SEHEMU YA 1
Leila ni binti wa miaka 22 tu, lakini majukumu aliyobeba kichwani yanazidi hata mzee wa miaka 40. Kila mtu kwao alimtegemea yeye😫.
Alikuwa anaishi na mama yake Bi Salma, mdogo wake wa kike Lulu mwenye matatizo ya figo, na mdogo wa kiume Leo ambaye bado alikuwa yupo darasa la nne. Baba yao alishafariki muda mrefu, na tokea hapo maisha yakaanza kubana mno💔.
Kila asubuhi Leila aliamka mapema kwenda kuchanja madafu kwenye mkokoteni wake pale Coco Beach. Ni biashara aliyo amua kuifanya baada ya kuhangaika sana kutafuta kazi.
Pesa yake aliyo pata iligawanyika mara tatu, alinunua dawa za Lulu, chakula cha nyumbani, na ada ya Leo. Mama yake, Bi Salma, naye alikuwa anachangia kwa kuuza vitumbua mtaani, lakini bado maisha yao yalizidi kuwa magumu😫.
Sasa siku moja Coco Beach kulikua na shamra shamra kama kawaida. Leila alikuwa bize na biashara hadi mida ya saa tano usiku, alibaki yeye na watu wachache ndipo akaamua kufunga biashara.
Akiwa anafunga madafu kwenye gunia, macho yake yakaona kitu cha ajabu pembeni ya beach. Aliona gari moja nyeusi ikisimama mbali kidogo na watu, kisha wanaume watatu wakateremka.
Walikuwa wamebeba kitu kizito, ni kama vile mwili wa mtu. Walimtupa kama gunia kando ya beach, kisha wakarudi garini na kuchapa lapa🙆♀️.
“Hawa ni kina nani tena?” Leila alijiuliza kwa sauti ya chini. Alipohakikisha kuwa gari limeondoka, alitoka taratibu na kwenda kuchungulia.
Kweli ulikua ni mwili wa mtu tena mzee mwenye umri kati ya miaka 55 kuelekea 60.
“Yani bado anapumua!??” Leila aligundua baada ya kumpima mapigo ya moyo.
Aliona pia jinsi alivyokua na damu nyingi mwilini, nguo zimechanika, inshort hakuwa hata na nguvu ya kuinua kidole.
Bila kupoteza muda, Leila alikimbilia mkokoteni wake, akauweka vizuri, kisha akarudi na kumuinua yule mzee kwa shida na kumlaza juu ya mkokoteni.
“Ivi wakinikuta hapa si wataniua na mimi” aligeuka nyuma kila dakika kwa uoga, alipoona kuna usalama
Alianza kusukuma mkokoteni kwa nguvu zote, kutoka Coco Beach mpaka hospitali ya karibu😪.
Kazi haikua rahisi, Leila Jasho lilimtoka kama mtu aliyepanda Mlima Kilimanjaro kwa miguu. Walipofika hospitali, wauguzi walimchukua yule mzee haraka na kumpeleka kwenye chumba cha matibabu.
“Nani yupo na mgonjwa?” muuguzi mmoja aliuliza.
“Mimi!” Leila alijibu fasta, kabla hajafikiria.
“Hakuna vitambulisho vyake?” aliulizwa tena.
Leila alitingisha kichwa “Hapana… nimemkuta Coco Beach akiwa hoi kabisa ivyo nikamleta” 😔
Muuguzi alimtazama Leila kwa macho ya mashaka, lakini akamuamini. Wakamuambia akae nje asubiri wakati wakiendelea kutoa matibabu.
Leila alikesha hapo hapo hospitali, macho hakufunga hata sekunde moja. Alikuwa na nguo zake za kuchanjia madafu hata hakua kabadilisha na wala hakujali🥱.
Asubuhi ilipofika ndipo daktari alitoka kwenye chumba cha matibabu na kusimama mbele ya Leila alie anza kusinzia
“Tumemstabilize. Amepoteza damu nyingi, lakini kwa sasa yuko salama. Tumemhamisha wodini”
Leila alipumua kwa raha maana usiku mzima roho yake ilikua juu juu. Akaona ni mda sasa wa kurudi nyumbani. Alitoka hospitali kurudi home, jua lilikuwa limeshaanza kuwaka vibaya mno😩.
Alitembea polepole, miguu imechoka hadi akafika mitaa ya kwao huko Tandale. Ile anafika tu anamkuta mama yake Bi Salma amesimama mlangoni, uso ukijaa wasiwasi.
“Leila! Ulilala wapi we mtoto? Mbona hujapiga simu? Unapenda kuniweka rohoo juu na huu uzee?” Bi Salma alilalamika😏
“Mama pole, simu yangu ilikufa chaji! Yani nilikutana na heka heka sio mchezo!” Leila alijibu huku akikaa kibarazani
“Aisee! Kuna nini kimetokea?? Tuambizane” Bi Salma alikaa pembeni ya Leila ili apate kusikia habari
Leila akaanza kusimulia kilicho mtokea usiku kucha. Kuanzia alipo msaidia yule mzee na kumpeleka hospitali
“Umefanya jambo la maana sana Leila lakini kwa hali ya sasa usikimbilie hatari ovyo. Yawezekana walio mtupa wangerudi kuangalia, unadhani wangekuona una msaidia wangekufanyeje???”
“Mimi mwenyewe roho ilikua mkononi siikufichi” Leila alijibu polepole.
“Ndo ukae mbali na mambo ya watu! Sio kila kitu unaingilia sitaki shida mimi, tulizo nazo zinatutosha”
“Sasa mama na wewe unaanza kulalamika mno”
“Silalamiki, nakuambia ukweli!”
“Sawa nimeelewa”
Baada ya maongezi, Leila aliingia ndani akaoga haraka haraka, akabadili nguo chap na kurudi kibaruani maana alikua kachelewa sana kufungua.
Alipofika Kama kawaida, alikaa sehemu yake ya kazi! Anapendelea mno kukaa karibu na mnazi. Ni kama kijiwe chake na wateja wake wanajua sehemu ya kumpata.
Aliuza hadi saa nne, kisha akafunga kidogo na kwenda hospitali. Moyo wake ulikuwa unataka kujua kama yule mzee ameamka au bado.
Alipofika hospitali, alielekezwa wodini alipolazwa yule mzee. Alipofika mule ndani, alifurai kumkuta kafungua macho.
Kabla Leila ajasema chochote Yule mzee akauliza kwa sauti dhaifu, “Wewe ndie ulie nileta hapa?”
Leila alisita kujibu🤐
Je nini kitaendelea???
Nakujaa……..
SEHEMU YA : 02
“Wewe ndo yule msichana uliyenileta hapa usiku?” mzee alimuuliza kwa sauti ya upole kwa mara ya pili baada ya kuona Leila hajibu🤐
“Ahhh…. Ndio Mzee ni mimi ndie nilie kusaidia”
Alijibu Leila akitazama chini
Mzee alimtazama tena Leila kwa upole, macho yake yakionyesha shukrani ya dhati.
“Asante sana mtoto wangu. Bila wewe sijui ningekuwa wapi leo. Kwa majina naitwa Mr Ghali. Mimi ni mfanyabiashara hapa mjini” alitabasamu☺️
Leila nae alitabasamu tu kwa heshima. Hakuwa anafahamu jina hilo, hakujua ni nani kabisa. Yeye alikuwa binti wa mtaani alie bize kutafuta hela ili familia yake ipate kuishi. Hakua na time ya kuangalia habari wala kusoma magazeti!
Angekua ana angalia TV pengine angegundua kuwa Mr Ghali ni mfanyabiashara mkubwa mno Tanzania. Ana pesa mno nani Top 10 ya Wafanyabiashara mahiri nchini.
“ahsante kwa kuniambia jina lako” alijibu Leila
Mr Ghali alicheka kidogo, alishangaa kwa Leila kutokumjua wala kushtushwa na jina lake ivyo akamuuliza “Una itwa nani wewe?”
“Naitwa Leila”😊
Wakiwa bado kwenye maongezi hayo, mlango wa wodi ukafunguliwa taratibu. Aliingia jamaa flanii ivii smart sana, ni mrefu kidogo, rangi ya chocolate! Mbali yakua smart ni very handsome! Na jinsi alivyo serious basi u-handsome wake unazidi kuongezeka mara dufu😍.
Leila alimsifia moyoni kuwa kweli jamaa si haba! Pongezi ziende kwa mama yake maana alizaa kifaa mno👌.
Mr Ghali aligeuka na kusema kwa furaha, “Zayn! Hatimaye umefika!”
Yule handsome man jina Lake ni Zayn! Mtoto wa pekee wa Mr Ghali. Basi Zayn alitabasamu kidogo, akamkumbatia baba yake kwa heshima.
“Pole baba… nilisikia uliumia vibaya!”
“Don’t worry now naendelea vizuri, ila huyu hapa! Huyu ndiye aliyeniokoa. Nisingekuwepo kama si moyo wake mzuri” Mr Ghali alinyoosha kidole chake kwa Leila alikua kimya akiwatazama.
Zayn aligeuka kumuangalia Leila kuanzia juu hadi chini kwa dharau. Kwa jinsi Leila alivyo kua amevaa Alionekana kabisa ni mtu wa shida hapo ndipo Zayn alipo muonyesha dharau😒.
“Okay” Zayn alijibu kwa sauti ya kawaida, bila hata kushukuru.
Leila aligundua kuwa Zayn alimnyali! Ile hali ya kumtazama kama mtu asiye na thamani ilimuumiza ivyo Aliinuka na kusema
“Mzee nitapita jioni kukuangalia tena! pole sana na ubaki salama” ☺️
“Asante sana mwanangu” Mr Ghali alijibu.
Leila akatoka nje akaondoka, Alipokuwa anatembea kulikaribia lango la hospitali, akasikia sauti ya kiume nyuma yake ikimuita.
“Dada!”
Leila Aligeuka, akakutana uso kwa uso na Zayn.
Zayn alisogea taratibu, akatoa wallet yake, kisha akachomoa noti za elfu kumi tano na kumpa
“Chukua hii ya usumbufu wa kumbeba mzee wangu”alisema kwa dharau😏
Leila alishtuka. Alimtazama kwa macho yaliyojaa hasira maana alimsaidia Mr Ghali kwa huruma na hakua akihitaji malipo.
“Unanipa hela ya nini?” aliuliza.
Zayn alijibu bila kumwangalia machoni, “Ya usumbufu. Umemsaidia mzee so najua hakuna kitu cha bure duniani”
Leila alikunja uso, akazipokea zile hela mkononi mwake, akazishika kwa sekunde chache kisha akazimrudishia.
“Mimi sikumsaidia kwa sababu nataka hela. Nilifanya vile kwa sababu nina utu. Hela zako zichukue, mie si omba omba”
Leila Aligeuka na kuondoka bila kusema chochote kingine. Zayn alibaki amesimama hapo akimwangalia Leila akipotelea mlangoni. Na yeye alirudi wodini, akamkuta baba yake Mr Ghali alikuwa katulia kitandani.
“Zayn, nina hisia kuwa aliyenifanyia hii kitu ni Mr David. Yule adui yangu wa kibiashara…” Mr Ghali aliongea kwa upole😔
“Hata mimi Nahisi hivyo, huyo mzee ni hatari. Ila baba, Hata huyo Leila si mtu wa kumuamini”
Mr Ghali alitikisa kichwa, “Hapana, yule binti ana moyo wa dhahabu. Alinibeba, akanisukuma hospitali, na alikuwa na mimi usiku kucha. Kama ni mtu wa kawaida angeniacha nife pale Coco Beach”
“Huyo ni masikini, baba. Masikini wakiona fursa wanapita nayo. Unaweza kushangaa ni yeye huyo huyo alitumwa akufanye hivyo halafu aonekane shujaa…”
“Zayn!” Mr Ghali alimkatisha. “Usiwe na roho mbaya. Dunia bado ina watu wema! Na najua hujampenda binti wa watu! Ila stop! She is not like others”😠
Zayn alikaa kimya, akamkodolea macho baba yake.
“Mimi siwezi kuamini masikini kirahisi, tena hawa wenye sura ya upole ndo wabaya kabisa! Kama alivyo Mama”
Mr Ghali alibaki ameduwaa, lakini hakuongea zaidi.
Je nini kitaendelea?
Nakuja……..
SEHEMU YA : 03
Jioni ile, Leila alifunga biashara yake mapema sana mbali ya kutokuuza sana siku hiyo, alitaka kwenda hospitali kumjulia hali Mr Ghali kama alivyomuahidi.
Alisukuma mkokoteni wake hadi nyumbani, akafunga, kisha akaoga haraka haraka na kuvalia dera safi lililokuwa limechakaa lakini bado lilivutia.
Alipofika hospitali, alisalimia walinzi na kuelekea wodini alipokuwa amelazwa Mr Ghali. Muuguzi mmoja alipomuona, alimuita
“Wewe ulikuja usubui kumuona yule mzee aliyekuwa kitanda namba nne?”
“Ndio, nimekuja pia kumjulia hali” Leila alijibu kwa upole.
“Aaah… yule mzee alishaondoka tangu mchana. Ameruhusiwa. Hali yake ilikuwa nzuri sana”
Leila alishusha pumzi ndefu. “Aaah, sawa basi. Nashukuru”😊 akaondoka
Wiki tatu zilipita bila Leila kusikia habari yoyote kutoka kwa Mr Ghali. Maisha yaliendelea kuwa magumu, Lulu bado alikua anahangaika na maumivu ya figo, Leo naye kila siku alikua analia kuhusu madaftari na viatu vya shule😭.
Siku moja, Leila akiwa kazini pale Coco Beach, akiwa anajitahidi kuuza madafu yake ilhali jua likiwa linawaka kama jiko la mkaa, alishtuka kuona gari moja jeupe aina ya Range Rover likisimama mbele yake.
Kioo kilishushwa polepole, na sura ya Mr Ghali ilionekana. Leila alishtuka, hakutegemea kabisa angekuja kukutana na Mr Ghali. Alisogea mpaka kwenye gari na kusimama pembeni
“Mzee! Karibu! Sijakutegemea leo”
Mr Ghali aliteremka toka ndani ya gari kwa tabu, “Nimekuja kukuona mwanangu. Nilihitaji kukushukuru vizuri, maana siku ile niliondoka haraka haraka”😊
“umejuaje nitakua hapa?”
“Nilijua unauza madafu coco beach maana muonekano wako ulifanya nijue toka siku ya kwanza, i hope sijakufanya ujihisi vibaya”
“Hamna shida, vipi utakaa?”
“ndio, kuna maongezi nataka kuzungumza na wewe”
Leila alimsogezea kiti, wakakaa pembeni ya ule mnazi. Mr Ghali akamuangalia Leila kwa jicho la huruma na kusema.
“Leila… nimefikiria sana. Nimehangaika sana kutafuta njia ya kukuonyesha shukrani yangu… lakini kila njia naiona haina maana. Ila kuna jambo moja nataka, nahitaji uolewe na mwanangu Zayn”
“Apana mzee. Sitaweza. Huyo mtoto wako ana dharau jamani sijapata kuona. Siku ile hospitali alinionyesha mimi ni mtu nisiye na thamani. Hapana kwakweli” 👎
“Zayn ana roho nzuri sana! Yupo vile kwasababu ya mama yake ila ukimjua vizuri utaelewa ninacho maanisha”
“Kama kijana wako ana roho nzuri kwanini umeona kuwa mimi namfaa?? Kuna wanawake wengi wazuri ambao watahitaji kuwa nae”
“Kwasababu Leila wewe niwa kipekee! Una roho nzuri ambayo wanawake wengi hawana! Ulinisaidia bila kuhitaji malipo yoyote! Utamfaa sana mwanangu”
“Asante ila hapana! Siwezi kubali”
Mr Ghali alibaki kimya kwa sekunde chache, akimtazama Leila kwa uso wa mshangao😳.
“Yaani umekataa kabisa kabisa?”
“Kwa moyo wote. Sina sababu ya kuolewa na mtu ambaye haniheshimu. Bora nibaki na shida zangu mzee” 🥱
Mr Ghali akasimama polepole, akavuta pumzi, “Sawa kama umeamua hivyo. Tutaongea baadaye Leila”
Mr Ghali Akaingia garini, akawasha na kuondoka huku Leila akimsindikiza kwa macho mpaka alipo potea kabisa.
Ilipofika jioni, Leila alirudi nyumbani akiwa amechoka maana siku hiyo alipata wateja wengi kidogo. Alipokua anakaribia kufika nyumbani alishangaa kuona Mbele ya nyumba yao kulikuwa na gari la kifahari, gari lile lile alilomuona nalo Mr Ghali mchana.
“Hili ni gari la Mr Ghali kabisa! Sasa anafanya nini hapa?? Kapajuaje nyumbani kwetu??” Leila alijiuliza huku Akiingia ndani.
Alikuta Mr Ghali ameketi sebuleni na mama yake, Bi Salma. Mama yake alikuwa amevaa kanga mpya na alikuwa anacheka cheka kana kwamba kaona hela🤣.
“Karibu Leila!” Mr Ghali alimsalimia kwa upole.
Leila alimtazama mama yake, kisha akakaa pembeni na kuuliza.
“Mr Ghali umejuaje nyumbani kwetu”
“Aaahh! Nimefanya uchunguzi wa hapa na pale nikapajua”
“Kwanini? Mbona tulishamalizana mchana Mr Ghali??” Leila alimtolea macho😳
“Nimekuja rasmi kuzungumza na mama yako kuhusu mpango wangu. Natamani uolewe na mwanangu Zayn. Nadhani hiyo ndo njia pekee ya kulipa fadhila zako”
Bi Salma kusikia vile alishikwa na furaha isiyoelezeka.
“Ee Mungu wangu! Asante! Jamani Leila, umesikia mwenyewe? Yaani haya maisha yetu sasa yatafunguka!”
“Mama, siwezi. Nimeshamuambia Mzew Ghali toka mchana naona Hanielewi. Sitaki jamani” Leila alikataa akitamani hadi kulia ili wamuelewe🥹
Mr Ghali kuona vile alitoa karatasi, akaandika namba ya simu na kuwaachia.
“Chukueni muda mfikiri. Mimi sitaki kuwabana. Lakini fursa kama hii haiji mara mbili Leila! Naomba ukubali tu ombi langu”
Baada ya kusema yale Mr Ghali Akaondoka. Alipotoka tu huku nyuma Bi Salma akamgeukia binti yake kwa hasira😡.
“Leila, una matatizo gani wewe? Huyu mzee anakupa nafasi ya kubadilisha maisha yako na ya familia yako yote! Lulu atapata matibabu, Leo atasoma vizuri! Na wewe unakataa tu sababu kijana hakucheka na wewe hospitali?”
“Mama…” Leila alijaribu kuongea ila mama yake akamkatisha.
“Apana! Ngoja nikuambie, usije ukalia huko mbele! Dunia haijawahi kuwa fair, binti yangu. Kama mtu anakupa mlango wa kutoka kwenye shida zako, si busara kuukataa” 🤨
Leila alishika kichwa, maana Alijua mama yake alikua anaongea pointi, lakini hakutaka kuolewa na mwanaume ambae alishaonyesha kumdharau toka siku ya kwanza.
“Kesho nahitaji jibu Leila!” Bi Salma aliamka, akaingia chumbani huku akiguna.
Leila alibaki sebuleni, kimya, akimwangalia Lulu aliyekua amelala kwenye mkeka. Alimwangalia Leo aliyekua anajisomea kwa taabu. Akashindwa kujua achukue maamuzi gani😩
Je, Leila atakubali?
Nakuja……….
SEHEMU YA : 04
Leila alikosa amani kabisa. Tangu Mr Ghali aondoke nyumbani kwao na kumuachia ile namba ya simu, akili yake haikupata nafasi ya kupumzika.
Kila akimwangalia Lulu aliyelala chumbani akihangaika na maumivu ya figo, moyo wake ulikuwa kama unachomwa na sindano💔.
Usiku mmoja, baada ya kumaliza kuosha vyombo, Leila aliamua kwenda kwa rafiki yake kipenzi Sinyati, mtaa wa pili sio mbali sana na kwao.
Sinyati na Leila walikua marafiki toka wanasoma. Na kila wakati Leila alipokosa mwelekeo, alimkimbilia Sinyati kuomba ushauri.
Alipofika alikuta Sinyati anajiandaa kwenda kazini jioni hiyo. Sinyati mda huo alikua anafanya kazi club flanii ivii inaitwa Club ONE.
“Aisee yani unakataa kuolewa na mtoto wa tajiri alafu unalalamika maisha magumu?” Sinyati alizungumza kwa sauti ya mshangao, macho yakimtoka😳
“Ni vile tu Sinyati Zayn hanipendi. Alinidharau… alinipa hela kama chokoraa pale hospitali, wallah sitakaa nisahau” Leila alijibu kwa sauti ya huzuni.
Sinyati alicheka kweli maana anajua yeye angeipata ile bahati asinge jiuliza mara mbil mbili
“Halooo! Acha mie ncheke! Leila, Watu hawapendani mwanzo kila wakati usiishi kwa kukariri. Maisha yanabadilika. Muda ukienda, anaweza kukuona thamani yako. Ila sasa hivi, think smart! Hapa tunaongelea matibabu ya Lulu na maisha mazuri ya familia yako”🥴
Leila alikaa kimya, akitafakari. Maneno ya Sinyati yalimwingia moja kwa moja kwenye moyo. Alikumbuka alivyoangaika kulipa ada ya Leo mwezi uliopita.
Alikumbuka vile alivyobeba mzigo wa familia peke yake kwa miaka yote. Labda huu ndo muda wa kuweka familia mbele, hata kama moyo wake haupo hapo💔.
Alirudi nyumbani usiku huo akiwa amechoka lakini kichwani alishajua nini atafanya. Alikuta mama yake Bi Salma akiwa sebuleni, anapanga vitambua kwenye karai vya kwenda kuuza kesho yake.
“Mama…” Leila aliita kwa upole
“Naam mwanangu”
“Nimeamua kitu! nitakubali kuolewa na Zayn.”
Bi Salma alitupa karai pembeni na kuruka kama binti wa miaka kumi na saba. Zile habari zili mkonga moyo mnoo.
“Yani umeamua kweli? Ee Mungu wangu! Asante baba wa mbinguni! Ahsante!” 🙏
Leila alitabasamu kwa lazima ila ndani ya moyo alijua atakacho pitia ndani ya ndoa! Hata macho yake yalionyesha huzuni aliyokua nayo.
Bi Salma hakuchelewa. Alitoa ile namba ya Mr Ghali aliyokuwa ameihifadhi kwa makini kwenye biblia yake, kisha akampigia bila kupoteza muda.
“Hallo mzee wetu!”
“Habari nani mwenzangu” sauti ya Mr Ghali ilisikika upande wa pili
“Ni mimi Bi Salma, mama wa Leila”
“Naam Bi Salma, habari?”☺️
“Nzuri tu bwana Ghali! Tuna habari njema. Leila kakubali! Amekubali kuolewa na kijana wako”
“Nini?? Unasema kweliii??”
Mr Ghali nae alishangilia kama mtoto aliyepewa ice cream🤣
“Ndio! Ni faraja kweli”
“Aisee! Hii ni baraka kubwa. Nashukuru sana. Na mimi nitahakikisha kila kitu kinaenda sawa sawa, usijali kabisa!” Mr Ghali aliongea kwa kujiamini.
“Hakuna neno Bwana Ghali”☺️
Basi Mambo yalianza kusonga fasta. Siku chache tu baadaye, taratibu za posa zilianza. Watu wa familia ya Mr Ghali walienda kwa akina Leila kwa magari matatu ya kifahari. Mtaa mzima ulizizima kwa ule ujio Ilikua fire juu ya fire🔥
Mahari ilitolewa tena pesa ndefu kweli, sio pesa tu hadi nguo, vitenge, sukari, mafuta, unga, yani mpaka Bi Salma akalia machozi ya furaha🥺.
“Leila, mwanangu, haya ndo maisha bora niliyokuwa nakuombea! Umeona mambo haya” alisema Bi Salma.
Lakini katika shughuli zote hizo kuanzia kutoa posa, mipango ya ndoa, hadi siku ya kulipa mahari, Zayn hakuonekana hata siku moja.
Hata kwenye picha za maandalizi hakutokea. Alimtuma tu binamu yake aliyekuwa akitoa taarifa, kwa kusema
“Zayn yuko bize, ana biashara nje ya nchi”
Leila alianza kuona dalili za ndoa kua ngumu. Alijua fika Zayn hakua na ubize wowote ni vile hakutaka kushiriki kwenye jambo lolote lile🥺.
“Huyu mtu hanitaki. Anakubali tu kwa sababu ya baba yake” alijiambia mara kwa mara😭
Haya, Hatimaye siku ya harusi ilifika. Kanisa lilipambwa vizuri sana. Maua yalikuwa ya bei, viti vilifunikwa vizuri, kwaya ilikua inaimba live, na kamera zilikuwa kila kona.
Leila alivaa shela safi sana, akapakwa make up iliyokaa fresh akawaka ile mbaya. Aliingia kanisani akitazama chini kwa uoga maana kuogopa ni jambo la kawaida.
Alipofika mbele ya madhabahu, ndipo alipomwona Zayn kwa mara ya kwanza tangu siku ile pale hospitalini. Zayn alisimama kama sanamu. Sio siri nae alibaruza hatari. Kama nilivyo sema mwanzo ni bonge moja la HB!
Ila sasa Hakumtazama Leila kwa mapenzi. Alionekana kama mtu aliye lazimishwa kuoa ikiwa hakua na mpango huo.
Waliposimama pamoja, hawakusemeshana hata neno moja. Zayn aligeuka upande wa kulia na Leila upande mwingine.
Wachungaji waliendelea na ratiba, wageni waliimba na kucheka, lakini wawili hawa walikuwa kama maadui walio lazimishwa kusimama pamoja😩.
Je nini kitaendelea???
Nakuja……….
SEHEMU YA : 05
Baada ya ndoa kufungwa, waliingia kwenye msafara wa magari kuelekea ukumbini. Watu waliimba, walishangilia, waliruka juu kwa furaha. Vibe lilikuwepo la kutosha hasa kwa ndugu wa Zayn🔥.
Lakini ndani ya gari aina ya V8, Leila na Zayn walikaa kimya kama hawajuani vile. Zayn alikua anachati na simu yake, Leila alikuwa akitazama nje kichwa kikiwa mbali kimawazo.
Walipofika ukumbini Sherehe ilianza kwa mbwembwe. DJ alikuwa wa moto mno hakutaka wageni wapoe.
Ulipofika mda wa kuserebuka akina mama walitwanga kisamvu katikati ya dancefloor. Mnajua staili ya kutwanga kisamvu nyie??? Najua hamjui nitawaambia siku nyingine inachezwaje ila for now tuendelee na stori.
Leila alikua anacheka kinafki ilimradi kuonyesha uso wa furaha mbele ya wageni. Basi walipomaliza kupata chakula na shamrashamra zote Mr Ghali alimsogeza Leila pembeni akitaka kuzungumza nae.
“Leila, mwanangu, Nimefanya hii ndoa kwa moyo wote. Sitaki kuficha, najua Zayn ana tabia ngumu lakini he is a nice guy. Na pia, nahitaji kusafiri kwenda South Africa kesho. Usalama wangu sio mzuri maana nimekua nikiendelea kupata vitisho! Nitaenda kukaa huko kwa mda nikishapata ushaidi wa kumfunga Mr David ndipo nitarudi”
“Unaondoka? Kesho?” Leila macho yalimtoka😳
“Ndiyo. Lakini usijali, utakuwa salama. Zayn yupo. Ukihitaji chochote, usisite kunipigia. Hata kama ni usiku wa manane, nipigie. Hili jina unalobeba sasa ni jina kubwa, kumbuka ilo”
Leila alitabasamu kidogo tu, lakini macho yake yalionyesha huzuni. Alijua fika, kama mzee Ghali ataondoka, basi atabaki mikononi mwa mtu ambaye si tu hamtaki, bali pia anamchukia💔.
“Baba uwe na safari njema”
“Asante binti yangu na mimi nakutakia baraka kwenye ndoa yako”
“Asante pia” 😊
Sherehe ilipo kwisha Zayn na Leila walitakiwa waende wakapumzike hotelini. Zayn hakutaka kusindikizwa, alitaka aende peke yake na Leila.
Aliwasha gari na kumwambia Leila waondoke.
Leila alidhani wanaelekea hotelini kama ilivyopangwa Lakini aliona gari linapinda barabara kuelekea Masaki moyo wake ukaenda mbio.
“Mbona hatuelekei hotelini?” Aliuliza kwa upole
“Forget the hotel (sahau kuhusu hoteli). Tunarudi nyumbani”
Leila hakusema kitu.Alitazama nje ya dirisha, machozi yakimdondoka taratibu. Ndani ya dakika 20 Walifika kwenye nyumba ya kifahari yenye gate la remote.
Ni bonge moja la mjumba very classic ina garden nzuri ya maua, apo nje magari yalijaa ya kila aina, ilionekana Zayn alipenda sana magari. Basi Zayn alipaki gari kisha alimwambia Leila ashuke.
Waliposhuka Zayn Alitangulia kuingia ndani huku Leila akimfuata kimya kimya bila kuuliza chochote.
Walipoingia ndani sebuleni Zayn alianza kuongea kwa dharau
“Let’s be clear from the start. Sikukuoa kwa sababu nakupenda. Umeolewa sababu baba yangu amenilazimisha”😏🥱
“Ndio maana hata hukuhudhuria mahari? Hakuna hata honeymoon?”
“Honeymoon ya nini? Mimi na wewe sio couple. Mimi nitalala chumbani kwangu, wewe nenda chumba chochote utakachopenda. Tusisumbuane wala kusemeshana. Sawa?” Zayn aliondoka zake, akapandisha ngazi na kuelekea chumbani.
Leila Aliketi taratibu kwenye sofa kubwa la velvet, akashusha macho chini. Alikaa pale wee akiwaza alipochoka akaingia kwenye chumba kimoja kizuri cha wageni ambako aliamua ndo atakua akilala huko.
Moyoni alikuwa na imani huenda siku moja Zayn atampenda ila sasa haitakua rahisi ikiwa amekua akimuonyesha chuki na dharau.
Je nini kitaendelea Pata mwendelezo kwa bonge Moja la ofaaaa full yaani mpaka mwisho kwa 1000 TU no ya malipo 0789824178 jina irene.