________________________________________*
*SEHEMU YA KWANZA*
Niliolewa nikiwa mdogo sana. Nikiwa na miaka 21. Na nilipenda mwenyewe. Unajua maisha ya kukosa elimu yalivyo. Sikuwa na namna. Nikaolewa na mume ambaye anajishuhulisha na uchimbaji wa madini. Nilimpenda sana. Akanipenda sana pia
Sasa nikisema akanipenda sio kwa kufuata zile 10 zako ambazo umepost juzi. La hasha.
Vigezo vyangu vikawa katika ninavyojua mimi.
Yani ukiolewa tuuu nahesabu ni kupendwa. Mume akikupa bank kadi yake na umshikie pesa nahesabu ni kupendwa .
Miaka mitatu ikaisha. Nikapata watoto mapacha.
Hapo tuna nyumba, mashine ya kusaga, costa nne zinaenda moshi arusha. Na mume ana gari yake ya kutembelea na mimi gari ya kutembelea. Yani tukiwa na miaka 26 kwa 30 tayari tuna huo utajiri.
Sasa watu wengi wa kazi hii huamini madini yapo tuu. Da Irene mume wangu akaanza kuuza vitu. Mbaya zaidi anauza kwa hasara. Alafu haambiliki.
Ilikuwa ni mifarakano kila uchao.
Akiuza sijui inakueaje anapata mawe ananunua ten mali. Mpaka akaitwa Kismati. Yani jina maarufu ikawa Kisimati.
Maisha yakasonga.
Hapo mimi nafanya kazi ya kusimamia tu mashineni. Napata pesa hasa. Naweza kupata kuanzia laki moja mpaka laki moja na nusu kwa siku. Ama elfu sitini kama kazi hakuna. Hivyo hiyo ni pesa hasa da Irene.
Siku moja sikuamini hajanishirikisha akaniambia anauza ile mashine na eneo kabisa. Akasema anataka milioni thelathini.
Akaja mteja ili ampatie
Da Irene nikasema nijiongeze. Nikamwambia kuna mteja anataka kwa milioni 40 cash money.
Akasema sawa.
Hapo nilijua kabisa miezi 10 nikifanya kazi napata kabisa hiyo pesa nalipa kama ni rejesho. Alafu nibaki na mashine mimi. Nimuuzie tuu mtu kivuli.
Da Irene nikakopa kikoba. Nikapata hiyo pesa. Nikaweka na rehani gold zangu zote. Nilikuwa na kama gram 300 hivi za Gold. Si unajua wake za wachimbaji? Yani Gold ndo ufahari.
Nikapata Milioni kama sita hivi. Wakati huo gram ya gold ni tshs 20000 mpaka 35000.
Basi maisha yakaenda nikatafuta ndugu wakae mashineni.
Da Irene ndugu kuna saa ni Nuksi.
Nilimuamini ndugu. Yani huwezi amini ananiletea elfu 30 ama 10 kwa siku.
Namwambia unit za umeme zilizotumika mbona nyingi kuliko mapato?
Gues what Irene,
Yani mtoto wa mama yangu mdogo kabisa akamuonyesha mume wangu msg zote. Haikuishia hapo tuu akatembea naye pia.
Maumivu yake usiombe
Na hapo nina Deni la kikoba. Milioni kama 25 hivi.
******************
*SEHEMU YA PILI*
Sasa umeshapata kashfa ya kununua mali ya familia kwa siri. Na haikwepeki. Mbaya zaidi shahidi ni ndugu wa familia upande wangu.
Ilikuwa ngumu sana. Maelewano nyumbani hamna. Mtoto wa mama mdogo ndo mke nwenza
Mume kaja juuu kasema mashine yake arudishiwe deni nitajuana nalo mimi. Familia pande zote wanakaa kusuluhisha ugomvi. Wakaamua mume achukue mashine na deni la kikoba alipe.
Mume anakubali. Walau natua mzigo mmoja wa deni.
Maisha yanasonga na ndugu yangu ndiye msimamizi. Na kila mwezi anaweka akiba yake na anajilipa mshahara na analipa yule mama wa kikoba. Ambaye namba anazo na masharti anayajua alipeje. Lini na wapi.
*SEHEMU YA TATU*
Maisha yanaendelea kwa mtindo huo. Unajua kabisa mdogo wako ana mahusiano ya mapenzi na mumeo . Huna pa kwenda. Ni wale watu ambao mama zetu na baba zetu wanaishi vijijini. Tayari kuna ugomvi wa kifamilia. Mama na mdogo wake hawaongei kabisa. Kisa na mkasa kanichukulia mume . Tena wazi wazi.
Inauma sana.
Yule mwanamke aliyezoeleka mrembo kanawiri leo kachoka na kukongoroka hasa. Maisha ya mateso yanaanza.
Mume ananitukana hadharani.
Anasema kabisa utaondoka mdogo wako aje.
Huwa mnasema sijui tuwape waume mdinyo tusijali , natamani kujua unampaje mdinyo mume wa hivi. Anayekuambia kabisa mdogo wako mtamu sana. Anakuambia mdogo wako mtamu anajua mapenzi.
Miezi inaisha
Mwaka unaisha.
Mwaka wa pili unaisha . Mara vaaap, mdogo wangu ana mimba. Namuona kabisa ni mja mzito . Sasa hata kama sikuwa naamini mahusiano yao sasa naamini mia ya mia .
Napata ugonjwa Depresion. Msongo wa mawazo mkali sana. Wazazi hawajui wafanye nini. Wanaamini sasa mdogo wangu kaniloga.
Naanza kuaguliwa.
Mume hajali kabisa.
OYA, SKIA. KAMA UNAONA VIPI NYANYUA. SIKAAGI NA MAKOKOOO.
Hii sentensi anasema mume wangu.
Nimekonda hasa. Ile ya kukongoroka hasa. Yani kama mzeee kabisa.
Naenda wapi,nina pa kwenda?
Mume anahama chumba . Anahamia chumba cha watoto wa kike ambacho nacho kina choo ndani. Ananunua Kitanda chake godoro na mashuka. Siwezi kulala na mifupa mimi.
Mwanamke asiyeridhika. Ananiambia.
Na kweli ukija utakuta kila kitu ndani. Maisha ya starehe hasa. Ila nakulaje?siwezi kula kabisa. Nawaza tuuuu.
*SEHEMU YA NNE*
Miezi tisa inaisha. Mdogo wangu anajifungua.
Dah. Kama kuna wakati nilipata maumivu makali na sijafa ni huu. Yani nilisema sitakufa tena.
Mume anapata mawe yani madini mengi sana huu usiku. Na anaambiwa mdogo wangu kajifungua usiku huooo. Halooo hilo shangwe halikuwa la kawaida.
Mtoto siakaitwa Kisimati. Kwa kifupi Kisiii.
Mama kisiiii.
Mdogo wangu akanunuliwa nyumba ya milioni mia . Akanunuliwa gari. Akaambiwa akitoka tuu uzazi anapewa super marketi. Mume akanunua petrol station. Na kaanza kukarabati super marketi.Ili mke uzazi ukiisha tuu apate ofisi.
Sasa utaona ni pesa nyingi alipata.
Mimi sikuambulia kitu
Mume akaniambia kabisa Ninadinya mzigo wa maana. Nadinya mahali pananipa maisha .Pananipa madini. Kuna wanawake wana k... za maana. Mwaka tuu nimedinya utajiri huoo. Nikidinya miaka kumi nini kitatokea?
Acheni nyie. Sikufa wakati ule sitakufa kwa stress tena.
Dah.
Nawaza kuondoka nasema tuu acha nivumilie. Maana naenda wapi. Nyie umasikini huuu. Mh. Kila mwanamke awe na pesa zake.
Awe na ndugu wenye pesa na upendo pia.
Mwaka sasa na ushee mume hanigusi.
Nimeenda kwa kila mganga hakuna matokeo.
Yani acha kabisa.
Mke katoka uzazi. Kanawiri hasa. Mimi maombi yangu apate ajali afe. Yani kweli laana ya kuku haimpati mwewe.
Nakesha naomba mabaya. Afe tuu jamani.
Sasa ndio asbh anaamka na mwanae na house girl wanaenda super maketi. Nyie nyie.Mh.
Matambo hasaa. Mtoto baba ndiye anamlisha. Naambulia tuu picha whats app status.
************
Ni jumatano moja naikumbuka sana. Tarehe 15 mwezi wa sita .
Ninatoka nyumbani naenda sokoni. Gari yangu ilishauzwa. Niko na bajaji. Naskia mtu ananiita yuko ndani ya gari nami nashuka kwenye bajaji.
Fulani, Fulani, anaita.
Nageuka.
Mambo? Za masiku?Pole sana Bwana.
Mwanaume anashuka kwenye gari ananipa pole. Umeugua nini?
Mwanzo nilijua pole ya matatizo ya ndoa.
Kumbe alijua nimeugua.
Asante najibu.
Machozi yananitoka .
Wala sijaugua. Namjibu. Nini hasa mamiii? Anaonyesha kusikitika sana.
Namjibu ni issue za ndoa Filex.
Nini hasa na jamaa ana mkwanja hivyo kasimamisha Dunia?
Mh. Naguna tuu.
Kwani hujui ana mwanamke mwingine?Najibu.
Sasa akiwa na mwanamke mwingine ndo ukonde hivi mamii?hivi unajua ule uzuri wako umeutupa?Mpaka kalio limeisha?Aisee hapana.
Sema vizuri.
Ananiambia kwa kumaanisha.
Una simu?Ananiuliza.
Hapana namjibu.
What?Sasa nikikuhitaji nakupataje?
Natulia kidogo. Amm hapana. Ataniua. Usinihitaji. Namjibu.
Anacheka. Ha ha ha. Sasa mamii.. umesema ana mwanamke wake. Kwa hiyo wewe utaishije?
Nitaishi tuu. Nitaishi tuu mpaka nife. Nikaanza kulia tena.
Filex akijiskia vibaya sana. Aliniambia hembu panda kwenye gari mara moja.hapa njiani usilie. Panda garini.
*SEHEMU YA TANO*
Naingia kwenye gari.
Anawasha AC. Kisha anaweka wimbo sauti ya chini sana. Your my african woman.... Alafu ananifunga mkanda. Ananitazama alafu ananiambia.
Natamani kukuona unafuraha. Nimeshtuka sana kukuona na hii hali. Nakujua sana Ulivyo mwanamke mrembo matamanio ya wanaume wengi. Naomba niruhusu tuu nikupe furaha urembo wako urejee . Natamani kukuona ukiwa na ule urembo basi. Natamani kukuona na urembo ule.
Filex anaongea. Kisha ananiomba aendeshe gari anipeleke mahali tuzungumze zaidi.
Natulia kidogo kisha nakubali. Sawa Filex. Ila naomba mume wangu asijue. Please. Naomba sana.
Filex anatabasamu.
Skia mamiii. Najua umeniambia una matatizo. Siwezi kukuongezea matatizo. Bali nataka kuyapunguza alafu kuyaondoa kabisa. Ninachohitaji kwako ni Usikivu, Utiii na Kunielewa na kufanya ninachotaka tuu basi. Sawa mamiii?
Natulia kidogo namsikiliza.
Ndio. Namjibu.
Hiii kwangu ni bahati sana kukutana na wewe. Bahati sana na matamanio yangu kitambo. Anaongea Filex.
Anawasha gari. Anaendesha kama dakika 20 hivi. Kisha Anaingia kwenye barabara ya vumbi. Kisha anaendesha tena kama dakika 10. Huko tunapishana tuu na magari ya utaliii. Mara tunaingia kwenye hotel kubwa sana ya kitaliii. Naona tuu neno Black Rhino Cottages .
Anapaki gari. Anakuja mhudumu kutupokea pale pale .
Mh nashukaje na hizi nguo?namuuliza Filex.
Mbona niko mchafu mchafu?namwambia.
Ha ha ha. Anacheka.
Mimi nakuona yulee ambaye siku moja kama unakumbuka tulipishan soko kuu nikakutania nikakwambia Mama unaniuaa... unakumbuka? Ha ha ha.
Anasema Filex.
Mpaka leo, sura yako, umbo lako,rangi yako na tabasamu lako vimegoma kufutika akilini na moyoni mwangu mamiii.
Hivyo usijali.
Natulia kidogo kuvuta kumbukumbu kwa tukio hilo.
Alafu nacheka.
Waooo... thats is my woman now. Tabasamu nimelipata ,Ile sura naiona sasa . Bado, rangi na umbo tuuu.
Tukacheka wote .
Nikarekebisha mtandio wa dera kichwani vizuri.
Usijali kabisa. Usijali mamii.Filex anasisitiza .
Mtapendelea kukaa wapi?mhudumu anauliza.
Naomba tukae kule garden kwenye wale Tausi. Si wapo?
Ndio bosi wangu. Wapo. Karibuni sana. Mhudumu alijibu na akawa katangulia mbele yetu tunaelekea garden.
Alitukaribisha. Na tukakaaa.
Utakunywa nini mamii?Filex aliniuliza.
Ammm... Juice tuuu.
Naomba Juice mbili tafadhali.
Na sambusa nne.
Mhudumu aliondoka kufuata oda yetu.
Karibu sana. Yani najiona mwenye bahati kubwa kuwa na wewe hapa. Niamini.
Naomba nichagulie majina ya kukuita kati ya haya.
Waridi,Malaika,ama Lulu.
Filex aliongea kisha akatabasamu.
Nilimtazama nami nikatabasamu.
Sema basi mamiii.
Alishika mikono yangu na kuchezea vidole. Kucha zangu zilikuwa hazijakatwa vyema. Na zikikuwa na weusi weusi kuchani.
Nilipata aibu.
Kucha mbaya ee. Nilisema.
Alinitazama akachukua mikono yani viganja vyangu na kuvibusu. Hapana. Sio mbaya. Ni mwanamke mchapa kazi tuuu. Wala usijali. Ulitamani nini?
Alihoji.
Nikitamani kubandika. Ila sina msichana wa kazi. Nabandikaje?
Nilijibu.
Usijali. Msichana wa kazi utampata. Na kucha utabandika. Sema kingine . Filex aliniambia.
Enhe Lulu wangu niambie... Filex aliita hilo jina na wakati huo mhudumu akitukaribisha.
Itaendelea.....
KWETU morogoro.