Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHHπŸ₯΅πŸ’ž SEHEMU YA 01

27th Jul, 2025 Views 57



Bryan Ni kijana maarufu na tajiri anaemiliki hoteli kubwa pamoja na kampuni kubwa ya usafirishaji, Ni mmoja ya watu maarufu Sana Bryan alikuwa Ni kijana mtanashati Sana wanawake wengi walivutiwa na utanashati wake lakini hakuna aliejaribu kumsogelea kutokana na ukali wake ,

na mwanamke yoyote alie jaribu kujipendekeza kwake alimdharau na kumtoa thamani. Mara nyingi Bryan akiwa hotelini kwake alikuwa anakaa sehemu iliyotulia na kupata kinywaji hakutaka usumbufu na mtu .

Pia Kuna wakati alikuwa anamkumbuka ajali waliyopata alipokuwa na miaka 5 na kusababisha vifo vya wazazi wake .

Ulipofika muda wa lunch wafanya kazi wa kike wa pale hotelini walikuwa wamekaa pamoja wanakula .msichana mmoja akaanzisha mada.
" Hivi hapa hotelini Kuna mtu jasiri anaeweza kwenda kuongea na boss?

" Mnajua mnashangaza Sana , kwanza kwanini mnamuogopa mtu kiasi hicho anameza watu Yule? Wenzake walimuangalia mmoja akamuuliza
" Inamaana humuohopi kabisa boss?
" Mimi siogopi mtu.
" Kwahiyo unaweza kuongea nae chochote?
" Naweza hata Sasa mkitaka nikaongee nae naenda.

" Yule pale hebu nenda tuone ujasiri wako. Maria alimuangalia boss wao Kisha akasimama na kujiweka vizuri alafu akaanza kupiga hatua ndogondogo akielekea Alipokaa . Wenzake walikuwa wakimuangalia na wengine walianza kusema
" Maria anaenda kupoteza kazi yake.
" Subiri tuone.

Maria alifika akasimama pembeni na kumuangalia Bryan." Utaongea kilichokuleta au utasimama hapo Kama sanamu? Bryan alimuuliza Maria akashusha pumzi na kufikiria kile anachotaka kuongea

" Samahani boss kwa usumbufu ,nimekuja hapa ninatatizo. Maria aliweka kituo Bryan alikuwa anamuangalia usoni kwa makini

" Aaaam naomba unisaidie sasampa (pesa) kidogo kwaajili ya nauli nataka kwenda hospitali nikamuangalie baba yangu anaumwa alafu sijui hata Kama amekula si unajua ananitegemea hakuna ndugu yoyote Wala jamaa wa kunuangalia.

Bryan hakuongea alitoa wallet na kutoa kibunda cha sasampa za shilingi elfu kumi akampatia . Maria alipokea kwa kunyenyekea.

" Asante Sana boss Mungu Akupe hitaji la moyo wako. Bryan alichukua grass ya kinywaji na kunywa . Maria aliondoka huku akiwa ana tabasamu

Akaenda kukutana na wenzake waliokuwa wanamuangalia na kusubiri mrejesho kwa hamu. Alifika na kukaa kwenye kiti chake alafu akaweka Ile hela juu ya meza .

" Niliwaambia Bryan si chochote mnamuogopa bure ona Sasa nimepata sasampaaa hahaaa hizi hapa sasampa kutoka kwa Mr Boss leo maisha mwenzenu ninayo na hela ya mchezo inatoka hapahapa .

" Hapana Maria utakuwa una dawa haiwezekani boss akusikilize na kukupa pesa kirahisi hivyo. Freya alimwambia

" Mimi ndio Maria bwana nimezaliwa na bahati zangu nikiongea na mtu hawezi kupindua
" Maria umeanza Mambo yako ya kujitapa hebu tugaie wenzako hata hela ya nauli.

" Mimi Maria niwape nyie hela ya nauli , aaaha poleni Sana . Maria aliweka hela yake kwenye kipochi chake Cha mkononi alafu akaendelea kula .

Siku hiyo maria alirudi nyumbani mapema kwa kisingizio baba yake anaumwa . Alipofika nyumbani kwao aliingia bafuni akaoga Kisha akakaa kwenye kioo akawa anajiangalia .Mara akasikia anaitwa

" Maria, Maria, Maria, . Aliyekuwa anaita Ni mzee Temba baba mzazi wa Maria . Maria alitoka mpaka sebleni na kuitikia wito.

" Abee baba .
" Maria umekuwa jeuri Sana Yani Mimi nakuita muda wote huo ndio unakuja saizi.

" Mzee una lawama wewe nimekuja Hali ndio hiyo je nisingekuja ingekuwaje?
" Sitaki maneno mengi nataka hela.
" Wewe mzee Jana nimekupa elfu 10, asubuhi nikakupa tena, na Sasa hivi unataka Tena hela . Aisee mzee Sina hela ya kukupa .

" Kwahiyo nisipokuomba wewe unataka nikamuombe Nani , mbona mabinti wenzako huwa wanawajali baba zao sio wewe zuzu sijui hela zako unaenda kuhonga kwa mabwana zako

" Kwani wewe unaenda kufanyia Nini Cha maana zaidi ya kulewa na kucheza kamari. Yani tangia mama afariki sijawahi haujawahi kunijali wewe Ni baba wa aina gani....

kabla hajamaliza kuongea alishituka Kofi kwenye shavu lake mpaka shavu likawa jekundu. Maria alishika shavu lake kwa maumivu , baba yake akaenda chumbani kwa Maria na na kuchukua pesa zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye kibubu ndani ya kabati na kuondoka .

Maria alishindwa kujizuia alilia sana huku akimkumbuka mama yake ambae amefariki.

Huko kwa Bamtu mr Bryan alifika nyumbani kwake mfanyakazi wake akataka kumpokea begi lakini alikataa na kuingia nalo chumbani kwake na kwenda kuoga maji ya baridi Kisha akatoka na kwenda kukaa dinning akakuta kashaandaliwa chakula .

Kabla hajaanza kula aliona kitu cheusi kwenye chakula alimuangalia yule mfanyakazi wake aliekuwa kasimama pembeni akamuuliza
" Nani kapika hiki chakula?

" Ni Mimi boss. Bryan alisogeza sahani kwa nguvu na kuanguka chini sahani ilivunjika na sahani ikapasuka yule mfanyakazi alishituka na kuomba msamaha

" Naomba unisamehe boss. Bryan alisimama na kusema
" huna kazi kusanya kilicho chako uondoke. Aliondoka na kwenda chumbani kwake na kuendelea kufanya kazi kwenye laptop yake huku akinywa mvinyo.

Muda ulienda baba yake Maria hakurudi nyumbani , Maria alikuwa na wasiwasi Sana Mara akasikia mlango unagongwa.

Maria alisimama na kwenda kufungua , baba yake aliingia bila kumsemesha na kwenda kukaa mezani akisubiri chakula , Maria alimuandalia chakula alipomaliza alienda chumbani kwake akapanda kitandani na kujilaza huku akisema
" Huyu mzee ashukuru tu Mungu kuwa Ni baba yangu lakini angekuwa mtu Baki sijui ningefanya Nini.

Asubuhi na mapema Maria aliamshwa na kelele za mlango ulikuwa unagongwa kwa fujo. Alitoka kitandani na kwenda kufungua mlango alishangaa kuwaona wanaume wawili wakiwa wamevalia suti nyeusi.

Wale watu walimkabidhi karatasi ambayo Maria aliipitia na kuisoma . Baada ya kumaliza kuisoma alishituka

" Haiwezekani nyumba yetu inauzwaje na huyo Alie wauzia Ni Nani au ndio mmekuja na misuti yenu kumbe Ni matapeli.

" Binti usitutukane alieuza nyumba Ni baba yako kwaajili ya kucheza kamari. Na mnasiku tatu tu za kukaa hapa la sivyo mtafukuzwa .

Wale watu waliongea Kisha wakaondoka na kumuacha Maria kaduwaaπŸ₯΅πŸ˜³πŸ₯Ί

Itaendeleaaaaaa

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

BAMTU MR SASAMPA UTAM WANGU MWENYEWEEEE AAAASSSSHHπŸ₯΅πŸ’ž SEHEMU YA 01  >>> https://gonga94.com/semajambo/bamtu-mr-sasampa-utam-wangu-mwenyeweeee-aaaasssshh-sehemu-ya-01
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest