_______________________________________
Nimefika chumbani nikamuuliza mtoto shida ni nini “ nimeota wamekuja kukuchukua na wewe wanataka kukuuwa…
“ usijali mwanangu hio ni ndoto tu na hakuna mtu ambae anaweza kunifanyia kitu chochote maana nina amini wewe pamoja na baba yako mnanilinda, nikasema na mwanangu akanikumbatia kisha akasema “ wakija nawapiga bunduki…
Basi paul alipika chai kisha tukanywa na baada ya kumaliza kunywa aliniita na kunambia kuwa ule muda wa kufunga ndoa kihalali mimi nay eye umefika, sikuwa na chaguo zaidi ya kukubali, akanambia kuwa anaenda kuangalia utaratibu wa namna harusi yetu itakavyokuwa…
Basi baada ya siku kadhaa ndio ikawa siku ya ndoa yetu, na paul akampeleka Jordan kwao maana alikuwa anawazaz wote ili waweze kumuangalia mtoto baada ya ndoa, ili walau tukale honeymoon nyingine na kama ikiwezekana tutafute katoto kengine…
Tunamshukuru mungu ndoa ilipita salama, ila nikashangaa mume wangu ananiambia kuwa tunatakiwa tukale honeymoon yetu kwenye royal hotel, sikukataa, na ajabu akachukua kile kile chumba ambacho ndio mwanzo wetu ulianzia hapo…
Chumba kilirembwa na paul akanichukua mpaka chumban na baada ya kufika nikashangaa mwamba ananikumbatia kisha akanikalisha kitandani na kunishika mikono huku akiwa anasema “ sijui kama hichi chumba kina kupa kumbukumbu mbaya au kumbu kumbu nzuri, ila ukweli ni kwamba mimi nakipenda sana, maana bila chumba hichi nina uhakika hata leo nisingekujua, ndani ya chumba hichi ndio mwanzo wa furaha yangu ilipoanza ingawa nilichelewa sana kuijua furaha yangu kama inaanzia hapa au laa, na ndio chumba ambacho kilizika mapenzi ambayo yalikuja kufufuka baadae, na kwa mara ya kwanza kwenye chumba hichi nilifanya mambo mengi bila kujitambua, ila leo natamani uhuhisi uwepo wangu, uhisi miguso na mapapaso yangu, maana nataka uone kila kitu na mimi nifanye kila kitu kwa akili zangu tumamu nikiwa najitambua, chichi unajua wewe ni zaidi ya zawadi kwenye maisha yangu, ni nuru ambayo huwa inakuja kila ambapo najihisi nipo gizani, ni faraja ya moyo na maisha yangu, na nitabasamu ambalo huwa lipo hai kila unapokuwa karibu yangu, na ndio mwanamke ambae umegusa mapigo ya moyo wangu, na urembo wako, pamoja na namna ambavyuo unajali ndivyo vilinifanya niwe kama kichaa kwako, na kwa mara ya kwanza ulipokuja nyumbani kwangu ndio ulinionesha thamani yangu, na ukanifanye nitambue mimi kama mume natakiw akuishi vipi na mke wangu, ulinitoa kwenye giza ambalo sikuwa nina uhakika kama nipo gizani, maana niliona kama nimependa hivyo nastahili kupitia maumivu…
“ chichi asante sana, asante kwa kuja kwenye maisha yangu na asante kwa kunizalia na kwa kunifanya niwe mwanaume bora sana kwenye hii dunia, na sio siri najihisi mwenye bahati kubwa sana kuwa na wewe kama mke wangu, na nina kuahidi nitakulinda kama mboni ya jicho langu na nitahakikisha nadumisha kila tabasamu utakalolitoa usoni mwako, maana nakupenda sana chichi…
“ na nina kuhakikishia utatoka hapa na kamimba, maana nimekupania balaa, akawa anasema mume wangu kipenzi paul
Mimi sikuwa na chakuongea zaidi sana nikaanza kumtuliza na busu na mwisho tukajikuta tunazama kuleee
Tulikaa hotelini kwaajili ya fungate kwa siku tatu kisha tukarudi zetu nyumbani kwa ajili ya kuendeleza maisha mengine, ila bana ukitaka kugundua shetani huwa anajificha kipjndi cha uchumba na anajidhihirisha baada ya ndoa ndio kilichonikuta mimi, na usipokuwa na mungu unaweza kuhisi labda unaonewa, kumbe unajionea mwenyewe…
ITAENDELEA….
OFFER MWENDELEZO MPAKA MWISHO SH 500
Njoo WhatsApp katika namba 0683944333.