Nianze kwa kukupa onyo msomaji wanguπ€¦ simulizi hii ni ya kichawi, maisha ya kweli niliyopitia na mwanaume wangu katika ndoa yangu. Maisha ya kichawi ambayo sijui nianzie wapi kusimulia lakini, maisha yangu yalibadilika mara baada ya mume wangu kupata utajiri. π
βNaitwa Zamda Bint Nassibu, ndio jina langu halisi. Nimezaliwa Namikupa wilayani Tandahimba mkoani Mtwara lakini kwa hivi sasa naishi hapa nyumbani kwangu Shangani West. Nina miaka 27
Iko hivi, Miaka sita nyuma niliolewa na mume wangu Kazumar Ibun Dharihi, nikaishi naye kwa amani kabisa.
Yeye alizaliwa katika eneo linaloitwa Naliendele, alikulia huko na Maisha yake yaani wazazi wake kwao ni huko, ni mtoto wa kwanza kwao kati ya Watoto wawili yaani yeye na Dada yake. Kuhusu mimi na yeye hadi tunakutana ni kwamba, tulikutana wakati ambao nilienda Naliendele katika unyago wa ndugu yangu mmoja hivi, basi hapo ndipo uhusiano wetu ukazaliwa. Nakumbuka ilikuwa mwaka 2015 hivi.
Baada ya uhusiano kukua huku tukiwa kama marafiki baadaye alinichumbia na tuliingia katika ndoa. Kama unavyojua Maisha ya ndoa ya mwanaume ambaye anapambana yaani hana kitu, unataka nawe mwanamke umuoneshe ushirikiano, usimkatishe tamaa, umpe moyo ili azidi kupambana. Nami nilimpa ushirikiano kisawa sawa maana sikuwa na elimu ya kutosha zaidi ya darasa la nne tena nilifeli, sikutaka kurudia. Kwakuwa wazazi wangu waliona kumsomesha mtoto wa kike ni hasara hawakutaka kujisumbua, pesa ya sare za shule wakaingiza katika mashamba ya korosho na Maisha yakaendelea.
Tukiwa kama mke na mume tulipambana kutoka chini yaani naposema chini namaanisha kulala kwenye mkeka kama sio utefu. Hatukuwa na godoro wala kitanda zaidi ya matumaini pekee ndio yalikuwa mbele yetu. Nilihitaji uvumilivu sana katika kipindi hichi maana nilichekwa mno na watu mbalimbali hasa wasichana wenzangu ambao nilikuwa nakaa nao karibu ama kupiga nao story. Lakini sikufa moyo wala kumuacha mume wangu, moyoni mwetu tukawa na Imani.Tuliimani kwamba tunaweza kufanikiwa.
Tulikuwa tunaishi katika kibanda kidogo ambacho tulipangishiwa kwa elfu tano palepale Naliendele lakini ilikuwa mtaa wa pili kutoka kwa Mama yake na Baba yake wanaita Mnali. Maisha mwanzo yalikuwa magumu mno, asikuambie mtu chini kunaumiza maana nakumbuka jiko la mkaa lilikuwa linawekwa ndani ya chumba chetu ambacho kama ungeingia ndani basi ungekutana na sufuria mbili, sahani moja, vikombe viwili, mwiko pamoja na sahani tu.
Ugumu ulipozidi nilirudi kijijini kuongea na Mama. Nakumbuka aliniambia kwamba "nauza shamba langu ili niokoe maisha yako mwanangu, mimi nimekwishazeeka sasa. Sina mbele wala nyuma, kwakuwa wewe na mumeo mna nguvu ya kupambana mnaweza kutumia hii hela kama sehemu ya mtaji. Mwanangu nenda kapambane na mume wako ili watoto wako wasife njaa lakini ifike hatua unikumbuke na mimi pale nitakapokuwa na uhitaji"
Nilikubaliana na Mama ingawa zoezi la kuuza shamba Baba alipinga sana kutokana na yeye kuamini kuwa lile ilikuwa ni sehemu yao ya msingi katika kuendesha maisha yao. Ugomvi baina yao ukaibuka na mwisho wa yote, Mama yangu alipokea talaka wakatengana na Baba. Ila yote haya Mama aliyafanya kwa upendo, alijitolea kwa ajili yangu.
Iliniuma kama mtoto, niliteseka lakini Mama aliniambia kwamba nenda kapambane na mume wako, nenda mkayatengeneze maisha ili Baba yako aone mafanikio yako na ajue kuwa nilikuwa sahihi katika kile ambacho nimekipanga. Nilirudi zangu Naliendele ambapo nilimshauri mume wangu kuhamia mjini kabisa maana eneo ambalo tulikuwa tunaishi ingawa lilikuwa limechangamka lakini sio sana kama ilivyokuwa maeneo mengi ya mjini.
Uzuri ni kwamba mume wangu alinikubalia na mwezi mmoja mbele tulihamia rasmi mjini kutoka Naliendele. Maisha ya mjini kama unavyoyajua yanakuwa tofauti na yale ya maeneo ya kando ya mji enhe? Ndivyo ilivyokuwa hata kwetu pia, tuliona kama mambo yamebadilika hivi lakini tulisema tunaweza kushinda haijalishi itakuwaje. Tukaanza maisha kwa pamoja, mapambano yalikuwa magumu mno lakini tulifanikiwa kufungua eneo letu la biashara maeneo ya Tandika ambako tulikuwa tukiishi.
Tukaanzia kuuza mboga mboga, ikawa kila siku asubuhi tunaamka na kwenda kuchukua mzigo sabasaba kisha tunakuja kuuza. Ilikuwa ndio kawaida yetu. Mwaka wa kwanza ukakatika bila hata mafanikio katika biashara yetu zaidi ya kupata hela ya kula, kunywa na kulipa kodi lakini tuliweza kujitambua kwa kudumisha hela ya mtaji. Mwaka huu mume wangu alinishikirisha mpango kwamba twende kwa Mganga ili tuweze kukuza biashara yetu kwa kuvutia wateja lakini sikuafikiana naye, nakumbuka tulirumbana sana. Sikuwa napenda uganga, sikuwa napenda ushirikina hata chembe.
Alinielewa ingawa ilikuwa kishingo upande lakini nilimwambia ukweli kwamba kama unataka kuleta mambo yako ya kichawi nakuomba mimi usinishirikishe, usinishirikishe kabisa. Nilikuwa najua endapo angenishirikisha basi huko mbeleni ingehitajika kafara, sijui kumwaga damu na mambo mengine ya hovyo.
Basi mwaka wa kwanza ukaisha na ukaingia mwaka wa pili ambao ulikuwa na mafanikio kiasi, tuliuza mno. Tulikuwa ni watu ambao kama tukibeba mzigo wa laki moja basi faida tunaipata kama laki na nusu hivi. Hapa ndipo hatua yetu ya mafanikio ilianzia. Maneno kwa majirani kwamba tunatumia uchawi yakaanza, watu walikuwa wakitusema.
Nikasema napaswa kumuuliza mume wangu kama kuna chochote kile. Alinikatalia na kusema tangu mimi nimkataze aliachana na yale mambo huku akinisisitizia kwamba sipaswi kusikiliza ya watu.
βUsione watu kila siku wanakuchekea ukadhani wanapenda jinsi ambavyo tunafanikiwa. Usiwasikilize, sisi tunasaidiwa na Mungu. Yeye Allah Subuhannah wataallah ndio kila kituβ Maneno ya mume wangu haya.
Nikasema hakuna shida acha tuendelee na Maisha nitajua huko mbele, kwakuwa nampenda na namwamini basi niliziba kabisa masikio na sikutaka kusikia lolote kutoka kwa watu. Tukaanza kukua kibiashara, akili ikapanuka kila mmoja akaweka wazo lingine la biashara. Mimi nilimwambia mume wangu kwamba tunatakiwa kuwa na Saloon za kike, naye akaniambia kwamba anataka kufungua Library maana anasikia zinalipa sana.
Kila mmoja alilichukulia wazo la mwenzake kama wazo huru na bora pia linatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka iwezekanvyo. Mume wangu alikuwa napete katika kidole cha shahada hadi kesho ile pete anayo, ilikuwa kila tukitaka kufanya tendo basi angeanza kuomba kupitia ile pete. Nilipomuuliza kwanini aliniambia hakuna, naomba tu. Ingawa nilikuwa na wasiwasi lakini nilijiambia kwamba acha tuone mwisho wake utakuwaje.
Mwaka wa tatu wa ndoa yetu ulitupa saloon mbili za kike tena kubwa haswa na Library nne ambazo hizo zote kwa majumlisho yake ilikuwa tunachukua laki nne mpaka saba kwa siku huku tukiajili watu mbalimbali. Mafanikio ya haraka mno, pesa za kushangaza tulizizoa kila dakika. Nakumbuka taratibu tulihamia kwenye nyumba ya wastani kidogo ambayo tulilipa elfu 50 kwa mwezi. Kama ujuavyo Mtwara kwa miaka ya 2017 ukilipia chumba kwa bei hiyo basi una hela haswa.
Baada ya kulipa kodi kwa muda mrefu, baadaye tukajiambiza kwamba pesa ambayo tutaipata basi tuitunze ili tuweze kujenga nyumba kutoka katika kupanga. Mungu si athuman, hatimaye mwaka wa nne ulipoingia tulikuja na wazo la kiwanja. Tulinunua kiwanja Shangani West yaani hili eneo ambalo umesimamisha wewe gari lako, ndilo tulilokanunua kisha matofari yakafuatia, tukamtafuta fundi wa kupaua na kujenga chini. Tuliwapata na kuwapa ramani ya kitu ambacho tulikuwa tukihitaji. Walitujengea nyumba kubwa mno ya kifahari ambayo sisi tunakaa hadi muda huu, kama ungepata nafasi ya kuingia ndani basi ungeona ukubwa wa jengo hili.
Mwaka wa tano ulipoingia tulinunua gari mbili za kifahari zote zipo mle ndani, mume wangu anaendesha kila siku katika Maisha yake huku akienda kazini na kurudi. Kuna gari lingine ambayo mimi nilikuwa naendesha kwa wakati huo lakini kwa hivi sasa siruhusiwi kuendesha chochote. Pia mwaka huu ulikuja na homa kwa Mama yangu, Mama alikuwa anaumwa mno.
Nikakaa chini na mume wangu, nikamweleza kuhusiana na kile ambacho Mama alikuwa anapitia.
"Mama sasa hivi ni mgonjwa, kama sio umauti unamuita kutokana na uzee basi atakuwa anaumwa kawaida tu lakini yote tunahitaj kumpa uangalizi wake" nilimweleza hivi ila mwenzangu aliniambia anapaswa kwanza kuwashirikisha ndugu zake.
"Napaswa kuzungumza na Mama pamoja na Dada, wao ndio wanapaswa kutoa ruksa katika hili" mume wangu aliniambia hivyo.
Nilishangaa, inawezekanaje kwa kitu ambacho anaweza kukifanya yeye mwenyewe hadi atake kuleta ndugu zake katika jambo lile. Lakini kwakuwa nilimheshimu sana mume wangu, nilikuwa nampenda na kumheshimu. Nilimwambia sawa, sawa hakuna shida ni wewe tu ndio nakusikiliza baba yangu.
Maneno yangu ya kukubali yaliingia na simanzi moyoni lakini baadaye nikajipa moyo kwamba huenda hata ndugu zake watakuwa wanatambua nini haswa ambacho kinaendelea na mafanikio yetu yametokana na nini. Wakati huo kila ndugu yake alikuwa na gari nzuri, aliwajengea nyumba huko kwao Naliendele lakini mimi nilipotaka kwenda kumsalimu Mama alinichimba mkwara wa kufa mtu. Akisema βUmeolewa na mke haruhusiwi kutoka nyumbani bila idhini ya mumeweβ hata nilipomgusia kuhusu kuboresha kibanda cha Mama yangu hakuacha kunichimbia mkwara, hakuacha kuwa Mkali.
Baada ya ile taarifa nakumbuka ilipita wiki bila hata majibu yoyote wala kikao chochote, ikakatika miezi kama miwili. Licha ya kimya chake lakini sikuacha kumsisitizia kuhusu hali ya Mama yangu. Nikaona napaswa kuongea naye ili kumuuliza. Siku hiyo nikamuomba chumbani kisha tulikaa na kuzungumza.
"Mume wangu, ni miezi miwili sasa bado hujanipa mrejesho wa kile ambacho nimekuomba"
"Uliniomba nini kwani?" Mume wangu aliniuliza.
Unajua nilishikwa na hasira, nilikuwa na hasira mno maana sikutegemea kama mume wangu angesahau jambo lile ambalo lilikuwa la muhimu sana kwangu na hata kwake pia. Nilijikuta nikidondosha chozi mbele yake lakini hakudiliki kunifuta, nikamtazama usoni mara mbili, mara tatu na mwisho nilitingisha kichwa changu. Hapa sikutaka tena kuzungumza naye, niliona napaswa kuchukua maamuzi mimi mwenyewe bila hata kumshirikisha mtu yoyote yule.
Sidhani kama zilikuwa ni hasira bali nilitaka kwenda sambamba na dharau zake, nilitaka kumuonesha kwamba uamuzi ambao yeye alishindwa kuuchukua ungechukuliwa kwa urahisi tu. Kwanza tulikuwa na pesa ambazo ziliogopesha kila mmoja na pia tulikuwa na kampuni ya kuuza pikipiki ambayo hadi leo tunayo. Pia tulikuwa na daladala sita ambazo zilikuwa zinachukua abiria kila siku. Bajaji 20 ambazo kila siku zilikuwa zikileta hesabu na mwisho kabisa jumlisha zile Library na Saloon, hapo kulikuwa na nini kingine ambacho kilisubiriwa ili kumsaidia Mama yangu?
Siku iliyofuata nilifunga safari hadi kijijini ambako nilimkuta Mama yangu akiwa katika hali mbaya mno. Ilifika hatua hadi akiongea anasema anahisi maumivu, watu mbalimbali walinicheka na kunilaumu. Waliniita mimi ni mjinga, mshezi n ani mtu ambaye sina akili maana namuacha Mama yangu anakiteseka. Namuacha mwanamke ambaye alinipamania ili niwe Tajiri akiwa hoe hae. Maneno yao yaliniumiza nisiwe muongo, machozi yalinitoka na kama mtoto wa pekee kwake nilimchukua Mama yangu na kurudi naye mjini.
Nilipofika nilianza naye matibabu katika hospital ya Rufaa yaani Ligula. Kwa muda wote wa siku nzima, mume wangu hakunipigia simu wala kuniambia inakuwaje kama ilivyokuwa siku nyingine katika maisha yetu. Mama siku hii alilazwa nami ilinibidi nirudi nyumbani kwa ajili ya kuandaa chakula na mambo mengine. Niliporudi nilimkuta mume wangu amefura kwa hasira huku akiniuliza.
"Ulikuwa wapi?"
"Si nilikuaga lakini hata kabla ya kuondoka"
"Usiniambie kwamba umeenda kumchukua Mama yako?"
"Ndio nimeenda kiijijini kwa Mama, hata hivyo nimemchukua yupo hospital"
"Yupo hospital nani ambaye amekupa idhini ya kutoa mguu wako humu ndani?"
"Kama nilishakueleza na umeshindwa kulifanyia kazi, kwanini nisichukue maamuzi mkononi?"
"Zamda, Zamda nikifirisika nitakuua. Nakuomba umrudishe Mama yako au unataka nimuue ndio ujue sitaki kumsaidia?β Mume wangu aliniuliza.
Nilihisi kutetemeka, mwili uliniisha nguvu. Kijasho chembamba kilianza kunitoka, nilishindwa hata la kujibu maana hasira zilikuwa mbele yangu, nilijikuta nikidondosha machozi. Nilimtazama mume wangu kwa sekunde kama 50 kisha nikamuuliza.
βInamaana umesahau wema ambao Mama ameufanya kwetu? Umesahau kama aliachika ili sisi tuwe na hizi mali?β
βHilo mimi alinihusu ila hapa kwangu simtaki Mama yako, nimeshasemaβ aliongea Mume wangu kisha aliondoka kuelekea chumbani. Nilimtazama hadi alipozama, nikashusha pumzi, mikono ikiwa kiunoni. Nilikaa kimya nikifikiria huku nisijue nilikuwa nafikiria nini. Mwisho nilishusha pumzi na kuanza kupiga hatua kuelekea jikoni ambako nilipika hadi nilipomaliza na kuweka chakula kwenye poti.
Nilienda zangu kuoga ili nijiandae na safari ya kwenda hospital kwa mara ya pili lakini nikiwa zangu bafuni nilisikia sauti kama ya Mume wangu akiongea na simu, ilinibidi nitegeshe sikio langu vizuri ili nipate kumsikia kwa vyema.
"Ndio dada kamleta, anasema kwamba yupo hospital. Nimempigia mkwara lakini hajanielewa. No, sio kwamba namchekea lakini ndio hivyo. Kwahiyo nifanyaje nami najua yule Mama akitoka hospital atakuja hapa nami sitaki iwe hivyo, sitaki kabisaaaa. Na nimepanga nimuue wewe subiri tu, nani ambaye anataka kuwa masikini hapa?" mume wangu aliongea hivyo.
Hamu ya kuoga iliniisha, nguvu zilinipotea. Nilijikuta nanyong'onyea maana sikuamini kama yule ambaye anaongea maneno ya aina ile ni mume wangu. Nikatoka bafuni kisha chumbani na kuvaa nguo baada ya hapo niliondoka zangu. Nikaenda hadi jikoni ambako nilikutana na hotpot yangu, nilihisi kama imefunguliwa lakini sikuwa na uhakika sana. Basi niliichukua na safari ya kwenda hospital ilianza.
Sikujua, sikudhani wala sikutegemea kama katika hotpot ile et mume wangu aliifungua na kuweka sumu kwa lengo la kumuua Mama yangu. Lakini ukweli utabakia kuwa hivyo, kwamba katika hotpot mume wangu alifungua na kuweka sumu kwenye chakula......
Weka Like.... Mwendo bado unaanzaπ₯°π€.