Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

*SEKRETARI NANAH* SEHEMU YA 0️⃣9️⃣

27th Jul, 2025 Views 3



Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani

Mawasiliano: 0763 595006

Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y

*ONYO*

Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.

KARIBU

"Uko sawa?" Aliuliza Shalha akimshika Bieber mkono na kumtoa ili atizame shavu lake.

"Kama umeanza kuvimba hivi" alijisemesha Shalha na kuanza kumpuliza shavuni mwake.

Usijali utakuwa salama.

Bieber aliondoka na kuelekea uwani, alipofika alisimama kwenye kioo na kubaki akijikagua shavuni mwake.

Kibao cha Nanah kilizidi kujirudia kwenye ufahamu wake wa akili.

👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠

"Huyo Hawara wako kampiga Bieber kibao".

"Hawara wangu ndo nani?" Aliuliza Brown na ghafla alitoa macho yake.

"Umesema Bieber amepigwa kibao?"

"Nanah amepiga Bieber kibao na sijui ana hali gani kwasababu amekimbilia uwani".

"Bieber yuko wapi?"

"Nimekwambia amekimbilia uwani"

Brown alitoka mbiombio akimfuata ndugu yake alipoelekezwa alipo.

"Nanah umefanya jambo ambalo hutalisahau katika maisha yako yote , niamini mimi" alitabasamu Shalha na huku akipiga simu ilipo pokelewa tu alibadilisha sura hadi na sauti.

"Mama......mama.....sijui itakuwaje yani"

"Kuna nini?"

"Ni Bieber " alijibu Shalha na kumfanya Everline ainuke alipokuwa amekaa akilitaja jina la mwanaye.

"Bieber!!! Bieber amefanya nini?"

"Mungu wangu hata sielewi itakuwaje?"

"Shalha, unanichanganya ni kitu gani kimempata Bieber?"

"Unamkumbuka yule Nanah?"

"Embu nieleze ya kuhusu Bieber, sitak ya mtu mwingine mimi".

"Bieber alimfumania na Brown wakiwa wanafanya mapenzi ofisini"

"Nini? Unaongea vitu gani wewe?"

"Ndiyo mama sasa Bieber akaja kuniambia mimi hapa, Nanah akashikwa na hasira na kumpiga Bieber"

"Unasemaje wewe? Amempiga Bieber? Yuko wapi mwanangu?"

"Amekimbilia uwani mama. Bieber ameenda kujifungia huko yani ni kama amechanganyikiwa".

"Nitamuuwa huyo binti mimi kwa mikono yangu mwenyewe"

Everline alikula kiapo hicho na kukata simu yake.

Shalha alitabasamu na kuonyesha sura ya ushindi sasa na siyo ile ya hofu aliyokuwa akiigizia alipokuwa akizungumza na simu.

👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠

Brown alimgeuza mdogo wake akimtizama usoni.

Alimkuta ameshaanza kuvimba shavu alilopigwa Kofi.

"Unajisikiaje? Twende hospital?" Aliuliza Brown.

"Hapana niko kawaida"

"Upo kawaida? Na umeshaanza kuvimba shavu?"

"Nipo kawaida, ni kwamba najisikia tu tofauti"

"Ndomaana nakwambia twende hospital sasa". Alizungumza Brown akimlazimisha.

"Mmmmhh siendi popote nimesema niko sawa. Ni mara yangu ya kwanza kupigwa kwahiyo lazima nijisikie kidogo tofauti".

"Una uhakika uko salama?" Aliuliza Brown.

"Ndiyo"

"Hapana embu twende hospital" Brown alimshika mdogo wake mkono na kuondoka naye akimpeleka hospital.

Baada ya dakika kadhaa Everline alifika na kupokelewa na Shalha aliyekuwa njee ya lango kubwa la kuingilia kwenye kampuni.

"Yuko wapi Bieber?"

"Brown amemuwahisha hospitalini".

"Unasema?"

"Haonekani vizuri kabisa mama"

"Nini? Ameenda hospital gani?"

"Sifahamu" alijibu Shalha na Everline alimpigia simu Brown lakini haikupokelewa.

"Ameenda Mega Hospital". Alisema hilo Doy kwani hakuwa mbali na hapo.

Shalha aliondoka na Everline mbiombio kuelekea huko hospital.

"Kurwaaa,Heeee shoga ako Bi Mkosi kautafuta mkosi kwelikweli"

"Sasa unadhani ataacha kuwa kwenye matatizo kwa kumpiga mdogo wake na Boss?"

"Siongelei hilo. Bieber ni mgonjwa na haruhusiwi hata kufinywa sasa shoga ako kambandika libao hapa navyoongea na wewe Bieber anahemea oxygen hospital".

"Hauko seriously sindiyo?" Aliuliza Bob akisimama alipokaa.

"Ndo alichokisema Shalha na Mama yake na Brown amefika hapa" alizungumza hilo Doy.

Bob alibeba simu yake na kuondoka akaenda uwani alimpigia simu Nanah.

"Na huyu shoga anataka nini sasa hivi, sitaki kelele mimi"

Nanah aliifunika simu yake ila iliita tena kwa mara nyingine.

"Anataka nini bwana?" Alijiuliza Nanah akigeuka upande mwingine wa kitanda na kuipokea ile simu.

"Wewe mtoto mjinga, kwanini na kupigia simu na haupokei?"

"Kuna nini bwana mimi nimeshaacha kazi".

"Siyo kuacha kazi tu na kukimbia ukimbie"

"Kwanini?" Aliuliza Nanah.

"Kwasababu huyo uliyempiga kibao ni mgonjwa na Kwasababu ya kibao chako anahemea oxygen sasa hivi"

"Nini?" Aliuliza Nanah na kuinuka kabisa kutoka kitandani.

"Ukweli ndo huo, Bieber yuko Mega Hospital anapambania maisha yake"

"Jamani, yani kile kibao kweli jamani kibao tu mtu anahemea oxygen? Tena mwanaume?"

"Nanah umesikia nilipokwambia anaumwa toka zamani? Na wanasema haruhusiwi hata kufinywa".

"Eeeeehhh Mungu wangu eeeh, kwahiyo yupo hospital gani tena"

"Mega Hospital, wewe ngoja unataka kufanyaje?" Aliuliza Bob na Nanah alikata simu yake.

👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠

"Yuko wapi mtoto wangu?" Everline alimnyaka dokta mmoja koti lake.

"Mama tulia kwanza embu vuta pumzi".

"Acha kuniambia nivute pumzi, yuko wapi mtoto wangu?"

"Mama, unapaswa kutulia ili dokta aweze kutuelewa".

"Mtoto wangu mimi, anapumulia oxygen ameletwa muda siyo mrefu ndo nauliza yuko wapi?"

"Ameletwa muda siyo mrefu na anapumulia oxygen?"

"Ndiyo alipigwa kibao".

"Mmmmhh" dokta aliguna na kumtizama Everline kisha akamtizama Shalha na kuona huwenda wamepata mfadhaiko na hawawezi kuelezea ndugu yao amekumbwa na nini hadi akaletwa hospital.

"Dokta mbona unatutizama tu?" Aliuliza Everline.

"Ndo ninaingia ofisini muda huu, so mkae hapo nikawaulizw baadhi ya waliokuwepo kisha niwaletee ndugu yenu". Alisema hivyo Dokta akitaka awape dakika kadhaa za kujituliza kisha aje awaulize tena wanamtafuta nani.

"Sawa ila sasa hivi" alijibu Everline na hapohapo alitoka Brown akiwa na Bieber.

"Bieber!!!" Aliita Everline akimfuata mwanaye na kumtizama .

"Amekupiga wapi huyo mbwaa?" Aliuliza Everline.

"Mama yuko sawa, tumefanya hadi X ray yuko sawa"

"Atakuwaje sawa wakati nimeambiwa na Shalha anahemea oxygen?"

Bieber na Brown walimtizama Shalha kwa pamoja.

"Nilidhani unapumulia oxygen , kwasababu nilikuona kama umeshindwa kuhema".

"Samahani nimemfuata, kijana mmoja niliyempiga kibao na anahemea oxygen" Nanah alifika pale na kumuuliza dokta yuleyule wa awali

"Embu ungana na wenzako wale pale".

"Mama niko sawa, just .
..... alisema Bieber akitabasamu

Brown huyu mdogo wako umempima akili? Kwanini anacheka? Aliuliza Everline.

"Nanah!!" Aliita Bieber aliyemuona Nanah na kujikuta akitabasamu.

Wote waligeuka na kumtizama Nanah ambaye alianza kutengenezea miwani yake vizuri kama mshamba fulani hivi.

"Mama huyo ndo aliyempiga Bieber kibao" Shalha alimnong'oneza Everline ambaye aligeuka na kuwa mbogo.

Alimfuata Nanah na kumlamba kibao.

"Mama" aliita Bieber kwa sauti kubwa na kwenda kumtizama Nanah sehemu aliyopigwa kibao.

"Kwanini umefanya hivyo?" Aliuliza Bieber kwa sauti kali na iliyojaa ukali akimuuliza mama yake.

Brown alienda kusimama mbele ya mama yake na kumzuia Bieber.

"Mwanangu amekuwaje? Aliuliza Bi Everline

Itaendelea In Shaa Allah.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*SEKRETARI NANAH* SEHEMU YA 0️⃣9️⃣  >>> https://gonga94.com/semajambo/sekretari-nanah-sehemu-ya-0-9
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 32💘💘

majario rewards 100 Comments 0
 

Simulizi: MAPEPE **

majario rewards 100 Comments 0
 

SEHEMU YA 30💘💘

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest