Mtunzi: @★abuu_lion
№0685086201
Baada ya kusikiliza kisa cha yule dada chote kifupi, nafsi iliniuma sana. Nilimpatia shilingi 30,000 ambayo nilikuwa nimeifanyia kibarua cha kuvuna alizeti kwa siku 4. Hivyo niliona nimpatie yule dada, kisha nikaondoka naye mpaka nyumbani kwetu. Nilimsihi asiwe na wasiwasi kwani siwezi kusema kuwa alitaka kumtupa mtoto—hiyo itakuwa siri kati ya mimi na yeye.
Nyumbani naishi na bibi na babu kizaa mama, hivyo ni ukoo mkubwa na tuko wengi kidogo.
Baada ya kufika nyumbani, tuliingia ndani na yule dada. Nilmkaribisha kwa tabasamu, kisha mama mzazi akanitoa nje faragha kwa ajili ya kujadili.
"Hashim mwanangu, huyu binti ni nani na anatokea wapi? Na kwanini upo naye?" Aliniuliza mama mzazi.
Nilicheka na kusema, "Mama umeuliza maswali mengi sana. Iko hivi, huyu binti ni rafiki yangu sana, nimesoma naye, ila alikuwa amesafiri. Hivyo kipindi anarudi, ndiyo akaona apitie kwa rafiki yake. Kwani kuna tatizo mama?"
Mama akaweka alama ya tabasamu usoni kwake na kusema, "Ok sawa, mimi nilitaka kujua tu yeye ni nani, maana watoto wa siku hizi hamkawii kuzalisha nje bila sisi wazazi kujua."
Mimi: "Sasa mama nizalishe nje na nisikupe taarifa, wakati wewe ndiye msaada wangu? Siwezi bana, haha!"
Mama: "Haya sawa mwanangu, lakini marafiki zako wote huwa unanitambulisha, mbona huyu hujanitambulisha?"
Mmh... niliona kama mama anataka kustukia mchongo, nikageuza maneno na kusema, "Aaah mama, sio wote naweza kukutambulisha mamy."
Mama: "Ok, lakini kuna taarifa hapa imekuja mwanangu—yale maombi yako sasa yametimia."
Nilikaza macho na kumtazama mama huku nikiweka alama ya mshangao. "Taarifa gani hiyo kwanza?"
Mama akaendelea kwa kusema, "Dada yako MERIDA amefanikiwa kufungua duka la nguo za kike, na hana mtu wa kumuuzia. Hivyo amekuteua wewe Hashim. Unatakiwa uende mjini. Hivyo mwanangu nakusihi sana, maana ulikuwa ukililia kazi sasa umepata. Hakikisha unakuwa makini kazini, achana na (uhuni) wa mjini, makundi ya walevi na wavuta bangi. Sihitaji hivyo mimi kama mama yako. Nakuonya."
Hapo tupo nyuma ya nyumba yetu kubwa, mama akiwa anazidi kunipa kama maagizo ya jinsi ya kwenda kuishi huko mjini. Ghafla tunasikia kelele huko ndani tulikomwacha yule dada mgeni niliekuja nae aliyetaka kumtupa mtoto wake. Mmmh... ni kama mtu alikuwa anapiga kelele ghafla, naona watu wanakimbia kutoka nje.
Nilirudi mbio ndani kujua nini kimejiri. Heee! Nilipofika ndani aisee sikuamini nilichokiona! Yule dada niliekujanae nyumbani alikuwa ametapakaa damu mwili mzima, tena akiwa amejing'ata mkono wake mwenyewe, huku akiwa amejichana mkono wake wa kulia kwa meno na akiwa anakunywa damu zake mwenyewe. Kheee aisee! Muda huo mtoto yupo chini analia, huku amekandamizwa na miguu....................
Itaendelea...
Usisahau kulike na kutoa maoni, asanteni..