Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

A.J.A.D SE03 EP02

27th Jul, 2025 Views 7



By Simon Thrteen|EsyDady
@EsyDady (Social Media)
+255620250249 WhatsApp

**********

Lisa alikuwa anaendesha gari kama kichaa, mwendo aliokuwa anaendesha haukuwa kawaida. Kichwani kulikuwa na wazo moja tuu la kutoroka nchini ili kwenda kuishi mbali na baba yake. Kila mara alikuwa anageuka nyuma kuangalia kama kulikuwa na anayemfuata nyuma.
Vijana wawili waliokuwa wamevaa kofia ngumu, wakifunika sura zao, walikuwa juu ya pikipiki kubwa wakiendesha kwa mwendo wa kawaida. Mmoja ambaye alikuwa kama abiria alikuwa na kifaa fulani mkononi, kifaa hicho kilikuwa na ramani maalumu ya mji, na kwenye hiyo ramani kulikuwa na kidoti chekundu sehemu fulani ya mji.
Wakaenda moja kwa moja mpka nyumbani kwa Lisa, tayari kikiwa ni kigiza cha saa moja hivi usiku. Yule aliyekuwa na kile kifaa akashuka kwenye pikipiki na kuelekea nyuma ya nyumba ambako kulikuwa na giza zaidi na taa hazikuwa na nguvu zaidi, wakati yule mwenye pikipiki akisogea mbali kidogo na kusimamisha pikipiki.
Yule aliyezunguka nyuma, akatazama kulia na kushoto na kisha kama nyani akarukia ukuta na bila kugusa zile waya za umeme zilizokuwa kwenye ukuta huo wa uzio, akatua chini bila kufanya kishindo. Na kwa kasi akakimbilia kwenye jumba la Lisa, akatazama kile kifaa akiwa amejibanza kwenye ukuta wa nyumba, kile kidude kilikuwa palepale, na kwa kutumia kifaa fulani akafungua mlango wa uani na kuingia ndani.
“Am in!” akaongea kwa sauti ya kunong'ona huku akiendelea kusonga mbele kuzikata kordo na mkononi alikuwa na bastola yenye kiwambo cha sauti. Akaelekea moja kwa moja kwenye chumba cha Lisa na kuusukuma mlango taratibu, peupe. Akatupa macho yake kitandani akaiona simu ya Lisa, akakema kwa hasira akimalizia na tusi kubwa.
“Hayupo, simu iko ndani Lisa hayupo!” akaongea jamaa huyo baada ya kumtafuta Lisa kila mahali na hakuwepo. Kama alivyoingia ndivyo alivyoondoka jamaa huyo, tayari nwenzake alishasogea karibu akadandia pikipiki na kuondoka.

*****

“Kwanini babaako anataka kukuua Lisa! Kuna nini kimetokea?” akauliza Claude akimtazama Lisa kwa mshangao.
“Claude, babaangu ni shetani, yule mtu ni shetani, kuna siri yake nimeijua ambayo sikupaswa kuijua na sasa najua atataka kuniua, na mimi sina mahali pengine salama pa kukimbilia zaidi ya hapa. Japo najua hapa napo hashindwi kutuma watu wake kuja kuniua!” akaongea Lisa kwa hofu kubwa na macho yake yalokuwa na machozi.
“Sawa basi usilie Lisa, kama tatizo ndio hilo, basi limeisha!” akaongea Claude na kumkumbatia Lisa akiendelea kumbembeleza mpaka alipopoa akatulia. Ingawa bado Lisa alikuwa na hofu kubwa lakini kifuani mwa Claude alijihisi yuko salama mno.

*****

“Amewatorokaje mtoto wa kike ambaye hata kuua panya hawezi? Lion, Tiger! Mmeanza kuwa mdebwedo ee??!” akauliza mzee Alfred akiwatazama vijana wale wawili ambao walikuwa wakifanana mno, na bila shaka walikuwa mapacha.
“Boss! Lisa hajatutoroka, ni kwamba wakati tunafika tayari alikwishaondoka, tumefuatilia simu yake na ndio tuliyoipata chumbani kwake, na yeye hakuwepo! Lakini usijali, nimebandika camera ya siri ambayo atakapoingia tuu nyumbani kwake tutamuona!” akaongea mmoja wa vijana hao na kumuonyesha mzee Alfred kupitia kile kifaa alivhokuwa nacho, kulikuwa na picha zinachukuliwa kutoka sebuleni kwa Lisa.

*****
Claude alikuwa chumbani kwake, na hii ni baada ya kuhakikisha Lisa amepata usingizi kwenye chumba cha wageni. Hakutaka kabisa kuuliza kuhusu zile picha, hakutaka kamwe kufungua ukuta uliokuwa unaziba maji ya mto akihofia dhoruba la maji.
“Huyu mzee naona sasa anataka kunipanda kichwani, atakuja kunisababishia hatari ambazo sikutaka kuziona kwenye maisha yangu! Ni lazima nifanye mpango wa kumnyamazisha kabla hajaninyamazisha mimi. Lisa pamoja na kwamba kwasasa hatuna maelewano mazuri, atabaki kuwa ni mwanamke ambaye nilimpenda na akanipenda kweli! Hili sio lake pekee yake ni la kwangu pia!” Claude akatolewa mawazoni na simu yake iliyopata uhai.
“Claude! Umeshalala?” sauti nyororo ilisikika masikioni mwa Claude, Alikuwa ni Vicky.
“Bado sijalala mamaangu, nilikuwa na kazi nafanya kidogo hapa!”
“Oh! Claude umeniita mama? Jamani natamani ungeniita hivyo kila siku, yaani najiona kama malikia na wewe ndio mfalme wangu, Claude utanipasua bichwa langu jamani!” akalalamika Vicky simuni.
“Vicky! Wewe ni mmoja kati ya watu wangu wa muhimu sana, japo tumejuana kwa muda mfupi huu lakini ukweli ndio huo kwamba wewe ni mwanamke wa muhimu sana kwangu!”
“Asante Claude, nilitaka tuu kukusikia na nijue unaendeleaje! Halafu kabla haujalala hapo mezani kwako kuna kitu niliweka hapo, kama utakipenda unipigie, usiponipigia nitajua haujakipenda! Kwaheri!” akaongea Vicky na kukata simu. Na ndipo haraka Claude akatazama mezani, na ndipo akaiona bahasha ndogo, haraka akaichukua na kuifungua. Akatabasamu baada ya kutazama kilichokuwa ndani ya bahasha hiyo, kisha akairudisha mezani na kujitupa kitandani.
Na hapo ndipo jambo lingine likaingia kichwani mwake, Joseph Steven.
“Huyu mzee hajui mateso na maisha niliyoyaishi mpaka kufika hapa, alikuwa wapi siku zote mpaka kuja leo na kusema eti yeye ni babaangu! I don't need him! Abaki huko na watoto wake wengine ambao wanamhitaji but for me babaangu ni babu yangu mzee Claude, ingawa sikuwa naye kwa muda mrefu lakini kwa muda huo ninamkumbuka kwa vingi sana ambavyo vimenifanya niwe imara mpaka sasa, na sio huyu mzee ambaye hata sijui anatoka wapi!” akawaza Claude na mwisho akapitiwa na usingizi akalala.

*****
Ilikuwa ni asubuhi tulivu, wakati Vicky alipoingia ofisini, lakini bado hakukuwa na simu yeyote kutoka kwa Claude. Akairudisha simu kwenye pochi na kuendelea na kazi, lakini kila mara aliitazama simu yake kama kuna chochote kinaweza kuingia.
Wakati hayo yakiendelea kwa Vicky, upande mwingine Claude yeye aliamka asubuhi na mapema na kwa kutumia gari yake aipendayo ambayo ina historia kubwa ya maisha yake ya Ford Ranger nyekundu, aliondoka na safari yake ilikuwa ya mwendo wa taratibu tuu akielekea mtaa ambao alikuwa amekulia akiishi na bibi yake. Mbele ya gereji moja ambayo ilikuwa ikitengeneza magari na vyombo vingine vya moto ndipo ilikuwa breki yake. Akashuka na moja kwa moja akaingia ndani, akatazama mazingira ya gereji hii na kumbukumbu nyingi za maisha yake ya utotoni zikarejea upya.
“Nikifika hapa huwa nakumbuka maisha magumu ambayo niliyapitia nikiwa hapa, nililala njaa, nilitukanwa, nilisimangwa na hata kupigwa wakati mwingine. Namshukuru sana Thom, alinisaidia sana yeye na babaake kabla hajafariki!” akawaza Claude wakati akisukuma geti la gereji hiyo.
“Ooh! Ricky, karibu sana kijana, naona sasa mzimu umefufuka! Hahahahah!”
“Msumi! Naona umegoma kabisa kuzeeka mzee!” akaongea Claude na kukumbatiana na mzee huyo kisha akamkaribisha ndani.
“Nini kimekuleta hapa Claude, nakumbuka mara ya mwisho nilikuambia kwamba tusionane tena mimi na wewe!” akaongea Msumi baada ya kukaa na Claude ofisini kwake.
“Ndio nakumbuka mzee wangu, Ila niko hapa kwa ombi moja tuu na nakuahidi sitarudi tena!” akaongea Claude na kumtazama Msumi ambaye alisimama na kuelekea dirishani akatazama nje kama anayetazama usalama, kisha akamgeukia Claude.
“Kuna nini Claude!” akauliza Msumi akirejea kitini.
“Kuna mtu nahitaji aondoke ili amani ipatikane kwangu na wanaonizunguka!” Msumi akashtuka kidogo baada ya kusikia hivyo.
“Unamaanisha afe?” akauliza Msumi.
“Yeah!” akajibu Claude na kutoa simu yake akamuonyesha Msumi picha iliyokuwa kwenye simu yake. Na mshtuko wa wazi ukaonekana kwenye sura ya Msumi.
“Huyu unayetaka kumuua unamjua vizuri?” akauliza Msumi akimtazama kijana huyo ambaye alikuwa mbele yake.
“Hapana! Na ndio maana nimekuletea wewe jambo hili, nakujua Msumi, najua kazi zako nyuma ya hii gereji, na sijaja hapa kukuambia kwamba nakujua, ila nimekuja kukuomba kama kakaangu na mtu wangu wa muhimu, ninakuomba ummalize huyo mtu!” Claude akaongea kwa sauti ya chini lakini yenye usiriasi mkubwa ndani yake.
“Hahahah! Claude, haujui kitu chochote kuhusu mimi, na ninakuonya kijana wangu, achana na huo mpango wa kutaka kumuua Mr Alfred, mimi ninakuomba ufurahie maisha yako na pesa zako ulizojaaliwa achana na vita za kujitakia, soma Biblia kwenye kitabu cha Waebrania 12:14 inasema “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.” Nakushauri badala ya kuitafuta vita na Alfred, tafuta amani!” akaongea mzee huyo na kuinuka. Claude naye akainuka na bila kusema neno akaufuata mlango, na kabla hajatoka akamgeukia Msumi.
“Msumi, utachagua upande wa kusimama ila nakuonya usisimame kwenye njia yangu, nafikiri unanijua vizuri!” akaongea Claude na kuondoka, moja kwa moja akaelekea garini na kuondoka.
Akiwa njiani Claude alikuwa na mambo mengi kichwani, lakini kubwa zaidi lilikuwa ni jambo la Lisa, na baada ya kuwaza sana akaona aliweke pembeni. Gari yake ilimpeleka moja kwa moja kwenye duka kubwa la mavazi la Isla Collection Centre. Akasimama mbele ya jengo hilo na kisha akashuka kwa mwendo wa taratibu, akalifuata duka la mavazi lililokuwa kati ya ofisi mbalimbali zilizokuwa hapo.
“Oh! Mr Claude, karibu sana ofisini kwetu! Naomba kupiga picha na wewe jamani kama hautajali!” mmoja wa wahudumu wa kike aliyekuwa ofisini hapo akamuomba Claude ambaye hakukataa akapiga picha na dada huyo lakini akamuomba asiitumie kwa maslahi ya kibiashara maana ana mikataba na kampuni zingine.
“Usijali na nitakutag kwenye akaunti yangu ya Instagram! Na kwa upendo wangu nakuomba uchague nguo yeyote hapa ninofa yangu!”
Nusu saa baadaye Claude alitoka ofisini hapo akiwa amebeba vifurushi kadhaa vya bidhaa alizonunua hapo ICC na kisha akaelekea garini na kuondoka kwa mwendo wa taratibu akiacha gumzo kubwa hapo ICC.
Akiwa njiani Claude alikuwa makini mno barabarani, na kwa umakini mkubwa alikuwa akitazama magari kadhaa yaliyokuwa nyuma yake, kuna gari aina ya Noa nyeusi ilikuwa inamfuata kwa muda mrefu, akakata kona ya makusudi na kubadilisha barabara. Gari hiyo ilimfuata na kukata kona hiyo hiyo aliyokata, taa nyekundu ikawaka kichwani mwake.

ITAENDELEA....................................
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

A.J.A.D SE03 EP02  >>> https://gonga94.com/semajambo/a-j-a-d-se03-ep02
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

gonga94 official track
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest