Tulitembea umbali mrefu sana mpaka tukafika eneo moja lililokuwa na nyumba kubwa sana ya kifahari hapo nje palikuwa na mkaka akimwagilia maua na pembeni yake kulikuwa na mdada akilisha mifugo kama ng'ombe na mbuzi...... karibu ...yule dada nilikuja nae aliniambia..... Tulisalimiana na wale watu pale nje ...kisha tukaelewa mlango wa kuingilia ndani
karibu ndani..... nilinyanyua dumu langu la maji na kutaka kuingia nalo ndani.....no hii iache hapo nje.....yule dada aliniambia niache dumu langu nje ......nililiacha kisha tuliingia mpaka ndani....mama mama mama....yule dada aliita ......oooh jmn karibuni .... alikuwa ni mama mtu mzima kidogo ambaye alikuwa ni mtu mwenye muonekano wa kidini sana....alivalia sketi ndefu kubwa na kichwani alijifunga upande wa kanga hata na hereni wala mkufu shingoni kwake alionekana mstaarabu sana......alikuja na kutusalimia........mama mgeni wako ndio huyu hapa ......anaitwa sikitu .....sikitu huyu ni mama ambaye utaishi naye hapa atakupa maelekezo yote.......sawa dada ..niliitikia
Mama nina haraka sana naomba tu hela ya boda ili niwahi majukumu ya familia....yule mama alitoa elfu kumi kumi tatu na kumpatia yule dada kisha akaondoka na kuniacha pale.......
Sikitu karibu sana hapa ni nyumbani kwenu pia jiskie fresh jipe uhuru na raha usiogope....sawa mama.....mimi naitwa mama lulu na wewe unaitwa sikitu tayari nimeshatambulishwa kwako .......twende chumbani kwako nikakuoneshe......tulipanda ngazi ghorofani na kufikia chumba kimoja tukaingia ndani.....hiki ni chumba ambacho utakuwa ukikitumia sawa sikitu....sawa mama.
Ingia bafuni uoge kisha uje sebuleni tuongee kwa kirefu zaidi.. niliingia bafuni kuoga kisha nikavaa gauni langu lenye harufu halisi ya mifugo....nilishaizoea harufu ile kwani nilikuwa nikichunga sana mbuzi na ng'ombe kule kijijini......nilienda sebuleni na kumkuta mama lulu akiwa ameketi mezani akiandaa chakula ......meza ilikuwa imesheheni vyakula ambavyo vilikuwa adimu sana machoni kwangu ....ubwabwa nyama juice pamoja na matunda ....daaah nakumbuka kijijini ubwabwa ulipikwa siku ya kuzaliwa kwa yesu krismasi vinginevyo ni mwendo wa ugali na chukuchuku tu....aaaash siyo ishu sana tayari nilishayazoea maisha yetu ya kijijini.......nilikaa mezani
Karibu sikitu pata chakula kwanza halafu tutaongea....nilipakua chakula kidogo tu si mnajua ugeni eeπ€£...nilikula Lkn sikushiba kabisaπ₯......ongeza chakula jiskie nyumbani...hapana mama huwa Sili sana..nilimjibu mama lulu Lkn bado minyoo ilikuwa inahitaji kula tumboni...Lkn ni ugeni tu nikishazoea hapa nitakula kama mchwa ...niliwaza kichwani hahaha.
Tulimaliza kula kisha tukaenda sehemu ya kupumziki na kuanza kuongea .......enhee umetokea wapi sikitu? Natokea nangukuru mama...ohooo sawasawa unamiaka mingapi....20.....okay hapa utakuwa ukifanya kazi moja tu ya kumhudumia mwanangu ambaye ni mgonjwa wa miezi nane sasa hautakuwa n kazi nyingine maana mara nyingi tunakuwa Bize anakoss mtu wa kubaki nae hapa nakupa kampani .....nitakupa laki mbili kwa mwezi maana najua utamfulia utamsindikiza toilet na pia utamlisha chakula maana ni mgonjwa......nilikodoa macho ......haaaaaaa....niliposikia laki mbili ushuzi ulinibana uharisho ukajitengeneza na mkojo ukakaribia kutoto.....ni pesa ndefu sanasana kwanza sijawahi kuishika mkononi......sawa mama hakuna shida niliitikia haraka asije akagairi bureπ€£π€£π€£......samahani mama huyo mtoto yuko wapi...nilimuuliza ...aaah siyo mtoto ni kijana wangu ni kaka yako kabisa ana 30 years Lkn ni mgonjwa na kwa sasa amepelekwa Clinik watarudi saa moja jioni utamuona tu nachoomba jitahidi kumpenda care na kumhudumia vizuri akifurahia nitakuongeza pesa .........mamamamamamamama nikachanganyikiwa.......nikawa sasa na ile hamu ya kuanza kumhudumia mgonjwa π€£π€£...asikwambie mtututu pesa tam........ Twende nikakuoneshe chumba chake.....tuliondoka na kupelekea chumbani kwa huyo mgonjwa.........mama lulu alifungua mlango tukaingia ndani.......jamani chumba ni kisafi sijapata kuona ....kinanukia marashi ya hatari vitu vimepanguliwa effectively yaan ni patamu balaaaa .....kabati limejaa nguo zimepangwa vizuri huwezi kuona mende yoyote nilibaki nimeduwaaa.....hapa ndo chumbani kwake ...mara nyingi anapendelea kunywa yoguart hivyo usishangae kuona Makopo mengi humu anapenda sana .........sawa mama......basi baadae unaweza kupanga panga vzr na kufuta palipo chafuka ...... sasa tafuta nn hapa mbona pasafi sana..niliwaza....tuliondoka na kurudi pale sitting room tukaendelea na story
Tayari ilikuwa ni saaa moja jioni
Piiiip pikipiki pikipiki ilikuwa ni jini ya gari ikilia ..........enheee Robby huyooo amerudi...Robby ndo Nani mana...niliuliza....aaah kumbe sikukuambia huyo mwanangu mgonjwa anaitwa Robby....
ITAENDELEA
FULL STORY UNAIPATA KWA KULIPIA TSH 1000
NAMBA YANGU YA WHATSAPP NA KULIPIA PIA NI 0715906120 MTANDAO YAS JINA LA USAJILI FLORA.