Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

SIMULIZI : NYOTA YANGU SEHEMU 06

31st Jul, 2025 Views 2



ENDELEA.......
Tulisikia Ngoma zinapigwa na matarumbeta.

"Mh! Kumekucha". Mama mkwe alisema hayo.

"Ni nani huyo amekuja na Ngoma" mmoja wa ndugu aliuliza.

"Bila shaka ni Samira". Najma alijibu na muda huo huo alitoka chumbani akiwa na furaha. Nilijiuliza Samira ndo nani maana nilikuwa simfahamu.

Ndugu walitoka chumbani na kutuacha Mimi na Samir.

Samir aliingia ndani na Ngoma zake pamoja na matarumbeta. Alikuja na mashoga zake na wapiga Ngoma na wapuliza matarumbeta. Walianza kukata mauno sio pouwa. Ndugu walibaki mdomo wazi. Ngoma zilipigwa Kwa fujo balaa hazikuwa Ngoma Tena Bali ni makelele Sasa.

"Samira unafanya nini". Bibi yake aliongea Kwa ukali. Ila Samira hata hakujali. Aliendelea kucheza na mashoga zake. Na wanakatika kweli kweli. Walikuwa wamevaa vijora sale basi wanavyojifunua sasa hawajali kama Kuna wanaume hapo.

"Samira ebu acha bhana unafanya nini Sasa. Bibi yake mdogo aliongea Kwa ukali huku anamvuta pembeni.

"Nini unafanya?".

"Bibi Leo shughuli jamani. Baba si ameoa. Nimeona nifanyie surprise kusherekea ndoa yake.

"Sasa hapo unasherekea au unafanya fujo?, uchezaji Gani huko na Kwanini umekuja na Ngoma si bola ungekuja na dufu".

"Khaaaa! Dufu la Nini?, ukiona wapi mie nacheza dufu?, ebu niache bhana". Aliyasema hayo na kuwaambia wapiga Ngoma na matarumbeta waendelee kupiga. Ngoma niliendelea. Ndugu jamaa na marafiki walibaki kuwashangaa tu. Mama mkwe wangu alichoka alikaa kwenye kochi na kushika tamaaa. Timu Ngoma ya kungwi ilikuwa Ngoma ya kungwi kweli kweli maana sio Kwa mauno yale.

Chumbani Samir baada ya kuona makelele yamezidi aliniambia anakuja. Alitoka chumbani na Mimi ndipo nilipata upenyo wa kukagua chumba vizuri. Chumba kilikuwa kizuri balaa. Kilipambwa vizuri. Kitandani palimwagwa maua mekundu. Yaani chumba kilijitosheleza. Kitanda, kabati, la nguo, sofa kubwa la watu watatu, meza ya chakula, Tv, friji dogo, kabati la viatu n.k. na vyote vilikuwa vya thamani..

Samir alifika sebleni alimkuta Samira anaendelea kukata mauno na hata alipomuona baba yake hakuacha kuendelea kucheza zaidi alizidisha kukatika.

Samir alimshika mkono mwanae Kwa nguvu na kumgeuza wakawa wanatazamani. Alimtandika kibao kimoja Cha shavu mpaka kupelekea kuanguka chini, hata mimi wa chumbani nilijisikia. Wenzake walivyoona mwenzao kapigwa walitoka mbio. Wapiga Ngoma na matarumbeta wao walikimbia.

"Nitakupiga nikuuwe wee mtoto". Samir aliongea Kwa hasira. Samira aliinuka pale chini alimpandisha baba yake na kumshuka alivyonza bonge la fonzo Kwa dharau na kutaka kutoka nje ila kabda hajaufikia mlango. Baba yake alimwambia.

"Ole wako uvuke icho kizingiti Cha mlango. Nitkulaza police wiki nzima wakufunze adabu maana unajifanya umepinda wewe".

Najma alimfuata Samira alimshika mkono na kumnong'oneza masikioni baada ya hapo waliongozana kupandisha juu gorofani.

Samir alitulizwa na kukaa kwenye kochi.
"Sijui kafuata wapi hizi tabia. Ni Binti mzuri ila hana maadili kabisa". Mmoja kati ya ndugu aliongea hayo Kwa masikitiko.

Nilikuwa nimekaa zangu chumbani niliona mlango unafunguliwa. Haraka nilijufunika na kukaa Kwa utulivu, sikujua ni nani aliyeingia.

Nilishangaa nimefunuliwa Kwa nguvu na kubaki wazi. Bado niliendelea kuinamia.

"Ndo hiyo mama wa jambo khaaa!. Mbona mdogo hivyo si kama Mimi huyu?".

"Shangaa na wewe?". Samira na Najma waliongea hayo nipo nilinyanyua sura kuwatazama tulikutana macho Kwa macho waliangua kicheko. Walicheka Kwa sauti mpaka sebleni walisikia. Haraka waliinuka na kuja chumbani Kwa speed. Baada ya kuwaona wakina mama wameingia niliinamisha kichwa Nini. Mama mkwe wangu alimkimbilia mtandio na kunifunika.

"Kumbe ndo maana mmemfunika watu wasimuona kukwepa aibu. Baba huyu si sawa na mimi huyu loooh!. Sasa mie nawezaje kumuita mama Kwa hivi alivyo?.

"Samira unaongea nini?. Kwanini huna heshima wewe. Awe mdogo awe mkubwa ndo mama Yako huyu ni mke wa baba Yako wa ndoa kabisa kwaiyo lazima umuheshimu". Mbaba mmoja aliongea hayo. Mpaka hapo nilikuwa hoi asikwambie mtu. Sio Kwa drama hizo. Yaani hata lisaa sijamaliza tangu nifike Ile matukio yashaanza. Sikujua kabda kama Samir anamtoto Tena mkubwa tu. Kwa mtazama mimi na Samir kimwili hatukupishana sana ila kimiaka nilimpita kama miaka mitatu au mnne hivi.

"Kwaiyo huyu namuota mama au shoga angu. Eti baba huyu namuitaje?. Ujue unanishangaza. Inamaana hujaona mwanawake mwengine zaidi ya huyu Nadra sijui?". Samira aliongea hayo Kwa dharau.

Mama mdogo alimshika mkono Kwa nguvu na kumtoa chumbani maana alipokuwa anaelekea sipo. Upande wangu nilijisikia vibaya maana madharau yalipita kiasi, kwamba Mimi si sifai kuolewa au ni vipi mpaka aseme hivyo. Ndoa imeingia kijui sio vile nilivyodhania. Ndugu walitoka chumbani walituacha Mimi, mama pamoja na Samir.

"Ni mjukuu wangu mtoto wa Samir anaitwa Samira. Niwie radhi Mimi Kwa kilichotokea mwanangu na unatakiwa kumzoea. Samira ni mkorofi mno hasikii haambiliki.

"Ni sawa mama nimekuelewa. Niliitikia kwa unyonge. Mama alitoka chumbani alimuacha wawili. Samir alikuwa amekaa kitandani amejiinamia yupo mbali kimawazo. Niliona anaunyanyua mkono wake na kuupeleka machoni. Niligundua kuwa alikuwa analia masikini..............
MUENDELEZO MPAKA 1000 TU WADAU WANGU.

NAMBA YA MALIPO 0743770612 JINA JOFREY.

UKISHALIPIA NICHEKI WHATSAP NAMBA 0683009150..
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

SIMULIZI : NYOTA YANGU SEHEMU 06  >>> https://gonga94.com/semajambo/simulizi-nyota-yangu-sehemu-06
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest