Apite mbele kabla sijamfuata, Nilitulia ili nione ni nani atakayepita mbele sababu najua barua niliandika mimi na kumpatia Side apeleke kwa Tina, Mwalimu alipoona hakuna anayepita mbele alikuja pale ambapo tumepanga mstari akamchukuwa mwanafunzi ambaye alikuwa anafahamiana na Side akampeleka pale mbele, Kisha akamwambia wewe ndio ulipeleka barua kwa Tina bas katuletee aliyeandika hii barua,
Yule mwanafunzi alikuja pale tuliposimama mimi na Side, Niliogopa nikajua ni mimi nafuatwa cha ajabu yule mwanafunzi alimshika Side na kuelekea naye pale mbele.
Mwalimu alimwambia Side chukuwa hii barua na uisome kwa sauti, Side alianza kuisoma ile barua hadharani kila mwanafunzi anasikiliza. KWAKO MPENDWA TINA, MATUMAINI YANGU UMZIMA WA AFYA, NINGEPENDA UJUE JINSI MAPIGO YA MOYO WANGU YANAVYOSIKIKA PALE AMBAPO NAWAZA KUHUSU WEWE, NATAMANI UJE KUWA MALKIA KATIKA UFALME WA MOYO WANGU, NAOMBA UFUNGUE MOYO WAKO UPOKEE UPENDO WANGU, NAKUPENDA SANA TINA NAOMBA TUWE WAPENZI. (mimi ni wako Side)
Maneno yalikuwa ni yaleyale ambayo niliandika lakini mwisho wa ile barua akataja jina la Side, Mh mimi nilishangaa kusikia jina la Side sababu mwisho niliandika jina langu David, Sikuelewa ilikuwa vipi hadi jina la Side likafika kwenye barua ambayo nilimuandikia Tina. Side kwakuwa amevunja maadili ya shule ikabidi apewe adhabu ya kuchapwa viboko 14, Alichapwa viboko hadi alilia kama mtoto mdogo, Kuanzia siku hiyo urafiki mimi na side ukawa umeishia hapo, Lakini mimi sikuelewa imekuwaje hadi kesi imemuangukia yeye.
Nilianza kuogopa kuwa karibu na Tina hata alipokuwa akinitumia barua za urafiki nikawa sijibu nilikuwa nazichoma moto au kuzichanachana vipande vipande, Muda ukapita sisemeshani na Side wala Tina.
Tukaendelea na masomo hadi form 4 hata hivyo Tina na Side tulikuwa tunasoma darasa moja, Lakini ndio hivyo tumenuniana.
Tumeingia form 4 Tina akawa amenifuata na kuniuliza mbona siku hizi hunisemeshi harafu toka tukio la rafiki yako hujibu hata barua zangu kwa nini?. Nilimjibu sitaki kujibu barua zako sababu sitaki uje unidhalilishe kama ulivyo mdhalilisha rafiki yangu side.
Tina akasema rafiki yako side alikuwa akinitongoza kwa kutumia jina lako na kuna siku aliniambia nimkute sehemu mimi nilienda nikiamini nitakutana na wewe lakini cha kushangaza nilimkuta rafiki yako side nilimtukana na kuondoka, lakini hakukoma nilipoona amezidi kunisumbua ndio mana siku ile nikaona nimseme kwa mwalimu,,,Lakini niambie yale maneno uliandika wewe kwamba unanipenda? (aliuliza tina)
Sikutaka kusubiri wakati mwingine. Nilimwambia Tina kweli nakupenda na ile barua niliandika mimi. Tina alionekana kufurahi,π₯° Alinikubalia ombi langu palepale. β€οΈ
Tayari tukaanza mahusiano mimi na Tina tukawa wapenzi pale shuleni, Tina alikuwa ni binti msafi sana, Kiufupi alikuwa ni binti anayejipenda sana, Ilibidi na mimi nianze kuwa msafi wakati mwingine hadi nyumbani wakawa wananishangaa mbona nimeanza kuwa msafi ghafla, Ilibidi tuwe na mahusiano ya siri kiasi kwamba hakuna mwanafunzi ambaye anikuwa anafahamu kama mimi na Tina tuna mahusiano ya kimapenzi.
Maisha yaliendelea tukawa tunakaribia kuhitimu form 4, Nilikuwa napenda kufuatilia masomo ya sayansi, Nilitafuta marafiki wawili nikawapa wazo la kuunda kengele ya kisasa ambayo itakuwa ni rahisi kuigonga na itakuwa na mlio wa hali ya juu inamaana kwamba itakuwa inasikika zaidi kuliko ile kengele ya pale shuleni,
Wale rafiki zangu wakawa wamekubali tukaungana watu watatu na kuanza kutafuta vifaa vya kutengenezea kengele...
Tutaendelea...βπ»
~Daudi~.