__________________________________
Dunia ni ndogo sana yaani sana, hamwezi amini aliekuwa mbele yangu ni mjeda, yaani uyu ety ndo baba Amina, nyie nilishindwa kujizuia hapo hapo nikakunja sura, nikicheki pembeni mtoto na yule mzee, nikatumia tu hekima uku nina hasira inaonekana kabisa...
Nilishika simu yake nikasema tu samahani nimepata dharula naomba niende nitarudi siku nyingine muda huo nishaanza kutoka...
Ilikuwa ghafra sana, kabla hata sijafika mbali Wala sikusuburi jibu, wakiwa wanatahamaki mjeda akaniwahi kwa mbele, akashika mkono wangu, niliogopa mpaka kisimu changu cha Tecno kipya Cha laki na nusu, kikadondoka Kwa hofu, nakusambaratika kabisa...
Mjeda alinitizama uku kanikaza mkono, afu akasema "najua huna dharura unanikwepa mimi, na mimi nakutafuta wewe, naomba tuongee kwanza, Amina na Mzee wakasogea, kwani ninyi mnajuana? Waliuliza kwa pamoja, mjeda akajibu zaidi ya kufahamiana namjua in deep...
Amina akatutizama, akasema baba itakuwa wewe ndo mgomvi, mama namjua vizuri hawezi kukuchokoza na hachukii ovyo utakuwa umemkosea kosa kubwa sana, nilikuwa naamini hujui kuchagua kumbe sikuizi unajua kuchagua baba Amina aliongea Ivo nakutabasamu, kisha akasema babu tuondoke...
Mimi kuona hivyo nikaforce kuondoka jamaa ata hakunielewa, nikamng'ata akasema, hujaacha tu kuuma uma, ujue mpaka leo mgongoni kwangu kuna alama za meno yako, watu wote wakacheka, niliona aibu, nikahisi kabisa watu wote wamejua nini kilitokea, machozi yakaanza kutoka na sauti nikatoa make maumivu niliyokuwa nayasikia hayaekezeki...
Amina alivyoona nalia akataka kuja, babu yake akambeba na kumuomba atupe muda, walitoka huku Mimi nalia naomba kuondoka lakini hakuna alienisikiliza...
Baada ya watu wote kutoka tena wakawasha na gari kabisa wakaondoka, mjeda akanibeba msobe msobe, mpaka kwenye chumba kimoja akafunga mlango Kwa kutumia alama za kiganja chake...
Alivyofunga sikuwa na uwezo tena wakufungua, nilibaki tu kulia, "Mariam acha utoto basi, nahitaji tumalize tofauti zetu leo, nimekwenda sana kwenu kukutafuta Ili nikuombe msamaa lakini sikufanikiwa kukupata, na hakuna aliekuwa tayari kunielekeza wapi ulipo, ni Mungu tu kaamua kunisaidia...
Natambua kabisa, nimekukosea sana, sikupaswa kuruhusu hasira iniendeshe, naomba unisamee, na uniruhusu nikuoe tafadhali, nakupenda Mariam...
Itaendelea ...οΏ½οΏ½
Full sh 1000
Njoo WhatsApp katika namba 0683944333.