Mshindi wa Taji la Mfalme wa Rhymes mwaka 2004, na moja ya miamba migumu kabisa (Hard Rocks) kwenye muziki wa Hip Hop nchini, Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele, ametusanua kuwa jina lake la sanaa, lilitoka kwa Mwamba na moja ya waasisi wa muziki wa Rap nchini, Mr. II maarufu kwa jina la Sugu pia, akiwa na A.K.A za kutosha.
Sugu ndiye aliyemtoa Afande Sele Morogoro na kumsogeza Dar es salaam, kipindi hicho Afande Sele kaenguliwa Jeshini (JWTZ) na karudi kitaa akijikita kwenye usafiri wa Tax. Kwa bahati njema ni kuwa Tax iliyokuwa ikimzungusha Sugu pale Morogoro akiwa na shows, ndio hiyo ambayo Afande alikuwa akiisimamia na ndio ukawa mwanzo wa kujitambulisha kwa Sugu kuwa hata yeye anachana, na Sugu akamwambia Sele asogee Dar.
Mwaka 99, Sele anakaa kwenye Intro ya wimbo wa Sugu uitwao Asalamu Aleykum, na kuwa wimbo wake wa kwanza kabisa (recorded), kutokea. Afande Sele anadai wakati anahangaika ajiite nani kama msanii, Sugu ndiye aliyesema “huyu si katoka jeshini? Basi aitwe Afande Sele”
Madini haya yametemwa kwenye mgodi wa kale wa The Classic ya EFM na Jabir Saleh..