Inno akamsogelea Zakia ,zakia anatetemeka akasema akhaa mi sijawahi kumfanya kitu!!
Mimi nasema hapana jamni ni huyo huyo ni zakia huyooo jamani sijui nimemkosea nini miee !!!
Sasa zakia hofu ikamzidi ukimtazama tu unamuona anavyo babaika akaweweseka maneno anauma umaaa, Alex alimuweka bonge wa kibaoo akamwambia nakuuwa
Hapo mkumbuke tupo private Room, wote tuliopo ni ndugu tu.
Mama akamuwahi alex mama mkwe sasa mama yangu hakuwepo akamwambia alex we ni mjinga eeeh unampiga sasa kwa niniii???
Alex akamwambia mama niache mama ake akamwambia hapana lazima tuongee nae taratibu, zakia baada ya kuona mama anamtetea akaanza kulia anasema wema wangu tu mie kuja kumuona mnanishika uchawi mie sijafanya kitu
Subira akasema embu subiri kwanza shemu mie mwenyewe kuna kitu sielewi huyu zakia ananiulizaga maswali mengi kuhusu dada huwa siyaelewi kuna siku anasema sijui dada aliiba mwanaume wa mtu ndio mana kawa hivi
Subira akanisogelea akaniuliza dada nataka kujua nawewe huwezi kuongea naomba nikuulize swali kama ndio Fumba macho yako sawa na kama hapana endelea kunitazama sawa nikafumba macho yaan kumaanisha Akasema safi
"Zakia analishakufanya kitu kibaya???" Nilifumba macho kama kusema ndio yaani ile nafumbua nakuta zakia anavuja damu hata sijui kapigwa sangap subira anamuamia alex anamvuta anasema subiri basii hata hatujui kitu gani labda alimtukana au alimsema vibaya shemu embu subiri
Alex anatetemeka inno katulia ananitazama yaan ananiangalia kwelii , subira akaridi kwangu akaniuliza
"Hicho kitu dada kinahusiana na wewe kulala hapaa" nilifumba macho na machozi yakaanza kunitoka natamani kuongea natamani zakia anijibu mimi mwenyewe kwaniniiii!!???
Inno akamwambia alex embu huyu niachie mie , wewe ulimfanyaje Salma
"Mimi sijamfanya kitu nyie mnasema alipata matatizo usiku mi usi..." hata hakumalizia inno alimpiga kichwa mpaka akazimia hapo hapo nikasema kivumbi leo hawa vichaa wawili leo wanaweza uwa hawaa!!
Alex akatoka akarudi na doctor, mwenyewe aliogopa kweli akasema amefanya nini ,Inno akampatia pesa akamwambia mtibu huyu tunakazi nae mtibie humu humu ndani
Basi kwenye pesa tena hata yesu alisalitiwa kweupee !!
Mpaka sa 5 usiku ndio Zakia anaamka hapo yupo hoi , inno akasema muache apumzike mana alex alikuwa kashapaniki hivyo akasema mwache apumzike kwanza huyu ,mimi nitamalizana nae
Zakia anatetemeka , tulilala humo wotee, mama mkwe yeye alirudi nyumbani, nikabaki na subira wangu ,alex na inno
Hakuna hata aliepitiwa usingizi asubuhi mama alikuja mama yangu mzazi alileta chakula ndo akamkuta zakia yupo kwenye ile hali akauliza Alex akamwambia mama hata usijali sisi wenyewe hatujui bado ila tutajua
Alex alivua mkanda kiunoni akamwambia zakia yaan ulipo gusa ni kwenye kitovu cha moyo wangu
Nakuuwa leo hapaaa na sintafungwa mie sawa na mazishi yako nitagharamia miee
Inno akasema mmmmh na kwanini ugharamie wewe kwani hana familiaaa?? Embu sogea huyu namuuwa mimi
Yaan walikuwa kama wanaigiza kila mtu anawatazaama wanavyomgombania zakia
Zakia anatetemekaa
"Haya utasema au hutasema??" Inno akaumuuliza huku anamsogelea kashika mkanda na yeye
"Hakuna kumuuliza inno piga azimie akizinduka kesho tunaendelea mpaka ataka....."
Hata kabla hajamaliza kuongea tulisikia ukunga wa nguvu zakia alipiga kelele baada ya kupigwa na inno
Ulikuwa mkanda mmoja tu
Jamani nisamehe sio mimi ni Juddy ndio anajua sio mimiiii "
Baada ya kusikia jina la juddy moyo ulipiga paah nilihisi wembe umepita nilihisi presha kupandaa kwa kasi ,
Nilikuwa natetemeka kwa hasira natetemeka
Kila mtu alishika mdomo wakaishiwa pozi ndo mama mkwe nae ameongozana na baba mkwe wanaingia wote wakasikia et juddy japo juddy tangu alipo tolewa kwenye nyumba ya alex akapangiwa sahemu ingine hajawahi kujulikana alipo hata pale alipo kuwa amepangiwa hayupo
"Ninii!!! Yaan juddy alifanya niniii???! Mama mkwe alimuuliza huku anaitoa miwani yake akasogea na kuketi pembeni ya zakia
"Naapa kwa mungu ,Juddy alinambia kuwa ametelekezwa akiwa mjamzito na baba wa mtoto wake nataka kumuoa salma ,aliniomba sana nimsaidie ili arudiane na baba mtoto wake ,, nilimuonea huruma nikakubali ndio akanipa hiyo juice nimpe anywe sikujua atapata shida gani ila juddy aliniambia kama akinywa hiyo juice ataanza kumchukia Alex na baadae yeye na alex wataachana .....'"
Kila mtu alishusha pumzi ,mama angu alianza kuliaa ,alex alishindwa kujikaza akaja kunikumbatia analia ananiambia salma mke wangu naomba unisamehe nakuomba mke wangu sikujua kama kuna siku utateseka kwa ajili yangu
Yaan salma tangu unijue mie hujawahi kuishi kwa amani mama angu hata sijui najihukumu vipiii miee , yaan wanakutesa hivi afu unawatoto kwenye tumbo lako mke wangu!!!alex alilia akaongea maneno mengiii
Mi nalia moyoni nasema alex wangu pamoja na yotee bado nakupenda bado nakuhitajii wala sijachukia haya maisha kama wewe upo na mimi hiyo inatosha baba yangu acha leo tupitie haya ili kesho tuwe imara zaidi .
Inno akamwambia zakia huyo juddy tutampata wapi??
Zakia akasema "mi sijui huwa ananipigia simu tunakutana tu sehemu hata sipajui anapo ishii"
"Mpigie simu!"
Zakia akachukua simu yake akampigia juddy iliita kidogo tu ikapokelew hapo imewekwa Loudspeaker..
"Enhee shoga angu jana nimesubiri simu yako nikaona kimyaa, ulimpaka huyo marayaaa!!!??"
Ilikuwa sauti ya juddy tena anafuraha kweli anaonekana...
ITAENDELEA.....
KWETU morogoro.