Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

Chozi la mdogo wangu SURA YA TATU

7th Aug, 2025 Views 15



Basi baba Dorini hakuwa na jipya maana akizidi kupinga ikafika kwenye sheria anaweza kujikuta anabaki na robo ya mali zake na huku mali zenyewe sio nyingi, basi walikubaliana na makubaliano yaliyo patikana ni kwamba wauze kila kilicho cha Baba Dorini kuanzia gari, nyumba mpaka miradi yake na wagawane fedha. Basi baada ya kuuza waligawana, nusu ya fedha ikaenda kwa baba Dorini na nusu nyingine akaichukua Lissa na hapo kila mmoja akashika hamsini zake, baba Dorini akayaanza rasmi maisha ya nyumba ya kupanga huku hajui aanzie wapi wala aishie wapi. Alipoulizia mkewe alipo akaambiwa kuwa tayari alishaolewa miezi kadhaa iliyopita, hivyo hakuna namna ya kumpata tena, basi maisha yake yakabadilika akawa mtu wa pombe mpaka fedha ilipopukutika kabisa, akawatelekeza watoto na kutokomea kusiko julikana.
Basi siku baada ya siku chakula kilichokuwa kimebaki kwa ajili ya akiba kikaisha, kodi nayo ikaisha, na mkubwa aliye baki ni Dorini mwenye miaka sita au saba kasoro hivi, akitakiwa kumlea mdogo wake ambaye kwa ana umri wa miaka miwili kuelekea mitatu, mtoto huyu bado pia ni mdogo na hata kutembea kwake bado hajawa imara miguu yake.
Dorini baada ya kuona ni takriban wiki tatu zimekatika na njaa inawakolokocha tumboni na baba yao hajarudi tena wala hakuwambia wapi ameenda na lini atarudi, alipata wazo la kuchukua mkeka mzuri na kwenda kuutandika dampo ambalo ni jalala kubwa la kutupia takataka mara nyingi za mji mzima, lengo lake ilikuwa waweze kujikimu kwa kujipatia chakula cha jalalani kuepuka kufa kwa njaa na huenda wakapata msaada. Ndiyo hivyo hana jinsi maana yeye bado ni msichana mdogo na kwake aliona hiyo akili itamsaidia pia mdogo wake asife kwa njaa.
Usiku wa kwanza wa kuyaanza hayo makazi mapya ulikuwa mgumu sana ukizingatia kuna harufu mbaya, mbu wa kutosha, na kelele za mbwa za hapa na pale zilizidi kuwashtua zaidi, asubuhi ilipofika magumu yakaendelea kuwa magumu sana, hii ni kutokana na njaa iliyo kuwa imewakabili, Frank njaa ilimuuma sana kiasi kwamba alianza kulia, Dorini alimbembeleza sana ila ilikuwa ngumu kumuelewa dada yake maana hata hivyo tumboni kulikuwa kukiunguruma kwa njaa tupu.
Ni nani wa kuwasaidia watoto hawa? wale waliofahamiana na wazazi wao waliishia kuwahuzunikia na kuwaonea huruma ila hakuna msaada ambao walikuwa wakiwapa, kuna wakati walikuwa wakipigwa pale ambapo walikuwa wakienda kuomba msaada kwao, wakati mwingine kuambulia kipigo hata pale wanapookota masalia ya vyakula kwenye meza mahotelini au kwa mama lishe, hakuna aliyejali maumivu wanayo yapitia watoto hao, sana sana walikuwa wakiwahuzunikia na kuwahurumia bila msaada, (Hakuna faida ya huruma kama hakuna msaada hata siku moja nasema hakuna..unaweza ukamuhurumia sasa ila kama ulikuwa na uwezo wa kumsaidia na hukumsaidia unakuwa hujafanya lolote).
Watoto hao hawakuwa na rafiki tena maana hakuna aliyewafaa kwa ile dhiki kama ule msemo usemao “akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki”.
Waliishia kwa kuteseka, kupigwa na baridi kali, kuumwa na mbu na kulala njaa kwao ilikuwa kawaida huku wengine wakila na kusaza na kutupa masalia majalalani ila hawakumbuki kuwa kuna watoto mtaani wanateseka huku wakikitamani hicho chakula wanachokitupa ila nacho hawakipati kabisa.
Frank alipokosa chakula alilia sana, kutokana na kuwa Dorini bado na yeye ni mtoto mdogo basi alipoona mdogo wake hanyamazi alianza kulia pia, hivyo ikawa tafrani pale dampo maana hakuna aliyembembeleza mwenzake, Dorini alie kwa kulaumu kwanini baba yao amemfukuza mama yao na kuwatelekeza peke yao wakiteseka bila kujua wanakula nini, Frank na yeye akilia kumlaumu dada yake kwa nini hajampa chakula mpaka muda huo. Walilia muda mrefu sana kila mmoja akilia na la kwake, huyu kwa kuwalaumu wazazi wake kwa kuwatelekeza wakiwa wadogo huku hakuna chakula wala mahala pa kulala na huyu kwa kukosa chakula.

Follow page yangu Story za Riwaya Tanzania.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Chozi la mdogo wangu SURA YA TATU   >>> https://gonga94.com/semajambo/chozi-la-mdogo-wangu-sura-ya-tatu
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

never give up harmonize
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest