Baada ya Laila kuondoka walibaki wawili kama wapenzi ama wazazi wapya ambao walitakiwa kuzungumza mambo mbalimbali hasa kile ambacho kilitokea muda mfupi uliopita. kila mmoja akimtazama mwenzake, uso wa Mayner ulipoteza tabasamu kabisa akasema.
“Mama yako nahisi umemsikia kile ambacho amekiongea si ndio?”
“Endelea kumvumilia mke wangu, sina siku nyingi nakamalisha ujenzi wa nyumba ya bururuga atakaa kule am ahata Igoma sio mbaya”
“Sidhani kama itakuwa suluhisho”
‘Ila”
“Kuzidisha matatizo maana ataendelea kuniambia mimi nina roho mbaya, sijui simpendi na maneno mengine ya kuuma” Maneno haya Mayner aliyaongea huku machozi yakimtoka, uso wake ulikosa matumaini kabisa.
Alikuwa ni mwanamke ambaye hakufurahia uwepo wa mkwe pale nyumbani, alikuwa akichukiwa hata kama alipofanya jambo jema. Muda mwingine aligomewa kama mtoto mdogo.
“Kama hamnipendi na mnataka mimi niondoke bora mniambie kuliko kumuua mtoto wangu. Nakuomba Garma kaa na Mama yako chini mfikie mwafaka”
“Mwafaka wa nini Mayner, wewe utabakia hapa. Utakuwa hapa kila siku na mimi nitakuwa hapa kama mzazi mwenzako, sitakaa kuona mama anafanya mambo yake ya kijinga”
“Furaha yangu inategemea mtoto, inategemea mwanangu ambaye naimani kwamba atakuja kuwa mzuri. Naomba umpigie wifi umwambie amuite jina maana yeye ndio alisema anataka kuita jina” Mayner alisema
Wifi yake ambaye ni ndugu wa Garma alikuwa upande wa Mayner, kwake alimpenda kupita maelezo na hata kabla ya kujifungua walikubaliana kwamba kuhusu upande wa jina basi ingekuwa upande wake. Naye hakutaka kwenda kinyume cha ahadi ile.
Garma alichezea simu yake na kumpiga kisha alimkabidhi Mayner ili apate kuongea na wifi yake.
“Kaka habari” sauti ya Rasma ilisikika
“Haha! Sio kaka yako bwana”
“Uwi! Kumbe wifi, naomba uniambie nini kinaendelea ushaleta mzigo au bado tukuongezee maji ya uchungu”
“Hahaha ka jinga hivi, ujue Rasma huna akili. Hayo maji ya uzazi vipi?”
“Khe! Kama umegoma kuleta mume wangu je?”
“Una mume basi ni namba yangu kabisaaaaaaaaaa, Utaniua mwenzio hata mapaja yote yanauma, kiuno usiseme. Kaja wa kike mume wangu” alisema Mayner huku akiweka tabasamu na kumwangalia mtoto wake
“Jamani, jamani mbona unanitamanisha nirudi hata leo nije nimuonea. Vipi kachukua sura yangu au?”
“Hahaha! Anakujua hadi achukue sura yak? nina damu nzito sana nimekuzidi kwenye nguvu hadi sura. Yaani ukimuona ni mimi kabisa huyu, kwahiyo mwaya jina muhimu” alisema kisha akamtizama mume wake na kuweka Loudspeaker
Kimya kilipita, kila mmoja alikuwa na hamu ya kusikia jina ambalo Rasma angelitoa, naye alionekana kama aliyekuwa akifikiria hivi kisha akasema.
“Muite Fazma”
“Mh! Ushaanza majina yako ya mitishamba” alitania Garma huku akimtazama mtoto.
“Hahaha! Babu we koma, usinipangie nisubirie nizae na mie ili uite jina” Rasma alisema huku akionekana kama mtu ambaye alikuwa na furaha hivi.
“Basi sawa, wewe ndio mume sidhani kama napaswa kukupangia. Hakuna shida, ataitwa Fazma” Mayner alisema na kuridisha simu kwa mume wake.
Aliendelea kumtazama mtoto wake huku akimsikiliza mume wake ambaye alikuwa akiongea na Dada yake kuhusu mambo mbalimbali hasa namna ya kuendesha kampuni na ufanisi mzuri wa kukuza biashara ambayo walikuwa wakiifanya.
“Kwahiyo nitakuwa naitwa Mama Fazma, jamani mbona raha. Ahsante Mungu” alijisema ndani ya moyo wake.
Haya ndio yalikuwa maisha mapya ambayo ameyapata, maisha yake baada ya kuwa na mtoto, alikuwa ni mwanamke ambaye tabasamu halikauki katika moyo wake ingawa alikuwa na wasiwasi kuhusu Mama Garma lakini alipoyakumbuka maneno ya mume wake na ile pete ambayo ilikuwa katika mkono wake alijiona anaenda kuwa na Maisha mengine kabisa.
Wakati wakiwa ndani, nje ya nyumba yao ilisimama gari na Mama Garma alienda kufungua mlango ili apate kuzungumza na mtu ambaye alikuwa yupo nje. Ilikuwa ni nyumba kubwa yenye hadhi ya kuitwa nyumba na sio kibanda.
Uzio mkubwa wa tofari ulikuwa katika nyumba hii ambayo haikupokea wageni hovyo, kwakuwa Mama Garma alikuwa anakaa sana nyumbani basi Garma hakuona kama alikuwa na sababu ya kuweka mlinzi pale getini. Mama yake alitosha kufungua na kufunga geti kwakuwa bado nguvu zilikuwa zipo katika mwili wake.
Baada ya kutoka nje alifungua geti, alikutana na gari ambalo alikuwa analifahamu. Katika gari kulikuwa na mwanamke wa miaka kama 27 hivi, hakuwa mwingine bali ni Ninah. Naye alikuwa mahala pale kwa lengo la kuthibitisha kama kweli mtoto amedungwa sindano ama lah.
Ingawa alikuja kwa gia ya kuona kichanga kipya, hii ilikuwa kama sehemu ya kufanya asijulikane haswa sababu ya kuwa pale ilikuwa ni ipi.
“Naona umekuja sasa Mama” Mama Garma alisema huku akiweka tabasamu
“Ndio, na nimetoka kuonana na yule daktari, kanipa damu hii hapa. Sijui utafanyaje” alisema huku akitoa kikopo kidogo katika pochi yake na kumkabidhi Mama Garma
Mkono wa Mama Garma ulipokea kopo lile, akatazama na kuweka tabasamu “Kama atakuja kuzaa labda sio mimi. Aya shuka tuondoke” alisema huku akiweka kopo katika matiti yake.
“Gari siingizi ndani?” Ninah aliuliza
“Mh! Machaguzi yapo juu yako”
“Ok, hakuna shida acha niache hapa” alisema na kutoa funguo kisha alibeba nguo pamoja na vitu vingine vya mtoto ambayo vilikuwa katika kitenga maalumu na kuongozana na Mama Garma, wakaingia ndani ya nyumba.
Walifika hadi sebureni ambapo walikutana na Laila aliyekuwa busy akichezea simu. Ninah alimtazama kisha alimsalimia.
“Nzuri tu, karibu” Laila alisema
“Ahsante”
“Kaa hapo Mkwe nakuja naenda kuwaita” Mama Garma alisema.
Kauli yake ilistua Laila ambaye alimtazama Ninah kwa jicho la kuibiwa hivi “Inamaana huyu ni mke wa Garma au?” alijiuliza bila hata kupata jibu “Au itakuwa ni mke wa ndugu mwingine? Bwana hayanihusu ngoja niendelee kuangalia mchezo tu” alisema na kuendelea kuchezea simu yake.
Dakika mbili mbele alitoka Garma pamoja na Mama yake, akasimama pembeni ya ukuta huku akiwa amekunja ndita.
“Inamaana mke wako humuoni mbona huchangamki?” aliuliza Mama Garma
“Mama! Usitake kunipanda kichwani sijui unanisikia? Narudia tena usitake kunipanda kichwani shauri yako” Garma alisema huku akionekana kuwa mtu wa hasira.
“Khe! Kwahiyo unataka kuniambiaje? Kwamba yule uliyemlaza huko ndani ndio mke wako au? Hivi wewe mtoto una nini mbona hunielewi au hadi nimuue ndio ujue kwamba simpendi na simtaki?” Mama Garam alisema.
Garma hakutaka kumjibu Mama yake badala yake alimtazama Ninah ambaye alikuwa akichezea simu, akamuuliza
“Umepitia mlango gani wakati unaingia ndani?”
“Kwanini? Ninah hakuna kutoka” Mama yaka alisema
“Nitakufumua tokaaaaa” Garma alisema kwa sauti kubwa.
Kuongea kwake kwa sauti kulimfanya Mayner ambaye alikuwa ndani kutoka haraka ili aje aone nini kinaendelea.
“Mume wangu kuna nini?”
“Nawe Malaya koma, acha kuuliza uliza watu hovyo. Msenge nini wewe” Mama Garma alisema huku akimtazama Mayner ambaye alikuwa amesimama, macho amayatoa.
Kilimshuka haswa, alibaki mdomo wazi. Akamtazama Mume wake kisha akasema.
“Baby, punguza sauti mtoto kalala”
“Mtoto au marehemu, kuzaa utazaa wewe. Kazi kumsingizia mwanangu kwamba ile ndio damu yangu mfyuuuuuuuuuu” Mama Garma alidakia
“Siongei na wewe. Nakuheshimu sana usitake nionekane mbaya”
“Tangu hapo umekuwa mbaya au huna kioo ukajitazama jinsi ulivyo, makovu kibao usoni kama caro light hujui ilipo. Mwaya ni 3000 tu inakufanya kuwa mweupe.”
“Unasemaje” Mayner alifoka kwa hasira, moyoni alikuwa na dalili zote za kupigana. Alichokuwa anasubiri ni mkwe wake kurudia alichokisema...
Ngumi kama ngumi🤪.