Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha usiku huo , barabara ilikuwa na unyevu unyevu uliopambwa kwa taa hafifu za barabarani alionekana msichana mmoja mrembo aliyevalia gauni lake la kitenge refu mpaka nchini akitembea kwenye mvua bila kujali chochote mwili wake wote ulikuwa umelowa sana na USO wake ulionekana kuwa na huzuni ,watu waligeuka kumuangalia ni wazi walimshangaa sana kwani hakuwa na kitu chochote Cha kumkinga na mvua Yani mwamvuli
Dakika chache tu zilitosha yeye kufika nyumbani kwao
" Winnie mjukuu wangu kwani hii mvua huioni utapata homa ungechukua hata bajaji " alisema bibi mmoja huku akimfunika yule msichana kwa kutumia kitenge chake
"Usijali bibi hata sikuloa sana mvua yenyewe imenianzia tu hapo barabarani sikuona haja ya kuchukua bajaji ningeharibu tu bajeti zangu "
" Basi ingia ukaoge maji ya moto "
bi flora alimuandalia mjukuu wake maji ya moto
Winnie aliingia chumbani kwake alikumbuka tukio lililotokea lisaa limoja lililopita
" Winnie shoga angu mbona Leo unatabasamu sana embu niambie na mimi nifurahi?"
Aliuliza Sonia rafiki yake kipenzi na Winnie
" Leo ni birthday ya Richard nimeandaa zawadi nyingi kwaajilia yake nataka kumfanyia surprise nikampikie na chakula kitamu"
Winnie alimnong'oneza Sonia
" Wacha weee watu na mabwana zana mjini ,sawa Sasa utaondokaje mapema ili uwahi ukoo kwa Richard?"
aliuliza Sonia
" Nimeshaenda kwa directa nimemuaga kuwa naenda hospital nahisi homa "
aliongea Winnie kwa sauti ya chini
" Chezea wewe kumbe unambinu kunishinda mimi mtoto mbaya wewe "
Sonia na Winnie walicheka kwa pamoja
" Sasa tutaonana kesho "
Winnie alichukua pochi yake akaondoka
Winnie Patrick ni binti wa miaka 25 ni mwalimu katika shule ya msingi ya private winners primary school, ni binti mchapa kazi sana anaishi na baba yake mzee Patrick , mama yake bi Regina na bibi yake bi flora
Winnie alikodi bajaji mpaka nyumbani kwa mpenzi wake Richard alifungua mlango na kuingia ndani Cha ajabu alikaribishwa sebleni na nguo zilizotupwa ovyo chini
" Richard jamani sijui ni lini atakua kila siku namwambia hii tabia aache "
Winnie aliongea huku anatabasamu aliweka pochi yake kwenye kiti akaanza kukusanya nguo
" Hizi si nguo za kike ?" Winnie alijiuliza kabla akili yake haijampatia jibu lolote alisikia sauti zikitokea chumbani hakuwa mtoto mdogo alijua kabisa ni sauti zitokanazo na nini Alihisi kuchanganyikiwa lakini alijikaza na kuelekea sauti zilikotokea
" Richard ..." Winnie aliita kwa mshangao baada ya kumkuta mpenzi wake akiwa na mwanamke mwingine kitandani
" Unafanya nini hapa ?" Richard aliuliza kwa kufoka alivuta shuka akamfunika yule mwanamke
" Babe huyu kikaragosi ni nani?"
Aliuliza yule msichana kwa dharau
" Zoya mpenzi wangu usimjali sana huyu ni mfanyakazi wetu atakuwa ameagizwa na mama aje kuniletea baadhi ya vitu vyangu " Richard alidanganya Winnie alijitahidi neno lolote litokee mdomoni pake lakini mdomo wake ulikuwa mzito sana
" Okay ,lakini why hana adabu alitakiwa kubisha hodi au asuburi mpaka tumalize "
Zoya aliongea huku anamuangalia Winnie kwa dharau
" Usijali mpenzi wangu ataadhibiwa ngoja nikaongee nae "
Richard alijifunga taulo alimvuta Winnie hadi sebleni
" Umekuja kufanya nini nyumbani kwangu bila taarifa Winnie?"
Richard aliuliza kama hakufanya makosa yoyote
" Richard mpenzi wangu niambie kuwa hii sio kweli na naota tu ?" Winnie aliuliza huku machozi yanamtoka
" Shhhhh ,usiniite mpenzi wako naomba uondoke tutaongea vizuri kesho "
Richard aliongea kwa sauti ya chini
" Kwanini unanizuia nisikuite mpenzi na nisiongee kwanini ? Yule mwanamke ana thamani kunishinda mimi ? Richard naomba uchague mimi au yule malaya wako ? "
Winnie aliongea kwa kufoka ambayo sio kawaida yake kuongea hivyo na Richard ,alitulizwa na kibao Cha shavuni
" Nyamaza tena nilikuwa nakustili tu Winnie hivi unalijua Hilo ? Zoya ndo kila kitu kwangu sio uzuri Wala pesa vyote amekuzidi "
" Kwahiyo unamaanisha hukuwahi kunipenda hata siku moja Richard ?"
Winnie aliuliza huku analia
" Hilo ndio jibu hata wewe hujiulizi mtu tajiri kama mimi niwe na mahusiano na mtu masikini kama wewe ulikuwa unajipendekeza tu kwangu na ulivyo mjinga ulikuwa hata hujiulizi kwanini sikuwahi kukugusa " Richard alienda kukaa kwenye kiti
" Ni kwanini hukuwahi kunigusa ?"
Aliuliza Winnie akiwa amesimama mbele ya Richard
" Ni kwasababu hukuwahi kunivutia wewe ni mshamba sio kuvaa tu hata mapenzi huyajui ,Yani ukiwa mbele yangu ni kama gogo tu nahisi wanaume wengine wanakuona hivyo hivyo pia ..well in short mbele yangu ulikuwa kama mfanyakazi "
Richard aliongea kwa dharau Winnie hakuamini macho yake kabisa alikumbuka maneno ya Richard miaka miwili iliyopita
" Winnie mpenzi wangu mimi nakupenda sana sitaki kukuchezea nakuahidi hatutafanya chochote mpaka tutakapofunga ndoa "
Winnie aliamini kuwa Richard alikuwa anampenda sana alijitolea kila weekend kwenda kumfanyia usafi nyumbani kwake kwanzia kufua , kusafisha nyumba na kupika
" Asante sana Richard nashkuru kwa yote uliyonifanyia ikiwemo na kunipotezea muda wangu "
Winnie aliongea kwa uchungu
" Ukimaliza kunishukuru unaweza kuondoka nyumbani kwangu na iwe mwanzo na mwisho Leo kukanyaga humu ndani laa sivyo tutaonana wabaya "
Winnie aliondoka akiwa haamini kilichotokea dakika chache zilizopia alikuwa mbali kimawazo alikuja kushtuliwa na sauti za watu waliokuwa wakiongea kwenye parking ya mgari ya jengo moja la kifahari
" Mr Drex kwanini unanifanyia hivi naomba unisamehe mimi nakupenda kweli "
aliongea dada mmoja huku ameshika mkono wa mwanaume mmoja aliyeenda hewani na handsome sana
" Unasemaje wewe ?" Sauti nzito ilisikika ikiuliza kwa ukali
" Nimesema nakupenda ..nilianza kukupenda tangia siku ya kwanza kukuona " alisema yule dada Winnie alisogea kidogo akachungulia
" Huyu si muigizaji maarufu Sarah mollel kwanini yupo hapa na kwanini anamuomba huyu mwanaume "
Winnie alivutiwa kuendelea kusikiliza alisogea kidogo akajificha nyuma ya gari
" Is that all?( Ndo hivyo tu ) "
Aliuliza yule kaka
" Mr Drex mimi nakupenda na sikuanza Leo kukupenda nimekuwa mwanamke wako kwa miezi miwili nimekuwa nikisubiri uniambie chochote lakini hukufanya hivyo " Sarah aliongea kwa kulalamika
" So unataka nifanye nini labda ?"
Aliuliza Mr Drex kwa sauti kavu na ya ukali huku akiwa ameweka mikono yake kwenye mifuko ya suruali
" Nataka unipende... kama mimi ninavyokupenda wewe "alisema Sarah
" We are done ( mimi na wewe basi )"
aliongea Mr Drex kwa sauti yake ya bezi
" Lakini kwanini Mr Drex?"
Aliuliza Sarah
" Sipendi kurudia rudia ninapo ongea nadhani tumeelewana "
" Hatuwezi kuachana kwa namna hii unakumbuka kama tulisaini mkataba kuwa nitakuwa girlfriend wako kwa mwaka mmoja "
" Miss sarah ..ivi uliusoma mkataba vizuri kweli ? "
Aliuliza Mr Drex kwa sauti ya ukali Sarah hakuwa na lakusema alikuwa kimya
" Malik njoo umsomee mkataba "
Mr Drex alimuita secretary wake
" Wanaongelea mkataba ... mkataba wa kuwa kwenye mahusiano ? Sikuwahi kusikia hiki kitu "
Winnie alijikuta anasahau maumivu yake ya kutendwa na kutafuta umbea
Alishuka kijana mmoja kwenye gari aina ya Range akiwa na karatasi mkononi
"Miss sarah ..haya nimakubaliano kati yako na Mr Drex sharti la kwanza unaweza kutaja chochote unachokitaka kama pesa ,gari ,nyumba lakini sio kuomba upendwe Na pili girlfriend wa mkataba atakapotaka kupata haki ya kupendwa basi atakuwa amevunja mkataba "
Alisoma malik dereva wa Mr Drex
" Mr Drex nakuomba unisamehe sitorudia tena kukuomba unipende "
sarah alipiga magoti
" Oh mungu wangu siwezi kuamini huyu huyu Sarah mollel muigizaji maarufu anaegombaniwa na kila mwanaume ,Leo amepiga magoti mbele ya mwanaume kulilia mapenzi ?"
Winnie alijiziba mdomo kwa mshangao
" Miss sarah naomba uondoke Sasa nadhani unanijua vizuri naweza kufanya nini mtu akinikera "
Mr Drex aliongea kwa kufoka Sarah alisimama na kuondoka huku akiwa analia
Winnie alimsindikiza kwa macho
" Jitokeze .."
alisema Mr Drex Winnie alishtuka sana alianza kutetemeka kwa uoga alijikaza akatoka alipokuwa amejificha
" Sogea hapa "
Mr Drex aliongea kwa amri Winnie taratibu alianza kusogea
" Mungu wangu naomba unisaidie sijui atanifanya nini huyu kaka , hata kama sikuja kanisani jumapili iliyopita naomba unisamehe mungu wangu na ukubali dua yangu nitoke hapa nikiwa salama " Winnie alijiongelea mwenyewe huku anasogea
" kumbe ni handsome hivi sishangai muigizaji maarufu kama sarah mollel kumlilia huyu mwanaume,maisha yangu yote sikuwahi kuona mwanaume handsome kama huyu, Richard na kuringa kote hamfikii hata robo" Winnie alimkagua Mr Drex juu hadi chini na alimpa asilimia mia moja
" Wewe ni nani ? Muandishi wa habari ? " Aliuliza Mr Drex huku anamuangalia Winnie kwa jicho Kali
" Hapana umenielewa vibaya mimi sio muandishi wa habari wala sikuwa na nia mbaya nilikuwa napita tu "
Winnie aliongea huku anacheka Cheka
" Umesikia kwanzia wapi ?"
Mr Drex alianza kumsogelea Winnie
" Nimesikia kidogo tu na samahani sana sikupanga kusikiliza kama nilivyokwambia nilikuwa napita tu " alijibu Winnie huku anarudi nyuma kwa uoga alifika mpaka mwisho wa ukuta
" Inaonekana unapenda sana rangi ya pinki "
Mr Drex alimkagua Winnie juu hadi chini alikuwa amevalia gauni la kitenge lenye rangi ya pinki ,pochi ya pinki , raba za pinki ,hereni za pinki na kibanio Cha nywele Cha pinki Cha kuchekesha ni kuwa hazikuendana hata kidogo nyingine ilikuwa ni pinki iliyokolea sana na nyingine ilikuwa imepeuka
" Ndiyo ...napenda sana rangi ya pinki tangia nipo vidudu "
Winnie alijibu huku sauti yake ikitetemeka kwa uoga
" Naijua sura yako itakuwa vizuri kama uliyoyasema ni kweli , tumeelewana miss Pinky"
Mr Drex aliongea huku anaondoka
" Subiri kwanza "
Winnie alijikuta anamzuia Mr Drex
" Unataka nini ?"
"Kwenye maongezi yenu nilisikia unasema unachukua... unachukua girlfriend kwa mkataba je ni kweli ?"
Aliuliza Winnie
" Why are you asking ( kwanini unauliza )?"
Mr Drex alimuangalia Winnie kwa jicho Kali
" Kama unahitaji girlfriend wa mkataba kwasababu umeshaachana na mpenzi wako wa zamani unaonaje ukanipa mimi hiyo kazi "
aliongea Winnie kwa kujiamini
" Nope siwezi kuwa tu na kila mtu huwa Nina viwango vyangu miss Pinky "
alijibu Mr Drex
" Niambie ni viwango gani unataka ?"
aliuliza Winnie
" Napenda mwanamke mrembo ,awe na shepu nzuri , anaevutia na wa hadhi yangu "
alisema Mr Drex
" Nipe muda nitakuonyesha nitakavyokuwa mrembo ,nakuhakikishia mimi ni mrembo kumzidi Sarah mollel"
aliongea Winnie kwa kujiamini
" Hahaha Sarah ni mrembo na anavutia ila jiangalie wewe kwanza umevaa kama bibi au huwa hujingalii kwenye kioo"
Mr Drex aliongea huku anacheka kicheko Cha dharau
" Nipe muda ukiona sifai ndo unaweza kukataa ofa yangu"
" Huwa natoka kimapenzi na wanawake wakubwa sitoki na watoto wadogo "
simu ya Mr Drex ilianza kuita aliondoka na kuingia kwenye gari lake
" Kumbe maneno aliyosema Richard ni kweli kila mwanaume ananichukulia mimi kama takataka "
mvua ilianza kunyesha Winnie hakujali aliamua kutembea kwenye mvua huku machozi yakimtoka
" Winnie mjukuu wangu unafanya nini huko chumbani maji bafuni yatapoa "
Winnie alishtuliwa kutoka kwenye mawazo na sauti ya bibi yake
" Nakuja bibi "
Winnie alifuta machozi alichukua kipande Cha kanga akaelekea bafuni
Kwa upande wa Mr Drex safari yake iliishia nje ya jumba moja kubwa la kifahari
Elian Marcel Drex ni kijana wa miaka 33 ni CEO wa kampuni iliyoitwa Purenex company
Elian ni mtoto wa Mr Marcel Drex na bi Carolina , kwao wamezaliwa wawili yeye na mdogo wake Ezekiel mwenye miaka 28 yeye ni mwanasheria
" Mama mbona umeniita hapa usiku huu Kuna kitu gani Cha muhimu?"
aliuliza Elian
" Elian kwani vibaya mama yako akikuita nyumbani kwenu au hukunimiss jamani "
bi Carolina mama wa Elian alisogea akamkumbatia kijana wake
" Mama unajua Nina kazi nyingi sana za kufanya " Mr Drex ama Elian alienda kukaa kwenye kochi
" Ni kumuhusu Levis mwalimu wake amepiga simu mzazi wake anatakiwa kufika shule kesho mapema sana inaonekana atakuwa amepigana tena na wenzake huko "
aliongea bi Carolina huku amekunja mikono yake kifuani
" Kwani Mr Marcel Yuko wapi ?"
Aliuliza Elian
" Elian yule ni baba yako kwanini unapenda kumuita hivyo ?"
Alifoka bi Carolina
" Hata nikimuita baba haibadirishi kuwa alinikataa nakusema mimi sio damu yake "
aliongea Elian huku anachezea saa yake
" Nimambo ya zamani sana Elian hembu acha yapite alisema vile kwasababu ya hasira tu "
" Usijali kuhusu Levis kesho nitaenda shuleni kwao "
Elian aliondoka bila hata kuaga
" Huyu mtoto kwanini habadiliki kila siku anazidi kutuona sisi kama sio wazazi wake "
alilalamika bi Carolina Elian alipanda kwenye gariA
Full 1000
Whatsp 0784468229.