Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Atakuja kwangu na kukaa siku kadhaa ndio aende nyumbani... Inaendelea... Sehemu Ya 10

31st Jul, 2025 Views 5



Nilifanya uchunguzi wa zile karatasi nikagundua zile ni hisa za biashara kutoka kwenye makampuni mbalimbali na zile pesa niligundua kwamba sio pesa halali wala hazikuwa kwenye biashara, Lakini sakina alikuwa anaziingiza kwenye mfumo wa biashara ili zitumike kihalali, Inamaana hapo mimi nilikuwa nafanya kazi ya kutakatisha pesa bila mimi kujua. Nilipogundua mchezo ambao sakina anaucheza nilikaa kimya ili nione ni nani anayeuchezesha. Niliendelea kumpangia mipangilio mizuri ya pesa.

Muda wa tina kuja kwangu ukawa umefika, Tina alinipigia simu na kuniambia nimpe maelezo ili achukuwe bodaboda aje hadi pale ninapofanyia kazi, Nikaona nikimruhusu tina aje pale ninapofanyia kazi, Sakina anaweza akafika na ikawa tatizo, Ilibidi nitafute guest ambayo ipo mbali kidogo na maeneo yale ya kazini kwangu, Kisha nikampigia tina na kumwambia achukuwe bodaboda aje mpaka pale kwenye ile guest, Kweli tina alifika lakini alionekana kutokupendezwa na kufikia guest, Sababu lengo lake alitamani apafahamu ninapoishi na ninapofanyia kazi. Nilimuacha tina guest nikarudi kwanza kazini kwa ajili ya kufunga hesabu, Wakati namalizia ili niondoke sakina alifika na kunipatia kazi ya kumpangia majina kwenye hisa zake na akaniambia kesho asubuh na mapema niwe nimeshakamilisha na atapitia nyumbani kwangu, Nikamwambia sawa.

Sakina alipoondoka na mimi nikafunga pale kazini na kuelekea kule nilipomuacha tina, Nilipofika tina alianza kuniuliza mbona kama vile una wasiwasi tatizo nini? Nikamwambia kuna gari imeachwa pale kazini kwangu pamoja na funguo kwahiyo mwenye gari kanipigia na kusema kesho mapema inabidi niwahi nikampatie funguo, Tina akasema ni hivyo tu au kuna lingine harafu kwa nini hujanipeleka kule unapoishi. Ilibidi nimdanganye kwamba kule huwa tunalala na washkaji kwahiyo hakuna sehemu ya kulala na wewe. Ilibidi aelewe,

Nililala na tina mpaka asubuh, Lakini ile asubuh nilichelewa kuamkia hivyo niliamshwa na mlio wa simu kuangalia namba SAKINA,nilivunga kwanza kuipokea, Niliinuka na kuanza kuvaa utazani naenda kuzima moto, Kisha nikamwambia tina mwenye gari kaijia funguo kwahiyo ngoja nimpelekee chap harafu nitarudi. Wakati huo simu kutoka kwa sakina inaita zaidi ya mara tatu na siipokei,nilipotoka nje na ile guest nilipokea simu ya sakina, Lakini kabla sijaongea chochote sakina aliuliza upo wapi maana mimi nipo nyumbani kwako hapa nimekuja kukupitia ukanipatie zile documents,harafu wewe umefunga! Nilimwambia tukutane kazini kuna kitu nilijidamka kwenda kununua. Nilitoka bila kupiga mswaki nikiwa nje ya ile guest niliangaza macho nikaona bodaboda nilimwambia bodaboda chap na haraka,nikapanda...

Nilifika kazini lakini kazi ya sakina nilikuwa bado sijaifanya ilibidi nijifanye kama sikuelewa namna ya kuipangilia nilimuita sakina kwenye kile chumba cha siri nikaomba anielekeze, Akaanza kunielekeza huku akiniambia nifanye haraka kuna sehemu anawahi, Nilimaliza na kumpatia akaondoka. Mimi nilifanya mpango wa kuwaachia maelekezo vijana wangu kisha nikarudi kwa tina. Niliburudika na tina siku mbili ikabidi nimwambie kuna safari tunaenda mimi na boss wangu na tutakaa zaidi ya wiki kwahiyo inabidi uende nyumbani. Tina aliona kama vile namfukuza akaniambia kama nimeshaoa bora nimwambie ukweli, Nikamwambia sijaoa lakini ni mipango ya boss na kazi, Na kuhusu malengo yetu ya kuoana yako palepale, Tina alinielewa na kuniambia nifanye yote lakini kamwe nisije nikamsaliti, Nilimwambia hakuna shida kuwa mwaminifu pia. Nilimfanyia maandalizi akawa ameenda kuwasalimia nyumbani. Nililazimika kumdanganya tina sababu niliona ananibana kufanya mambo yangu, Sababu sakina angejuwa kama nina mwanamke mwingine ingekuwa shida.

Maisha yakaendelea tukaendelea kupiga pesa, Mwanamama sakina akanielewa sana hadi akaamua kunimilikisha ile sehemu ya kuoshea magari, Lakini kabla ya kunimilikisha. Aliniambia nibadirishe jina langu lakini la baba nitatumia lilelile, Nilikubali na jina akaniambia nitakuwa naitwa Sadiki, Kuanzia hapo jina langu la David nikaliweka kando nikawa naitwa Sadiki Ntai. Mwanamama sakina alianza kuniamini na kunimilikisha malizake zote, Nilianza kuwa na pesa hadi watu wakawa wananishangaa nilikuwa nikienda kijijini kwetu kuwasalimia,hadi wale marafiki zangu wa mwanzo wakawa wanasema nimekuwa freemason,

Lakini pale kijijini watu wanaonifahamu pamoja na wazazi wangu walishangaa pale nilipowaambia nimebadirisha jina, Siitwi tena David lakini naitwa Sadiki, Baba alionekana kushangaa sana aliposikia kuwa kwa sasa naitwa sadiki. Nilikuwa nikiwasaidia pale nyumbani kwa kila kitu, Lakini mimi kule mjini nilikuwa bado nimepanga. Lakini pia tina alikuwa tayari yupo mwaka wa tatu pale chuoni inamaana kwamba alikuwa anaelekea kuhitimu,

Nikaanza kuishi maisha ya kitajiri polepole kupitia mwanamama sakina, Sakina alianza kunipeleka katika makampuni yake na kunitambulisha kama msimamizi mkuu, Niligundua mwanamama sakina ni tajiri kuliko nilivyokuwa namfikiria hapo mwanzo, Kumbe hata ile hoteli niliyolala siku ya kwanza kufika mjini nayo ni hoteli yake. Makampuni yake yote akabadirisha jina na kuweka jina langu la Sadiki Ntai, Mwanamama sakina akaninunulia mpaka gari ya kutembelea kwenye mizunguko ya biashara zake, Mwanamama sakina akafanya mpango wa kuninunulia nyumba ya kifahari, Nikajikuta naishi maisha ya kitajiri kuliko nilivyotegemea, Lakini kule kazini ambapo ni sehemu ya kuoshea magari bado nilikuwa naenda sababu mipango yote ya biashara ilikuwa inafanyika huko, Lakini sakina alianza kuniweka wazi kuhusu mipangilio yake ya biashara,

Nilipozifahamu vizuri kazi za sakina ikabidi na mimi niongeze juhudi kwenye kuboresha mipangilio ya kununua hisa na kuuza, Kwa elimu yangu ya kufeli form four nilianza mpango wa kuwa nayapangia matumizi yale makampuni yote yanayoshirikiana na kampuni ya sakina, Hadi tukawa juu yao lakini palikuwepo na kampuni moja ambayo ilikuwa inaleta ubishi ila haikuweza kuzuia mipango yetu. Sakina alinipenda sana lakini kitendo cha kushiriki nae tendo ndio ilikuwa bado.

Lakini pia mahusiano mimi na tina yalikuwa bado yanaendelea nilijikuta namsomesha tina sababu nilianza kumlipia hadi Ada ya chuo, Siku moja nikiwa nimepumzika pale kazini kwangu ambapo huwa tunaosha magari. Ilikuja gari moja aina ya V8 alishuka mzee wa makamo, Kwa mwonekano ni kama mwanasheria mstaafu au jaji mkuu, Maana alishuka kwenye gari akiwa amevaa miwani usoni,na mkononi mwake kabeba kitabu.

Yule mzee alikuja na kusimama karibu yangu nilimsalimia na kumpatia kiti akae, Mzee alisogeza kiti kando yangu na kukaa, Kisha alifungua kitabu chake na kuniomba anisimulie kidogo hadithi zilizomo ndani ya kile kitabu alichonacho, Kwakuwa niliona ni mzee wa busara na heshima, Nilimwambia nisimulie mzee wangu huwenda na mimi nikapenda hiyo hadithi na nikanunua kitabu kama chako. Mzee alianza kunisimulia...

Na Nukuu. Tajiri mmoja alimuita mfanyakazi wake ambaye ni masikini sana, kisha akamuuliza kwanini nyie masikini mnaogopa kuwa na pesa nyingi. Yule mfanyakazi alikataa na kusema hapana hatuogopi kuwa na pesa sema pesa ndio hatuna. tajiri akasema sawa kaendelee na kazi,

Ilipofika mida ya usiku yule tajiri alimuita yule mfanyakazi wake na kumpatia begi llililokuwa limejaa pesa za noti ambazo ni elfu kumi,kumi, Tajiri akamwambia chukuwa hili begi lenye pesa nenda nalo ukalihifadhi sehemu yenye usalama zaidi na kama patakucha salama utaniletea begi langu pamoja na pesa zote zilizomo, lakini kama hapatakucha salama hizo pesa utatumia wewe na familia yako.

Yule mfanyakazi aliuliza kwanini pesa zote hizi unipatie mimi wakati huku kwako ndio kuna usalama zaidi, mimi naona bora hizi pesa zibaki huku kwako. Tajiri akamwambia hapana haiwezekani kubaki kwangu kwa sababu kuna wavamizi wanaweza wakaja kuniua au kutaka kuiba hizi pesa kwahiyo wewe kwakuwa hakuna anayejua kama una pesa, hivyo hakuna wa kuja kukuvamia, wewe chukuwa hizi pesa nenda nazo ukafiche pale unapoona ni salama.

Yule mfanyakazi masikini alizichukuwa zile pesa na kuenda nazo hadi nyumbani kwake, alipofika nyumbani kwake aliwaza kama tajiri yake ameogopa kukaa na zile pesa akihofia kuvamiwa na kuuawa, yule mfanyakazi akaona huwenda ni mtego, aliamua kuchukuwa lile begi la pesa na kwenda kumpelekea rafiki yake, alipofika kwa rafiki yake, Yule rafiki yake akamshauri ampatie pesa yeye akae nazo harafu kama boss atavamiwa na kuuawa wao watagawana, Rafiki wa yule mfanyakazi akajitoa muhanganga kubaki na zile pesa, harafu yule mfanyakazi akarudi nyumbani kwake,

Asubuh yule mfanyakazi aliamka na kwenda kumuangalia boss wake kama atakuwa mzima, Alifika na kumkuta boss wake ni mzima wala hakuvamiwa. Yule boss wake akamwambia kaniletee lile begi la pesa. Yule mfanyakazi alienda hadi nyumbani kwa rafiki yake ambaye alimuachia begi la pesa, alifika nyumbani kwa rafiki yake lakini hakumkuta, inamaana kwamba rafiki yake alitoroka na begi lenye pesa. MWISHO WA KUNUKUU.

Yule mzee alipomaliza kunisimulia ile hadithi aliniuliza je kama pesa zimepotea ni nani wa kulaumiwa...

Itaendelea...✍🏻

~Daudi~.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Penzi La Siri Na Mke Wa Tajiri Atakuja kwangu na kukaa siku kadhaa ndio aende nyumbani... Inaendelea... Sehemu Ya 10  >>> https://gonga94.com/semajambo/penzi-la-siri-na-mke-wa-tajiri-atakuja-kwangu-na-kukaa-siku-kadhaa-ndio-aende-nyumbani-inaendelea-se
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest