Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

MJEDA TARATIBU BASI SEHEMU YA SABA

27th Jul, 2025 Views 60


Namba ya WhatsApp- 0683944333
________________________________________

Tulivyoshuka tu mbele yetu, tukamkuta, baba Sophia na Saphina, alikuja kunipa barua ya kazi niliomba kazi ya ualimu shule binafsi, kupitia baba Sophia mkoa wa Kilimanjaro, tulipata kazi Mimi na Sophia, Saphina yeye alisomea unesi, sisi ualimu wa shule ya msingi, na Mungu kawa upande wetu, tumepata kazi shule Moja...

Sikuwa na simu ya kueleweka kile kisimu changu kilizima toka juzi, nimepigiwa simu, hawakunipata, hii kwetu ilikuwa habari njema, japo huzuni kukaa mbali na familia sijazoea, hili swala mwanzo mjomba alikuwa ameshalipinga lakini kutokana na matatizo yaliyotokea aliona bora niende mbali watakuwa wanakuja kuniona...

Ilibidi shangazi apewe mkanda mzima, muda huo nilikuwa chumbani, sikuwa tena mtu wakucheka kama mwanzo, alivyosimuliwa tu, ata hakuweza kuvumilia hajazima hapo hapo, tukiwa tunatoka kumrudisha hosptal...

Mjeda akafika mbele yetu, aisee binamu zangu walishindwa kuvumilia, wakataka kumvaa mjomba akawazuia na kusema, " kijana naomba utoke nyumbani kwangu mara moja uliyoyatenda yanatosha...

Mzee naelewa, sijaja kwa ugomvi, nimekuja kuwaomba radhi, ukweli sikukusudia ni hasira tu, nimekaa nimetafakari nikaona nimefanya kosa kubwa sana, Mimi hata sikutaka kusikia chochote nilimwambia Isa, anisaidie tumuwahushe mama, wanao sikiliza huyo shetani, wabaki Ili afanye mauaji kabisa, niliongea huku nasaidiana na Isa...

Binamu zangu wakubwa, walikuwa wakimtizama Kwa chuki mbaya mno, wakati tunahangaika ety akaja kunizuia, aisee nilimuweka ngumi ya tumbo, lakini kwake ata haikuwa na nguvu aliushika tu mkono wangu, huku ananitizama...

Toka nijitambue sijawai kuomba msamaa kwa yeyote, ila Kwa sababu yako, LLleo niko hapa kuomba msamaa usinipuuze, Isa hasira ilimpanda, akaokota jiwe akamtwanga nalo, aligeuka tu akamtizama, hakumrudishia kama anavyofanya siku zote...

Aligeukia familia nzima nakusema, kama kunipiga kutawapa furaha nipigeni, sitorudisha ata ngumu moja kwenu, Kila mtu alimpita tukapanda usafiri nakumuacha, kwangu ilikuwa maumivu makali,nilijikuta nakumbuka maumivu, na bado sijapona vizuli natembea kama ninavidonda katikati, najikaza tu kwa sababu ya shangazi...

Lakini kabla hata hatujaondoka, shangazi alipata fahamu alivyoniona tu, akanikumbatia huku analia, tulishuka kwenye usafili turudi tu ndani, bado mjeda alikuwa kasimama pale pale, na leo alikuwa na kofia kabisa ya kijeda, mama alijua moja kwa moja ndo muhusika, alimsogelea binamu Juma, akavuta kisu kutoka kwenye kiuo, Juma huwa anatembea na kisu muda wote na ndo kijana mkubwa...

Wakati mjomba ameshasoma akili ya mke wake, anakimbia kumuwahi, tayari shangazi alimkita kisu Cha mbavu mjeda,na alitaka hata kumuongeza kingine, ilibidi wamtoe shangazi kwanza na mjeda aliondoka uku anachechemea...

Tulikaa ndani Kwa hofu siku hio mimi na mama na Sophia tulikatiwa ticket tuondoke na binam Juma mpaka Moshi kituo changu Cha kazi, hatukuwa tumejiandaa ila Kwa hili tibwili lililotokea, pesa zilichangwa chap chap tukaondoka...

Wanaume wabaki Sasa kuendelea na msala uliotokea, tulisafiri kimya kimya mpaka moshi mjini, tulianzia Kwa shangazi yake Sophia, tulikaa Kwa siku tatu huku tukitafuta chumba cha kupanga tukashauliana tushee chumba Ili tuchangie kodi, kupunguza gharama...

Juma aliondoka kurudi nyumbani, tukabaki watatu Mimi mama na Sophia tuliamua kuchukua chumba na sebule self,tulianza maisha, Kila tukipiga nyumbani wanasema kuko shwari zilipita wiki mbili, tunatakiwa kulipot kazini...

Tayali nilikuwa nimeshapona ila moyoni bado nilikuwa naugulia,sikuwa tena natabasamu, ni mpaka nijilazimishe, shangazi alijitahidi kuniweka sawa..

Niligiza Niko sawa mbele yake Ili kumpa amani, mwanzo nilitamani kujiua, ila nilivyoona Hali ya shang'azi nikaogopa anaweza kufa, alionesha upendo wake kwangu Kwa ukubwa sana, kuliko hata mjomba wangu alieshare ziwa na mama...

Niliona naweza kusababisha binamu zangu wakawa yatima kama Mimi, tena ila Mimi nimepata upendo mkubwa utazani Niko na wazazi wangu, vipi kuhusu wao, watapata wapi mlezi bola, niliamua kujikaza nisogeze tu siku...

Upande wa nyumbani, mjomba alisubili timbwili wapi, wakahisi huu ni mtego, tukisahau waje kulipiza, Kila mtu aliwaza lake kichwani mwake, upande wa mjeda alikuwa anauguza jeraha lake, halikuwa kubwa sana kisu hakikupenya sana, alikuwa kashaanza mpaka mazoezi...

Aliwaza arudi tena, nafsi yake ilikuwa iki muuma mno, na kile alichokifanya kilikuwa kikimrudia Kila siku, na kutengeneza hisia zaidi...

Hakumshilikisha hata rafiki yake wa karibu,alipambana na janga lake mwenyewe, alifunga safari mpaka nyumbani, watu walikuwa waamesambaa hata Juma na Hussein, binamu zangu wakubwa walikuwa wameshaondoka kurudi makazini kwao...

Alifika nyumbani akakuta watu wote wako ndani, akagonga mlango....

Itaendelea...οΏ½οΏ½
Full sh 1000

Njoo WhatsApp 0683944333.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MJEDA TARATIBU BASI SEHEMU YA SABA  >>> https://gonga94.com/semajambo/mjeda-taratibu-basi-sehemu-ya-saba
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest