Asubuhi ilipopambazuka, bado afya ya Rasma haikuwa nzuri π. Akili yake ilisema kile ambacho hata yeye mwenyewe hakuweza kukielewa. Wakati mwingine alikwenda jikoni na kutafuta kisu, akitaka kunyoa nywele zake akisema kwamba zinamuwasha π°.
Muda mwingine alitishia kuchoma nyumba moto π₯, hadi ikafika hatua ambayo Mayner alijuta kwanini alienda kwa mganga. Alifikiria afanye nini. Alienda kwa baadhi ya watu kuulizia kwa zaidi ya siku mbili mfululizo, lakini hakuna aliyempa jibu la maana π€·π½ββοΈ.
Wengi walimshauri kwamba kama inawezekana, aende kwa mganga kwa mara ya pili ili kujua nini hasa kinamsumbua Rasma. Lilikuwa ni wazo ambalo kwake aliona linaweza kuzaa matunda, kwani siku baada ya siku, afya ya akili ya Rasma ilizidi kuwa mbaya sana π’.
Alianza kutembea uchi kutoka chumbani hadi chumba kingine, bila hata kujali wala kuona aibu π³. Hii ilimuumiza sana Mayner π. Aliumia kuona mtu aliyempambania katika hali ngumu sasa ameweuka na kuwa chizi.
Aliumia zaidi alivyokumbuka ushauri mzuri aliowahi kupewa na Rasma. Alikumbuka maneno yake siku aliyomwambia waende kwa mganga kutafuta dawa π₯Ί. Alizidi kudondosha chozi π. Kila kumbukumbu nzuri ilipomjia, alijikuta anakuwa mpole, sura yake ikapoteza mvuto, macho yakawa na machozi mengi π₯Ή.
Wakati pekee ambao Rasma alikuwa akipumzika ni usiku, tena kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja. Ila baada ya hapo, alikuwa akitema mate, kusimulia hadithi ambazo yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa anazijua kuanzia wahusika hadi mazingira.
"Natakiwa nikupeleke tu kwa mganga kwa mara nyingine ili nijue nini shida," alisema Mayner akiwa amekaa pembeni ya kitanda alicholala Rasma, majira ya saa 9 usiku π.
Asubuhi ilipowadia, hakuwa na lingine la kufanya. Alimpa Piriton tatu Rasma ili alale, kwa imani kuwa dawa zile zingemsaidia kulala π΄. Mungu alimsaidia, Rasma akalala. Mayner alitumia mwanya huo kumchukua na kwenda naye kwa mganga π.
Alipofika kwa mganga, mbele yake kulikuwa na watu wengi sana π―. Alishangaa kuona umati mkubwa ukiwa umefurika pale, kila mmoja akiangua kilio π’. Kabla ya kushuka gari, alimuomba dereva asimamishe pembeni ili aende kuuliza.
Dereva hakuwa na hiyana, alisimamisha gari. Mayner akashuka, akamuacha Rasma akiwa amelala ndani ya gari. Alipiga hatua hadi katika eneo lile na kumuuliza mmoja wa kina mama aliyesimama karibu:
"Kuna nini mayo?" π£οΈ
Sauti hii ilimfikia mama yule, akageuka na kujibu:
"Kafariki." π
"Nani?"
"Mganga."
"Alikuwa anaumwa?"
"Hapana, ni mipango ya Mungu tu."
"Mungu wangu! Nitafanyaje?" π© Mayner alisema huku akiweka mikono kichwani.
Watu wengine walimgeukia kumtazama. Akiwa amejaa aibu, hakutaka tena kukaa pale. Alirudi kwenye gari.
"Tuondoke," alisema kwa sauti ya kutetemeka π, akimtazama Rasma aliyekuwa bado amelala.
"Kuna nini mbona watu ni wengi vile?" dereva aliuliza huku akiwashe gari.
"Kafariki mganga."
"Mungu wangu! Kwahiyo huyu mgonjwa je?"
"Sijui... hadi nachanganyikiwa. Yeye ndiye niliamini angerudisha hali ya Rasma. Ila sawa, hakuna shida. Ngoja nijue la kufanya," alisema Mayner huku akimtazama dereva.
Akili yake iligoma kukubali ukweli alioukuta pale. Aliona kama ndoto ya mchana.
"Ndio maana tunaambiwa tusitegemee watu aisee," alisema dereva.
"Kwanini?"
"Hubadilika. Muda mwingine wanapata matatizo kama sisiβwanaumwa, wanakosa chakula, na mwisho kabisa wanakufa."
"Mh! Nashindwa hata la kusema... lakini sawa, twende," Mayner alisema kisha akachezea simu yake.
Alikuwa akimpigia Laila, mtu aliyemwamini angemsaidia kwa karibu.
π "Baby, nahitaji msaada wako?" Mayner alisema.
"Upi huo?"
"Kama inawezekana, nenda kaongee na Garma. Mwambie ndugu yake kawa chizi, nahitaji msaada wako, please ππ½."
"Mh! Atakubali kweli?"
"Nina imani atafanya hivyo. Nenda halafu utanipa majibu, sawa baby?"
"Ok, acha niende," Laila alisema, simu ikakatwa.
---
"Mzee, sijamuona wife kitambo sanaβ¦ au anasimamia ndoa nini?" π
aliuliza mmoja wa wafanyakazi wa Garma, akiwa anamuuliza boss wake aliyekuwa amekaa ofisini.
"Hayo ndiyo mambo yanayosogeza kampuni mbele?" π Garma aliuliza kwa hasira.
"Mh! Hapana, ila sidhani kama kuna kosa kwenye swali langu. Siwezi kujua kuhusu familia yako, kumbuka mnataka kufunga ndoa?"
"Ndoa na...?"
"Mayner. Au zoezi limekufa, ile suti yangu nikaivae sasa hivi?" π
"Haha! Allaw bwana, unajua yule demu siyo kabisa. Nimeachana naye ni mwa..." kabla hajamalizia...
Mlango ukagongwa πͺ.
"Nani?"
"Angelina."
"Aah! Angelina si umetoka hapa muda si mrefu, yani hata nisiongee na washikaji zangu? Ok, unataka nini?"
"Hapana boss, kuna mgeni wako."
"Wa kike au wa kiume?"
"Wa kike, ni kale karafiki ka mke wako."
Sura ya Garma ikabadilika ghafla π . Akamtazama Allaw, kisha akasema:
"Allaw, tutaongea baadaye. Acha niongee na huyo binti. Na vipi kuhusu watu wa idara ya maji, bado hakuna maji?"
"Wapo kwenye ukarabati," Angelina alijibu.
"Sawa basi, mwambie aingie," alisema Garma.
Dakika mbili baadaye, aliingia Laila. Alimtazama kuanzia juu hadi chini, kisha akakohoa kidogo na kusema kwa hasira:
"Kuna nini?" π€
"Mh! Mbona mi hasira tena? Anyways, nimeambiwa nije nikuletee taarifa⦠ndugu yako kawa chizi. Msaada wako unahitajika."
"Msaada wa nini yani? Na nani anahitaji msaada?"
"Khe! Inamaanisha hujanielewa? Ok, namaanisha hivi β Rasma anaumwa. Inahitajika nguvu yako ili aweze kuwa sawa," Laila alieleza.
Lakini badala ya kushtuka, Garma aliangua kicheko kisicho cha kawaida π€£, hadi Laila akashangaa.
"Laana za wazazi hazimuachi mtu salama. Nisikilize, unaiona hii ofisi?" aliinua kidole kuonyesha.
"Usithubutu kuja hapa na taarifa ya Rasma au yule mbwa mwingine! Nimemaliza, unaweza kutoka!" π―οΈ
"Garma! Kumbuka Laila ni ndugu yako?"
"Sina ndugu duniani. Mama aliniambia Laila si ndugu yangu, alikuwa tu anasaidia kulea. Ondoka!" Garma alifoka kwa hasira kali.
Sauti yake ilisikika hadi mapokezi, Angelina akajikuta akiwahi ofisini.
"Boss, kuna nini?"
"Bora umekuja! Huyu mbwa," alisema akimnyooshea Laila.
"Asikanyage hapa tena! Wape taarifa walinzi. Sio yeye tu, bali Rasma pamoja na yule malaya anayeitwa Mayner. Sawa?" π‘
"Sa-sa-sawa Boss," Angelina alijibu kwa kigugumizi π¬.
"Toka na huyu, halafu waambie wafanyakazi wote β nitakuwa na kikao nao kesho muda kama huu," alisema huku akisimama.
Laila hakuwa na jinsi. Ilibidi aondoke... lakini matusi aliyoyapokea yalimuumiza mno... ππ’...
Hivi ulishawahi kununua kitu kutokana na hela uliyokuwa nayo..!? Vile mfuko wako upo muda huo, ndivyo unafanya manunuzi ya kitu unachokipenda.
Tupo kwenye dunia huru na salama zaidi. Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..