Nikamwambia kwa sasa itakuwa ni vigumu lakini nitafikiria, Sakina akawa ameniomba sana siku hiyo ya mimi kutoa ushahidi nisikosekane, Lakini tina aliniangalia kwa kutamani kuongea na mimi ila sikujali nikaondoka zangu.
Nilimpelekea Edina zawadi na alifurahi kweli lakini wakati huo zilibaki siku 20 ili kufunga ndoa mimi na Edina, Lakini pia nilikuwa bado sina simu nikawa nimefanya mpango nikanunua simu ila sikutaka Edina awe na simu sababu nilihofia akiwa na simu, Sakina anaweza akavuruga ndoa yetu isifanyike.
Siku ya kwenda kutoa ushahidi ikawa imefika lakini niliwaza sana niende au nisiende, Nikaona bora niende ili nimalizane na Sakina, Tukaingia mahakamani kwa ajili ya kesi, Mimi nikasimama kama shahidi wa mali za Sakina, Nikasema zile mali sio zangu wala sijawahi kumiliki mali nyingi kama za Sakina. Sakina alipoona nimekataa kusimama upande wake na yeye akaamua kusema kwamba mimi nina nyumba ambayo nilijenga kupitia mali na biashara zake, Hivyo na mimi ninyang'anywe ile nyumba...
(lengo la Sakina ni kwamba kwakuwa yeye amekosa basi na mimi nikose)
...Mahakama ikaamua yeyote ambaye alishilikiana na sakina lazima afilisiwe kwahiyo lengo la Sakina likatimia na nyumba yangu ikaunganishwa kwenye mali za yule mzee. Baada ya hapo mahakama ikasema wote turudi nyumbani harafu siku inayofuata turudi mahakamani kwa ajili ya Sakina kupewa talaka na mahakama kufanya maamuzi ya mwisho,
Nilirudi nyumbani nikaona kama vile naelekea kupoteza kila kitu sababu nyumba yangu tayari ipo kwenye orodha ya mali za yule mzee, Kingine zimebaki siku chache kufunga ndoa,kwakweli nilianza kuhisi kuchanganyikiwa, Lakini wakati yote haya yanaendelea Edina sikumwambia chochote,
Siku inayofuata ikabidi tufike mahakamani lakini sakina hakufika ikasemekana anaumwa ikabidi kesi iahirishwe hadi siku nyingine. Mwanamama sakina akawa ni mgojwa kila inapofika siku ya kwenda mahakamani, Lakini wakati huo siku ya ndoa mimi na Edina ikawa imekaribia zikawa zimebaki siku kadhaa,
Baada ya mahakama kuona sakina kama kuna kamchezo anacheza, Mahakama ikaamua kutuma wapelelezi ili kugundua kama ni kweli Sakina anaumwa, Mahakama ilipofanya upelelezi ikagundua Sakina anasingizia kuumwa lakini ni mzima,inamaana kwamba sakina anacheza na mahakama.
(Mzee alimfuata sakina kule hospitali na kumwambia kama unataka kutoa siri zangu tambua kwamba nitakuua kabla ya kinywa chako hakijasema chochote, Sakina nae huwa hakopeshi akamjibu usiponigawia chochote nitahakikisha dunia nzima inajua siri zako)
Mahakama ilipobaini kwamba sakina kuna mchezo wa kitoto anaufanya, Mahakama ikaamua kumwambia sakina kama ataendelea kusingizia kuumwa mahakama itamshtaki kwa kusingizia kuumwa wakati haumwi.
Sakina alipoona mambo yatazidi kuwa magumu ilibidi afike mahakamani na kesi ikaelendelea. Mzee akaandika talaka na kumpatia sakina, Mahakama ikafikia uamuzi kutokana na sakina kufanya udanganyifu mkubwa kwa kumdanganya mume wake kwamba Sadiki ni mtoto wa mzee, kumbe sio kwahiyo mali zote za sakina pamoja na nyumba yangu zitakuwa ni mali za yule mzee,
Lakini mahakama ikasema kwakuwa mzee ameishi na sakina muda mrefu inatakiwa amgawie nyumba kwa ajili ya yeye kuanza maisha mengine, Mzee hakuwa mbishi ikabidi mzee amuachie sakina moja ya nyumba ambazo alikuwa nazo. Kesi ikaisha na kuanzia hapo sakina wakaachana na yule mzee.
Changamoto ikaanza kwa Sadiki kutaka kumjua baba yake, Lakini wakati huo Tina aliendelea kuishi kwa Sakina sababu mpango wao wa kufunga ndoa ulivurugika, ikabidi waanze kupanga upya, lakini pia sakina alikuwa amechukua mkopo kwa ajili ya biashara yake wale wanaomdai walianza kumfuata wakitaka kuuza ile nyumba aliyoachiwa na mzee.
Lakini mimi nikaona yule mzee na yeye hana shukurani sababu nimemsaidia kutoa ushahidi harafu anachuwa na nyumba ninayoishi Dah iliniuma sana lakini sikuwa na namna, Ukizingatia na siku ya kufunga ndoa imekaribia nikaona hata nikienda kushtaki naweza nikamkosa na Edina, Ilibidi nikae na Edina na kumueleza kila kitu hadi ile siku nilikamatwa na kupelekwa kituoni nikakaa wiki nzima, Lakini Edina alikuwa ni mwanamke anayenipenda sana pamoja na misukosuko yote iliyonikumba lakini bado alisema atabaki na mimi na ndoa itafungwa,
Ikabidi nifanye mpango wa kuhama kwenye ile nyumba yangu sababu tayari imeshakuwa ya mzee, Nikaenda kutafuta chumba cha kupanga, Chumba nikawa nimepata nikalipa na pesa nikaona bora nianze kuhamisha vitu vyangu vyote, Lakini wakati narudi nyumbani nikakuta ile gari ya yule mzee imepaki pale kwangu nikaona hapa mzee kaamua kuja kunifukuza, Nilifika nikamsalimia na kuingia ndani kuanza kutoa vitu vyangu,
Yule mzee akaniambia huna sababu ya kuhama kwenye hii nyumba sababu hii nyumba ni yako na itabaki kuwa yako lakini nashukuru kwa kusimama kama shahidi katika kesi yangu na Sakina, sababu bila wewe nisingefanikiwa, lakini pia nimesikia umepata mchumba na upo njiani kufunga ndoa nakupongeza kwa hilo, chukuwa na pesa kidogo kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya harusi yako,
Yule mzee alitoa kiasi cha laki tano akanipatia kama sehemu ya shukurani na akaniachia na ile nyumba, Dah niliona kama miujiza, Lakini hadi hapo zikawa zimebaki siku tano kwa ajili ya ndoa, Ilibidi niongee na baba tukaanza maandalizi ya ndoa haraka,haraka sababu kulingana na mambo kuwa mengi mda ulikuwa hautoshi, Baba yeye akasema atakuja baa ya kuwa zimebaki siku tatu,
Mimi nikawa nimeenda sokoni kuhemea mahitaji kwa ajili ya siku ya ndoa, Lakini nikiwa kwenye mahemezi nikakutana na Tina, Tina akaniambia nasikia unaoa kwahiyo umeamua kuniacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine au huyo mwanamke ni mzuri sana kuliko mimi,kama nimekukosea naomba unisamehe,
Tina alisogea na kunishika shati na kuanza kulia watu wote pale sokoni walishangaa kumuona binti mzuri na mrembo kama Tina analia kisa mapenzi, Kumbe wakati huo Sadiki na mama yake hawakuwa mbali walisogea na kushuhudia Tina anavyoumia baada ya kusikia kwamba kuna mwanamke nataka kumuoa, Tina baada ya machozi kumtoka akasema kama nitaoa mwanamke mwingine yeye atakunywa sumu ili afe, Sadiki alishuhudia kwa macho yake tina akinililia na kusema atakunywa sumu kwa ajili yangu,
Mwanamama Sakina alisogea na kumshika Tina kisha akamwambia usijali hata hiyo harusi sisi ndio tutakao amua ifanyike au isifanyike...
Itaendelea...
~Daudi~.