Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa

MY LUNA SEHEMU YA : 06

31st Jul, 2025 Views 28


Maisha ya ndoa baina ya Zayn na Leila yalikuwa yasiyo hata na chembe ya furaha. Ilikua ni ndoa kwa jina tu. Zayn alikua haonekani nyumbani, hata Jumapili ambazo kwa kawaida watu hutumia kukaa na familia, yeye alikuwa sehemu isiyojulikana. Na kama Akirudi basi hujifungia chumbani kwake, na siku nyingine hakuonekana kabisa🤦‍♀️.

Leila alizoea ukimya. Alizoea upweke na kutokuhesabiwa kama mtu wa muhimu. Mlinzi wa getini ndiye aliyebaki kama mtu pekee ambae alikua akiongea nae.

Hata hivyo, hakuacha kwenda Coco Beach kuuza madafu kama zamani. Ile sehemu ndo ilimpa amani na pia ni sehemu ya kupatia hela ya kuendesha maisha yake.

Mr Ghali kabla ya kuondoka kuelekea South Africa alimkabidhi Leila Golden Card yenye pesa nyingi. Alimwambia, “Ukihitaji kitu chochote, Leila, usisite kuitumia. Maisha ya ndoa yana changamoto”

Lakini Leila aliiweka kadi hiyo kwenye pochi, akaiangalia tu kila siku. Hakutaka kutumia hata mia. Na hii nikwa sababu Hakutaka aonekane kama aliolewa na Zayn kwaajili ya pesa peke ake.

Hivyo, akaendelea kutumia hela ndogo anazopata kwenye biashara ya madafu, hela ambazo nyingi alikua akimtumia mama yake.

Na pia Mama yake, Bi Salma, hakuwahi kujua Leila anapitia hali ngumu. Leila alifanya siri. Hakutaka kulalamika. Hakutaka kumuudhi Mr Ghali, wala kumsononesha mama😩.

Miezi ikasogea. Siku zikapita. Mwezi mmoja ndani ya ndoa ukakatia! Leila aliishi kama mpangaji kwenye nyumba kubwa ya kifahari. Sasa Siku moja asubui Leila alipokea simu toka kwa mama yake aliekua analia

“Leila, Lulu kazidiwa… tupo hospitali, mwanangu hali yake si nzuri”

Leila moyo ulimdunda kwa kasi. Akavua dera lake la nyumbani harakaharaka, akavaa abaya nyeusi na kutimka kuelekea hospitali.

Alipofika, alikuta mama yake akiwa ameketi pembeni ya kitanda. Mdogo wake Lulu alikua na mashine puani, hali ilikua mbaya kweli hata macho hakuweza kufungua

“Tunahitaji kuisafisha figo yake haraka. Lakini itagharimu shilingi laki saba” alisema Daktari

Leila alishika kichwa chake. Hakuwa na hiyo hela. Akakumbuka ile Golden Card aliyokabidhiwa na Mr Ghali. Haraka akaelekea benki ya karibu kutoa pesa.

Alipofika benki, Leila alitoa ile kadi na kumpa karani wa benki

“Tafadhali, naomba nitolee shilingi laki saba tu. Haraka please”

Karani alipoingiza maelezo kwenye kompyuta, akamwangalia Leila kwa mashaka.

“Samahani dada, lakini kadi hii ilizuiwa muda mrefu sasa”

“Imezuiliwa? Na nani?” Leila alishangaa😳

“Maelezo ya mfumo yanaonesha ni mmiliki mwenzako wa akaunti ndiye aliezuiwa matumizi kwa sasa. Jina lake ni Zayn Ghali”

Leila alipatwa na mshtuko na kujiuliza ni Kwanini Zayn afunge kadi ambayo alipewa na baba yake?Alikuwa hana muda wa kujiuliza sana.

Akatoka benki kwa haraka, akapanda teksi kuelekea ofisini kwa Zayn. Mtu pekee aliebakia ambae angeweza kumsaidia kwa mda ule ni Zayn! Leila alitegemea msaada toka kwake japo hawakua vizuri🤦‍♀️.

Alipofika alikutana na jengo refu lenye vioo vya kisasa, akapanda lifti haraka hadi floor ya saba. Huko alipokelewa na Secretary mmoja ambae alimsindikiza hadi kwenye mlango wa kuingilia ofisini kwa Zayn.

Leila alikua kapaniki hata hakukumbuka kubisha hodi akaingia ivyo ivyo. Ile kaingia tu anamuona Zayn akiwa amemkumbatia Tatiana, secretary wake mwingine.

Tena kwa jinsi walivyokua wamekumbatiana Leila aligundua huenda walikua na mahusiano ya mda mrefu. Kusema kweli moyo ulimchoma maana Zayn ni mumewe💔.

Kwa Aibu Leila alitazama pembeni huku Zayn akionekana hajali hata kama alifumwa. Alimuachilia Tatiana na kujiweka sawa.

“Sorry, Naomba tuongee, Zayn” alisema Leila

Tatiana alimwangalia Leila kwa dharau, akambusu Zayn shavuni kisha akatoka nje awapishe wazungumze.

Tatiana alipotoka, Zayn aligeuka na kumwangalia Leila kwa jicho kali lililo jaa hasira😡

“Tumeanza kufuatana hadi ofisini sasa?? What do you want??” 😒

“Nahitaji laki saba. Tafadhali ni emergency”

“Laki saba? Kwa ajili ya nini? Saluni? Au shopping??”

“Sitaki kusema ya nini. Ni muhimu tu. Tafadhali, nisaidie hiyo hela” Leila alijibu kwa upole

“Naona ushagundua kuwa ile golden card nime ifunga. Zile pesa zilizoko kule kwenye kadi ni jasho la mzee wangu na mimi pia, huna hadhi ya kutumia hata senti tano. By the way si bado unauza madafu Coco Beach wewe? Hela unapeleka wapi??” 🥴

“Zayn…”

“Hiyo ndo shida ya wanawake maskini. Mnataka kuolewa na watu matajiri ili mpumzike. Nenda kajiuze kama unataka hela haraka. Ni njia rahisi ya kupata hela ya chap chap” 🥱

Maneno yale yalimuuma Leila, yalikua kama kisu kilichopita moyoni mwake. Hakuweza hata kujitetea. Alichofanya ni kugeuka taratibu na kutoka ofisini kwake uso ukiwa umejaa machozi😭.

Zayn hakujua hata hiyo laki saba ni kwa ajili ya nini. Hakujua Lulu, dada yake Leila, anapambana na kifo hospitalini. Hakujua ni namna gani Leila alikua kwenye wakati mgumu.

Angejiuaje ikiwa hakua na time nae?? Hata nyumbani hakulala.

Je, Leila atapata wapi hiyo hela ili kuokoa maisha ya Lulu? Apo ndipo stori inapoenda kuwa tamu.

Nakuja………..

SEHEMU YA : 07

Apo ni Saa nne za asubuhi, jua limeanza kupanda taratibu. Leila alikua kachanganyikiwa, macho yamevimba kwa kilio cha mda mrefu. Hakujua atatoa wapi laki saba ya kumsaidia mdogo wake🥺.

Alipofumba macho, bado maneno ya Zayn yalimrudia kichwani:

“Nenda kajiuze kama unataka hela haraka. Ni njia rahisi ya kupata hela ya chap chap”

Alipofungua macho Alimkumbuka shoga yake Sinyati, hakua amewasiliana nae toka alipo olewa. Alionea haya hata kumpigia simu😔.

“Labda atajua pa kuanzia! Nitamfata kwake”alijisemea

Akiwa njiani kuelekea kwa Sinyati, mama yake alimpigia simu kutaka kujua kilichojiri maana alitoka mbio mbio na hakua amerudi

“Leila… imekuwaje? Hospitali wameanza kuulizia tena. Vipi Umepata hela?”

“Mama, kuna process nafanya, wameahidi leo jioni pesa itakua tayari. Tuwe wavumilivu” Leila alidanganya

“Mwanangu nakuamini. Ubarikiwe”

Leila akakata simu haraka kabla machozi hayajamtoka tena. Hakutaka kumdanganya mama yake ila sasa angefanyaje?? Hakua na namna.

Basi safari iliendelea Akafika kwa Sinyati saa tano kasorobo. Aligonga mlango wa chumba cha cha rafiki yake mara kadhaa ndipo Sinyati akafungua mlango akifikicha macho yake yaliyojaa usingizi.

“Leila ni wewe??? Makubwa Kumbe bado upo duniani?”

“Nisipokua duniani nitakua wapi tena Sinya”

“Aah ndo uniambie au tuseme ndoa ilinoga mno ukamsahau shoga ako?? Labda ulidhani nitakua nakuomba hela baada ya kuolewa na tajiri??” Sinyati alibinua mdomo juu😏

“Embu niangalie tu Sinyaa, naonekana kama naishi maisha mazuri??”

“Mhhh! Ila umeisha sio uongo shida nini??”

“Ndo unataka niongee hapa nje kila mtu asikie? Tuongee ndani bhana”

“Karibu ndani mama!” Sinyati alimpisha, Leila akaingia ndani na wakafunga mlango

Leila alikaa kwenye sofa dogo huku Sinyati akamiminia juisi ya embe ya baridi na kumpa. Leila alikunywa glass nzima bila kupumzika. Kiu aliyokua nayo ni balaa.

“Yani Sinyati ndoa yangu na Zayn ni kama gereza. Haji home hata Jumapili. Nimekaa mwezi mzima kama mjane. Hana muda na mimi. Kaizuia hadi kadi ya benki niliyopewa. Sasa mdogo wangu Lulu anaumwa figo, wanataka laki saba ya kusafisha. Nimemwomba msaada akanitukana mbaya. Sina mtu, nimebakiwa na wewe”

“What?? Leila! Hujaniambia hata kidogo kuwa unateseka namna hii?” Sinyati alimuonea huruma😫

“Nilinyamaza tu. Niliona kama ni mojawapo wa mtihani wa maisha”

“Yani Zayn anakutukana ivo?? Eti jiuze? Mtu kama wewe? Aisee!” 😡 Sinyati alivuta pumzi iliyojaawewsira akaendelea kuongea akisema

“Unajua ungefanya nini? Umtafute Mr Ghali tu, si baba mkwe wako? Atakusaidia!”

“Hapana. Mr Ghali akijua, Zayn atanichukia zaidi. Itakuwa balaa juu ya balaa! Mimi sitaki matatizo”

Sinyati akavuta tena pumzi ndefu, kisha akanyamaza kwa sekunde kadhaa. Akamgeukia Leila.

“Listen… kama unataka hiyo laki saba haraka, kuna njia moja”

“Njia gani?” Leila alikua na hamu ya kujua🤷‍♀️

“Uje Club One! kwenye ladies night wanatoa tip nzuri kwa madansa wapya especially wazuri kama wewe. Ukienda leo jioni, trust me, unaweza kutoka na zaidi ya laki nane cash. Unapata hela ya matibabu ya Lulu na nyongeza juu” 😋

“Wait… unamaanisha nicheze? Yani Nicheze mbele ya wanaume, kisa pesa?? Niwe striper??”

“Si lazima uvue nguo bwana, ni dancing tu. Sexy dance, utapata hela”

Leila alitetemeka maana iyo kazi inahitaji moyo kweli kweli tena bila aibu. Kwa mtu kama yeye asingeweza.

“Sinyati, mimi ni mke wa mtu. Siwezi. Hata kama ndo maisha ya mdogo wangu… siwezi kipenzi” Leila alikataa🙅‍♀️

“Na ukikaa hivi bila pesa, unadhani Lulu atasalimika? Sometimes tunapigana vita kwa silaha zisizotupendeza, lakini ndo zinatuokoa! Mimi sikuchagua kuwa dansa (striper)! But si unaona maisha yangu yalivyo nyooka?? Mama yangu kijijini anaishi vizuri! Also najiheshimu sijawai lala na mwanaume yoyote kazini”

Leila akakaa kimya. Akainuka, akapiga hatua kuelekea mlangoni.
“Ahsante sana, lakini nitatafuta njia nyingine. Najua Mungu atafungua milango”

“Haya, ukishafunguliwa milango unikumbuke na mimi”🤣🤣 Sinyati alimtazama Leila akiondoka bila kugeuka nyuma.

Je nini kitaenda.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

MY LUNA SEHEMU YA : 06  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-luna-sehemu-ya-06
#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Afande sele ft Belle 9 dini tumeletewa
SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+
Mambo ya wakubwa hayo soma kwa uangalifu 18+

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


majario rewards 100 Comments 0
 

MTOTO WA MAMA LISHE

majario rewards 100 Comments 0
 

MY LUNA SEHEMU YA : 06

majario rewards 100 Comments 0
 

NDOA YA MIE ... 8...

majario rewards 100 Comments 0
 

LUVIE binti wa malaya

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest