Mama loveness alinikaribisha nilijua kafanya vyote hivyo ndani ya nyumbani kufagia na kupiga deki ili tu apate cha kunisema . Nilitulia kamaa nimenyeshewa na mvua na sikuwa na jipya la kusema zaidi ya kujua kuwa nimeshayakanyaga kwa mama mwenye nyumba..
Hapo hapo Mzee makani aliamka na kutusalimia " habari za asubuhi" mimi nilimuamka na mama alimjibu na kuanza kunisema kwa mafumbo . " Baba loveness sikuizi wa miliki wa nyumba mmekuw wawili?
" Kivipi mke wangu,mbona sikuelewi?
" Wewe unaamka saizi na mfanyakazi wako naye ana amka sahizi. Sisi ndo tudeki , tuoshe vyombo.
" Mke wangu sikuelewi ?
" Namaanisha yaani huyu maiko uliyemleta analala kiasi kwamba kazi tunafanya sisi?
" Mmmh mke wangu atakuwa kapitiwa tu.
" Wewe kazi yako ni kumtetea tu ,unamlemaza."
" Hapana mama kweli ni bahati mbaya"
" Kelele siongei na wewe! Naongea na mmiliki wako"
Ilibidi nikae kimya mpaka pale mzee makani aliponiamuru niondoke na yeye atazungumza na mke wake. Niliondoka na kwenda kumwagilia bustani . Muda huo naye Loveness anatoka nje ..mimi nilikuwa mbele kidogo ya ngazi na yeye alikuwa ndio anazishuka.Sasa alizikanyaga vibaya zile ngazina kujikuta anataka kuanguka .
Nilimdaka kwa kumshika kiuno ili asianguke .Akawa ananitazama na mimi namtazama yaani macho kwa macho . Hapa ndipo nilipogundua kitu kuwa huyu loveness ni mrembo kuliko kawaida kwa mbali ni wa kawaida ila kwa hapa hapana SHE IS SO BEAUTFULLY ( Ni mrembo haswa)
Sio macho sio mdomo hata kashingo laiti ningekuwa vampire damu yake ni halali yangu.Tulitazamana na hapo kila mtu anawaza vyake ni ngumu kuvisema kwa kuwa tuliangaliana sana. Baadaye akili zilirudi alijitoa kwangu haraka na kusema kwa hasira.
" Nani alisema unishike kiuno?
" Nilikuwa nakusaidia love"
" Ndio unishike kiuno"
" Samahani bossi lady"
" Okay usirudie tena"
" Sawa nimekuelewa"
Alivaa vizuri kiatu chake lakini mguu ulikuwa kama umeteguka. Alikuwa anatembea vibaya vibaya akataka kuanguka niliwahi na kumshika nikamnyanyua mpaka kwenye gari nikamkalisha siti ya mbele na kumshika mguu.
" Buana niachie mguu wangu niko sawa"
" Hapana hauko sawa "
" Kwani we inakuhusu nini? Au inakuuma nini ?
" Kwa sababu wewe ni mtoto wa bosi wangu"
Alinitazama nilimshika mguu na kuanza kuunyosha taratibu " asiii aaaaam naumia fanya taratibu jamani" nilikuwa nauzungusha ili ukae sawa . Nilipomtazama usoji alikuwa anadeka kama katoto kadogo.Nilitabasamu na kumwambia " kumbe we ni mrembo hivi"
" Nyosha mguu acha mazoea na mimi"
" Tayari unaweza kwenda , siku nyingine uwe unatembea vizuri"
" Toka hapa ! Sitaki mazoea na wewe "
Basi nilimpisha akafunga mlango na kuliwasha gari kisha kutoka nje taratibu lakini macho yake kwangu na yangu kwake yani tulikuwa tukitazamana nikajisemea" huyu lazima awe wangu" Nilirudi na kuendelea kumwagilia maua kwenye bustani ambayo unaweza kusema ni edeni ndogo yaani maua ya kila rangi....
Hapo hapo baba mwenye nyumba mzee Makani alitoka akiwa kanyonga zake suti na kuniambia kuwa anawahi kwenye mkutano na kuhusu suala la mama tumwshalimaliza . Nilifurahi na nilimshukuru kwa upando wangu kwake . Ni mtu anayenipambania niendelee kubaki kwa kuwa namsaidia vingi....
Baada ya yeye kutoka tulibaki mimi na mama loveness .niliendelea kuweka mazingira bora zaidi na ndio kazi yangu inayonipa uraji lazima niifanye kwa weledi mkubwa sana.
Lakini nikiwa pale nilimsikia mam akipiga kelele ndani msaada nilitoka mbio na kuacha mpira na mkasi wa kukatia majani mbio mbio kuelekea ndani . Nilipofika nilishtuka nilichokiona ...........
FULL 1500
0699286085.