Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
Follow channel yangu ya youtube kwa simulizi fupi za kusisimua 💗💗
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Brown na Shalha walimtizama Bieber ambaye alimgeukia Nanah na kutabasamu.
Nanah alibaki akimtizama Bieber na kushindwa kumuelewa amepatwa na nini.
"Twende" Bieber alimshika mkono Nanah aliyebaki akiwa ame stuck tu.
Bob Risky alifika na kuutoa mkono wa Bieber kisha akaondoka na Nanah.
Bieber alimtizama Nanah akiwa anaondoka kwa tabasamu mwanana na zito sana tena lililojaa furaha ndani yake.
Brown, Shalha na Bi Everline wao ndo walizidi kumshangaa Bieber kwa namna alivyoweza kubadilika.
"Hii inamaanisha nini? Mbona anamcheka cheka tu? Kwamba amempenda baada ya kumpiga kibao?" Aliuliza Shalha akitoa macho kwelikweli kwa mshangao na wivu.
"Bieber unataka kusema nini? Kwamba umempenda Nanah?"
"Wewe" Brown alimfuata Bieber na kumgeuzia kwake.
"Hicho unachotaka kukianza kiache mara moja"
"Mmmhhhh inauma eee?" Aliuliza Bieber akimchekea kaka yake kisha akawa serious na kumwambia.
"Ndo kwanza nimeanza, dem wako atalipa kwa hichi kibao alichonipiga leo na atakilipia kwa kunipa mwili wake"
"Bieber" aliita Brown akimkwida mdogo wake.
"Wewe mshenzi" aliita Bi Everline alikwenda akampiga kibao cha mgongo Brown na kuitoa mikono yake kwa Bieber.
"Unataka kuniulia mwanangu eee? Uko sawa mziwanda wangu?" Aliuliza Bi Everline na Bieber alimkumbatia mama yake huku akimcheka kaka yake.
Brown aliondoka akiwa amefura kwa hasira kwelikweli, cheko lile la Bieber hata Shalha aliliona na ghafla tu sura halisi ya Bieber ilijirudi.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Amechanganyikiwa au?" Aliuliza Nanah.
"Hata mimi nahisi hivyo"
"Alikuwa akinichekea chekea na kunikumbatia kumbatia sijamuelewa ujue"
"Embu mkono wako" Bob Risky aliuomba mkono wa Nanah na Nanah alimpatia.
Aliushika kwa kuupapasa papasa.
"Kuna nini?"
"Naangalia kama mkono wako ni mgumu, huwenda umeenda kumchanganya ubongo kwa kibao ulicho mpiga"
"Jamani!!" Alisema hilo Nanah na Bob alimwambia
"Hata siyo mgumu mbona wa kawaida? Au ulimvutia sana?' Aliuliza Bob Risky.
"Mi sikumbuki bhana, kwanza nishaacha kazi" alijibu Nanah.
"Umeacha kazi? Uko seriously?" Aliuliza Bob Risky.
"Ndiyo kwani vipi?"
"Kwahiyo ushawalipa million 3 zao"
"Million 3? Million 3 za nani?"
"He eeeeee Million 3 za nini? Kwamba umeachaje kazi bila kutoa Million 3"
"Ndo za nini sasa?"
"Ukivunja mkataba unalipa Million 3"
"Jamani, mshahara wenyewe laki 7 haya hiyo Million 3 ya kuacha kazi mi natoa wapi?"
"We ulisaini vipi mkataba bila kusoma? Yani upande wa designer ndo hivyo ukitaka kuacha kazi ni million 3 uweke mezani ,wao wakiwa hawakutaki ni million 3 wanaweka mezani, walifanya hivyo kwasababu watu wana acha acha kazi sana wakishakuwa maarufu".
"Mmmmhh haya masikini mimi million 3 natolea wapi?" Aliuliza Nanah.
"Kama hauna basi kitulize tu, we shukuru Mungu huyo uliyemzibua kibao ubongo wake umetikisika lakini umekupenda" alisema hilo Bob Risky na kumfanya Nanah acheke.
"Una cheka eeee?" Aliuliza Bob Risky.
Embu twende kwanza.
Bob Risky alimshika mkono Nanah na walianza safari ya kuondoka pale.
"Nanaah!!" Ghafla tu sauti kubwa ya Brown ilisikika nyuma yao tena yenye ukali.
"Kaa mbali na Bieber nimekwambia kaa mbali naye".
"Niache unaniumiza". Nanah aliutoa mkono wake huku akimtizama Brown kwa mshangao .
"Brown unafanya nini hapo?" Aliuliza Shalha akiwa nyuma yake.
Brown alishindwa kusema chochote na kuondoka akitangulia ndani ya gari lake.
Bieber alimtizama ndugu yake na kurudisha macho yake kwa Nanah.
"Twende mwanangu una uhakika uko sawa lakini sindiyo?" Aliuliza Bi Everline.
"Niko sawa Everline" alijibu Bieber.
"Tunaenda nyumbani".
"Mmmhhh hapana, ile ni nyumba yako na Brown"
"Kwanini iwe yangu na Brown tu. Kumbuka baba yako hayupo nilishamfukuza".
"Everline, sitarudi kwenye ile nyumba kwasababu ina kumbukumbu mbaya na chafu kwangu".
"Lakini ni kitu gani kilitokea baina yako na Brown, mbona sielewi".
"Mwambie mwanao Brown akwambie kama anaweza"
"Yeye hataki kuniambia, wewe hutaki kuniambia. Nini kilitokea wiki hizo mbili tu ambazo mimi nilikuwa njee ya nchi?"
"Mama ni vyema usijue".
"Najua ni mwanamke lakini mpaka leo sijamtambua ni nani. Ila siku nikimtambua nakuhakikishia huyo atalipa mpaka na ya huyo mwanamke aliyetembea na baba yako".
"Una uhakika?" Aliuliza Bieber.
"Unamaana gani?"
"Mmmhhhh" Bieber aliguna kwa tabasamu na kuondoka zake akimuacha mama yake kwenye wasiwasi kidogo.
"Amemaanisha nini huyu mtoto? Kwamba mwanamke aliyewafanya wao wawili wakatengana namfahamu au?"
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
Mchana wa siku huyo uliisha na usiku wake uliingia.
Bieber alikuwa palepale kwenye kibaraza chake ambacho mara nyingi amekuwa akimtizama Nanah akiwa anafanya shughuli zake za ndani hadi kwenda bafuni kutokana na pazia lake jepesi lililomuwezesha kuyaona hayo yote.
Na wakati huu alikuwa akitizama kivuli cha Nanah kikivaa kitop chake pamoja na nguo yake ya ndani kisha bukta na kuelekea sehemu ambayo mara nyingi hupenda kukaa na ku design vitu vyake.
Kwa mara ya kwanza tangu Bieber awe anamchungulia Nanah leo usiku aliona akizungumza na simu na alitumia muda mrefu kwelikweli
"Anaongea na nani muda wote huo?' Alijiuliza Bieber akiinuka alipokuwa ameketi na kwenda kuegemea chuma ambazo zipo kwenye ukingo wa baraza yake.
Anaongea na nani muda wote huo? Alijiuliza na kutizama saa yake na ilishatimu saa 6 kasoro.
Nanah alitizama na yeye saa yake na kukata simu.
Alijinyoosha akapanda kitandani na kulala zake huku akizama taa na kuacha taa yenye mwanga mdogo iliyokuwa karibu na kitanda chake.
Bieber alitoka pale aliposimama na kuelekea chumbani kwake sasa.
Alipanda kitandani na kulala zake.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Yani umedhubutu kuja tena?" Aliuliza Shalha alipomuona Nanah kazini asubuhi.
"Kama hunitaki ni rahisi sana, lipia million 3 and am out of this shit".
Shalha alimtizama na kumeza mate yake.
"Huna hela sindiyo? Sasa punguza kiherehere mtoto wa kike"
"Umeniambiaje wewe?" Aliuliza Shalha na kumshika Nanah kola ya shati alilokuwa amelivaa.
"Toa mkono" alisema hilo Nanah na akiweka sura ya kutisha kwelikweli.
Shalha aliondoka mkono wake Taratibu kwani aliona namna alivyokuwa wa tofauti.
"Waambie hao mbwaa wako, wasinisogelee leo nitawaumiza".
Nanah alimpita Shalha kwa kumpiga kikumbo.
"Shalha, huyo ni Bi Mkosi ndo amekupiga kikumbo". Aliuliza Doy.
"Kaeni mbali naye, amekuwa kama mzuka leo"
Doy na Kurwa walitizamana kwa mshangao.
Itaendelea In Shaa Allah.