Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Pyar Ho Jane Dushman

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMMπŸ’˜πŸ’πŸ’˜ SEHEMU YA (19__20)

30th Jul, 2025 Views 92



"Mama ni nani huyo kijana Aliekuja kuweka umeme???"

"Salma Kwani unawanaume wangap😳??"Dah huyu mama nae nikakata simu nikaona anani changanya tu..sasa huyo alieko nyumbani ni nani lakini??"

Em subiri nikampigia mdogo wangu ,ye bado anaishi na mama hapo hapo nyumbani..

"We subira et hapo nyumbani kuna niniii??"

"Kuna nini niniii!???"

"Si mama ananiambia sijui mnaweka umeme"

"Mmh kwani we hujui nikajua we ndo umemuomba shemu atuekee??"

"Shemu wako yupi ,embu acheni up😒uzi "

"Si shem inno!!!" What😳😳 inno?? Em ngoja nikakata simu kwanza"

Subhanallah yaan huyu inno kaenda kuweka kwetu umeme ?? Afu imekuwaje yaan mpaka wanamuita ita shemeji, amejitambulisha hivyo auu??

Sikupenda hata kidogo nilikata simu ya dogo nikampigia Inno muda huo huo ,nikamuuliza uko wapii?? Akasema nipo tu around vipi Salma??

Nikamwambia naomba tuongee sasa hivi akasema poa ,nakutumia mtu anakufata uje nilipo nikasema poa

Nikaoga nikavaa kijora changu tena kile cha kushindia nilihisi kuwa na Hasira na inno basi tu , kwanini afanye vitu bila kunishirikisha??

Sijapenda bwana pale ni kwetu mi na yeye hatuna makubaliano hayo kwanza wala sina mazoea nae kiasi cha kufanya vitu bila kunishirikisha ..

Ilipita lisaa lizima ndio inno akanipigia simu akasema huyo mtu anaenifata amefika hapo nje kwangu ,nilitoka nikafunga mlango nikaelekea ilipo gari.. nilimkuta tu mkaka kwenye gari nikamsalimia nikapanda .

Akanipeleka mpaka nyumbani kwa inno , mashaallah naye anamjengo wa maana kuliko hata kule kwa kina Felix ila ile nyumba ya alex ni balaa ni bonge la jumba limetuliaaa kama zile nyumba za kwenye movies..

Inno alinikaribisha vizuri tu huku anacheka cheka ,"Karibu mrembo, simu yako imenishtua!!'" Baada ya kukaa inno akaanza mada mi nilikuwa kimya namtazama nimuanzie wapi ila nataka kumchana kweli sivutiwi hata kidogo na mambo anayoyafanya

"Asante inno nilishukuru huku naketi"

"Nimefurahi leo walau umefika kwangu " akachukua juice akanipa ,nikaipokea nikavuta ilikuwa na mlija"

"Inno, Samahani kaama nitakukera lakini hili lazima nikuambie" wakati namwambia nilikua naeka ile juice juu ya meza baada ya kuvuta funda mbili mfululizo kabla ya kuanza kuongea"

"Yes salma ,usijali"

"Siku za nyuma niliwahi kuambiwa umepeleka nyumbani kwetu zawadi na sio mara moja imekuwa mara kadhaa, sikuwahi kukuambia asante naomba leo nikwambie, Asante "

"Aaah usijali salma kawaida wala hukupaswa hata kufanya hivyo hamna kabisa"
Akawa anacheka cheka kama hajiamini hivi mi namkata tu jicho tena kavuu namtafutia upenyo bado"

"Inno , tumejuana kwa muda sasa, lakini mi nawewe hatuna ukaribu kiasi hicho mpaka kufikia hatua uliyo fika... "

Nikatulia nikawa namtazama ile kujiamini yote iliisha kabisa ,akabaki anatoa toa tu macho ,Afu sikumpa nafasi ya kujibu nikaendelea hapo hapo

"Unaweza kuniambia kwanini unaenda kufanya vitu nyumbani kwetu pasipo kunishirikisha mimii?? Leo hii umeenda kuweka umeme ni sawa kutusaidia ila nataka kujua kwanini unafanya bila kunipa taarifa? Na kwasababu gani unafanya ??"

Inno alishusha pumzi ,afu akanitazama kwa zaidi ya dakika Moja ,huyu kaka anamacho mazuri ni mzuri tu kiufupi tena weusi wake umetulia kwelii ,ilibidi nikwepeshe macho yangu mana sikuona Dalili ya yeye kuacha kunitazama usoni

'"Salmaaa!!! Mi pia naweza jiuliza hivyo hivyo kwanini nafanya?? Sikuhitaji kuongea na wewe leo wala mazingira haya siku zote niliaamini muda wa kuongea bado"

Salmaa Samahani kama kuna mstari nitakuwa nauvuka Nisamehe sana ,lakini kwako nimeshindwa kabisa kusimamia hsia zangu ,

salma najua nitakuwa labda aahhmm yaan ,yeah Salma ukweli ambao siwezi kuudhibit niii.. nakupenda sana Salma nakupenda sijui utanichukulia vipi lakini please isiwe tu kunikatalia ,,

Nipe nafasi salma nakuomba mama angu nakuombaa , nafanya yote hayo sio kwasababu natak kuununua moyo wako noo!!! Nafanya kwa sababu moyo wangu unataka nifanyee.... "

Mungu wangu wee nilijua vizuri sana kama huyu kaka hili ndio analo waza nilimjua tangu mwanzo macho yake hata mambo yake ,

na siku hiyo nilijiandaa haswa maana sijawahi kuwa hata na chembe ya hsia nae , mimi nampeenda Alex na sio yeyeeee Nampnda alex mimiii sio inno...

Mimi ninapo muona alex nakuwa na amani sana ,nafurahi kuliko nikimuona mwanme yeyote yulee hata mama angu nikiwa nae sijawahi kuwa na furaha kama ninayoipata nikiwa na alex..

Ni bora nimwambie inno ukweli ili aondoe matumaini kwangu..nilijivika ukakamavu nikasema moyoni hapa namchana ukweli yaan natoa duku duku langu wala simpi moyo

"Inno Asante kwa muda wako na kila kitu lakini unacho kitaka kwangu hakita wezekana hata kama ukanipa miaka elfu ya kufikiria ,jibu langu litabaki hili ,mimi nawewe hatuwezi kuwa,"

"Acha sasa kila kitu unacho fanya achaa tafadhali..."nilimaliza kuongea nikainuka kwa ajili ya kuondoka, kabla hata sijapiga hatua inno akanishika mkono akiwa naye amesimama"

"Noo!!! Salma nilitanguliza Samahani nafikiri huu haukuwa muda sahihi wa kukuambia hilii, naomba usinijibu kwa panic mi naweza kusubiri mpaka utakapo kuwa tayari "

Nilimgeukia tena nikiwa Serious nikamwambia

"HAIWEZEKANI INNOOO NIELEWE" niliongea kwa sauti kalii tena yenye uchungu nilimkazia inno macho yote mawili bila kuyapepesa.."

"Nikamwambia unamjua alex ,sijui ni kaka yako au mdogo wako ,si unamjua eh??yule Alex anaujua mwl wangu ukiwa hauna ng..ΓΉo"

"Namimi ninamjua akiwa hana ng..ΓΉo si hilo tu mimi hapa inno NAMPNDA ALEX yule Alex ndugu yako nampenda sanaa mimi sikutaki wewe namtaka yule ndugu yako ndo awe mtu wangu"

"Kama ukiweza tafadhali kaa mbali na utuache na amani acha kila kitu unachowaza kuhusu mimi kwa sababu kamwe siwezi kuwa na wewe inno"

Nilimaliza kuongea nikaondoka bila hata kusubiri neno la inno ,inno alikuwa amepigwa na butwaa mdomo wazi ananitazama haamini kabisa kama yale maneno nimeongea mimi..

Hata mimi niliongea kama naropoka tu wala sikupanga kuongea yote hayoπŸ˜”πŸ˜”nimeshasema hadi habari za kumpnda Alex vipi kama inno atalifikisha kwa alex ,

huyo Alex atanichukuliaje na alishasema hana hsia na mimi, vipi akikasirika kama mimi nilivyomkasilikia inno?? Nilijikuta natembea kama zombi..

Nilifika getini mlinzi akanifungulia geti inno wala hakunisemesha ni wazi hakutegemea nilicho mwambia ,alijua mimi ni wake eeh

Nilitoka nje ,sijui naelekea wapi ,sina hata kumi zaidi ya simu yangu ndio nilibeba wakati natoka nyumbani ..

Nilisimama pale nje kama dakika 5 ,nikasikia napigiwa honii ,nilipo geuka alikuwa yule kaka alienifata nyumbani ,akanambia ingia nikupeleke

wala sikujibu nikaingia kwenye gari mpaka kwangu ,akili ilikuwa imechoka naye muwaza ni inno natamani nimwambie asimwambie alex chochote lakini naanza wapi..

Nikatembea zangu kuingia ndani ,ile namalizia tu mguu wa mwisho, nyie hii siku yangu ni siku ingine tena ambayo ilikuwa mbayaaa siwezi kuisahu kabisaa...

Nilishangaa navutwa kwa nyuma kijora kika chanika nikaangukia mgongo , sijakaa vizuri bado nawenge naona teke la uso nikajiinua kwa kasi kukwepa bado sielewi nini kinaendelea mara watu tayari washajaaa

Maisha yangu yamekuwa na heka heka siku hizi hili sijamaliza kulivutia pumzi linakuja hiliii haya sasa niliinua uso kumwangalia anaenipga si mwingine alikuwa mzee Amos .

Watu wameshamshika anang'ang'ania wamuache anifunze adabu sijui mi mly yaan maneno kibao nikawa hata simuelewi ,baba mwenye nyumba akaniuliza salma kwani kuna niniii??

Nikasema mi hata sielewi naona tu navamiwa hapa , muda huo mwenye kiti akawa amefika
Akamuuliza mzee Amos kwanini unakuja kumfanyia bint wa watu fujo mbona huyu dada hanaga hata shida hapa tangu amehamia??

"Huyu mwanamke mpuzi sana kaenda kumtafutia watu wampige mke wangu , yaan anatafuta wahuni wampige naomba twende police naomba twende policee ,hili siwezi kulivumilia "

Khaa nikabaki kushangaa mimi na kutafuta watu wapi na wapi ??

Mwenyekiti akamwambia mke wako anakaribu mwezi wa pili hayupo hapa mjini haya kapigiwa wapii?? Mzee amos akabaki anatoa macho tu et akasema mke wangu mdogo ,

khaa yaan watu wote wakaguna na huyo juddy wake washamchoka aisee , akaambiwa mwite juddy hapa aseme hao watu wamempigia wapi ,

akasema ameumia sana hawezi kutembea, mwenyekiti akamwambia mzee amos fanya mambo kama mtu mzima wewe ,huwezi kumkurupukia bint wa watu haya kama umemuumiza hapa?? ,

utafanyaje hapa ni kwake una uhakika kama juddy amepigwa na watu ambao amewatuma salma , et likasema hawezi kusema uongo mfyuu yaan linanikera hili zeeπŸ˜’πŸ˜’

walai nngekuwa na uwezo ningelihamisha duniani likapumzike kwanza kwa mungu hukoo , nilijikuta namsonya kwa nguvuuu .

Basi mwenyekiti akamsema sana mzee Amos, akamwambia aende kuongea vizuri na huyo anaemwita mke wake aseme amepigwa na nani na sio kuja kupigana hovyo na mabint za watu .

Wakawa wameondoka , na watu wakasambaa ,namimi nikaingia ndani huku nalalamika mwenyewe moyoni..

Nikachukua maji nikaenda kuoga , lile tukio la mzee Amos nikalisahau akili yangu ilikuwa imetawaliwa na Alex tu..nimeshasema huko mambo kibao sijui atayachukuliaje akiambiwa..

Nilioga nikiwa namuwaza alex tu muda ulizidi kusonga nikawa nakumbuka mara ya kwanza mimi kuonana na Alex ni kweli aliniona nikiwa mtpu lakini hatukufanya kitu..

Hata mimi pia nilimuona akiwa na ng.uo yake ya ndn tu hajawahi kuniambia kama ananpnda lakini nikimwangalia macho na matendo yake yanasema kitu juu yangu..

Giza liliingia nikawa nimejilaza kitandani, nawaza tu mambo yangu sielewi maisha nimeyaharibu au vipii hata sijui , huyu Juddy sasa atakuwa kweli kapigwa au anaigiza ,

Na kama kapigwa sijui kapigwa na nani na kama kweli kapigwa afadhali wamemkomesha anajikuta sanaaa huyuu kidudu mtu...

Wakati nayawaza hayo ghafla Nilishangaa mlango umefunguliwa bila hata hodi,nilishtuka akili yangu ikasema huyu hapa mzee Amos amerudi tena huyu mzee atakuja kuni ua walahπŸ₯Ή

Nilijikurupua kitandani kwa uoga huku najuta kwanini sikufunga mlango..

Wakati najiweka sawa kwa lolote ghafla nikashangaa anaeingia ndani sio mzee Amos bali ni Alex😳😳baada ya kumtizama Alex usoni niligundua jicho lake moja limevimba na limekuwa jekundu sanaa kama amepigwa ngumi,

Usoni pia alikuwa na michubuko halafu yupo Serious sivyo nilivyomzoea kabisaπŸ₯ΉπŸ₯ΉπŸ₯΅

Nilimsogelea haraka huku namuuliza kuna nini Alex?? Nilimuuliza huku nikiwa na hofu ya kweli moyoni..

"Alex ni niniii!!!" Nilimuuliza tena baada ya ile ya kwanza kutojibiwa😒 wala hakunijibu tena nilizidi kuogopa nikabaki nimetulia tu nawaza mungu wangu sijui hata itakuwaje.."

Alex alizidi kuniangalia mpaka nikawa nashindwa kumtizama.. nilikwepesha macho nikawa naangalia pembeni..mawazo yalienda mbali zaidi nikawa nahisi kuchanganyikiwa..

Alex alipiga hatua mpaka sehemu niliposimama aliukamata uso wangu bila kusema neno ,nilibaki mwili unanitetemeka baada ya kuhisi radha ya mat ya alex kwenye mdmo yangu..

KHEEE ILIKUWAJE KWANI???

KWETU morogoro.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

NILIZANI MWIZI KUMBE MMMMπŸ’˜πŸ’πŸ’˜ SEHEMU YA (19__20)  >>> https://gonga94.com/semajambo/nilizani-mwizi-kumbe-mmmm-sehemu-ya-19__20
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Pyar Ho Jane Dushman
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
offa ya msimu wa nanenane
offa ya msimu wa nanenane

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

majario rewards 100 Comments 0
 

A.J.A.D SE03 EP02

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest