Kulia kwake aliamini kwamba ndiyo sehemu sahihi ambayo ingemfanya kupoza machungu kwa kile ambacho alikuwa anapitia π. Wakati akiendelea kulia, aliona taxi nje ikisimama π.
Akili yake ilimwambia kwamba kulikuwa na mtu ambaye alishuka katika taxi ile. Alipiga hatua hadi kwenye geti na kufungua.
"Kaka, mbona kama ulikuwa unalia?" π
Sauti hilo halikuwa la mwingine bali ni Rasma, ambaye alikuwa mahala pale akitokea Dar es Salaam ποΈ.
Garma hakuwa na jinsi zaidi ya kumweleza ukweli dada yake kwa kile kilichotokea π. Ilikuwa ni sehemu ya masimulizi ambayo yalimuumiza Rasma. Alijikuta anapatwa na hasira π‘, akatupa mizigo chini na kutaka kuingia ndani, lakini kaka yake alimzuia.
"Muache, hata usimpige wala kumgomea," alisema Garma huku akiwa amemshikiria ndugu yake π€².
"Kaka, huyu mama unavyomchekea ndivyo anavyozidi kukuzoea! Anazidi kukuzoea na si kwamba hana akili? Sawa, mtu hampendi, ndiyo amuumize hata siku ya msiba jamani?" π
"Mama naamini ni mtu mzima, tena mtu mzima hasa, na anafahamu anachokifanya," π§
"Ujinga! Hebu ngoja bwana!" Rasma aling'aka na kujitoa mikononi mwa kaka yake kwa nguvu π€.
Alipofanikiwa kuporonyoka, aliingia ndani na kumkuta mama yake akiwa amesimama karibu na mlango huku akimtazama π. Hasira zake zilimfanya amrushie maneno makali bila hata salamu π .
"Kwa hiyo hapo ndipo umefurahia? Una furaha sasa hivi si ndiyo? Hivi mama, hii roho utaiacha lini? Mbona unaniogopesha hadi kuzaa?" π°
Rasma alikuwa akitetemeka mwili, mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kasi, huku kijasho kikimtoka π¦.
Alimwangalia mama yake ambaye alikuwa amenywea. Ule upole na ubaridi ulikuwa kwa mwanamke yule ambaye alimweka tumboni kwa miezi tisa π€°.
Wanasema kila shetani na mbuyu wake, mtu na mtuwe. Wembe ni mdogo lakini unakata nywele, lakini ukubwa wa shoka umeshindwa kukata nywele πͺβοΈ.
Mama Garma mbele ya Rasma hakuwa mzungumzaji. Pindi mwanawe huyu wa kike alipotoa neno, basi alikaa kimya πΆ. Hakuwa mkali kama ilivyokuwa kwa Garma.
Hii ilitokana na sababu moja yenye kujigawa mara mbili:
Sababu yenyewe ni kwamba kujifungua kwa Rasma kulikuwa kwa njia ya upasuaji π₯, hivyo alimchukulia mwanae kama yai π₯. Alimpenda mno kuanzia utotoni hadi anakuwa π.
Kisiele kingine ni kuwa Rasma alikuwa wa mwisho, licha ya kuwa wa mwisho pia alikuwa ni mwanamke, hivyo mapenzi yalizidi mno kwa mtoto huyu π§.
Kuzidisha kwa mapenzi yake kwa Rasma kulimsababisha ajikute anamsikiliza sana, anamwelewa, na muda mwingine hakutaka kumbishia wala kumjibu pindi aongeapo π«’.
Hii ilifanya hata leo, anapogomewa kama mtoto, ashindwe kujibu lolote.
"Narudia tena, hii tabia unayoifanya hapa iwe mwanzo na mwisho. Mtoto amefariki kikawaida, lakini wewe unataka kuonyesha kama amekufa kwa kurogwa π§ββοΈ. Nimechoshwa na tabia zako. Kama mtu humpendi, huna sababu ya kumfanyia vituko wala madhira ya kukera kama haya π€. Muache aendelee kuishi. Chuki yako haitamfanya achukiwe na dunia nzima."
Alisema kisha aliingia zake chumbani ambako alimpoza Mayner π.
Kauli za Rasma zilipoza kelele zote za Mama Garma. Zilifanya nyumba ile itambulike kuwa kulikuwa na msiba na si muziki tena πΌπ«.
Watu mbalimbali walikusanyika na taratibu za kufanya mazishi zilianza π―οΈ.
Hawakutaka kuchelewesha sana kutokana na maiti kuwa ya mtoto mchanga πΆ, hivyo walihisi ingeharibika kwa haraka zaidi. Walipofanikiwa kuzika, maisha ya kawaida yalirudi.
Lakini kwa upande wa Mayner, alikuwa kama amechanganyikiwa π΅βπ«.
Wiki mbili sasa, bado akili ya Mayner haikuwa sawa π§ π. Alikuwa mwanamke ambaye amechanganyikiwa. Amani katika maisha yake ilipotea kabisa ποΈπ«.
Hakuna alichokuwa anazungumza zaidi ya kulia π’.
Muda mwingi alikuwa akijifungia chumbani na kuangua kilio π. Alilia kuhusu mtoto wake, akizungumza neno moja tu:
"Mwanangu hajafa." π
Watu mbalimbali walikuwa wakifika pale kumpa pole, lakini hakuacha kuwahadithia jinsi alivyokuwa amejifungua. Hakuwacha kuwalalamikia na kuwaambia jinsi gani Mungu alivyokuwa katili kwa kuchukua kiumbe chake ππ.
Mayner aliichukia dunia ππ«. Alitamani angalau impe muda wa kwenda kaburini kuzungumza na mtoto wake.
Muda wa kulala ulikuwa akiweka mdoli pembeni, basi ikifika usiku sana anajaribu kumnyonyesha maziwa ambayo yalikuwa yakitoka π§Έπ₯Ί.
Hii ilimuumiza sana Garma π. Kama mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwa mke wake π, alikuwa na wakati mgumu.
Kile ambacho alikuwa akipitia mke wake kilimfanya ajihisi kama mmoja wa watu wasiokuwa na thamani π.
Kwake, alimchukulia Mayner kama sehemu ya mwili wake π«. Alimheshimu na kumpenda β€οΈ. Akampa moyo wake wote, akampa akili na afya pia.
Hivyo, kitendo cha kumuona akiwa hana furaha kilimnyima amani zaidi.
Alikuwa mtu ambaye akifika nyumbani, basi ataenda kuzungumza na mke wake huku machozi yakimtoka π’. Baada ya hapo angerudi tena kufanya mazungumzo na dada yake.
Mazungumzo yao yalihusu namna ya kumweka sawa mpendwa wao π£οΈ.
"Nataka nifanye utaratibu wa kumweka sawa Mayner. Anateseka, halafu mimi sipendi awe katika hali hii π. Moyo wangu unaumia," alizungumza Garma huku akiwa amekaa katika gari kwenye eneo la maegesho π, pembeni yake kulikuwa na ndugu yake.
Walikuwa katika kikao kidogo ambacho kwake alikiona ni cha muhimu. Kilikuwa cha muhimu kwa sababu alihitaji namna nzuri ya kumtibia mpenzi wake π.
"Hapo naona suluhisho ni kumtafuta mtu wa saikolojia tu," Rasma alisema π§ .
"Kwahiyo namtoa wapi? Najua anateseka, na vinginevyo anaweza kuwa chizi huyu. Mama naye amekuwa si mtu wa kujali," Garma alijibu kwa huzuni π.
"Mama unataka ajali vipi? Kama damu yake anakutukana kisa Mayner, atashindwa kumuacha Mayner mwenyewe. Mimi nitafanya utaratibu wa kumtafuta daktari," alisema Rasma.
"Bora iwe hivyo, nawe kama inawezekana hamia hapa kwangu basi," Garma alisisitiza.
"Sio jambo baya, nitafanya hivyo. Hakuna hata shida," Rasma alikubali π.
Wiki moja mbele, walifanikiwa kumpata daktari ambaye alikuwa ni mwanasaikolojia π©ββοΈ. Daktari huyu alifanya juu chini ili kumweka Mayner sawa.
Kwa uhodari wa hali ya juu, alitumia wiki moja kumjenga na kumuimarisha Mayner kiakili π§ββοΈ. Alimfanya awe mtu ambaye ameanza kurudisha matumaini, hata tabasamu kwake lilianza kurejea π.
Furaha katika nyumba ilirudi, tabasamu kwa kila mmoja lilirudi π. Lakini kwa upande wa mama yao bado alikuwa na kinyongo, huku akipanga mikakati zaidi ya kuhakikisha kwamba anafanikiwa kumuondoa Mayner katika nyumba ile π.
Pindi alipoweza kuzungumza na Ninah pamoja na mama yake, hakuacha kumwelezea hali ilivyo.
"Haha! Amekuwa kama chizi hivi. Akili yake imeruka. Sasa hivi kaweuka na bado hajaanza kunuka, ila siku si nyingi!" π€ͺ
"Shoga haya mambo sijui hata umejifunzia wapi?" π€·π½ββοΈ
"Wee! Nakosaje kuyajua mie? Nina udigo ndani yangu hata kama unaona nakandamiza maneno π. Sipendagi mwanangu awe na wanawake wa ajabu ajabu. Mwanamke ukimtazama unatamani kutapika π€’. Ninah ndiye anaendana na mtoto wangu, siyo yule!" aliendelea kujimwambafai π€.
Hizi ndizo zilikuwa hoja na maongezi yao. Kila walipokutana, basi habari kuu ilikuwa ni kuhama kwa Mayner kwa kumtengenezea ugonjwa, huku wakiamini kuwa siku si nyingi zoezi hilo lingekamilika π€.
Nisingependa nikupangie bei katika kununua simulizi hii. Natamani kuona unanunua kwa bei yako mwenyewe. Pesa yako unaijua, matumizi yake siwezi kukupangia. Je, unataka kununua kwa Tsh ngapi? Njoo Whatsapp namba ni 0717255498..