Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

MPENZI WA DADA S2 SEHEMU YA 36__37

27th Jul, 2025 Views 34



MTUNZI : RITHA STORIES

WHATSAPP 0763 826152

FB RITHA STORIES &HADITHI ZA RITHA

SONGA NAYO..................

Nilimaliza nikatoa vyombo nakuingia chumbani bila hata kuongea nilipanda kitandani na kujilaza, kimya kilipita huku tukiwa tumepeana migongo.
Kwa namna kichwa changu kilivyokuwa na mambo mengi sikutaka kujisha kuongea, dakika kadhaa zilipita Julie akaniita na kusema.

"Kwa hiyo umeamua kutoka na Felix?"

"Julie! mimi Sina uhusiano wowote na Felix naomba uelewe basi"

"Huna uhusiano nae ila unampenda ?"

"Haina maana ila haiwezi kuwa "

"Mmmmh! Yangu macho mie ,ila sio mbaya kama ukitoka nae "Sikutaka kumjibu nikachukua shuka nikajifunika tayari kuutafuta usingizi.

Usiku ulipita kesho yake asubuhi niliamka mapema nikajiandaa na nilipokuwa tayari nikamuaga na kutoka nje , ajabu nilikuta gari la Felix likiwa limepark.

Sasa sikutaka kuongea nae hivyo nikalipita kwa mwendo wa haraka , Felix alishuka na kunifuata kwa kukimbia , bahati mbaya nilikuwa nimevaa viatu virefu hivyo nikaona bora nisimame.

Felix baada ya kunifikia akanambia " Lolah! kwanini unanikimbia ?"

"Nadhani unajua kwanini, mh nimesimama ongea nikusikie"

Felix alishusha pumzi na kusema " how was your night "

"Good ,sijui wewe"

"I'm fine , sorry kama hutojali tunaweza kuingia kwenye gari maana nimekufuata ili nikupeleke kazini"

Nilitaka kukataa ila nikamuona Julie akiwa juu anatuangalia, sasa sikutaka aelewe lolote maana kwasasa simuelewi.

Basi tuliongozana na kuingia kwenye gari baada ya kufunga mkanda akawasha gari tayar kuelekea kazin, kimya kilitawala nikabaki nikiangalia nje .

Safari iliendelea tulivyofika mbali na nyumbani nikamwambia " Felix simama " bila kuniuliza akatoka nje ya bara bara na kupark , baada ya kupark akaniuliza.

"Kuna nini why umetaka nisimame?"

"Nataka tuongee "

"Okay ,tunaweza kuongea ukitoka kazin maana mda huu ni mda wa wewe kuwa kazin "

"No saizi ni bora, Felix naomba ukae mbali na maisha yangu "

"Una maana gani kusema nikae mbali na maisha yako?"

"Acha kuniuliza maswali ambayo majibu yake unayo, sikia Felix haya mambo ya mapenzi siyataki wala sipendi kuona ukinifuata fuata"

Felix alikuna pua na kwa sauti ya upole akasema " nilijua yameisha kumbe bado, ona Lolah tutakuwa tukirudia hii mada kila siku ila bado itabaki pale pale kuwa mimi na wewe tuko pamoja"

"Mko pamoja na nani?, Felix nimesha sema you and I we will never ever be together so please niache "

"Never ever!! unaongea haya maneno ukiwa unajisikia kweli au unaongea out of anger ?"

"Ninaongea nikiwa serious Felix, so natumai kuona ukisikiliza sauti yangu na ukae mbali"

Niliongea na kutaka kushuka akanishika mkono huku akiwa ameweka uso wa serious na kusema " Lolah! Naweza kusikiliza lolote na kufanya chochote kutoka kwako ila si hili.

Siwezi kukuacha wala kukaa mbali nawewe and nikukosoe wewe na mimi hatuwezi kuachana ,tutakuwa pamoja leo kesho na hata milele "

"No haiwezi kuwa, Felix wewe ni shemeji yangu nitakuwa mjinga kama nitaingia kwenye mahusiano na wewe .

Kwanza umesha kaa ukafikilia kuwa familia yangu italichukuliaje hili swala au unafanya vitu kwa mihemko?"

"Sijawahi wala staki kufikili lolote kwasababu wewe ni wangu,na nimesha kwambia kuwa siogopi neno wala hatua za mtu .

Na kama kuwa nawewe ni kosa basi niko tayari kulifanya bila kujali adhabu wala madhala, so wazo la kutokuwa na mimi ulifute coz I'm yours forever "

Aliongea na kuniachia mkono, haraka nilishuka na kwenda kupanda bajaji, Felix baada ya kuona nimepanda bajaji aligeuza gari na kuondoka.

Kutoka na kuwa karibu nilitumia mda mchache nikafika, kama kawaida niliwasalimiana wenzangu kisha nikaingia ofisini kwangu.

Kufika nakashangaa nakuta kuna breakfast ikiwa mezani tena ilikuwa na vitu vinono kuliko hata ya jana, na pembeni kulikuwa na maua kama yale ya jana .

Nilikumbuka jana Vice alisema ilitoka kwa Felix ,haraka nikageuka ili nikamuulize leo imetoka wapi ila akawa ameingia huku akimung'unya lollipop 🍭 .

Nilimsalimia na kumuuliza " Vice hivi vitu vimetoka wapi?"
Vice alitoa lollipop yake mdomoni akanipa huku akisema " Shika hii pipi kwanza naona utamu wake unanifanya nisisikie vizuri, mh umesemaje "

Nilimuangalia kwa hasira maana anajifyatua kama jinga 😏, alivyoona niko kimya akaniuliza "bibie mbona unaniangalia jicho la uke wenza, ongea nikujibu nikafanye kazi zangu mie"

Nilishusha pumzi na kusema" nimekuuliza hivyo vitu vimeletwa na nani?"

"Oooh! kumbe ulikuwa unasema hivyo, aam kama jana tu Mr miraba minee ndo kaleta "

"Vice kuwa serious basi,Felix nilikuwa nae mda si mrefu nawezaje kuwa yey?"

"Kumbe mr miraba minne anitwa Felix sio mbaya , mh turudi kwenye mada ,bidada hatuko miaka ya mababu tuko kizazi janja so usijifanye kama hujui mambo ya derived.

SEHEMU YA 36

Kwanza mda si mrefu kinakuja kingine kutoka kwa our boss so my future madam naomba nichukue hicho cha Mr miraba minne maana huna tumbo la kula vyote."

Bila hata kupewa ruhusa alisogea mezani akachukua vitu vyote na kuondoka, nilibaki nikimsindikiza kwa macho hadi akapotea.

Jamani huyu Vice ni spy wa kampuni yaani hakuna kitu au taarifa ya mtu asioijua kila mtu anataarifa zake, na cha kujiuliza anajuaje maana mda wote yukogo bize na kazi.

Na ukija kwenye suala la kazi anaipenda sana kazi yake hakuna mfano, kiufupi kati ya wanaoshika namba za juu kwa uchapazi yeye humkosi.

Basi taratibu nilirudi kwenye kiti changu na kukaa,mara ukaingia ujumbe kutoka kwa Felix kufungua ujumbe ukawa unasomeka.

,"usiwe na hasira ,kula kwa wakati na fanya kazi kwa umakini tutaonana baadae love you."

Niliweka sm pembeni bila hata kujibu lolote , kichwa kilijaa mawazo sana , moyo ulitamani sana kulipokea pendo lake lakini kila nikifikilia familia yangu nachoka.

Nilikaa na kujikuta nazama kwenye dimbwi la mawazo, sasa wakati nikiwa katika kuwaza mlango uligongwa nikaruhusu mtu anaegonga kuingia.

Baada ya kuruhusu mlango ulifunguliwa akaingia kijana akiwa na breakfast iliyotoka kwa Mr Abel, akasalimia na kuweka mezani kisha akaondoka.

Dakika kadhaa mlango ukagongwa tena kuruhusu akaingia Mr Abel ,,haraka nikaondoa mawazo na kuweka tabasamu pana usoni.

Mr Abel alifika na kuvuta kiti akakaa na kunisalimia kisha akaniuliza " jana ulikuwa bz sana maana nilikutafuta sana ila haukupokea wala kujibu text zangu"

"Ulinitafuta!!?"

"Yeah "

"Mh! huwezi amini sijaona simu wala ujumbe wowote kutoka kwako"

"Acha matani,mi nusu saa baada ya kuachana na wewe nilikutafuta na mida ya saa nne nikapiga na kutuma ujumbe ila ukawa kimya "

Nilishangaa na kuchukua sm nikaangalia mara mbili mbili sikuona ujumbe wala missed calls , kwa ushahidi akanionesha kwake kweli ilionesha amenitafuta.

Sikutaka kuichosha akili yangu maana nilihisi itakuwa mtandao, basi aliniongelesha kidogo kisha akaomba kuondoka huku akinisihi kunywa chai kwanza .

Niliitikia sawa huku nikitabasamu , na baada ya kuondoka macho yangu yaligeukia sm yangu ambayo ilikuwa ikiita.

Niliingalia huku mapigo ya moyo yakienda mbio, jamani simu ilikuwa ikitoka kwa mama , kwa upole niliichukua nikapokea na kumsalimia"

"Shikamoo mama"

"Shikamoo na wewe kama ni mali, hivi hadi sasa umefikia wapi au ndo umeamua kujitenga na familia yangu"

"Samahani mama ni.....!" Hakutaka kusubiri nimalize kuongea akakata sm, niliinamisha kichwa kwenye meza huku nikikuna kichwa.

Mda huo huo ukaingia ujumbe kutoka kwa mama ,kinyonge nilifungua na kusoma , ujumbe ule ulisomeka hivi.

"Kwanzia leo tafuta mama mwingine na sio mimi tena , na usije kukanyaga nyumbani kwangu mpuuzi wewe"

Nilikosa cha kujibu nikaweka simu pembeni na kufuta machozi yaliyokuwa yakinitoka .

FULL TSH 1000 NAMBA YA MALIPO 0763 826152 JINA MODESTA KUDUHU.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MPENZI WA DADA S2 SEHEMU YA 36__37  >>> https://gonga94.com/semajambo/mpenzi-wa-dada-s2-sehemu-ya-36__37
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest