Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

SIMULIZI : NYOTA YANGU SEHEMU 07

31st Jul, 2025 Views


SEHEMU 07

ENDELEA.......
Nilimsogelea kwa ukaribu na kukaa pembeni yake. Aliponiona nipo pembeni yake. Haraka alijifuta machozi na kujitengemeza vizuri usoni. Samir alitengeneza tabasamu bandia usoni mwake ila moyoni nilijua ana umia.

Nilinyanyua mkono wangu na kumshika bega japo sikuwa na jiamini sana mbele yake kwasababu sikuwa nimemzoea kabisa.

Baada ya kumshika bega Samir alinitazama huku akiwa anatabasamu. Nilimuangalia Kwa macho yenye utulivu huku nikiwa na tabasamu hafifu pia.

"Nisamehe kwa kilichotokea, Samira,". Kabda hajamaliza kuongea nilimnyamazisha kwa kumuwekea mkono wangu mdomoni mwake. Alibaki ananiangalia tu na mimi niliendelea kutabasamu.

"Usijali kabisa kuhusu Samira. Nakuahihishia lazima atabadilika na kuwa mtoto mwema".

"Nimefanya Kila njia kumbadilisha mwanangu ila nimekwama. Naumia mwanangu Bado ni Binti mdogo ila amekuwa na mambo yasiyopendeza. Samira haniheahimu sijui ananichukuliaje, Nadra kumbadilisha Samira huwezi si unaona kwanza anavyokuchukulia?, naomba uwe nae makini na umpuuze. Nisamehe pia kwa kukuvunjia heshima ila ndivyo alivyo". Samir aliongea hayo Kwa masikitiko. Nilimuonea huruma sana.

"Nakuahidi lazima Samira atabadilika. Nitasimama kwenye nafasi yangu kama mama na pia nitakuwa rafiki yake mzuri ambaye naweza kumjenga na kuhakikisha anakuwa Binti mzuri, mtulivu na mwenye heshima".

"Ni sawa". Samir aliitikia lakini aliamini haiwezekani Samira kubadilika. Katika kupepesa pepesa macho yangu ndipo nilikutana na picha kubwa ukutani juu ya kitanda. Ni picha ya mwanamke mrembo, baada ya Samir kuniona naangalia Ile picha alizungumza.

"Ni mama Samira. Ameshatangulia mbele ya haki. Nadhani nilishakwambia kuhusu yeye?"

"Ndiyo, uliniambia. Alikuwa mrembo mno".

"Yeah, sema kazi ya MUNGU Haina makosa".

"Ni kweli kabisa".

Samir alitoka chumbani aliniambia yupo chini sebleni mala Moja. Nilibaki mwenyewe chumbani.

Muda mchache alikuja mama na mama mdogo. Walikaa pembeni yangu. Mama mkwe wangu alinishika mkono wangu Kwa mikono yake miwili.

"Sijui kwanini nimekupenda Kwa moyo wote. Najikuta tu nakupenda Nadra".

"Kwakweli dada huyu mwanamke ana kitu na naamini kupitia yeye mambo mengi humu ndani yatakuwa shwari. Hata mimi amenivutia sana sio Siri. Karibu sana mkwe wangu Nadra na yote utakayokutana nayo vhukulia kama mtihani tu wa maisha na utapitia sawa". Mama mdogo aliongea hayo.

"Sawa nimekuelewa".

"Nadra. Mwanangu tangu afiwe na mke wake hana furaha. Samir alimpenda sana mke wake na mbaya zaidi kifo chake kilikuwa Cha gafla sana. Alipata ajali na kupoteza maisha. Nisiwe muongo. Samir amekuoa wewe kwaajili yangu. Mimi ndiye niliyemlazimisha akuoe na naamini nipo sawa kukuchagua wewe. Mapungufu utakayomuona nayo naomba umvumilie na pia Fanya kadri ya uwezo wako kumfanya akupende kuliko alivyompenda mke wake.

"Samir alimpenda sana mke wake mama Samira ila siku zote hakuwa na amani mwenye ndoa yake kutokana na tabia za mke wake. Nisingependa kuongelea mapungufu ya marehemu ila kiufupi hakuwa na sifa nzuri, naweza sema huenda Samira amelithi Kwa mama yake.

"Mwanaume anapenda amani ndani ya nyumba, haeapendi makelele. Naomba uwe mtulivu na umpe amani mwanangu. Naamini ukimpa amani atakupenda kuliko alivyompenda mama Samira". Mama mkwe wangu aliongea hayo. Nilimuelewa vyema na kumuahidi nitaishi vizuri na mwanae.

Nilifurahia pia namna walivyonipokea Kwa upendo, unaambiwa hakuna Raha ukweni kwama kupendwa na mama mkwe. Basi mie mkwe wangu Hana baya alinipokea Kwa mikono miwili mwenyewe.

Wakina mama walitoka chumbani. Muda mchache Samir aliingia akiwa amebeba sahani ya chakula. Aliweka chakula kwenye meza ndogo na kunikaribisha.

Nilienda kukaa kwenye kochi na kuanza kula.
"Wewe mbona hauli?". Nilimuuliza Samir.

"Hapana usijali kuhusu mimi, kula upumzike maana najua umechoka". Sikutaka kulazimisha maana angeniona wa ajabu na vile hatujazoeana. Niliendelea kula yeye alikuwa amejilaza kitandani anachezea laptop yake. Nilipotosheka nilijisafisha, nilibeba vyombo ili kupeleka jikoni hata hivyo sijui jiko lilipo.

"Hauluhusiwi kutoka chumbani Kwa Sasa mpaka pale utakapomaliza fungate. Acha ntavipeleka Mimi". Samir aliniambia. Niliacha vile vyombo Samir alikuja kuvibeba akatoka navyo chumbani.

Baada ya dadika chache aliludi alinikuta nimelala kitandani. Alipanda na yeye kitandani na kujilaza. Yeye alilala kwa kuangalia juu ya paa na mimi nililala ubavu. Usiku wa fungate yetu haukuwa kama ule wa Wana ndoa. Kwetu ilikuwa tofauti. Tulilala pasipo kushiliki tendo na hata kugusana miili yetu.

Palikucha asubuhi. Niliamka kwa kuchelewa kidogo. Nilitazama kando yangu sikumuona Samir. Nilishuka kitandani na kuingia bafuni kujimwagia maji. Baada ya kumaliza kuoga nilitoka bafuni ndipo niliona karatasi ya mwandishi imewekwa mezani.

"Matumaini yangu umeamka salama. Sikutaka kukusumbua. Nimetoka mala Moja tutaonana badae Nadra". Baada ya kuusoma ule ujumbe mfupi wa maandishi nilitabasamu.

"Sikumbuki mama nilikuja na begi la nguo zangu uwiiii!. Nitavaa nini Mimi?". Niliongea hayo mwenyewe na kukaa kitandani. Nilifikilia kwa muda mrefu na kuvunja shauri. Nilisogelea kabati la nguo la Samir nilifungua. Ajabu nilikuta nguo za kike.

"Imaana Bado tu nguo za mke wake amezihifadhi kabatini. Huyu jamaa ni kweli alikuwa na mapenzi mazito sana Kwa mke wake". Mala mlango uligongwa nilinitrngeneza vizuri na kumluhusu amayegonga mlango aingie.

Mlango ulifunguliwa aliingia mama mkwe wangu.

"Umeamkaje mkwe wangu".

"Salama mama, na wewe upoje?".

"Nipo salama. Nimekuletea chai".

"Nashukuru mama". Mama Alitaka kutoka chumbani ila kabda hajatoka nilimuongelesha.

"Mama samahani. Nahisi mama hakuwapa nguo zangu. Sina nguo za kuvaa".

"Onhooo! Kwanza kawaida yetu waislam mtoto wa kike akiolewa haondoki na nguo kwao siku hiyo hiyo. Pia anakuwa ameandaliwa nguo za kuvaa Kwa mume wake na baada ya kumaliza fungate ndipo anaweza kwenda kwao kufuata vitu vyake".

"Anhaa sawa".

"Kuna nguo zako zipo humo kabatini, Samir hakumwambia?".

"Hapana hajaniambia". Mama alilisogelea kabati alilifungua na kuniambia.

"Hizi nguo zote unazoziona ni zako. Ni mpya kabisa. Samir alizinunua na kuzihifadhi humu". Mama aliongea hayo nilibaki nimeshangaa. Nilijua nguo zile ni za mama Samira kumbe zilikuwa mpya na special kwaajili yangu..... ........MUENDELEZO 1000. KARIBU KULIPIA KWA NAMBA 0743770612 JINA JOFREY.

UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAPP KWA NAMBA 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : NYOTA YANGU SEHEMU 07  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-nyota-yangu-sehemu-07
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest