Imeandikwa na Salma Rasheed Ramadhani
Mawasiliano: 0763 595006
Kujiunga na Channel yangu ya WhatsApp : https://whatsapp.com/channel/0029Vb5TUYyG8l5677chYs0Y
*ONYO*
Hauruhusiwi kunakili simulizi, kufuta au kuongeza kitu chochote bila idhini yangu.
KARIBU
Alitoka na kurudi muda ule ule.
Nanah!! Aliita kwa tabasamu pana na kuzama ndani ya ofisi ya Bieber.
"Ooohh!!! Kumbe unakula? Sikukuona sehemu ya kula nikahisi tu utakuwa hujala so nikakubebea chakula".
"Asante' alijibu Nanah akimuonyeshea ya kuwa anakitu mkononi mwake chakula.
"Basi itabidi ule vitu vyote rafiki yangu, au Mr Handsome unasemaje?" Aliuliza Bob Risky huku akimchekea Bieber.
"Ni sawa maana hata hayo ma apple anayokula siyo chakula chamaana". Alijibu Bieber.
"Umesikia Mr Handsome kasema ule".
Bieber alimpatia ule mfuko na kumbusu shavuni kisha akaondoka zake.
Bieber aliinua macho yake akimtizama na alimuuliza Nanah.
"Ni rafiki yako?"
"Ndiyo"
"Yani umekosa marafiki wa kuweka hadi uweke urafiki na mashoga eee?"
"Umeona ofisi nzima hakuna anayenipenda hata mmoja Bob pekee ndo mwenye roho ya upendo juu yangu".
Bieber alimtizama bila kumjibu kitu na alirudisha macho yake kwenye karatasi alizochora Nanah akizidi kuzipitia pitia.
"Unajua huku juu huwa unafanya vizuri shida chini ndo humaliziagi kwanini?' Alihoji Bieber.
"Chini kunanipaga wakati mgumu sana kumalizia na napenda nikae nikiwa nimetulia kabisaa ndo nimalizie".
"Ehaaaaa ni vizuri pia" alijibu Bieber.
"Ila michoro yako yote miwili kwangu imekuwa plain sana, embu tafuta kitu cha maana ambacho atavaa atakaye host siku hiyo, tena mimi na mawazo yangu haya nilikuwa nimependekeza anaye host asiwe mmoja tena wawe wawili".
"Wanawake wawili? Mmmmhh naona kama haitavutia bora abaki tu mmoja"
"Wapi nimesema wanawake mimi?"
"Means mwanaume na mwanamke?"
"Yeeeeh tena wafungue kwa dance flani hivi ya taratibu unaonaje?"
"Wazo zuri".
"Sasa hao ndo nataka nguo zao mbili, ya ku dance, alafu ya ku present sasa kama ma hostess".
"Nimekuelewa Boss".
"Nashukuru Sekretari Wangu Nanah, nisikuchukulie muda wako sana. Unaweza ukaenda ili uendelee na kazi yako. Ila make sure unakula chakula ndo ufanye kazi".
"Sawa" alijibu Nanah akitabasamu na kupokea karatasi zake kutokea kwa Bieber akiinuka.
"Nanah" aliita Bieber akim stopisha Nanah aliyefika mlangoni.
"Yes Boss".
"We mrembo sana".
Nanah alibaki akiwa ame stuck na kumshangaa Bieber aliyeachia tabasamu.
"Asante" alijibu kwa sauti ya upole tena baada ya sekunde 10 kupita na kutoka njee ya ofisi ile.
Aligeuka nyuma na kuitizama ofisi ile aliyopo ndani Bieber.
Alienda kuketi na Bob alikuwa akimtizama kwa macho makali kwelikweli.
Alipoketi Nanah na kumtizama Bob, Bob Risky alijenga tabasamu na kuinuka haraka haraka akimfuata.
"Vipi amekwambia nini?"
"Hamna ni kazi tu amenisisitiza niimalize kwa haraka".
"Ooohh!!! Nilidhani amekwambia anakupenda"
"Bob!!" Aliita Nanah akimtizama kwa kumshangaa.
"Yeah anaonekana kama anakupenda".
"Natumaini mimi ndo nitakuwa mtu wa mwisho wa kupendwa na Bieber".
"Hahaha unamaanisha kwamba Kama nitabaki mimi na wewe Bieber atanipenda mimi?" Alihoji Bob Risky
"Hahahahah" alicheka Nanah na kumjibu kwa utani.
"Ndiyo, yani mimi siingi kwako hata kwa sekunde ujue"
Bob alitabasamu na kumwambia
"Nafurahi kwakuwa umetambua ukweli".
Aliondoka na kurudi kwenye kiti chake akiwa amejawa furaha kwelikweli.
"Hawa ushoga wame uanza lini?" Aliuliza Doy
"Mmmmhhh namimi ndo nashangaa. Yani hapa ndani wewe na mimi ndo tunaonekana kama mashetani nakwambia".
"Hili naenda kumwambia Madam Shalha"
Doy mwandishi habari wa kujitegemea aliinuka ili kupeleka umbea wake sehemu husika.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Kaniitie Nanah" aliagiza Brown.
"Sawa" alijibu Sekretari wake na kutoka.
"Nanah, Boss Brown anakuita".
"Mimi?" Aliuliza Nanah akishangaa.
"Ndiyo"
"Sawa nakuja" alijibu Nanah na Bob alikuwa akimtizama tu chini kwa chini.
Aliinuka na kutoka pale ofisini.
"Mchawi mkubwa wewe" alisema hilo Bob akimtizama kwa hasira Nanah na Kurwa aliliona hilo.
"Vipi mwenzetu mbona unamtizama shoga ako kwa hasira hivyo".
"Nyamazaaaa" alifoka kwa sauti kubwa hadi kumshtua Kurwa aliyeshika karatasi lake na kuendelea na kazi zake.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Nini? Bob anampenda Bieber? Ni uchafu gani huo?" Alihoji Doy.
"Hahahah, mwache huyo Nanah ataonyeshwa kazi. Naamini Bob anamtosha yani baki kimya kama hutambui chochote kinachoendelea. Mwache amfanye adui yake rafiki yake atakutana nacho huko mbele kwa mbele".
"Mmmhh lakini inatisha, yani Bieber atawezaje kuwa na Bob huyo mwanaume mwenzake? Bob amelitolea wapi wazo hilo la kijinga namna hiyo?"
"Amelitolea kwangu" alijibu Shalha na Doy aliguna
Mi naenda kisha akaaga na kuondoka zake.
👠👠👠👠👠👠👠👠👠👠
"Umeniita Boss Brown".
"Kaa pale".
Nanah alienda kuketi na kumtizama Brown aliyeinama akabeba kitu chini ya meza yake na kumfuata pale alipo.
Ulikuwa mfuko ule ule ambao Bieber alimpatia awali.
"Sijakuona kule wakati wa kula, hivyo nikasema nikubebe kitu kidogo ili ule".
"Asante ila Bieber aliniletea kitu cha kula"
"Bieber?" Aliuliza Brown
"Ndiyo Bieber".
"Mmmhh kwahiyo Bieber unamuita Bieber alafu mimi ndo unaniita Boss Brown sindiyo?"
"Hapana nilikuwa namaanisha Boss Bieber".
"Lakini sivyo ulivyosema awali Nanah" alijibu Brown tena kwa sauti ya hasira.
Nanah aliinua macho yake na kumtizama.
Brown alitoa pumzi yake njee na kuzungumza kwa sauti ya chini.
"Nanah, Bieber hawezi kuwa mtu mzuri kwako. Namfahamu mimi yule ni mdogo wangu mimi jamani".
"Lakini hakuna chochote kinachoendelea baina yetu".
"Kipo Nanah, kipo imagine umeshaanza kumuita Bieber na mimi unaniita Boss Brown. Inamaana umeshanisahau mapema hivyo Nanah? Au mapenzi yako juu yangu hayakuwa ya kweli?"
Nanah alimtizama Brown kwa kumshangaa kisha akamezea maneno aliyotaka kuyasema juu yake.
"Tafadhali kama hamna kingine naomba niondoke".
"Umesha mmisi tayari sindiyo?" Aliuliza Brown
Shalha aliingia pale bila kubisha hodi na hiyo ilimpa uhuru Nanah kuinuka pale na kuondoka.
"Amefuata nini hapa?" Alihoji Shalha.
"Hilo swali nikuulize wewe umefuata nini hapa?"
"Mimi ni mkeo Brown, hupaswi kuniuliza hilo swali".
"Nitakuuliza kwasababu hapa ni ofisini na siyo chumbani kwetu. Umefuata nini ofisini kwangu?"
Shalha alimtizama Brown na aliona kabisa amesha badilika hadi masikio yake na kuwa mekundu kama nyanya.
"Nimekuja kukuletea sketch ya nguo ambazo nita present siku ya ......"
"Mpeleke mchumba wako Bieber yeye ndo anahusika na hii events iliyopo mbele yetu"
"Mchumba wangu?" Aliuliza Shalha
"Ndiyo au siyo mchumba wako tena?"
"Mmhh hivi Brown mbona kama hasira za huyo mchepuko wako unataka kunipa mimi?"
"Toka ofisini kwangu Shalha sasa hivi"
Brown alikaza macho yake kwelikweli na kumfanya Shalha aondoke bila kusema lolote.
Alielekea ofisini kw Bieber moja kwa moja na kuwapita wote bila kusema neno.
Alitupa file lake mezan kwa Bieber.
Bieber aliinua macho yake na kumtizama kisha akatizama file alilotupiwa mezani alafu akarudia tena kumtizama akisubiria maelezo kutoka kwake.
Lakini Shalha alibaki kimya tu akiwa ameifunga mikono yake kwa hasira.
"Vipi unahitaji maji?"
"Yanini?" Aliuliza Shalha.
"Kutuliza hasira zako, au unataka nikukumbatie ili utulize hasira zako kama nilivyokuwa nikifanya tulipokuwa wapenzi?"
Itaendelea In Shaa Allah.