Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Nanah aliingia ofisini na kuitupa pochi yake mezani kisha akaketi.
Bieber alishakuwa ndani ya ofisi yake na alikuwa akimtizama tu Nanah.
Nanah aliwasha pc yake na muda huo huo nao Doy aliingia ndani na Kurwa.
Walipita na kwenda kuketi eneo lao husika huku wakimtizama Nanah.
Doy alimshtua dada yake ajaribu kulianzisha.
Kurwa alichukua file na kumrushia mezani kwake.
"Utafanya hiyo kazi, uhakikishe imekamilika kabla ya saa 7".
Nanah alimtizama Kurwa na baada ya kumaliza kumtizama alishika lile file na kumrushia vilevile bila kusema neno lolote lile.
Doy alitizamana na Kurwa na Doy alishika lile file kisha akaenda nalo hadi mezani kwa Nanah na kulitupia hapo.
"Tumesema ufanye hii kazi hadi saa 6 iwe imekamilika".
Doy aliondoka na kurudi kwenye kiti chake akipishana na Kurwa huku wakigonga mikono yao.
"Mmmhhh" Nanah alitabasamu kwa dharau kisha akasogeza kiti chake nyuma na kubeba lile file akielekea meza ya Doy.
Alifika na kulitupa file style ile ile aliyotumia Doy kumtupia.
"Wewe siyo bosi wangu hapa, kwahiyo fanya kazi zako mwenyewe". Alijibu Nanah na kurudi kwenye kiti chake.
Bieber alikuwa ndani ya ofisi yake na hakuna hata mmoja aliyemuona mpaka wakati ule japo ofisi ilikuwa ndani palepale ni kioo tu ndo kiliweza watenganisha ila wangeweza kuonana vizuri tu pindi pazia zitakapokuwa zimefunguliwa.
"We Bi......
"We koma wewe. Alafu usitake kunizoea sana. Mimi na nyie tumesoma tu shule moja na darasa moja lakini haimaanisha ya kuwa mnanifahamu".
"Haya kuna nini?" Aliuliza Bob Risky akiingia baada ya kupokelewa na kelele zile.
"Bob unamuona huyu Nanah? Yan kwa......
"Oooohhh Mr Handsome" alisema Bob Risky baada ya kumuona Bieber aliyekuwa ndani pale.
Nanah, Doy pamoja na Kurwa na wao walipeleka macho yao huko alikopeleka Bob.
"Mungu wangu!!" Alisema hilo Doy akimtizama ndugu yake.
"Ametuona eee?"
"Sasa kama tunamuona unadhani hatuoni?"
Bieber alitoka ofisini kwake na kusimama mlangoni akiwatizama.
"Shikamo Boss" wakwanza kusalimia alikuwa Kurwa kisha akapokea Doy.
"Hi Mr Handsome" alisalimia Bob Risky na sasa alibaki Nanah ambaye hakuwa amesalimia.
Aliinua macho yake na kukuta watu wote wanamtizama yeye asalimie.
"Good Morning " alisalimia hivyo akitizama chini kama mtu mwenye aibu kweli.
"Good Morning" alijibu Bieber
"Nyie Mapacha".
"Yes Boss"
"Mkinisalimia za asubuhi itatosha, sina uzee huo mimi".
"Ndiyo"
"Na vipi kuhusu mimi Mr Handsome?" Aliuliza Bob Risky akimchekea na kumpungia mkono wake.
Bieber alimtizama na hakumjibu chochote kabisa.
"Naah njoo ofisini kwangu"
"Naaah!!!?" Doy na Kurwaa waliuliza kwa mshangao baada ya jina la Nanah kufupishwa na Bieber.
"Mapacha, kuna tatizo?"
"Hapana Boss hamna" walijibu wote kwa pamoja na kutabasamu chini kwa chini.
"Sawa" alisema hilo Bieber na kuingia ofisini kwake.
"Hiyo ndo nini jamani, mi sionekani au? Mbona sijasemeshwa kabisa?" Aliuliza Bob Risky kwa sauti huku akiuvuta mdomo wake.
Nanah aliingia ofisini na Bieber alimuonyeshea akae.
Nanah alikaa kwa aibu na kutengenezea miwani yake.
"Mmmmhhh, unavyojua ku akt sasa, unafahamu mi najua wewe ni mwongeaji sana na mkorofi eee?"
Nanah aliinua macho na kumtizama.
"Na wala huna haja ya hiyo miwani ili kuona".
"We sema umeniitia nini bhana"
"Jana ulinipiga kibao unakumbuka?" Alihoji Bieber.
"Nadhani na wewe hujasahau sababu ya mimi kukupiga" alijibu na yeye Nanah.
"Nataka nikufungulie kesi ya kile ulichonifanyia kwasababu nina matatizo ya kiafya."
"Jamaniiii!!" Alizungumza Nanah akivuta na kuweka sura ya huzuni
"Hahahaha" alicheka Bieber na kumgeuzia Nanah karatasi lililokuwa mezani na kwa upande wake.
Nanah alilitizama.
"Ni makubaliano hayo ya wewe kuwa Sekretari wangu".
"Lakini mimi tayari ni Sekretari wako" alijibu Nanah.
"Jana tu umeleta barua ya kuacha kazi. Unadhani naweza kukuamini tena?".
"Kampa kitu gani asaini?' Aliuliza Kurwa.
"Nani anajua sasa? Ila huyu mwenzako nyota yake inawaka kwelikweli. Yani ndugu wote wawili wamechanganyikiwa juu yake?"
"Ni nini hiyo anasaini jamani, natamani kuona mimi". Alisisitiza Kurwa.
"Heeeee ngoja kwanza mimi nipeleke umbea"
Doy aliinuka na kutoka mbiombio.
Nanah alimaliza kusaini na kumrudishia.
Bieber aliichukua karatasi ile na kuwasha mashine ya kutolea kopi.
Alitoa kopi mbili na kumpatia.
"Mbona kopi mbili?"
"Kwasababu hiyo moja kuna mtu ata ihitaji".
Wakati Bieber anasema hilo hapohapo Brown aliingia.
"Kwanzia sasa hivi Nanah atafanya kazi, chini ya ofisi yangu mimi. Wewe chukua mizigo yako tunaenda"
"Sasa mpe nakala yake moja kwasababu nimekwambia tu ata ihitaji"
Nanah alimtizama Bieber ambaye alimpatia ishara ya ampe tu wala haina shida.
Nanah alimpatia nakala ile moja.
"Nini?"
"Hayo ni makubaliana baina yangu na Sekretari wangu Nanah, kwa lugha fasaha naweza kusema ni mkataba".
"Nini million 200?" Aliuliza Brown na kumtizama ndugu yake Bieber.
"Ndo mshahara wangu?" Aliuliza Nanah kwa mshangao na alianza kusoma kile alichoweza kukisaini.
Haya ni makubaliano baina ya Nanah ka......
Namba 1. Endapo mwajiriwa atataka kuvunja mkataba huu atapaswa kulipia faini ya shilingi million 2000.
"Heeeee yani hii kampuni inakulipa elfu 10 ila ukitaka kuondoka utoe billion, mmmmhhh"
"Namba 2 baada ya mwajiriwa kutoa faini ya shilingi million 2000 ataondoka na mwajiri wake na kwenda naye Marekani..... Hii ni nini?" Aliuliza Nanah akiinua macho yake juu na kumtizama Bieber.
"Na Namba tatu endapo nitahama ofisi hii utaondoka na mimi na mkataba wa kampuni hii haichangamani na mkataba huu mpya"
Brown alilielewa sasa lengo la mdogo wa kufanya vile, yani hakuacha upenyo hata mmoja ambao ungeweza kumfanya Brown ampate Nanah.
Brown aliikunja kunja lile karatasi na Bieber alimuonyeshea original lililokuwa mkononi mwake.
Brown aliweka karatasi lile mezani na kutoka zake kwa hasira
"Samahani, huyo anayetakiwa kulipa hizo milion 200 ni nani kati yetu?" Alihoji Nanah.
Bieber alitabasamu tu.
"Hi Bieber " alisalimia Shalha akiingia pale ofisini huku Doy akienda kukaa kwenye kiti chake na kutizama balaa gani ameweza kumletea Nanah.
"Niliambiwa ume be assigned na kutengeneza nguo kwaajili ya tukio linalokuja".
"Ilikuwa hivyo ila sasa hivi nimepewa kazi nyingine".
"Unapaswa kufanya hivyo tena" alizungumza Bieber.
"Bieber, mimi ndo huwa nafanya kazi hiyo na nina uzoefu nayo. Hivyo huna haja".
"Samahani kwa kukwambia hili Shalha, ila kwanza sasa mimi ndo Mkuu wa hichi kitengo na nachagua nani afanye nini nakwa wakati gani"
"What?".
"Kafanya nilichosema natumaini ndani ya siku hizi mbili tatu, nitaona draft ya hicho ulicho ki design.
"Sawa Boss" Alijibu Nanah na kutoka pale ofisini
"Karibu nikusaidie nini?" Alihoji Bieber na Shalha aliondoka akiwa amefura kwa hasira huku akielekea ofisi ya Brown.
Itaendelea In Shaa Allah.