Alipozaliwa alipewa jina la Agness lakini taratibu lilibadilika na kuwa Laviollete La Chapelle wengne wakimwita kwa kifup Lavio na wengne wakimwita LALACHA Mwili wake uliojaa vizuri sio kwa afya bali shughuli pevu ya kusonga sufuria ya ugali katika mgahawa mdogo wa mama yake,sura yake ilipambwa na mikunjo ya hasira kwenye paji la uso hyo ikimaanisha hataki mchezo awapo kazini,ilikuwa si jambo la kushangaza kumkuta akiwa amekabana mashati na wateja wakorofi bila kuogopa jinsia zao na wakati mwingne ilifikia hatua ya kupigana kabisa.
Licha ya yote hayo Lavio alikuwa mchapa kazi hasa hakuwa legelege hata kidogo hicho kiliwavutia wateja wengi sana. Kwa mising hyo pia hakuna mwanaume aliyefikiria eti huenda Lavio huwa anapata fursa ya kuwaza mapenzi au kumfikiria mwanaume yeyote yule,alikuwa bize yeye na genge genge na yeye basi. Mama yake alimpenda sana mwanaye huyo pekee.
* * * * *
Rahim Rahman kijana wa kiarabu aliyekulia uswahlini kwake yeye vurugu na matusi vilikuwa vitu vya kawaida na kuwabadili watoto wa uswazi wanaojipendekeza ndio ilikuwa jadi yake."Wazee,mi nataka nifukuzie yule mtoto wa mama lishe anaitwa Lavio mnampata?" aliwaambia jamaa zake walipokuwa kijiweni,wote walicheka wakiamini Rahim anatania lakini hawakujua kama yupo serious mwenzao.
Umukuria intina.