_______________________________________
Ibu wetu akatoka kukaribisha mgeni, alivyofungua tu, akakuta ni mjeda, hakusubili kuambuwa funga, akaamua kufunga ila mjeda akamuwahi, na kuzuia mlango, dogo najua unahasira sana na Mimi, ila naomba uniache niingie tuweke sawa hili, sisi wote ni binadamu...
Lakini Ibu hakutaka kumuelewa, pamoja na mdomo wake lakini alijizuia Ili asilete balaa tena, mjeda akamchana ivi unatambua kama wewe ndio hasira yangu, kupanda zaidi, ulikuwa ukiwasimulia nini watu pale pembeni ya uwanja...
Hapo hata Ibu, aliishiwa nguvu, nakujihisi hatia sana, usijilaumu ni kosa kwangu zaidi kutumia hasira Kwa mtu ambae hahusiki na kusambaza maneno, nilishindwa kujizuia mimi ndie mwenye makosa zaidi...
Nahitaji muelewe, tuweze kuyamaliza haya, aliongea huku akiingia ndani, alivyoingia tu watu wote sebureni wakasimama, " umefuata nini wewe Ibilisi , sikia bro nahitaji tumalize tofauti zetu sote sisi tunamakosa, japokuwa yakwangu yamevuka mipaka, lakini hatuwezi kubadilisha chochote...
Kuliko tuendeleze uadui ni bora tumalize hili bifu, " kijana sisi hatuna shida na wewe, unaweza ukaenda familia yangu haitakusumbua, unaweza ukaenda sasa...
Samahani mzee najua umeongea, Ili tu niondoke hutamani kuniona mbele yako, naomba kuweka wazi jambo moja mzee, tayari sisi wote ni familia, sio vyema kuwekeana vinyongo, naomba uniruhusu nimuoe binti yako...
Hapo kila mtu alipandwa na hasira, japokuwa walizuiwa kuongea chochote lakini walishindwa, ivi we jamaa unajielewa kweli, baada ya kumdhalilisha dada yetu, unakuja kumsanifu, umuoe ili umgeuza ngoma...
Tena mwanangu, hujui tu dua ninayokuombea, itapendeza kama utakaa mbali na sisi, hasa dada yetu, unajua anapitia wakati gani mpaka dk hii? " Nimeshatambua kosa langu ndio maana niko hapa, simuoi kwa sababu yakusahihisha makosa yangu, naumia kwa sababu nampenda...
Ndio maana alipokosea kuingia eneo la jeshi, nilimuachia bila adhabu, kwa sababu tayari nilimuelewa, lengo la siku Ile ilikuwa tu kuwapa onyo lakini sio kwa njia ile, nilitaka tu kumvua nguo na kumwacha, Ili isijekujirudia kunichafua mtaani,....
Lakini kwa sababu tayari, nilikuwa na hisia nae, nilishindwa kujizuia, naomba mniruhusu niongee nae yeye mwenyewe kwa kina, kama kuna mtu anahitaji kunipiga hasila zimuishe, niko tayari, mjomba alimjibu tu kifupi...
Itaendelea...οΏ½οΏ½
Full sh 1000
Njoo WhatsApp katika namba 0683944333.