Asubuhi ilipopambazuka, taratibu za ndoa zilianza huku Mayner akiambiwa aende akaongee na rafiki yake ili awe kama mshenga, na Garma angechagua mmoja wa wafanyakazi wake ili awe sehemu ya washenga pia.
Walitaka kufanya haraka, walitaka kuharakisha jambo hili ili ndani ya mwezi liwe tayari limekamilika. Ilikuwa ni sehemu ya amani kwao bila kujali kwamba mama angependa ama lah. Kuchukia kwa mama ama kupenda kwake kwao hakukuwaogopesha wala kuwafurahisha, zaidi walihitaji kutimiza nusu ya dini. ππ
Mayner alienda kuzungumza na Laila ili wajue wanafanyaje. Alimkuta yupo kazini kwake saloon, naye alimuita pembeni ili wazungumze kwa uzuri zaidi.
βKwahiyo ndio mmepanga mwisho wa mwezi au?β aliuliza Laila.
βNdio, lakini naomba uwe mshenga wangu kama hutojali.β π
βMh! Unajua natamani sana kushiriki katika ndoa yako lakini ile familia uwi, kale ka mama jamani hata sijui nisemaje?β π
βBwana achana naye, sisi ndio tumependana. Hata hivyo nimezungumza na mume wangu, anasema kwamba atafanya utaratibu nyumba ya Buzuruga iishe kwa haraka ili aende kule.β π
βKale ka bi mkubwa kalivyokuwa na mambo ya kishamba atakubali kweli?β
βSina hakika. Lakini Laila, ndoa ni muhimu kwanguβ alisema Mayner. π
Mkono wake wa kulia uliendelea kuchezesha funguo huku akimwangalia rafiki yake ambaye alikuwa kimya kidogo. Akahema na kusema:
βNaijua ndoa kama sehemu ya utumwa, naijua ndoa kama kaburi, naijua ndoa kama msitu mkubwa. Ndoa ni jehanamu tena pale ambapo upande mmoja wa familia ukiwa haufungamani na upande mwingine. Penzi lako tayari kuna mtu ambaye anataka kuingia, sijajua hatima yake ilaβ¦β
βIla nini? Nataka kuolewa, nahisi kama kila changamoto ambayo kwangu inanisumbua itakuja kuisha. Ndio, itamalizika maana ndoa ni baraka. Mungu atapigana nami.β π
βNalijua hilo lakini baraka nyingine huwa na laana, kama hii hapa. Ila sawa, kama ni hivyo, hata hakuna shida,β alisema.
βWe, nikubalie tu au unahisi kwamba nitakusumbua kila migogoro itakapokuwa inatokea?β π€·ββοΈ
βHapana, ila nachokiwaza ni kuhusu maisha yao. Kama ikiwezekana ongea na mume wako kale ka mama yake kasikae pamoja na wewe. Utakonda, utaisha, hata sehemu ya kuvalia wigi utakosa.β ππ©βπ¦±
Yalikuwa ni mazungumzo marefu kidogo, mazungumzo ambayo hatima yake ilikuwa ni kukubaliana na ukweli kwamba lazima Mayner aolewe. Ukweli huu ulikwenda sambamba na kukubali kwa Laila kuwa angekuwa mshenga kwa upande wa kike.
Baada ya mazungumzo, aliondoka na kwenda kazini ambako alikutana na mume wake akiwa katika kikao na baadhi ya wafanyakazi. Naye alisogea karibu yao akiwa kama sehemu ya watu wa ile ofisi.
βJamani, kikao cha leo hakitahusu ofisi ila kitahusu mmoja wa watu muhimu wa hii ofisi,β alizungumza Garma huku akimtazama Mayner ambaye alisogea katika kiti na kukaa. π
Kila mmoja alitupa jicho kwa mrembo huyu mwenye shingo ya twiga, dimpoz kubwa katika mashavu yake pamoja na macho ya kuvutia ambayo yalijaa maji maji hivi. ππ§ Mwanya mdogo kiasi ulikuwa katika meno yake, ulifanya kila anapotabasamu avutie zaidi, huku pua ya kihindi ikipendezesha vyema uso wake na kumfanya awe mwanamke mrembo kuliko hata wafanyakazi wengine ndani ya ile ofisi. π
Mmoja wa wafanyakazi ambaye alikuwa ni wa kike alimtazama Mayner kwa zaidi ya dakika mbili, moyoni mwake akasema:
βInamaana wakati Mungu anamuumba huyu alitumia udongo gani? Mbona amekuwa mzuri hivi?β π
Lilikuwa ni swali ambalo jibu lake lilikosekana, zaidi ni kuondoa macho kutoka kwa Mayner hadi kwa Garma.
βKwahiyo kila mmoja hapa, nahitaji ushiriki wenu katika harusi yangu. Sitaandaa kamati ya ndugu na watu wengine ila watu wa kamati mtakuwa ninyi hapa. Nina jambo la ndoa mimi na mke wangu. Baby, ebu njoo basi,β alisema Garma akamuita Mayner. π
Mayner alinyanyuka kutoka sehemu ambayo alikuwa amekaa huku akiwa na tabasamu ambalo lilifukuzwa na aibu ndogo iliyomkumba. Alifika hadi mbele ya mume wake, akampiga busu shavuni π na kukaa pembeni.
βMayner, nadhani wengi mnamjua. Huyu ndio mke wangu, nampenda sana na ananipenda. Nimekuwa naye kwa muda sasa katika kampuni hii akifanya kazi kama Afisa Masoko. Nimeuona muda mwafaka wa kufunga ndoa na kukamilisha nusu ya dini umefika,β Garma alisema hali ambayo ilifanya wafanyakazi wapige makofi. ππ
Furaha ilikuwa ni sehemu ya kila aliyekuwa mahala pale. Walitabasamu na kuona watu ambao walikuwa wakiwalipa mishahara wanenda kufunga pingu za maisha. ππ Lilikuwa ni jambo jema mno.
βAsante mume wangu. Jamani mimi ni mtu wa aibu sana ila naomba mnipe ushirikiano wenu katika hili,β Mayner alisema. π
βAnh usijali, jamani makofi kwa Mayner ake,β alizungumza mmoja wa wafanyakazi wa kike ambaye alikuwa akimpenda sana Mayner.
Sauti ya makofi ilisikika huku ikiambatana na vigeregere π₯³π. Waliokacheka walicheka, waliokainamia chini kwa aibu waliinamia, ilimradi kila mmoja awe na tabasamu.
βKwahiyo ndoa lini?β aliuliza mfanyakazi aliyekuwa amekaa viti vya mbele.
βWiki mbili kutoka leo, yaani tarehe 17 ya mwezi huu.β π
βBabu we! Kijola changu kiko poa, nitaserebukaje!β π alisikika mfanyakazi mwingine huku akisimama na kutingisha manyonyo yake. π
Mayner aliweka tabasamu. Kwa jinsi ambavyo watu walivyoonesha ushirikiano katika kikao kile, aliimani kuwa ndoa yake ingekamilika na kwenda kwa amani kabisa. Maana penye wengi pana Mungu. π Kupata baraka ya wafanyakazi wenzake wa kampuni anayoimiliki mume wake, ilizidi kumpa amani ya moyo. ποΈ
Muda wa kikao ulikuwa umeisha na kila mmoja alirudi katika majukumu yake. Mayner aliongea na mume wake na kumjuza kwamba anataka kwenda nyumbani ili kuweka mambo sawa, ikiwemo kuandaa chakula. π½οΈ
Kwa Garma hakuona kama kulikuwa na tatizo. Aliamua kumruhusu naye aliondoka mahala pale. Akiwa katika gari aliangalia picha ya mume wake, akaangalia pia picha kipindi ana mimba.
βUsiwe unatazama vitu ambavyo vilikwisha kuumiza. Kama una picha ama video za ujauzito wako basi futa maana ukiziona zitakuumiza zaidi,β aliyakumbuka maneno ya Mwanasaikolojia. π§
Machozi yalianza kumtoka π’. Ilikuwa ni ngumu kwake kufuta picha zile ambazo zilimkumbusha mambo mbalimbali enzi za ujauzito wake. Hakuwa na jinsi, ilibidi azifute kisha akaanza safari ya kuelekea nyumbani. π
Kwa mwendo wa dakika 45 alifanikiwa kufika Busweru ambako alisimamisha gari pembeni, bila hata kutazama vizuri kama kulikuwa na gari nyingine mahala pale. Alishuka na kupiga hatua hadi ndani, lakini alipofika sebuleni alikutana na Mama Garma.
βUnaenda wapi wewe?β Mama Garma aliuliza kwa jazba kidogo huku akimzuia, zuia hivi. π
βShikamoo,β Mayner alijishusha kwa salamu huku akipiga magoti ikiwa kama sehemu ya heshima zaidi. πββοΈ
Macho ya Mama Garma yalisafiri hadi katika eneo la sehemu ya siri ya Mayner, akatazama kama kwa sekunde nne hivi kisha akauliza:
βNa leo umevaa tena chupi ya pink?β π Lilikuwa ni swali ambalo lilimuacha mdomo wazi Mayner, alibaki ameduaa. π³
Hakuelewa kwanini aliulizwa swali kama lile ambalo lilikuwa tata, kutokana na mtu ambaye aliuliza. Alimheshimu sana.
βKajuaje kwamba nimevaa chupi ya pink?β alijiuliza huku akijitazama kama kuna sehemu chupi yake ilikuwa inaonekana, lakini hakuona. π
βKwanini unaniuliβ¦β kabla hata hajamaliza kuzungumza, alimuona Ninah akitoka chumbani kwake huku akiwa ameshika chupi mkononi.
βMama hii hapa nimeipatβ¦β Ninah alisema huku akionyesha chupi kwa juu. Ghafla alikaa kimya mara baada ya kumuona Mayner mahala pale, alipoa na kuficha ile chupi katika eneo la matitiβ¦ πΆβπ«οΈ
Raha ya kununua ipo pale ambapo muuzaji anakuambia, Lipia kwa pesa unayotaka. Leo, simulizi hii unaweza kununua kwa pesa yako mwenyewe. Nitext WhatsApp, namba ni 0717255498. Nunua kwa pesa yako..