Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MKASA WA MAISHA YA MWANAMKE MAGRET J MASAMA MWENYEJI WA MBEYA Sehemu ya Kwanza ( 1 )

27th Jul, 2025 Views 5


*************
@Kila Mtu
πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’πŸ’
...............kwa jina naitwa magret j masama") mwenyeji wa mbeya nakumbuka ilikuwa mwaka 2003 nimetoka zangu shamba kuchimba viazi mkononi wa kulia nilikamata gunia la viazi vitamu,uku mkono wa kushuto ukiwa na jembe ,uso wangu ulijaa tabasamu mwanana sio sababu ya kupata viazi vingi laha hasha.
Kulikuwa na sababu kubwa katika maisha yangu sababu ya yote nikuwa nimefanikiwa kuvuka kidato cha nne na kuingia cha tano nilifikiria maisha yangu yanavyoenda kuwa mazuri maana ni kama bahati baada ya matokeo kutoka majina ya watu 7 pekee ndiyo waliofanikiwa kwenda kidato cha tano na jina langu lilikuwepo nikiwa ni mwanamke pekee kati ya wanaume sita waliofanya vizuri uku nikijinyakulia daraja la pili nukta 19 ulikuwa ufaulu mzuri .
fikiria hiyo nafasi wengi waliikosa tulikuwa zaidi ya watu mia lakini Mungu aliweza kuniona sikuweza kuificha furaha ile kila niliyekutana naye aliliona hilo ,nilipanga nikaongee na baba maana yeye kila wakati alikuwa akinidharau ungesikia kuwa"wanawake sio watu wakusoma kabisa apa mtu wa kutegemewa ni Jose"alikuwa akisema baba mara nyingi alikuwa akimpa nafasi kubwa Jose mdogo wangu anayenifatia maana kwenye familia yetu tulikuwa wawili ambae alikuwa kidato cha tatu ,ukiangalia matokeo yake ya kidato cha pili alikuwa na d moja ya kiswahili maneno yale yalinichoma sana katika mtima wangu na juhudi zote niliziamishia katika masomo yangu japo niliweza kukutana na changamoto kila kukicha lakini Mungu alivyomkubwa niliweza kufanikiwa.
Nakumbuka ile siku nilifika nyumbani mida saa kumi na moja jioni nilikuta wageni wakiongea na baba ,niliwasalimia na kuingia jikoni uko nilikutana na mama akiwa anachochea kuni kwa ajiri ya kuivisha makande .
"Mama za muda huu ,leo jambo nina jambo moja linalonipa furaha "nilimwambia
"Jambo gani we mtoto au baba ako kashakwambia teyari maana achelewi navyomjua"
"Hajaniambia chochote mama ila nimefanikiwa kufaulu mtiani wa kidato cha tano
"Shule hiyo unajipeleka mwenyewe nilijua kitu cha maana "aliongea mama jibu hili lilinishangaza sana
AkaendeaKumbe wewe humjui baba ako eeeh maswala la shule si alishakataa tukakubaliana atasoma Jose peke yake imekuaje umefaulu sasa akati haina umuhimu "aliuliza mama
Nilijiliza kutoka moyoni"ivi huyu ni mama angu kweli mbona anaongea kunikatisha tamaa dah sio mbaya subiri nimsikilize baba" nilitafakari mwishoe nikatoa jibu kwaiyo mama wewe unamsikiliza sana baba sindiyo nimejitaidi nimesoma kwa nguvu zote leo mama unanijibu ivi uku machozi yakinitoka nakumbuka sana nililia sana siku hii
Nililia sana siku hii kwa uchungu ,nikijilaumu kuwa jinsia ya kike"Hamna mwanangu usilie baba yako yeye ndo mwenye maamuzi mkielewana utaenda iyo kidato cha tano kama kweli wewe ni msomi"alisema mama uku akiepua makande inaonekana dhahiri mama alimuofia baba na hakuwa na maamuzi binafsi
Mara baba alikuja jikoni"Mama jose wageni ndo washaenda sasa hapa.....gafra! alikatisha maongezi baada ya kuniona nalia. Heeee uyo analia nini kuna msiba au kang'atwa na nyoka "aliuliza baba
"Muulize mwenyewe mbona anajua kinachomliza apo "alisema mama
"Unalia nini mage"aliuliza baba
"Nimefaulu kidato cha nne naitaji kuendelea na shule baba sasa nashangaa mama simuelewi"
"Unataka usome uwe nani magret et mwanangu alikuwa akiongea kwa upole"mpaka nikamlaumu mama ambae muda huo alibaki ametahayari akuamini macho yake ata Mimi nilishangaa
"Nataka kuwa dactari baba maana masomo niliyofaulu yanaruhusu kusomea kozi hiyo"
"Ivi ukiangalia hapa majani ya chai,kuna mwanamke ambae ni dactari katoka Kijiji hiki kaja na mafanikio utaenda kuniletea mimba tu unadhani udactari kama kuchimba viazi "aliongea kwa ukari kidogo
"Lakini baba...." Alinikatisha Funga mdomo wako haraka sana kabla sijaukata
"Inapotokea mtu kaleta barua hapa nikuipokea tu hakuna cha shule wala nini Jose ndo mtoto anayetakiwa apate huduma ya elimu kama tungekuwa na uwezo ila sio wewe magreti wewe ni wa kuolewa tu alisema baba tena ikishindikana ni bora ukaaa nyumbani ukachimba viazi mpaka uzee kama mama ako"alisema kwa ukari mpaka mishipa ya shingo ikawa imemsimama😑😑kwa hasira sikujua hasiri hizi anazitolea wapi ,ilibidi nitoke jikoni na kuwaacha na mazungumzo yano
*************************************Ilipita miezi sasa lakini habari za shule niliishia kuzisikia redio kabisa ,hakukuwa na dalili ya Mimi kwenda shule japo baadhi ya wanafunzi wenzangu walikuwa washaanza kuandaa mazingira lakini sio kwangu mimi "dah nimefaulu lakini sipelekwi shule hii yote ni umaskini na roho mbaya tu katika familia yangu na ubaguzi katika familia angekuwa Jose wangemfanyia hivi lakini sio mbaya nitapambana kwa njia nyengine"siku moja nilikaa chumbani nikiwa nawaza haya lakini sikupata jawabu la mambo haya
Nakumbuka jioni moja nikiwa nimerudi kutoka shamba ,nilifika nyumbani nilikuta ng'ombe wanne na mbuzi watatu wakiwa pale nyumbani,sambamba na vitu kibao
"Aaaah baba kanunua ng'ombe tena pesa kapata wapi inaonekana kuna dili amepiga huu ni utajiri wa wazi hapa kuna dalili ya kurudi shule naiyona "hamna siku niliyofurai kama siku ile ,sikujiuliza mara mbili nilifungua mlango na kuingia ndani ila nilijikuta napata mshangao wa gafra!
Nilikuta wageni wengi tu wakiwa pale ndani haikujulikana kulikuwa na sherehe ya kitu gani kwa muda ule
"Jamani nadhani binti yetu ndo huyo kashawasili tunaweza tukaendelea na jambo letu"nilimsikia baba akiwa waambia wageni ambao wote walijawa na tabasamu.
Nakumbuka mama aliniita jikoni kwa muda ule akaanza kunipa mawili matatu japo sikumuelewa
"Mwanangu unaolewa na leo unaelekea dar es salaam ,kila kitu kitamalizika leo nakuomba usije ukatutia aibu"
"Heeee nilibaki nashangaa sio sababu ya ndoa nilihisi ni ndoto inayoendelea katika maisha yangu kuolewa katika umri huu "ivi mama mbona hamjanitendea aki mnaniuza kama kuku"
Aliniangalia kwa hasira"Naona una nikosea heshima mwanangu umri huo ulitaka uzeekee nyumbani ,hiyo ni kama baraka katika familia yetu tena umepata mume anayejiweza atakulea kama mtoto wake "
"Mama ni wakuongea maneno haya au sio mama angu mzazi anakuwa sawa na baba nilijiuliza "lakini mama mbona Mimi sijataka kuolewa ,nikama baba angu yule"nilimwambia uku machozi yakinilenga
Gafra! baba alikuja jikoni kuongea na mama mawili matatu ,nilipomuona nilitoka nje uku macho yakiwa mekundu nilishidwa ata niongee nao vipi ningeweza kuongea nao chochote nilihisi kama maadui zangu.
Nakumbuka ile siku sikuwa na namna wala wa kuzuia swala like ndoa ilifungwa na rasmi niliweza kuondoka na kuelekea dar es salaam.
Ilipita mwezi sasa nikiwa katika maisha ya ndoa ambayo haijawai kunipa furaha kabisa na niliwaza nilikuwa na mkosi gani kwa Mungu wangu aliyeniumba
Mume wangu akuwa mtu wa kutulia kabisa mara nyingi hupenda kurudi usiku wa manane akiwa amelewa vibaya sana mara nyingi huishia kunitukana tu na huniambia "najua wazazi wako ni tamaa ndiyo iliyowafanya wakuozeshe na kwa kuomba ela sasa hawajambo hahahah kama yatima " ,huongea na sauti yake ya kilevi mwishoe hubaki akicheka cheka najiuliza kwanini wazazi wangu wanakuwa hivi bado hawaliziki bado haikuniingia akilini kama kweli wanaendelea kumuomba licha ya vitu vyote walivyopewa kwenye mahari yangu
siku moja ilikuwa majira ya saa nane na nusu mume wangu alirudi kama kawaida yake "magret fungua mlango umekuja kulala hapa"aliita kwa sauti kubwa uku akinifokea haraka nilifungua mlango kabla mambo hayajawa makubwa
"Wewe ni kama baamedi nimekununua tu mie siwezi oa mwanamke mbaya kama wewe mambo yote kataka mama oa matokeo yake ndo hivi navyokuona kama malaya anayejiuza anasubiria ela yangu ili twende akanipe raha gafra! alinirukia alianza kunichania nguo uku akinitukana kwa matusi mbali mbali ya nguoni sikujua sababu..ya haya yote ........πŸ€”πŸ€” Nyieeeee....Mambo ni ya motooo.πŸ˜‚ Kwani wewe auogopi Usipite bila kulike na kukomeniti fanya ku share kabisa ili sehemu inayofuata isikukose maana ndiyo sehemu balaaaπŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯.
Jamani comment zenu zikiwa nyingi naleta mwendelezo fasta.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MKASA WA MAISHA YA MWANAMKE MAGRET J MASAMA MWENYEJI WA MBEYA Sehemu ya Kwanza ( 1 )  >>> https://gonga94.com/semajambo/mkasa-wa-maisha-ya-mwanamke-magret-j-masama-mwenyeji-wa-mbeya-sehemu-ya-kwanza-1
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest