_________________________________
Kumtizama hivi, nilishtuka ilikuwa ni ghafra sana kuwaona mbele yangu nilijua hata wameshaondoka, alikuwa ni yule dereva wake wa siku zote, anaemleta Amina shule, aliomba tuongozane wote, familia imeomba nikajumuike nao kwa mlo wa jioni, yaani matajiri hata hawajaniandaa khaa, nikaomba nikajiandae kwanza, alikubali nilifunga…
Nikaenda kujimwagia nikapiga pamba zangu, Nina mwili wa nguo yaani hata nivae nini lazima nitapendeza, nilivaa kawaida ila mwenyewe nilijiona kabisa nimevutia..
Nilitoka nikapanda hao kwao Amina , muda huo nimeshatoa taarifa kwa ndugu nikitekwa wajue pakuanzia nilituma plate no za gari,na maelezo mafupi kabla yakutoka, Kisha hao tukalianzisha kwenda huko kwao Amina binti yangu kipenzi…
Amina alimuomba dereva atupitishe dukani kwake, nikashangaa hee haka katoto ka miaka 6 ety kana duka��, mmh nikafunga mdomo mie, tumefika ni bonge la duka sio la kitoto bango tu gharama yake ni milioni Sasa vitu vilivyomo ndani vinathamani kiasi Gani��, duka la nguo za wadada na wakaka mikoba yaani lilikuwa full, kalifika…
Kakakagua wafanyakazi, na Mimi nikaambiwa nichague nguo, aisee nikicheki hapo hakuna nguo ya Bei chee, yaani nguo ya bei ndogo hapo ni laki tena ni kiblause tu, nikaogopa mwenzenu sijawai kuvaa ata ya alfu 50, nikivaa ya gharama sana ujue nimeshona na haizidi 35 hapo ujue ni kitambaa na pesa ya fundi humo humo…
Afu ety nichukue kakibode Kwa laki, si bora nipewe hio laki nikanunue mwenyewe za elf 5, niliogopa ata kuongea Amina alijua tu ni uoga kaka amua kunichagulia, nguo kali za laki tatu kwenda juu aisee nilijikuta tu naumia hadi machozi yakanitoka, huyu mtoto anajua hela zilivyozashida jamani, hakuishia hapo akamchukulia na shangazi gauni tatu na vitenge pea tano, akaomba nichagulie na mjomba nyie ata kuchagua ilikuwa mtihani nilimuonesha tu size akachagua pea tatu na viatu juu, mimi na vipochi, yaani nilivyochukuwa na saa ya gharama kweli …
Tulipitia stend akatuma mizigo kwenda nyumbani, akahemea mpaka mchere gunua, yaani mizigo ilikuwa mingi mno, Kisha akamwambia dereva aturudishe tena tikajiandae upya…
Tulirudi Amina akaomba nivae nguo aliyonichagulia, nilitaka kupinga kakaomba kweli, ikabidi tu nivae aisee nilipendeza mno…
Na kenyewe nilikaosha japo hakapendi ila sheria angalau nikaogeshe mala Moja Kwa wiki, tulishakubaliana, na Leo ilikuwa siku ya kuogeshwa, nilimuosha nikamuandaa, tukatoka sasa rasmi kwenda kwao hapo tayari ilikuwa saa moja jioni…
Tulienda mpaka kwenye nyumba moja ivi kubwa ya kifahari, kufika tu Cha kwanza getini kuna mlinzi tena sio wale walinzi wa mtaani ni walinzi wamakampuni…
Tuliingiza gari mpaka ndani ndio tukashuka, hapo mwenzenu natetemeka, nikicheki pembeni kuna mimbwa Ile ya kijeshi, inayopewa mafunzo kabisa, nilipitishwa kutambulishwa Kwa mijimbwa kwanza, nikajikuta nashangaa Yaani natambulishwa hadi kwa mbwa��, ila matajili, tulivyomaliza tuliingia ndani, huku moyo wangu unadunda, nilikuwa na hofu sio kawaida, tulikaribishwa na mfanyakazi wa ndani mtu mzima kiasi, na mbabu Yaani babu yake Amina, nilisalimia kisha tukakaa, Amina aliambiwa akamuite baba ake, alienda kumuita muda huo Mimi nilikuwa nimeinama simu nachart na binam Isa na mama nawapa ubuyu wa ninayokutana nayo…
Nilisikia hatua za watu zimefika, nikaamua kutulia kwanza nikainuka uso ili tusalimiane nyie nyie hii Dunia hii ��…
Itaendelea.....
Full sh 1000
Njoo WhatsApp katika namba 0683944333.