ENDELEA......
Siku Saba za fungate ziliisha. Asubuhi ya siku ya nane siku hiyo niliamka mapema kwaajili ya kumuandaa Samir kwenda kazini. Cha kwanza kabisa nilimchagulia nguo za kuvaa na baada ya hapo nilizinyoosha. Nilimchagulia viatu na kuviweka katika hali nzuri. Baada ya hapo nilifanya usafi wa chumbani kwangu. Nilienda jikoni nilimkuta mdada wa kazi anapika vitafunwa. Nilisalimiana nae na baada ya hapo nilichemsha maziwa kidogo na kuyabeba kwenye kikombe cha udongo.
Niliingia chumbani Samir Bado alikuwa amelala. Niliaangalia saa ya ukutani ilikuwa Unasoma ni saa Moja. Nilianza kujishauri kumuamsha. Nikiwa nawaza naanzaje kumuamsha. Namshika wapi π
nilimuona mwenyewe anajigeuza. Haraka nilimgeuzia mgongo. Nilianza kupiga hatua za taratibu mpaka kulifikia kabati la nguo. Hakuna chochote Cha maana milichofuata ni basi tu viaibu vya kijinga π
.
Samir aliamka pale kitandani. Na kunisalimia.
"Umeamkaje Nadra?, upo sawa kweli?".
"Nipo sawa Samir".
"Mbona umeamka mapema sana Leo?".
"Amna". Samir aliingia bafuni kuoga muda mchache alitoka alinikuta nimekaa kwenye kochi nasoma kitabu.
Baada ya kumuona ametoka akiwa amejifunga taulo kiunoni na juu akiwa kifua wazi na vile anakifua kizuri balaa ninyanyua kitabu na kusogeza usawa wa uso wangu ili kujiziba.
Samir alinitazama na kuachia tabasamu. Alishangaa baada ya kuona nishamuandalia Kila kitu. Aliniangalia Tena Bado nilikuwa nimejiziba na kitabu.
Alivaa nguo pamoja na viatu baada ya hapo aliniita kwa jina langu.
"Nadra!".
"Abee!". Niliitikia na kushusha kitabu, tayari alikuwa ameshavaa mwenyewe.
"Naenda kazini tutaonana badae".
"Sawa ila nimekuandalia maziwa". Nilisema hayo na kuyachukuq Yale maziwa. Nilimsogelea Samir na kumpatia kile kikombe. Alikipokea na bila hiyana alikunywa Yale maziwa. Gafla tulisikia mlango unagongwa Kwa fujo.
Nilienda kufungua mlango Samira ndiye aliyekuwa anagonga.
"Karibu". Aliniangalia Kwa kunipandisha na kunishusha baada ya hapo alinisukuma na kuingia chumbani. Sio kwamba nilikuwa nimemzuia mlango ila ni fujo zake tu.
Alimkuta baba yake amekaa kwenye kochi anakunywa maziwa.
"Nimeishiwa Hela na nataka niende shopping Leo". Aliongea hayo hata kabda ya Salamu.
Samir alichomoa wallet na kuhesabu noti kadhaa za elfu kumi. Baada ya hapo alimnyooshea mwanae kumpa.
"Haitoshi ongeza". Samira aliongea. Nilibaki nimepigwa na butwaa. Pesa alitompa haikuwa chini ya laki tatu ila anasema haitoshi.
"Ebu kwanza Samir. Nipe hizo Hela". Nilimwambia Samir. Samir aliniangalia na mimi niliendelea kuinyoosha mkono wangu kutaka zile pesa. Samir alinipa zile Hela.
"Nipe na hiyo wallet Yako". Samir alinipa wallet, Samira alikuwa ananiangalia kwa dharau.
Niliziweka zile pesa kwenye wallet na kumgeukia Samir.
"Huyu ni nani Yako?". Nilimuuliza Samira huku nikimnuooshea kidole Samir.
"Inamaana hujui au, alafu wewe kama nani mpaka uniulize hivyo?".
"Nimekuuliza huyu ni nani Yako?".
"Baba". Samira alinijibu.
"Umemsalimia baada ya kuingia humu chumbani au ulionana nae kabda?".
"Bhana weee! Achana na maisha yangu. Fuata kilichokuleta humu ndani".
"Okay basi ni hivi. Pesa hupati hata Senti. Unamuombaje pesa baba Yako hivyo kwani una mdai?, kwanini unamkosea adamu baba Yako?.
"Baba unanipa pesa hunipi?". Samira alimuuliza baba yake Kwa ukali.
"Hakupi hata Senti mimi ndo nishasema. Ukijifumza kumuheshimu ndipo utapata pesa yake. Samir naomba kuanzia Sasa huyu mtoto niachie mimi". Niliongea hayo na kumfanya Samira afulu Kwa hasira. Alitoka chumbani akiwa amechukia na sikumpa hata Senti maana wallet nilikuwa nimeshikilia mimi.
Samir alikuwa ananiangalia tu. Nadhani hakuamini kile nilichomfanyia Binti yake.
"Kunywa maziwa my dear". Nilimwambia baada ya kuona ananitazama kwa mshangao. Nilimludishia wallet yake aliipokea.
Alipomaliza kunywa maziwa aliniaga akaondoka. Alipotoka niliona simu yake kitandani nikajua ameisahau. Nilitoka nayo Ile simu na kushuka nayo chini. Nilimkuta anafungua mlango wa gari, Nilimuita.
"Samir". Aligeuka na kunitazama, nilimsogelea na kumpa simu.
"Asante". Alinishukuru na baada ya hapo alipanda gari na kuondoka. Nilimtazama mpaka alipoishia, nililudi ndani nilikutana na mama Sebleni. Nilimsalimia Kwa heshima zote na baada ya hapo tulisogelea meza ya chakula kunywa chai. Muda mchache Najma na Samira walikuja nao kunywa chai.
"Nasikia Leo mkweo amemfanyia roho mbaya mwanangu". Najma alimwambia mama yake. Nilimuangalia Najma na kumuangalia Samira. Mama hakumjibu Wala kumuuliza chochote aliendelea kunywa chai.
"Eti unawezaje kuingilia Mamlaka yasiyo Yako?. Wewe wa kumpangia Samir Cha kufanya Kwa mwanae?, life style ya humu ndani achana nayo. Fata kilichokuleta". Najma aliongea hayo.
"Hata wewe pia upo upande wa Samira. Unaona sawa mtoto anavyofanya kutokumuheshimu baba yake ambaye ni kaka Yako. Nilitegemea labda upo mstari wa mbele kukemea mabaya ya Samira kumbe ndo kwanza unamuunga mkono. Huna Imani na ndugu Yako Kwa anayopitia juu ya mwanae?. Wewe ni shangazi wa aina gani?".
"Hata kama ndo umnyime hela. Hii sio haki kabisa".
"Ni haki kwasababu Hana heshima. Akiwa na heshima atapewa. Kwanza anakujaje chumbani Kwa baba yake anagonga mlango kama ameenda kumfumania bwana Ake, pili anaelezaje shida zake kwa mabavu pasipo salamu, tatu, kwanini haridhiki Wala kutoa shukrani anapopewa anachotaka. Ajifunze nidhani na akishindwa nitamfunza Mimi". Niliongea hayo kwa kujiamini".
"Nadra yupo sahihi. Na ukiweza kumfunza mfunze haswa. Samira huna adabu kabisa Kwa baba Yako hili hata mimi naumia sana".
"Hivi unajiamini nini wewe, unanini kwanza Cha kunitishia Mimi?".
"Utajua ujui, ila utanyooka tu na majibu ya maswali Yako utayapata tu mdogo mdogo. Mimi ndo mama Yako sawa mwanangu mzuri?"........Nyie sikutaka kujifanya mnyonge maana nishauelewa mziki wa Samira ukikaa kinyonge hata kukupiga atakupiga...............MUENDELEZO 1000 TU. KARIBU KULIPIA KWA NAMBA 0743770612 JINA JOFREY.
UKISHALIPIA NICHEK WHATSAPP NAMBA 0683009150..