πΎπππππππ: πππππππ πππππππππ πππππ πππππ π
ππ§ π½πͺπ§πͺπππ£ - ππππ’πππ§π
*SEHEMU YA KUMI NA MBILI { 12 }*
_Tulipo ishia_ ππ¦
kufungua mlango na kumkuta Shemeji yake huyo akiwa anatabasamu.
*Endelea sasa* ππ¦
"Nisamehe sana baby haikuwa Akili yangu kusema vile na kukudhalilisha, naomba unisamehe jamani Japhet" Flora alisema kwa unyonge. "Nimeshakusamehe tayari lakini naomba usiniite baby wala mpanzi, wewe ni Shemeji yangu mke wa kaka yangu kwahiyo naomba tuheshimiane" alisema Japhet kwa msisitizo.
"Basi sawa nimekuelewa lakini baadae naomba uje kule saloon kwangu tuongee vizuri Shemeji" alisema Flora.
"Nije tuongee kuhusu nini tena? kama una kitu cha kuniambia naomba uniambie hapahapa nakusikiliza" alisema Japhet.
"Mmh basi tutaongea jioni nikirudi hapa nyumbani, uwe na siku njema nakupenda sana my love Mmwaaaaaa" alisema Flora na kummwagia busu la mbali Shemeji yake Japhet. Kijana Japhet aliishia tu kumshangaa huyu Shemeji yake na kumuona kama vile amechanganyikiwa.
Baada ya Flora kuwa ameondoka kabisa kuelekea saloon kwake huku nyuma Japhet akarudi tena chumbani kwake na kujifungia mlango. Punde akausikia mlango unagongwa tena ikabidi aende kuufungua na kumuona Rozi ndie ambaye alikuwa anagonga. "Baby nakwambia hapa tayari ndio kimeshanuka" alisema Rozi huku akiingia humo chumbani.
"Kimenuka kivipi tena mpenzi wangu?" Japhet aliuliza. "Huyu Shemeji yako mcharuko kesho asubuhi anataka kunisafirisha kunirudisha kijijini kwetu Iringa" Rozi alisema huku akicheka na kwenda kuketi kitandani kwa Japhet.
"Duuh kwahiyo na wewe upo tayari kurudi kijijini kwenu?" Japhet alimuuliza Rozi.
"Nipo tayari kuondoka, lakini sipo tayari kuondoka na kukuacha wewe hapo mpenzi wangu ni lazima tuondoke wote Japhet" Rozi alisema huku akitabasamu.
"Hapana Rozi siwezi kwenda na wewe huko kijijini kwenu" Japhet alisema.
Rozi akacheka kidogo halafu akasema:
"Sio kama tutaenda kijijini kwetu Japhet, tunaondoka hapa tunaenda kupanga chumba chetu au wewe unahitaji kubakia na huyu Shemeji yako na hivi visa vyake?" Rozi aliuliza. Japhet akajifikiria kidogo na halafu akasema: "Sio kama mimi nataka kubakia hapa Rozi, lakini pesa niliyokuwa nayo ni ndogo sana haiwezi hata kupangisha chumba" alisema Japhet.
"Usiwaze kuhusu pesa baby wangu, hizi hapa ni shilingi tatu na nyingine atakuja kunipa Shemeji yako jioni leo akirudi" alisema Rozi. Japhet akuamini macho yake baada ya kuziona pesa hizo kwa Rozi. "Hivi umewezaje kuwa na pesa zote kama hizo mpenzi?" Japhet aliuliza.
"Nilikuwa naweka kidogokidogo ili nimtumie Mama huko kijijini ajengee anagalau nyumba nzuri maana nyumba yetu ni mbovu sana na inavuja wakati wa mvua zinaponyesha" alisema Rozi.
Japhet akashusha pumzi ndefu na halafu akasema: "Sasa mpenzi wangu kwa nini usimpelekee mama yako hizo pesa, kwa maisha ya hapa mjini shilingi laki tatu ni hela ndogo sana kwenda kupangia chumba na huku tukiwa hatuna hata kitanda na godoro pamoja na vyombo vidogovidogo hebu fikiria upya mpenzi" Japhet alisema na kutoa ushauri wake.
"Sikiliza Japhet ngoja nikuambie kitu maisha ni popote na Riziki anayetoa ni Mungu hivyo hatupaswi kuwa na uwoga hata kwenye boksi chini tutalala cha msingi ni tuwe kwetu na maisha yetu" alisema Rozi kwa kujiamini.
Japhet akamsogelea Rozi na kumkumbatia halafu akasema: "Yaani wewe binti ndio maana nakupenda sana unajiamini mno" alisema Japhet.
"Sasa chumba tutakipata wapi?" Rozi alimuuliza Japhet. "Mmh yaani hata sijui kwani mimi sina uzoefu kabisa hapa mjini" alisema Japhet kwa sauti ndogo.
"Mimi nafikiri tungepata chumba maeΓ±eo ya mbali na hapa ingependeza zaidi" alishauri Rozi. Japhet akajifikiria kidogo halafu akasema: "Nimekumbuka yupo rafiki yangu mmoja tulikuwa tunaishi wote Dodoma, lakini kwa sasa na yeye yupo hapahapa mjini anaishi maeneo ya Yombo Buza sijui nimjaribu yeye labda anaweza kutusaidia kupata chumba" alisema Japhet. Rozi akatabasamu na halafu akasema: "Hebu jaribu kumpigia simu kama namba yake unayo atusaidie" Rozi alisema. Japhet hapohapo ikabidi achukue simu yake ndogo aina ya Tecno ile ya batani sio Smartphone aliyoletewa na Shemeji yake Flora. Japhet akapekua namba kadhaa zilizokuwa kwenye simu hiyo na kufanikiwa kuipata namba ya huyo rafiki yake na akaweza kumpigia.
Baada ya muda simu ikaweza kuita upande wa Pili na kupokelewa. "Aloo nani mwenzangu anaongea?" Sauti ya upande wa Pili ilisikika ikimuuliza hivyo Japhet.
"Oyaa Mussa ni mimi hapa Japhet wa Dodoma" alijibu Japhet. "Oohoo Japhet niambie mchizi wangu, vipi upo pande zipi?" Mussa alimuuliza Japhet.
"Mimi kwa sasa nipo huku maeneo ya Ukonga Banana kwa kaka Lukasi, sema nini mzee baba nilikuwa na shida ya kuonana na wewe siku hii ya leo" alisema Japhet. "Poa hamna noma rafiki yangu mimi nipo tu hapa nyumbani, wewe panda tu gari za Tandika zinazopitia Buza halafu teremkia kituo kinachoitwa Kanisani na baada ya hapo utanipigia simu nitakuja kukufuata" alisema Mussa.
"Daah poa sana best yangu ngoja hapa nijiandae fasta tu nitakuwa huko" alisema Japhet na kukata simu yake halafu tena akamgeukia Rozi na kumuambia: "Sasa mpenzi wangu mambo yote yako vizuri jamaa anasema niende nikamuone" alisema Japhet. "Yaani baby mwenzio hata bado sijaamini, hebu fanya haraka kamuone huyo rafiki yako" alisema Rozi huku akimkabidhi Japhet zile Pesa zote.
"Hapana mpenzi wangu usinipe Pesa zote laki tatu, nipe kwanza laki mbili " alisema Japhet na kumrudishia Rozi shilingi laki moja iliyobakia. Baada yΓ hapo Japhet akaenda kufungua begi lake na kutoa Pesa nyingine ni ile shilingi laki moja Pesa aliyopewa na Shemeji yake Flora siku aliyofanya naye mapenzi kwa Mara ya kwanza na sasa Pesa hiyo anampa Rozi aihifadhi. "Naomba uitunze hii Pesa mpenzi wangu itatusaidia kwa kuanzia maisha yetu tukifanikiwa kupata chumba" alisema Japhet na Rozi akaweza kuipokea. Baada ya hapo Japhet akajiandaa kwa kuvaa vizuri na halafu akamuaga mpenzi Wake Rozi. "Mimi ndio naondoka sasa lakini sitachelewa kurudi, kama Shemeji atarudi na kuniulizia mwambie aujui nilipoenda" alisema Japhet na baada ya hapo akaagana na Rozi kwa mabusu motomoto yaliyo na Mahaba mazito ndani yake. Japhet akaondoka zake kwenda kuonana na huyo rafiki yake aitwae Mussa. Hapo nyumbani akabakia Rozi akiendelea na kazi ndogondogo. "Yaani namuomba Mungu huko aendapo Japhet afanikiwe kupata hicho chumba tuondoke humu ndani tukajinafasi kwa raha zetu, tumuache huyu mwanamke na hilo pepo lake la Ngonoβ alijisemea Rozi huku akionekana kumchukia sana Flora.
Kijana Japhet naye akaweza kufika hadi kilipokuwa kituo cha kupandia daladala na kupanda gari ya kuelekea Tandika kwa kupitia Yombo huko anapoishi Mussa.
"Haina Jinsi itabidi nihame tu nyumbani kwa kaka yangu, haijalishi nitaishi maisha gani na Rozi huko tutakapohamia kuliko kuendelea kumsaliti kaka kwa kufanya mapenzi na Shemeji" Japhet alijisemea moyoni mwake huku akiwa ameketi kwenye siti ndani ya daladala hiyo. Mara ghafla simu yake ikaanza kuita ikabidi aangalie ni nani huyo anaempigia simu. Japhet alipatwa na mshtuko mkubwa sana baada ya kuona huyo anaempigia simu hiyo ni kaka yake Lukasi ambaye yupo safarini Mwanza. Japhet akajikuta anaingiwa na mchecheto kwa hofu ya kile alichokifanya na Shemeji yake (Flora) ambaye ndie mke wa kaka yake huyo. Mwishowe akajikaza na kupokea simu!.
Japhet akajikuta anaingiwa na mchecheto kwa hofu ya kile alichokifanya na Shemeji yake (Flora) ambaye ndie mke wa kaka yake huyo. Mwishowe ikabidi ajikaze na kupokea simu hiyo.
"Aloo kaka habari za huko?" Japhet alianza kwa kumsalimia kaka yake huyo.
"Za huku ni nzuri mdogo wangu, vipi huko mnawndeleaje?" Lukasi alimuuliza hivyo mdogo wake Japhet kwenye simu.
"Za huku pia ni nzuri kaka" Japhet alijibu.
"Sasa ni hivi mdogo wangu, kesho Mungu akipenda nitakuwa huko Dar es salaam" alisema Lukasi na kuongezea tena: "Kwahiyo nilikuwa naomba uje wewe na Shemeji yako kunipokea pale Ubungo nitawasili na basi la mchana" alisema Lukasi. "Sawa kaka hakuna shida nitakuja na Shemeji kukupokea, tumekumiss sana" alisema Japhet huku akitabasamu.
"Nami pia nimewamiss sana, yaani nilijua nitakaa huku Mwanza kwa wiki mbili kama vile nilivyowaaga lakini nashukuru biashara zimeenda vizuri narudi huko mapema" alisema hivyo Lukasi.
"Nafurahi sana kaka kusikia hivyo, vipi lakini Shemeji umemjulisha kama hiyo kesho unarudi nyumbani?" Japhet aliuliza. "Yeah nimetoka kumpigia simu sasa hivi na kumjulisha, halafu ndio nikakupigia wewe mdogo wangu" alijibu Lukasi.
"Basi sawa kaka karibu sana nyumbani" alisema Japhet.
"Ndio hivyo mdogo wangu Japhet wala usijali nikirudi huko hiyo kesho, nitaanza kufuatilia kuhusu wewe kupata kazi kama nilivyokuahidi" alisema Lukasi.
Baada ya Japhet kuongea na simu na kaka yake hatimaye wakamaliza hayo mazungumzo yao wakaweza kuagana na kukata simu zao.
"Daah afadhali kaka anarudi nipumzike na hivi visa vya Shemeji" alijisemea Japhet.
Baada ya mwendo wa nusu saa hatimaye daladala alilopanda kijana Japhet liliweza kufika maeneo ya hapo Buza Kanisani kama alivyoelekezwa na yule rafiki yake Mussa kuwa ndio anapotakiwa kushuka kwenye kituo hicho. Baada ya Japhet kuwa tayari ameshateremka kwenye ile daladala hapohapo akampigia simu Mussa kumjulisha kama tayari ameshafika. "Oyaa mwamba mimi ndio nimeshuka hapa tayari kwenye gari" Japhet alisema. "Poa tayari nimeshakuona rafiki yangu" alisema hivyo Mussa na kukata simu.
Japhet akiwa bado anashangaashangaa maeneo ya hapo Mara ghafla akahisi anashikwa begani ikabidi ageuke nyuma na kuweza kumuona Mussa akiwa yupo amejawa na tabasamu usoni mwake.
"Ooho best yangu huyo niambie" alisema Mussa huku akimkumbatia Japhet.
"Daah hata siamini kama kweli tumeweza kuonana tena" alisema Japhet.
"Ndio hivyo tena best yangu wahenga wanasema milima haikutani lakini sisi binadamu tunakutana, haya sasa twende nyumbani ukapaone ninapoishi" Mussa alisema. Baada ya hapo wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Mussa huko anapoishi huku njiani vijana hao wakipiga story mbili tatu za kukumbushiana mambo ya zamani walipokuwa wanaishi wote huko kijijini kwao mkoani Dodoma.
Baada ya muda mfupi wakafika hapo nyumbani kwa Mussa ambapo ilikuwa ni nyumba tu ya kawaida na Mussa hapo alikuwa amepanga vyumba viwili alivyokuwa anaishi na mkewe pamoja na mtoto wao mdogo. "Karibu sana ndugu yangu, hapa ndio nyumbani na huyo hapo unaemuona ni Shemeji yako" alisema Mussa wakati alipokuwa anamkaribisha ndani Japhet. "Ahsante sana nashukuru pia kumfahamu Shemeji yangu" alisema Japhet huku akitabasamu. Baada ya hapo Mussa akamtambulisha huyo mkewe kwa kijana Japhet na kuweza kufahamiana.
"Enhe niambie ndugu yangu, vipi maisha yanasemaje?" Mussa alimuuliza Japhet.
Maisha ndio hivyohivyo yanasogea nipo kwa kaka yangu ndio ninapoishi" Japhet alisema. "Ok ni vizuri sana, vipi lakini kaka ajambo?" Mussa aliuliza tena.
"Kaka ajambo sana, amesafiri kibiashara yupo Mwanza, lakini leo amenipigia simu ya kunijulisha kuwa kesho anarejea" alisema Japhet. Wakati wanaendelea na mazungumzo ya hapa na pale ndipo mke wa Mussa akamkaribisha soda Japhet ya kupooza koo angalau. "Karibu soda Shemeji" alisema mwanamke huyo huku akimmiminia soda hiyo kwenye Glass.
"Ahsante sana Shemeji," alisema Japhet.
Baada ya hapo mke wa Mussa akaelekea jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula cha mchana. Huku wakabakia Japhet pamoja na mwenyeji wake Mussa wakiendelea na maongezi yao huku wakionekana kufurahi kwa kuonana kwao. Japhet akaona sasa ndio hapahapa kwa kumueleza Mussa shida yake iliyomleta huku. "Ndugu yangu kwanza naomba unisikilize kwa umakini haya nitakayoambia, lakini nitaomba iwe ni siri yako na nitahitaji msaada wako" alianza kwa kusema hivyo Japhet.
Mussa akajiweka vizuri kwenye Kochi alipokuwa ameketi halafu akasema: "Kuhusu hilo ndugu yangu wala usijali, niambie tu nakusikiliza na nitaitunza hiyo siri pia nitakusaidia" alisema Mussa.
Japhet akashusha pumzi ndefu na kuanza kumsimulia Mussa mambo yote yanayoendelea kule nyumbani kwa kaka yake Lukasi ambapo yeye (Japhet) ndio anaishi bila hata ya kumficha Mussa akamsimulia jinsi Shemeji yake (Flora) anavyomsumbua kimapenzi na kutaka kufanya naye mapenzi lakini akamficha kuhusu alivyofanya naye mapenzi ile siku moja na akamueleza pia uhusiano wake na Rozi ambaye ni dada wa kazi (House Girl) kule nyumbani kwa kaka yake.
"Kwahiyo ndio hivyo ndugu yangu, msaada ninaouomba kwako naomba unisaidie kupata chumba maeneo ya huku ili nihamie huku na huyo binti niepuke vishawishi vya Shemeji" Japhet alisema. Mussa baada ya kumsikiliza Japhet kwa umakini naye akasema: "Duuh kwanza nakupa pole ndugu yangu kwa hayo majaribu ya kutakiwa na huyo Shemeji yako kimapenzi, Pili nikupongeze kwa uamuzi wako wa kuhama hapo nyumbani kwa kaka yako na huyo binti kumkwepa huyo Shemeji yako" alisema Mussa. "Ndio hivyo sasa ndugu yangu naomba msaada wako unitafutie chumba" alisema Japhet. Mussa akafikiria kidogo na kusema: "Kuhusu hilo jambo la chumba ondoa shaka kabisa kitapatikana kwani yupo Mzee mmoja hapa jirani nafahamiana naye nyumbani kwake kipo chumba anapangisha" alisema Mussa. Japhet alifurahi sana kusikia hivyo haraka sana akasema: "Nipeleke hata sasa hivi kwa huyo Mzee nikakione hicho Γ§humba, hapa nilipo nimekuja kabisa na Hela ya kodiβ alisema Japhet. "Basi kama ni hivyo sawa ndugu yangu, twende ukapaone ni sehemu nzuri sana nina imani utapapenda" alisema Mussa huku akinyanyuka kwenye Kochi.
Baada ya kumuaga mke wa Mussa kuwa wanatoka Mara moja lakini wangerudi baada ya mfupi kuja kula chakula kwani wasingechelewa huko wanapoenda. Mussa na Japhet wakaweza kuondoka.
*ITAENDELEA* ππ₯°π¦
Soma mpaka mwishoooo kwa sh 1000
Njoo WhatsApp 0743433005.