asubuhi na mapema alex aliamka wa kwanza yeye , akanambia ye anatangulia kuweka vitu sawa ,atamtuma mtu aniijie nikasema sawa ,alienda kwenye gari yake akaja na mfuko akanipa
Huku ananiambia hiyo ndio nguo natakiwa kuvaa muda ukifika nikasema sawa
Moyo unanidundaa, mimi ndo mama shuhuri sijawahi hata siku mojaa ,nilikuwa nawaza nikifika nitaanzia wapi niishie wapii leo kazi ninayo ..
Muda wote nilikuwa natizama saa tu muda naona kama umeganda mana masaa hayasogei ,siku ilikuwa ndefu kweliii
Zakia alinipigia simu anipitie twende mana nilimwambia awepo hiyo siku ya ufunguzi na wenzie ili apajue , nilimuelekeza nikamwambia mtaenda tu mi nitakuja kuna sehemu naenda ,sikutaka kuongozana nao kwa sababu ya maelekezo ya alex
Muda ulienda kama kinyonga alievunjwa mguu mmoja , yaani taraatibuuu mpaka nikawa nasema au hii ni siku ingine huenda nilipitiwa usingizi enhee
Mpaka inafika sa kumiii ,nilishajiandaa muda mrefu mpaka nahisi inaanza kunuka jasho sasaa ,
Nimevaa na kiatu kabisa kilikuwa kiatu kirefu gauni nayo ni ndefuu afu mpasuo wake haloo!! Paja lote waziii
Sa kumi na moja nishakata tamaa natamani nimpigie simu alex kumuuliza jamani mama shuhuri huku mmenisahau auuu?? Hee mana nilichoka nahisi nilikuwa nimependeza mpaka nikaanza kujiona kawaida tena hahah
Alex alinipigia simu hiyo sa kumi na moja akanambia toka nje kuna mtu amekuja kukuchukua , jamani nusu nianguke mana sio kwa mbio hizoo .
Nilitoka nikakuta kuna gari , mkaka tu hivi hata simjui akanambia madam ,nimeambiwa nikuchukue , nikasema Asante huku naingia kwenye garii , tukaondoka
Eh bwana nafika SallyFood pamenogaa jamani pamenogaa mpaka nikatetemeka mwili kwa furahaaa , mbele kabisa kulikuwa na picha yangu aisee kubwaaa mwenyewe haa, pamepambwa kila konaa jamani pamependeza sio poaa ,
Wadada wamenoga,shamra shamra kila konaa jamani palipendeza kuanzia watu mpaaka eneo , yule kaka akanifungulia mlango nikashuka watu wotee mwacho kwangu hee afu gauni langu sasa lilikuwa lina bwebwelaa huko nyumaa kama mkiwa wa Tausii Refuuu hatari
"Haya jamani mgeni wetu Rasm, C E O wa Sally V.I.P Food Point , Bibie salmaaa ndo huyu kafika" Mc alijua kunitia aibu jamani nusu niangukeee sijawahi haya mambo mie afu unajua ndo kwanza nilikuwa nimeshuka kwenye gari aisee niliinama chinii,
Kuna mdada hata simjui ,alikuwa amependeza nayeye mmh akaja akanipa mkono akanambia madam ni huku ,hee mie huyu naitwa madam jamani nyiee , akawa ananiongoza mpaka pale mbele kulikuwa na viti viwili nikawa nimeketi hapo hata alex sijamuona kwanza hata kuangaza macho siwezii naanza wapi sasa??
Mc akawa ananipamba hapo jamani nyie watu wapo kupiga makofi tu mie tena uwii aibu hatari kucheka nashindwa afu unajua nipo peke yangu hapo mbele na huyo mc mpenda sifaa ..
" jamani tafrija yetu hii ya leo , kuna point mbili zimetukutanisha hapaa , kubwa na mlilo ambiwa ni ufunguzi wa Restaurant yetu pendwa lakini la pili naomba nisiwe msemaji sanaaaa , tumsubiri bwana mkubwa kubwa haswa alilo tuitia hapa ni niniii??" ..
Mmmh nikabaki nawaza kumbe kuna lingine sa n nini hiloo??" Sec hiyo hiyo nikamuona Alex anaingia eeh bwana yaan leo kauwaa alex aliuwa kila kitu kaka alipendeza mpaka akapendeza tenaaa , nilijikuta namuonea hata wivuuu huyu mkaka mzuri hivii wanataka kunipokonya jamani ,tutauwana aisee
Alex aliingia mc akasema embu mpigie makofi kidogo, Mr kwa alivyong'aa anapendeza kabisa kuzaliwa kwenye koo za kifalmee ,hahaha nikacheka hata kwa sauti
Alex akaja akanikiss kwenye paji la uso wee afu kila mtu ananitazama mie mmh nikainama ndo kabisa akaniongezea aibuh yaan huyu kaka , akaninong'oneza Et umependeza mke wangu hadi naona wivuuu
Nilicheka mana mi mwenyewe nilikuwa namuomea wivu kwa jinsi alivyoonekana super , Mc akasema anaanza Rasmi shuhuri yetu
Alex akachukua Mic akasema
Jamani nawashukuru woote kwa kuja kuungana nasi siku ya leo , nasema asanteni sanaa na karibunii, lakini naomba kabla ya kuzindua huu mpango wetu naomba niwakaribishe hapa ,
Kutakuwa na chakula cha kisasa kabisa na kitapikwa na wapishi wenye uzoefu , popote ulipo chakula utaletewa tena kwa wakati sahihiii , naomba niwakaribisha ,chochote ulichoshika hapo na unakula basi jua kimetengezwa hapa SallyFood Point (all of Us we're VIP) so lazima tujipe heshimaa"
Watu paa!! Paa!! Paa!! Wakapiga makofii nami nikajipigisha vimakofi hapo nilikumbuka naonaga kwenye Tv mume akiwa anahutubia mfano watu wakampigia makofi huwa na mke anapiga kwahiyo nikafata na mimiii
Alex alitulia kidogo afu akaendelea ,
"Lakini leo ni siku moja muhimu sana mwangu siku ambayo haijawahi kutokea kwenye maisha yanguu, " alitulia afu akageuka kuntazama kwa sec , alitoka alipo simama akaja kwangu akanipa mkono huku akinipa ishara nisimame ,nami nikasimama tukasogea mbele kidogo afu akaendelea kuongea
"Mnamuona huyu mwanamke??" Watu wakasema ndio!!
Akasema "she's my woman'"
Watu wooote wakapiga makofii afu akaendelea
"Sikuwahi kujiona mimi ni mkamilifu mpaka ile siku nilipo kutana na salma , salma ni mwanamke alietimia kwangu Yeah labda niseme kuwa kila mwanaume anatamani mwanamke kama huyu lakini mimi nimempata ...
Naomba leo niitumie siku hii kumuweka wazi mwanamke wa maisha yangu mbele ya kila mtu na mumjue , Salma ambae ndie C E O, ndie mke wangu mtarajiwa..."
Jamani hii moment hii nilihisi mimi dunia ni yangu ,nilihisi mie tu ndo nastahili kuishiii kwenye mapenzi yenye raha jamani hii mbona mi inazidi hiyo raha yenyewe
Niliona alex anaenda chini akapiga goti moja , mbele yangu khaa nikashika mdomo wangu huku nimeuacha wazi waaah!!! Baada ya alex kutoa pete akishika mkononi
Akasema Naomba Salma uwe mke wangu , nakupenda "
Machozi hata sijui yalitoka wapi wakati mi nawashangaaga wadada wanaojiliza et wakivishwa petee mnisamehee miee jamani nilikuwa siijui hii moment na wala sijawahi kuifatiliaaa
Nilimpa mkono huku nalia yaani nalia huku nasema asante mungu , Asante kwa huu ushindii , ndoa sooon...
Nilivishwa pete bwana, mbele za watu tena kwa hadhi ya kimamtonii sio kiswahili jamani
Alinikumbatia alex akasema nakupenda kila siku Salma wanguuu
Nikamwambia nakupenda kila sec alex wanguuu hapo tunaongea kila mtu sikioni kwa mwenzie yaani
Basi pale tulipo simama watu walikuwa wanakuja kutupa mkono wa hongera mana hawakuwa na zawadi wala taarifa kwamba kuna watu wanachumbiana ..
Sasa sindo nikamuona Subira unajua sikuwa nimemuona hata mara moja ila nilipo kuwa natoka nyumbani niliongea nae akanambia ye kashafika yupo hapo
Jamani wameongozana na inno ,subira mdogo wangu alivyopendeza hee mpaka nilimsahau hiyo make up ,hiyo nguo yakee nyiee ,afu kilicho nichoshaaa nguo wamefanana na inno aisee tena wanatembea wameshikana mkono mmmmmh nikasema hapa hakuna kaziii hapaaa
"We mbona hujiaminii!??" Subira alinishtua vile nilikuwa namshangaa
ITAENDELEA...
Hii story bado ndefu sanaaa ndio kwanza tupo nusu yake. Saa 10 jion tukumbushanee tuendelee
KWETU morogoro.