Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMH SEHEMU YA 40πŸ’˜πŸ’˜

27th Jul, 2025 Views 100



"ushampaka huyo marayaa??" Moyo ukafanya paa nimepakwa nini tenaaa
"Ah mh upo et wapi" Zakia aliuliza kwa kubabaika kama juddy alishtuka ile simu ilikatwa hapo hapo

Ilivyopigwa tena haikuwa inapatikana , walipiga sana simu haipatikani
Alex alikuwa natetemeka analia tu yaan mwanaume alikuwa mwekunduuu sio macho sio usoo

"Kumpaka ninii??" Inno akamuuli, hapo kila mtu alikuwa ameshika shavu lake mama angu ndio amechoka hata kulia wala kuongea amebaki tu kusikiliza

Zakia akatoa kichupa hivi ,vile vichupa huwa vya Jancho au wengi wanaita piko ile , na wengine wanawekea ugolo , akakitoa
Akasema
"Alinipa hii nije kumpaka kwenye unyayo wa mguuu'"

Mungu wangu ,nilitamani nimrukie yaan zakia mie ningekuwa nimeponaaa walai angelala hospital kwa kipigo kikali kutoka kwangu ,nilikuwa natamani niruke nijirusheee hapo alipo kuwa amekaa

Natizama tu macho hata najitahidi ulimi ucheze siwezi kuongea sana nikilazimisha mdomo unaenda upande naaanza kutoka mate nyiee uchawi upo aisee uchawi upoo mimi salma maskini nilikuwa mzimaaa wa afya telaa et leo nimelala kitandani kwa sababu tu nikamilishe furaha ya mtu ambae aliichezea mwenyewe wakati ameikumbatiaa?? Inauma sanaaa

Sijui ile dawa angenipaka mguuni ingekuwaje sijui ndio ningekufa sijui ningezidi kuwa dhoofu hata sielewi

"Alimwambia ni dawa ya ninii??" Mama mkwe wangu aliuliza akiwa kachoka kabisa

"Hapanaaa!!"

"Jamani hapa wakumtafuta ni juddy ,juddy lazima patikane hapaa" inno akasema kwa msisitizo wote wakakubaliana Alex akasema nitamtafuta hata akiwa kaburini nitamtoa huko

Mama yangu akasema naomba Salma niende nae nyumbani, hakuna haja ya yeye kuendelea kuwa hapa"

"Nitamchukua mimi, naomba hiyo nafasi salma tayari amebadili dini naomba Nianze nae maombi ya kiroho naamini atafunguliwa kila sehemu" mama mkwe nae akanitaka , lakini mama akakataa kabisa hawezi kuniacha

Inno na alex pamoja na baba mkwe alimuomba mnoo mimi nikahangaikiwe kule ukweni kwangu
Kishingo upande alikubali , siku hiyo hiyo waliomba ruksa ,nikaruhusiwa kutoka , yaan mie nabebwa nimelegea kila mahala ..

Nilifikishwa nyumbani kilitengenezwa chumba kwa ajili yangu aliletwa doctor wa kuwa ananinyoosha misuli na kunipa.huduma zingine hapo hapo nyumbani walau kufanya viungo vyangu viwe haii
Zakia hakuachwa aondoke ,alikuwa benet na sie walisema mpaka atakapo patikana juddy ndio ataachiwa

Zilipita siku tatu nafanyiwa maombi ya nguvuu ya kuvunja na kuteketeza uchawi watu hawalali usiku wote wanakemea, sikuona hata dalilii

Mama mkwe aliwaambia kina alex wamtoe zakia hataki kumuona anaweza muwekea sumu hata, ilibidi zakia afukuzwe hapo , huku juddy alitafutwa kila kona hakuwahi kupatikana

Siku zote nilikuwa naamini mwezi hauta isha mimi nitakuwa nimeinuka Kitandani nina furahia na alex wangu
Uliisha mwezi sina dalili hapo kitandani , Jitahidi za kila rangi walifanya
Ikawa miezi miwili , hatimae tumbo nalo likawa linakuwa mwanzo mama mkwe alisema labda ile mimba itolewe tu aisee nilipo sikia Sikia hii kauli nililiaa mbona walikoma akaja na kuniomba msamaha akasema anaona kama nateseka moyoni nikasema watoto wangu wanaendelea vizuri sa kwanini wawauwe??

Kila tarehe yangu ya Clinic alikuwa anakuja nesi hapo ananipima maendeleo mazuri anasema , nilikuwa nakonda kwa mawazo nawaza hii hali mpaka linii
Alex aliisha kipenzi changu alikondeana alikua kama kichaa hata kuchana tu nywele ilikuwa kazi

Maombi na maombi kila mahala mie nilifikishwa , mpaka manabii wa nigeria sijui wapi kote nilipelekwa na wengine walikuja nyumbani pale lakini hakukuwa na dalili salma mie kama kesho nitainuka

Hakukuwa na taarifa zozote za judy wala zakia maana baada ya siku chache walimfata zakia kwako wakaambiwa hajulikani alipo aliandoka tu bila hata kuaga, nikawaza huu ndio mwisho wangu umefika pengine nitafia hapa kitandani ile siku najifungua au hata siku ya kujigungua isifike nikafa mie

Alex alikuwa karibu mno na mimi asubuhi ananiweka kwenye kiti kile cha mataili ananitoa nje , ananiambia mke wangu umekaribia kupona mke wangu utakuwa na afya tutafunga ndoa baada tu ya wewe kujifungua
Mke wangu, tunakuwa na watoto wetu mapacha mungu ametupa baraka uzao wetu wa kwanza kabisa huu

Basi ananipigisha story nasikia vya kucheka nacheka lakini sasa ndio moyoni usoni nipo tu kawaida ..

Tumbo nalo lilikuwa miezi 6 watoto wangu wanacheza humo nawasikia kabisa ilikuwa mimba yangu ya kwanza natamani kumwambia alex embu shika uone mateke ya watoto wako lakini naweza vipii siwezi hata kidogo naishia kulia tu kwa huzuni mabayo ilitakuwa kuwa furaha , hapo nilikuwa nimeandikiwa tayari Operation, yaan nitajiungua kwa Op

Alex alikuwa akibahatisha wakati kashika tumbo anasikia wanacheza anafurahi ananipongeza anasema salmaa anakuumiza mi natabasam tu sijui kama hata alikuwa anaona tabasam langu ...

Mama yangu mzazi akasema ataanza kutafuta maostaz nitibiwe kiarabu mama mkwe akawa mbishi sana anasema tusichanganye , tunakuwa kama tunamchanganya mungu , lakini alex akasema yaan chochote kitafanywa , ilimradi salma ainuke hata kuroga au kuwanga nitawanga bado natafuta mganga wa muijiza huo

Mungu ndie anajua ipi njia sahihi n tunachofanya hatudhuru mtu sieee!!
Kishingo upande mama mkwe alikubali maana huyu mama na yesu ni kama mapacha humwambii kitu...

Siku moja alikuja subira mdogo wangu akanambia yaani dada leo nina furaha sanaa nikamuuliza kuna jipya gani mdogo wangu?? Hapo nauliza tu moyoni sina hata uwezo wa kufungua mdomo

Akanambia dada huwezi amini baada ya kipindi chote inno amenambia ananipenda , hahhah nilicheka sana hicho ndio kitu nilikuwa natamani mno kukisikia mnooo
Kumbuka hapo nacheka hakuna anaeona mie nacheka, yaan mie nafs yangu ni mzima kabisa mzima kabisa sijui tu kwanini siwezi kujitigisha
Kanambia et tufunge ndoa hivi karibuni alisema atakuja kukuambia lakini mi mbeaaa"
Basi akanihadithia alivyoambiwa hapo mi nafurahi kweli hatimae mdogo wangu amepata mwanaume sahihi sana kwenye maisha yake alinambia dada mi siolewi mpaka wewe uamke hapo ,
Dada mkubw analinga sana kasikia sasa hivi tunamaisha mazuri et ndo anapiga simu kila siku mnafiki kweli "

Moyoni nikasema msamehe tu ndio dada yako hakuna njia hapo...

Subira aliondoka baada ya kupiga story akanambia biashara inaenda vizuri ameongeza mtaji umekuwa mkubwa na ameongeza mpishi mwingine ambae anapika vyakula vya kirusi et akanambia wanaoda mpaka za watalii alex aliwaunganisha na wateja wengi sana wale VIP
Nikamshukuru mungu...

Baada ya subira kuondoka , muda kidogo tu alikuja inno akawa amekaa pembeni yangu alinitazamaaaa afu akani kiss shavuni akanambia hichi tu naomba nifanye na usinikasirikie , nilicheka kaanza visa vyake sa ndo nini kunibusu mie shemeji yake

"Nampenda subira unaniruhusuu??" Nilifumba macho kusema ndio
"Asante salma ,Hope uinuke hapo haraka mana kasema hataki tufunge ndoa mpaka wewe uwepo kwenye harusi ucheze mpaka basii "

Helllo Vipenzi mkasa wetu wa Bibie Salma umekuwa mrefu kidogo namie naomba niishie hapa kwa muda , Na huu ni msimu wetu wa pili wa mkasa huu naomba tukutane msimu wa tatu ambao utakuwa msimu wa mwisho kabisa wa mkasa huu ...

Salma atajifungua akiwa bado yupo hapo kitandani ama itakuwaje
Vipi kuhusu juddy na zakia ...

HUU NI MWISHO WA SEASON YETU YA PILI

10 KAMILI JIONI.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMH SEHEMU YA 40πŸ’˜πŸ’˜  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilizani-mwizi-kumbe-mmmh-sehemu-ya-40
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest