mama yake akamwambia kwahiyo unanifokeaaa??
Inno akasema naomba tuongee nje mama sasa hivii
Nyie inno ni mwehu aisee , mama ake akainuka wakatoka nje akanambia nakuja salma nikasema sawaaa akaondoka
Baada ya kama nusu saa ndio inno alikuja akaniuliza amekwambiaje nikamwambia alivyosema anataka alex aende nyumbani akasema msamehe hatokufata tena ,wamalizane wenyewe kwani namba ya mwanae si anayo siku akija niambie nikasema sawa
Alinipa siku kubwa nzuri ya kisasa, akanifungulia WhatsApp, akanambia Alex alisema atakupigia akifika nikasema sawa basi nilifanya kazi zangu ,usiku kama kawaida nilipiga hesabu nilivyoambiwa mtaji na faida nikawapa posho kila mtu akaenda,
Unajua zakia nilikuwa namkwepa sikutaka tuzoeane kazini na kuleta undugu ile mimi kumpa tu kazi ilitosha sanaaa , sikuwa na ule ukaribu nae tenaa hata umbea alishindwa kunipigisha sikuwa nacheka cheka tena kazini
..
Alex alikuwa ananipigia WhatsApp video call tunaongea na mpenzi wangu Karibu kila siku ,sikumwambia habari za mama yake kunifata ila juddy mara mbili alikuja ofisini kwangu kunitukana bado sikuwa na muda wa kumwambia alex mana najua yupo kazini haifai kumchanganyia mambo
Siku moja nilikuwa zangu ofisini, homa kama ilinizidi mana nilikuwa najiskia hovyo hovyo karibu siku nne za nyuma ila nilihisi itakuwa uchovu , lakini hii siku niliona kama nazidiwa nipo hovyoo
Nilimpigia Dereva aje baada ya kuja niliondoka kwenye kupima hospital,
Nilimwelezea Doctor shida zangu ni hizi na hizi akaniandikia kupima..
Baada ya majibu kuja Doctor akanambia kwanza hongera afu punguza majukumu ya kazi nikasema Why??
Hapo naongea vile vi English vya kutupia tupia
Akanambia wewe ni mjamzitoaa , Mungu wangu nikamwambia Doctor eeeh unasemaaa?? Akanambia Hongera una mtoto kwenye tumbo lako aiseee
nilimuuliza muda gani akanambia niende nikacheck Ultrasound nilienda hapo hapo sikutaka kulaza damu , umri wa mimba nilioambiwa nilipiga hesabu zangu ,
Ziligonga ile siku ya kwanza kabisa kulala na alex , oooh mungu wangu nikamkumbuka yule bibi kumbe alijua naeza kuwa mjamzito ndio.maana alinambia nirudi baada ya wiki mbili mmmh ..
Hii siku iliingia kwenye siku zangu zile za furaha iliyopitiliza kwanza natoka hospital nikasahau hata kama nilikuja na gari hapo nililetwa jamani,
Nakumbuka nilitoka nikapanda bajaji hata sijui ilikuwaje mi nashangaa nashuka nyumbani kwangu khaa nikamwambia we kaka mbona umenileta huku??
Nae akanishangaaa et we si ndio umenielekeza dada angu nikasema mimiii?? Ndio wewe ..
Mpaka nilicheka kwa uchungu jamani , hivi mimi ndo nimekuja nyumbani moja kwa moja khaa
Nikamwambia Dereva sawa Asante nikampa hela yake , wakati mie naingia ndani nikaitwa kugeuka alikuwa yule Mzee amos ,
Nikataka kuingia ndani akanambia salma Samahani naomba huongea na wewe!!
Kwa jinsi alivyoongea kwa upole ilibidi nisimame akanisogelea nikamwamkia ila hapo moyoni nasema we mzee ukileta ujinga wako safari hii naenda kukufunga sitaki utani
Akanambia salma mama naomba kwanza unisamehe '"
Mmh mtu mzima anaomba msamaha nikasema mi yalisha isha kuwa na amani ,akasema nashkuru sanaa sanaaa nilikuwa mzee mjinga kweli kweliii nakiri hilo
Ila nimerudi kuwa sawa, juddy bwana niligundua ana mimba hata sio yangu sijui nini sikumpa yule bint .
Nikamuuliza we ulijuaje ile mimba sio yakooo??
Mana mimi mpaka leo nilikuwa naamini ile mimba ni ya huyu mzee na hata alex anauhakika sio yake kwasababu ya huyu sasa huyu nae anasema sio yake ,nilihisi kuvurugwa akili
Akanambia mimi na yule bint mahusiano yetu yalikuwa na miezi miwili tu lakini ile mimba ilikuwa na miezi mitatu kwahiyo alipata kabla yangu!!
Uuuh nilihisi kuchoka mwili na akili nilimwambia sawa mzee kwaheri mi hayanihusu nikaingia ndani kwangu jamani kwahiyo mimba ya juddy kweli y alex mungu wangu mimi nina ndoa kwel hapaa??
Nilichukua simu yangu nikamwambia mdogo wangu subira akanambia we kaa kimyaa usimwambie alex mwache aamini ile mimba sio yake kila mtu atacheza fainal yake kwenye kujifungua ,nikasema sawa ila usimwambie mama kwanza nipo hivi akasema hilo limeisha hata simwambii nikasema sawa ilibidi nijisahaulishe maneno ya yule mzee kama vile sikuambiwa kitu..
Nilimpigia simu Dereva nikamwambia aniijie nyumbani ye mwenyewe alishangaa nimwambia Samahani sikuwa sawa kidogo Nisamehe akasema haina shida madam...
Nilikuwa namsubiri Alex kwa hamu nikaona kama siku hazitembei ,juddy si alikuwa analingia mimba okay namimi hii hapaa , kila mmoja atafute huruma ya bwana sasa kwa mpango wake wenyewe
Ile siku Alexa akanipigia simu nipo tayari Uwanjani ilikuwa mida ya sa kumi na mbili hivi jioni akanambia nakuja hapo ofisini mke wangu mi naona kama nimwambie paa baba uje paaa uje mpenzi wanguuu
Nilikuwa namsubiri muda wote nachungulia nje nikisikia tu garii nachungulia njee kumbe watejaa jamani nilimpigia nikamwambia jamani mbona hufiki
Alichekaaa akanambia salma mke wangu kweli umenimiss mama, yaan nimekwambia nakuja hata dakika saba bado hazijapita mamaaa
Hee ndo nikashituka kweli kutazama ni kweli amenipigia muda sio mrefu sa mbona mi nikiona kama masaa yamepita mmh nikatuliza komwe langu hapo ..
Alipo fika alex kwanza sio kwa kum_Miss huko , kwanza nikafunga mlango wa ofisini nipate makiss na baby wangu wiki zima limepita sijamuona mwenzangu kuna mtu kwani ananidai humo humo kwanza ofisini mana wanasema mapenzi popote bwana afu yale yasiyokuwa Rasmi huwa yanakuwa matam hatari basi ndo ikawa hivyo ofisini hapo tukamjazia mtoto ubongo atulie huko ..
Nikawaza hapa nitaenda kumwambia nyumbani tukifika ,nikamwambia ye aende nyumbani akapumzike mie nitakwenda akakataa tutaenda wote Ni mbishi Alex afu mama yake ananiambia mi ndo nimtumue arudi kwao?? Hahaha naweza kwanza sitaki arudi huko na nina jua sasa mimba ya alex aaah watanisamehe mwenzangu
Tulipo fika nyumbani sasa, tukaoga vizuri, wakati tupo kitandani nikamwambia mpenzi wangu eeh akasema naam laazizi wangu nikamwambia fumba macho nataka nikupe Surprise hapaa!!
Akasema mmmh hayaa akafumba nikachukua ile picha ya Ultrasound nikawa nimpa mkononi afu nikawambia fumbuaaa!!! .....
ITAENDELEA....
KWETU morogoro.