katika eneo ambalo Brandina alikuwa ameguswa na Sammy lilikuwa likidondosha damu taratibu na baadaye ilikauka. Kwakuwa alisema kwamba palikuwa na mdudu basi tulihisi huenda mdudu amempa madhara kumbe haikuwa hivyo bali uchawi ndio ulipandikizwa kwa namna ile….
Nunua kwa 1500Tsh badala ya 3000Tsh. Nitext WhatsApp namba ni 0717255498.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.